Haitoshi kuwa na fedha, inatosha kuona fedha kwa akili siyo macho

Mpulusi

Member
Apr 15, 2016
35
31
Kijiweni sometimes kuna mambo mazuri ya kujifunza ila usikae sana, kaa kama sababu zipo.

Kuna jambo lilikuwa linanitatiza sana hapo awali, kwa nini wengine wana hela na wengine hawana, je hela kweli huwa zinaisha? Zikiisha huenda wapi? Nani hasa mmiliki wa hizi hela ni watu binafsi na mashirika au serikali?

Nikagundua kwamba huu ni mchezo usiohitaji hasira, lazima ujue kanuni za mchezo huu ndio uucheze, vinginevyo utaingia kwenye football ukacheza netball.

Kumbe lazima uzione hela akilini kwa asilimia 95 na kwa macho yako ya nyama asilimia 5 tu.

Pia ujue hesabu na uwe rafiki na fedha, mwishowe zitakufuata.

.. Tuongezee mengine wadau ili Afrika nasi tujitoe kwenye hili dimbwi la umasikini
 
Kweli kabisa, yaani kuziona akilini kwa asilimia 95 maana yake ni kwamba lazima uwe na wazo kwanza kama unataka kufanya biashara, ndiyo hatua ya kutafuta mtaji ifuatwe. Maanake haiwezekani uwe una wazo kupata kiasi fulani cha pesa bila kujua utafanyia nini? Hapo kwenye kujua hesabu na kuwa rafiki wa fedha ni kwamba, kama unataka kuendelea ni lazima kiasi kinachoingia ( mapato) kiwe kikubwa kuliko kinachotoka ( matumizi) hivyo unakuwa rafiki wa fedha kwani muda wote utakuwa nazo, nazo zitakuwa na wewe beneti.
 
Nakubariana na mtoa mada, tatizo la watu wengi wanaamua changamoto ya kutokua na pesa/mtaji kukatisha Mawazo ya kutengeneza vizuri idea zao vichwani! Wanasahau pesa Ni ideas na sio makaratasi, ukitengeneza ideas pesa zitakuja, hata kama hauna pesa wapo watu/Kampuni wana pesa wanatafuta new ideas kuweza kuwekeza! Sema kwa Tanzania Kuna shida ya kuwasaidia watu wenye ideas kutimiza malengo Yao, Kuna rafiki yangu yupo Germany anasema kule Kuna Tv show ambazo hutoa mitaji kwa watu hasa vijana wanaokua na ideas nzuri, na misaada yote ya kitaalam, pia Serikali, lakini Tanzania utasikia kila siku watu wakilalamika kuibiwa ideas zao na matajiri au Kampuni!
 
Watu wengi hufeli kwa kudhani pesa ni makaratasi yenye thamani ya fedha,hivyo wakiyashika ndio hujisikia wanapesa

lakini kiuhalisia pesa huwa haipo real pesa ni mipango au mchakato wa ufanikishaji upatikanaji Wa fedha kichwani,kutajirika na kuwa masikini inategemea na mzunguko wa kichwa chako unatengeneza pesa nyingi au chache,Pesa ikishafanya transform kutoka akilini hadi kuwa halisia hapo tayari inakuwa imebadilika umiliki inakuwa sio ya kwako tena kuna mtu mwingine tena ambae yeye ni pesa kwake iko kichwani inabidi umpelekee so ikiwa halisi wewe unakuwa muwakilishi tu unaipokea na kwenda kuitoa kama sio dukani,shuleni NA kadhalika kwa ajili ya mahitaji hivyo umiliki halali wa pesa uko kichwani zaidi ya halisi...

ukitaka kutajirika ni kutengeneza pesa nyingi zaidi kichwani zenye uhalisia kuliko pesa halisi.
 
wengi hua wanalalamika tatizo mitaj ila ukiwauliza ukipata huo mtaji utafanyia nn hua wanashndwa kujielezea mawazo yanakua hayana mashiko
ukishakua na idea kwamba nataka kufanya kitu fulan hata mtaji haitokua tatizo kuupat
 
Back
Top Bottom