Mwanagandila
Senior Member
- Oct 9, 2011
- 182
- 100
Wafanyakazi wa Shirikisho la Soka Tanzania -TFF sasa wametimiza miezi mitatu bila ya kulipwa mishahara yao, baada ya kulipwa mara ya mwisho Februari 15, 2016.
Kwa kipindi cha miezi mitatu Machi, Aprili, Mei 2016 wafanyakazi hao wameendelea kufanya kazi zao za kila siki, huku Katibu Mkuu wa TFF ambaye ni mtendaji mkuu wa taasisi hiyo akiwa anapishana kimya kimya na wafanyakazi wake, kutokana na kuwapa ahadi hewa tangu mwishoni mwa mwezi Machi 2016.
TFF yenye wadhaminj wengi kama TBL, Azamtv, Vodacom, NHIF, StarTimes, StartTv inashindwaje kuwalipa mishahara wafanyakazi wake mpaka kufikia miezi mitatu?
Naona taasisi hiyo ina matatizo ya kiuongozi kuanzia Rais wake Jamal Malinzi, wajumbe wa kamati ya Utendaji na Katibu Mkuu ambaye ni mtendaji wa kazi za ka siku za ofisi hiyo.
Napatawa wasiwasi na ufanisi wa kazi kwa watu wa taasisi hiyo, mfanyakazi mwenye familia na majukumu anawezaje kuishi miezi mitatu 3 pasipo kulipwa stahiki yake? Nazani hili linapelekea watumishi kuomba milungula kwa wageni wanaofika ofisini hapo kwa shida mbalimbali.