Haji Manara, Jerry Muro...jipu lingine la soka TZ...

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,229
116,840
Hivi umewahi kumjua msemaji wa timu yeyote ile ya Ulaya?
mnawajua wasemaji wa Man U?au Barcelona?

hivi mnafikiri hizi club kubwa kabisa duniani hazina idara za habari?
zinazo tena zina watu veyr very qualified..

ndo maana zina TV zao kabisa na wasemaji tele
but mnajua why makocha wakikataa kuongea na press before au after
mechi wanaweza kuadhibiwa?

Hivi hatuoni aibu mpira wenyewe huu wa kihuni huni halafu sasa
tunakubali 'wasemaji' wa timu hizinow ndo wanakuwa 'superstars'
wakubwa kabisa wa timu hizo?

Watu wengi sasa wanafuatilia mpira kumsikia Jerry Muro atasema nini
au Manara atamjibu nini

Sura zao ni maarufu kuliko za Donald Ngoma au Hajib au Mayanja..

kila siku wao ndo 'main players' kwenye media.....

halafu tunaulizana why mpira uko hivi?
 
Ndio aina ya maisha tuliyoyachagua, Wa Kimataifa vs Wa Matopeni....
 
Kuna ulazima gani wa kufuata kila tamaduni ya mzungu?acha ushamba we mbumbumbu fc,kila mahala pana aina yake ya furaha,hao ma mc wa timu wanavyotambiana smtm ina waconvice mashabiki mpaka uwanja unajaa,vitu vingine ukitaka kuvizungumza angalia na mazingira,we umeona ulaya tu?unajua america style yao na timu zao?
 
Mtoa mada uko sawa. Lkn shida ni kwamba humu jukwaani ni kama unawapigia mbuzi gitaa.
Hawa wasemaji ni reflection ya 'wadau' wenyewe wa mpira. Wadau wanawaza hivi hivi, wanataka hivi hivi.
Hata viongozi wa klabu hizi wanawaza hivi hivi. Watu competent kabisa kwenye nafasi hizi hawawezi kudumu hadi pale wanapokuwa ma-MC fulani hivi!!!!

Kazi zenyewe hasa za wasemaji hazifanyiki. Angalia kwa mfano tovuti za timu kongwe aibu tupu. Habari zilizopo ni za miezi 2 nyuma. Muda wanaotumia kutoa mipasho kwa wiki ungeweza kutumika kuupdate wavuti za klabu ili madhumumuni ya wavuti hizi yafikiwe- kuitangaza klabu dunia nzima.

Lkn haya ndio maisha yetu na itachukua muda mrefu kubadilika. Fuatilia watu wengi waliojaribu kuingiza professionalism kwenye mpira wetu wameondoka kwa aibu au kimya kimya. Mastaa zaidi ni watu wajanja wajanja, wahuni, watoto wa mjini, na watu wenye sifa hizo za kusahaulisha watu vitu muhimu.
 
MAKOCHA wanazungumzia mechi, WASEMAJI wanazungumzia taarifa za ndan za klabu.

Sio kwamba Ulaya hawapo, wapo sana ila wao wanatumia mitandao ya kijamii zaid (Facebook, twitter n.k) na wao hawana vijembe kama hiv vya kwetu.

Kwahiyo nadhan kinachokukera ni vijembe sio uwepo wao, ila kumbuka kwa watan wa jadi vijembe ni lazima..!!
 
The Boss tatizo sio kina Muro na Manara tatizo ni waandishi makanjanja tulionao wengine tunafikia kuwapa ubunge.

Angalia taarifa ya habari ITV maswala ya afya anahojiwa mwananchi maswala ya daraja kuvunjika na way foward anahojiwa mwenyekiti wa kijiji...na habari inakamilika bila opinion ya mtaalamu na Chombo cha habari kinapewa tuzo na kujiita super brand
 
Hawa wana habari Wa hizi timu sijui awajui kazi zao au ni makanjanja tangu lini afisa habari akaelezea mchezo wakati timu zina makocha kocha ndio anajua mapungufu ya timu Yake Na kwa nini ilifungwa hawa walitakiwa wasimamie habari za mitandaoni Na press za timu zisizousu uwanjani
 
Back
Top Bottom