Haiingii akilini bandari kutegemea malori

Escobar

JF-Expert Member
Sep 16, 2011
574
440
Baada ya miaka 52 ya uhuru tumeshindwa kuongeza hata mita moja ya reli, bandari ya Tanga almost chali, Mtwara nako hali ndiyo hiyo hiyo. Na kwakuwa hata treni tuliyoachiwa na wakoloni nayo imekuwa mzigo tumeshindwa kuiendesha wala kuiboresha, na kwa kuwa takwimu zinaonyesha katika tani milion 13 zinazoshushwa na meli ni tani laki 3 tu ndizo zinasafirishwa kwa treni huku zaidi ya tani milion 12 zikisafirishwa na malori, na kwa kuwa wamiliki wa malori ni wanasiasa na wafanyabiashara ambao wengine ni wanachama na wafadhiri wa vyama hivi hivi vinavyotuongoza, na kwa kuwa wasafirishaji wameonyesha nguvu na ushirikiano wa ajabu kwa kuwa wanajua hali halisi ilivyo katika sekta husika yaani ya usafirishaji maana hakuna mbadala, bila malori no upakuaji mizigo bandarini wala kusafirisha mizigo mikoani na nchi jirani. Je itakuwaje siku wenye malori wakiamua kwenda holiday ya mwezi mmoja kama wachina wafanyavyo? Magufuli anasimamia sheria zilizotungwa lakini kwa kutambua udhaifu na mapungufu yaliyopo Mramba enzi hizo akiwa waziri wa wizara husika akaamua kuipiga kapuni sheria hii lakini bila kusema for how long na wala bila kuirudisha bungeni kwa marekebisho. Inasemekana katika siku hizi tu za mgomo serikali imepoteza 20 bilion lakini pia wenye malori nao wanapiga hesabu kuona wamekula hasara kiasi gani, si hilo tu bali hata bandari pia ili-pause kwa muda kupakua mizigo. Swali ni je, hii kauli ya TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA inakuwaje hapa? BIG RESULT NOW kwenye sekta hii imejipangaje?
 
mulize yule jamaa anae binjua mdomo kama beberu kwa majivuno aliewambie watu wa kigamboni kama awawezi kulipa tshs 200 waogelee yule aliowambia wenye malori wayaweke sebuleni kwao yule jina na baba yake pombe
 
Kuna watu wachache waliamua kuua reli iLi wanufaike wao Kwa kutumiaa barabara kwakuwa wanayo Karoli makubwa. Na Ni miongoni mwa viongozi wetu wa sirikali ya Tanzania Ni jambo ambayo hatuna uwezo nalo mpaka watakapo amua wenyewe. Sasa wewe hata upigekelele vipi utaonekana huna akili.
 
Baada ya miaka 52 ya uhuru tumeshindwa kuongeza hata mita moja ya reli, bandari ya Tanga almost chali, Mtwara nako hali ndiyo hiyo hiyo. Na kwakuwa hata treni tuliyoachiwa na wakoloni nayo imekuwa mzigo tumeshindwa kuiendesha wala kuiboresha, na kwa kuwa takwimu zinaonyesha katika tani milion 13 zinazoshushwa na meli ni tani laki 3 tu ndizo zinasafirishwa kwa treni huku zaidi ya tani milion 12 zikisafirishwa na malori, na kwa kuwa wamiliki wa malori ni wanasiasa na wafanyabiashara ambao wengine ni wanachama na wafadhiri wa vyama hivi hivi vinavyotuongoza, na kwa kuwa wasafirishaji wameonyesha nguvu na ushirikiano wa ajabu kwa kuwa wanajua hali halisi ilivyo katika sekta husika yaani ya usafirishaji maana hakuna mbadala, bila malori no upakuaji mizigo bandarini wala kusafirisha mizigo mikoani na nchi jirani. Je itakuwaje siku wenye malori wakiamua kwenda holiday ya mwezi mmoja kama wachina wafanyavyo? Magufuli anasimamia sheria zilizotungwa lakini kwa kutambua udhaifu na mapungufu yaliyopo Mramba enzi hizo akiwa waziri wa wizara husika akaamua kuipiga kapuni sheria hii lakini bila kusema for how long na wala bila kuirudisha bungeni kwa marekebisho. Inasemekana katika siku hizi tu za mgomo serikali imepoteza 20 bilion lakini pia wenye malori nao wanapiga hesabu kuona wamekula hasara kiasi gani, si hilo tu bali hata bandari pia ili-pause kwa muda kupakua mizigo. Swali ni je, hii kauli ya TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA inakuwaje hapa? BIG RESULT NOW kwenye sekta hii imejipangaje?
Hii ni serikali ya slogans/kaulimbiu sio utendaji. Kasi mpya, ari mpya, nguvu mpya, maisha bora kwa kila Mtanznia, kilimo kwaanza, big results now, kasi mpya zaidi, ari mpya zaidi, nguvu mpya zaidi, endelea na zingine ukishslewa kajilalie ili kesho iji na single ni zilezile lakini tuko palepale.
 
Back
Top Bottom