Haikuwa kazi rahisi kwa Yanga-Nimeicopy na kupaste kutoka sehemu

bujashi25

JF-Expert Member
Jun 17, 2013
623
112
Naipenda YANGA
'SINGO' TAMU YA MAREHEMU MWALUVANDA KATIKA
ALBUM BORA YA PLUIJM.
Sishangazwi na mafanikio ya Yanga wanayopata kwa
kutawala soka la ndani, Sijaona ajabu kwa kikosi hiki
kubeba ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara wakiwa na
mechi 3 mkononi, hata wakibeba kombe la shirikisho
nchini mei 25 kwa kuifunga Azam FC katika fainali
kwangu bado haitakuwa habari kubwa.Naizungumzia
Yanga ya kocha mtaalam na mzoefu wa soka la Afrika
Hans Van Pluijm akisaidiwa na Juma Mwambusi, hii ni
Yanga inayoendeshwa kisomi mno chini ya uongozi wa
Yussuf Mehbub Manji.Yanga hii kubeba vikombe vya
ndani sio habari ya kushtua, Azam FC wanaopepesuka
ama Simba SC walio ICU wataizuia vipi Yanga hii iliyotimia
kila idara?kwa ubora huu wa Yanga inapaswa kutoka nje
ya mipaka ya Tanzania, huko ndiko habari kubwa,
kushtua na za kusisimua tutazipata____ Yanga kuibuka na
ushindi dhidi ya TP Mazembe kule Lubumbashi, Etoile
Sportive du sahel kuiombea Yanga ambaye ni kinara wa
kundi A afungwe zaidi ya magoli 7 katika uwanja wa Taifa
dhidi ya Mo Bejaia ili watunisia hao watinge nusu fainali,
hizi ndizo habari za kusisimua ambazo Hans Van Pluijm
anataraji kutuletea, mechi zetu zitarushwa na Supersport
huku Thomas Mlambo ama Terry Mbe wakiyataja majina
ya Kamusoko, Mwashiuya kwa lafudhi ya kiingereza
yenye kubabaika.
Matokeo ya jana katika uwanja wa Estadio Sagrada
Esperanca Dundo kwa Yanga kufuzu hatua ya makundi
kuna baadhi ya watanzania hawajapendezwa nayo, Yanga
imepigana ki-yatima huku wakijua kuna watu
wanaikandamiza maksudi!hawa ni wale watu waliotaka
ubora wa Yanga usionekane kimataifa. . . Baada ya
mchezo dhidi ya Yanga hapa Dar, Grupo Desportivo
Sagrada Esperanca walipewa muda wa kujiandaa
ambapo walicheza mchezo mmoja tu huko kwao,
shirikisho la mpira wa miguu nchini Angola likahairisha
mchezo wa klabu hiyo dhidi ya Recreativo da Ceala
uliopaswa kucheza jumamosi ( 14,May) hii yote
kuwaandalia mazingira mazuri mshiriki wake.Hali ilikuwa
tofauti Tanzania, Yanga waliokuwa wanalalamika ugumu
wa ratiba waliendelea kulazimishwa kucheza katika
viwanja tofauti kama mbio za mwenge kitaifa,kuna
wengine walifikia hatua kushtaki kwa waziri mwenye
dhamana ya kuendesha michezo nchini Mh. Nape
Nnauye wakitaka Yanga wamalize viporo vyao, Yanga
walijaribu kukata rufaa hata hivyo shauri lao likatupwa
hakukuwa na namna Yanga ikabidi wacheze wakilazimika
kutumia usafiri wa anga ili kuepusha uchovu kwa
wachezaji wake (tar 10, may) Yanga walikuwa Mbeya
dhidi ya Mbeya City, ratiba ikionesha (13, May) wana
mchezo dhidi ya Ndanda katika uwanja wa Nangwanda
Sijaona mkoani Mtwara kisha warudi Dar ndipo waende
kucheza dhidi ya GD Sagrada Esperanca (18 May ) katika
mji wa Dundo kaskazini mwa Luanda takribani Km 1300,
TFF haikujali wala wenye dhamana ya mchezo huu pia
hawakujali, uongozi wa Yanga ulipoona jahazi linazama
ukaomba msaada Ndanda mchezo huo ufanyikie Dar,
