Kansigo
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 2,670
- 2,156
Nianze kwa kukiri kuwa mimi bado ni mwanaCCM
Ni ukweli usiopingika kuwa vyama vya siasa vya upinzani na wanasiasa wa upinzani ni nguzo muhimu katika ujenzi wa demokrasia ya uwakilishi. Vyama vina kazi nyingi kama vile kuelimisha, kushawishi watu kushiriki katika michakato ya kisiasa, kutafuta wanachama, kuandaa viongozi, kutunga sheria kupitia bunge, na kushiriki katika chaguzi.
Historia inaonyesha huko nyuma kabla ya awamu ya nne kuingia madarakani, wenye fikra za kukipinga chama tawala, CCM na Serikali walikuwa wakitengwa na hata kupewa majina mabaya na kwa wengine unatafsiriwa kama ni uadui, na wakati mwingine ni uhaini.
Hali ilibadilika sana awamu iliyopita chini ya raisi jk. naipongeza serikali ya awamu ya nne ambayo ilikuza demokrasia na kuwachukulia wapinzani kama ni sehemu muhimu ya utatuzi wa matatizo ya kijamii na kisiasa. wapinzani waliitwa ikulu kujadili mambo mazito ya kitaifa pale ilipobidi.
Mpendwaa Rais Magufuli haikuwa sahihi kuwawaambia neno lile "nonsense" wanasiasa ambao walipinga utaratibu uliotumika kuwafukuza wanafunzi wa SPECIAL EDUCATION UDOM.
Wachukulie wapinzani wako kama ni partners katika kuwaletea watanzania maendeleo kama alivyofanya mtangulizi wako Jakaya. Utumiaji wa maneno bila kuangalia athari zake baadaye ni hatari sana