Wana JF,
Habari za kushambuliwa kwa WABUNGE WAWILI wa CHADEMA na wahuni ambao kwa uhakika ni WAFUASI wa Chama Twawala na Chama Cha Mafisadi-CCM zinasikitisha sana na KUCHOCHEA HASIRA MIONGONI MWA WATANZANIA WAPENDA HAKI,AMANI NA DEMOKRASIA ya kweli.
Sipati picha kwanini hili litokee kwa Wabunge wa CDM na siyo kwa Wabunge wa CCM. Hii kitu haiwezi kuruhusiwa iendelee kwa mara nyingine tena. It must be once and for all. Vinginevyo CCM wanataka nchi hii iwake moto. CCM wasifikiri sisi Watanzania ni wapumbavu kiasi hicho cha kuanza kunyanyasa Watanzania simply because wako upinzani. Hili halikubaliki hata kwa yodi moja.
Sasa mimi nasema hivi maadamu Uchaguzi wa Arumeru Mashariki umekwisha kwa Ushindi wa Kishindo kwa CDM, nawaomba Viongozi waandamizi wa CDM wafuatilie swala hili kwa karibu na wale WOTE WALIOHUSIKA kwa njia moja au nyingine lazima washikishwe adabu. Inashangaza mpaka sasa POLISI MWANZA HAWAJAKAMATA MHUNI YOYOTE WA CCM wanaendelea kuzuga tu na kujaribu kupotezea. Hii ni NO,NO,NO,NO and NO again.
Tunataka RPC Mwanza awajibike kwa upuuzi huu maana mazingira tu yanaonyesha kuwa hii kitu ilikuwa planned from the very beggining. Waheshimiwa Wabunge walipiga simu police immediately baada ya kuona wamezingirwa lakini polisi hawakuchukua hatua yoyote na mpaka sasa hawajakamata mtu yeyote.
Dr. SLAA,Mhe. Mbowe,Zitto Kabwe na viongozi wengine tunaomba hili jambo lifuatiliwe mpaka mwisho na tuone kuwa SHERIA INACHUKUA MKONDO kwa haraka sana.
Tunajua Rais Kiwete na IGP wake Mwema wanajua na wana full details kuhusu huu upumbavu uliofanywa na Jeshi la Polisi Mwanza. Kwa heshima na Taazima tunaomba wachukue hatua. Kunyamaza kwao kimya tutajua wao ndiyo waliotoa maelekezo ya Wabunge wetu kupigwa na pengine kulikuwa na mpango wa kuwaua.
Siamini kama haya yanatokea ndani ya Tanzania. Anyway yote hii ni dalili ya KIFO CHA CCM.