hippocratessocrates
JF-Expert Member
- Jul 1, 2012
- 3,598
- 1,539
Katika uchaguzi huru na wa haki, kila mpiga kura huwa na uhuru wa kuchagua mgombea yeyote anayeona anafaa lakini pia huwa huru kwa lolote ikiwa kura yake ameiharibu, amechagua kiongozi ambaye hatafaa au yule anayefaa.
Katika uchaguzi wa mwaka 2020 Tanzania, inaweza kuonekana ulipagwa kwa ubora (ubora wa siku zaidi ya moja) za upigaji kura, ikipendekezwa kwa makundi maalumu mfano wanausalama kama vile Jeshi la polisi,ulinzi,wanajeshi n.k
Tukumbuke Jeshi lolote humtii Amiri Jeshi mkuu na halipaswi kuenenda kinyume na matakwa ya amiri jeshi mkuu. Na hivyo katika uchaguzi wa mwaka huu 2020 Tanzania, "uhuru" wa wanausalama n.k kwenda kupiga kura siku tofauti na "raia" wengine ni kuondolewa uhuru wao.
Ni nani asiyejua kura zinahesabiwa?
Katika heshima ya watumishi wa umma, jeshi n.k kuwa mkubwa yuko sahihi siku zote. Ni mwana jeshi gani -anga,ardhini,majini n.k atakayekuwa na uhuru wa kupiga kura kinyume na chama tawala cha amiri jeshi mkuu na awe salama?
Makundi ya wahitaji maalumu mfano walemavu, wazee sana, wajawazito n.k kwanini hawa hawakuwa na siku yao pekee? Ikiwa walipishwa na mahali pengine kuwekewa msururu/ mstari/ foleni yao pekee kwanini ishindikane kwa wanaulinzi na usalama?
Ni dhahiri ni njia ya utisho usioonekana kwa macho na kwa urahisi kwa wanausalama, jeshi, watumishi wa umma n.k ili kujihakikishia kura kwa kiongozi mkuu wa umma na jeshi.