ombi ambalo lilikubaliwa ndipo mchezo ukafanyika
jumamosi (14 May) watu wasioitakia mema Yanga ndipo
wakaanza kupinga uhalali wa mchezo huo kuhamishiwa
Dar, wacha- Mbuzi wa michezo na waandishi uchwara
wakashika kalamu zao na kuanza kuponda kitendo hicho
cha kizalendo na maslahi kilichofanywa na viongozi wa
Ndanda____ hatimaye Yanga wakaondoka kuelekea
Angola alfajiri (16 May), huko ilikuwa vita sio mpira tena!
kwa ubora wa timu yetu tumeshinda (Ahsante Mungu),
sijasahau Nape alipowaagiza Yanga wafanye uchaguzi
mkuu wa viongozi wa klabu hiyo mwezi April akitoa
takribani wiki 2 tu zoezi hilo kukamilika siku chache kabla
ya kuwavaa Al Ahly____ hakuna aliyejali kuwa mafanikio
Yanga yatawafaidisha TFF kwa kupewa pesa, ama idadi ya
klabu za Tanzania katika michuano ya CAF itaongezwa
kutoka mbili hadi tatu pia kuwa nchi yetu inatangazwa na
kuletewa sifa,au wachezaji wazawa uzoefu wanaoupata
utasaidia kuimarisha timu ya Taifa, ilikuwa vita dhidi ya
TFF ambao walishindwa kutuandalia mazingira mazuri
Yanga kama mshiriki wake kimataifa, vita dhidi ya wote
wenye dhamana ya mpira wa mguu, mwisho wa siku
tumeshinda Ubingwa wa ligi kuu, tumefuzu robo fainali
kombe la shirikisho barani Afrika pia tupo fainali ya
kombe la shirikisho nchini, aibu yetu ama aibu yao??
Puijm amenikumbusha mwaka 1998 hii ni baada ya
hapo jana kupiga wimbo wa marehemu Tito Mwaluvanda
(Pumzika kwa amani)___ Marehemu Mwaluvanda alipewa
timu akiwa hana umaarufu wowote ambapo mwenyekiti
wa Yanga wakati huo marehem Rashid Ngozoma
Matunda alimtambulisha mbele ya wanachama kama
msimamizi wa mazoezi huku timu ikiendelea kusaka
mwalim wa uhakika, cha ajabu Mwaluvanda akaiwezesha
klabu ya Yanga kuchukua ubingwa wa ligi kuu, Kombe la
Muungano na kuifikisha timu hiyo hatua ya makundi
klabu bingwa Afrika rekodi ambayo haikuweza kufikiwa
na kocha yeyote kabla na baada ikiwa takribani miaka 18
sasa, hata hivyo Mwaluvanda na msaidizi wake Fredy
Felix Minziro waliondolewa kwa kigezo hawana uwezo wa
kuifundisha timu katika hatua ngumu ya makundi klabu
bingwa ndipo wakaletwa Raoul Jean Pierre Shungu,
aliyekuwa anasaidiwa na Abeid Mziba 'Tekero', Tayari
Hans Van Pluijm ana ngao ya jamii, Ubingwa wa ligi kuu,
yupo fainali ya kombe la shirikisho nchini kabla ya hapo
jana kutukumbusha wimbo mtamu wa Tito Mwaluvanda
katika album yake.
Waambieni wale walioponda mapokezi pale Dida
alipobebwa Airport baada ya Yanga kutolewa dhidi ya Al
Ahly tulikuwa na maana yetu, mapokezi yale yaliwapa
deni vijana wetu na jana wamelipa!nakukumbusha kama
ulikuwa na mpango wa kuuza decorder yako ya Dstv
usifanye hivyo bali ilipie ili uweze kuishuhudia timu
yako_____ Timu yetu leo italala Afrika Kusini itawasili JNIA
hapo kesho.
Nakutakia siku Njema Mwananchi.
Admini Hissan Salum Iddi.
 
Duh, aisee.............nimependa ulivyoandika, na kupeleka ujumbe mzito
 
Hata kama ume copy umefanya jambo jema kueleza namna viongozi wetu wa TFF walivyo mambumbumbu na utaifa haupo hapo.
 
Back
Top Bottom