kijazi07
JF-Expert Member
- Feb 14, 2016
- 1,036
- 2,238
Hajanambia
Aseeh wanawake wanawake [emoji1311] miez mitatu sasa imepita toka nilipo enda moro kumtembelea mamdog nili kaa wiki mbili pale kwake nikapata wasaa wa kumkanyagaa mtto mmoja wa pale mtaani nilimkanyaga mara 3 basi tumeendelea kuwasiliana kwa kipind chote iko hajawah nambia kama alishika ujauzito...
Nimemaliza soo wazee wakazi
Nilipofika nikakuta ndugu zake kibao mm upande wangu nilikuwa na mamdogo tu ila wengine wote walikuwa upande ule mwingine . basi wakanipa wasaa wakujieleza nikajieleza nilisema ukweli tupu nilitaja mpaka duka nililienda nunua condom. Ikafika wakati wa demu kujielezea akawa bado ananikandamiza mm ngoma ilikuwa ngumu sana aseeh nilihis huyu demu alikuwa na malengo na mm kutokana na kitu nachofanya kwa sasa
Mm ni mwanafunz wa udaktar so na idea na mambo kama hayo nikamuuliza maswali magumu sana iliopelekea baba yake ambae ni daktari nae ashtuke na nikaanza kuongea nae lugha moja yaan kisayans zaid kiukwel mkomboz wangu alikuwa yule baba baada ya kugundua ile mimba ilikuwa na miez mitatu nyuma na mm nilikutana nae mwez mmoja tu uliopita chumba chake kilisachiwa wakakuta picha za ultrasound za muda sana kabla hata mm sijamgusa
Basi wakambana sana mwisho akasema ngoma ilikuwa ya jiran yao ambae ni mjeda na alipo mwambia alimtisha kumuua ndo maana alitafuta mtu wa kusingizia nimeandika kifupi tu ila haikuwa rahis sana
Nipo na malizana na mamdogo kisha nirud zang Dar