Tiba
JF-Expert Member
- Jul 15, 2008
- 4,604
- 3,163
Wana JF,
Naomba mniruhusu niwashirikishe kitu kimoja kilichonifurahisha jioni ya leo. Nimepata bahati ya kupelekwa Haiti na moja ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kwa ajili ya kuangalia mwenendo wa uchaguzi. Uchaguzi huo umefanyika leo tarehe 20 March 2011 na mimi niko hapa Port-Au-Prince Haiti kuanzia tarehe 15 March 2011. Juzi tarehe 18 Rais wa zamani Jean Betrand Aristide alirudi Haiti baada ya kukaa uhamishoni kwa muda wa takribani miaka 7. Alipoingia mjini Port-Au-Prince kila kitu kilisimama kwani trafiki jam ilikuwa kubwa na watu walishindwa kuwahi kwenye shughuli zao.
Jioni ya leo baada ya kushuhudia uchaguzi ulivyokwenda, nilirudi hotelini kwangu na nikiwa chumbani nilifungulia TV channel 18 ambako walikuwa wanaonyesha mapokezi ya kiongozi huyu wa nchi wa wazamani. Akiwa pale airport alipewa nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari na kwenye hotuba yake alitumia lugha mchanganyiko kama kifaransa, kiingereza, kispanish, creory na cha kufurahisha zaidi alitumia pia kiswahili. Alisema "umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu na mtu ni watu" kwa kweli nilikunwa sana na maneno yake haya ya kiswahili na nilijikuta napiga makofi kabla ya kugundua kwamba niko peke yangu chumbani.
Mkubwa huyu amepromote kiswahili, je sisi kama watanzania tunachukua hatua gani kuhakikisha lugha hii inaendelea kutambuliwa kimataifa?
Tujadili.