Haitakuwa na Afya kwa Bunge na Mahakama historia itakapoandikwa, Spika wa Bunge aondolewa kwa kutoa maoni yake

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,161
1,493
Mheshimiwa Rais, hakika umeonyesha ukikasirika hutaki utani, umeonyesha hasira zako na ukuu wa Cheo chako.
Mama yetu mpendwa, naamini baada ya kumjibu ndugu Ndugai umemaliza na unaendelea kuchapa kazi, Watanzania wako nyuma yako wanakuombea leo na kesho.

Mama yangu SSH, nikuombe kamwe usiruhusu Spika akaondolewa maana tayari watu wameshaanza kuwa aondolewe.
Kwa ustawi wa ukuaji wa demokrasia nchini, uhuru wa kutoa maoni, itakuwa pigo kwa Mahakama na hata Spika anayekuja pale historia itakapoandikwa spika aliondolewa kwa kutoa maoni yake binafs kama Mtanzania.

Mama yetu, tunaona juhudi zako kubwa, tunaona vyumba vya madarasa zaidi ya 15,000 yaliyojengwa, vituo vya kutolea huduma za Afya, umaliziaji wa maboma, ujenzi wa hospital, ujenzi wa shule mpya, ukarabati wa shule kongwe, ujenzi wa barabara, Watumishi kupandishwa vyeo...

Mungu ibariki Tanzania
 
Vipi mpaka sasa ina afya au haina afya?

Ndugai alivuna alichopanda. As well as Bashiru, Makonda na Sabaya
 
Back
Top Bottom