Kazi ya waangalizi siyo kuzuia wizi wa kura. Kumbuka kuwa hawatakuwepo kwenye kila kituo cha kupigia kura nchini. Kimsingi kama jina lao linavyosomeka kazi yao ni kuangalia tu hata kama kura zitaibwa. Sana sana watakachofanya ni kuandika ripoti zitakazo laumu wizi wa kura wa hapa na pale na kisha watahitimisha kuwa huo wizi mdogo mdogo hauwezi kubadilisha matokeo ya jumla.
Ulinzi wa kura ni wa wapinzani wenyewe. Hakuna mjomba toka ulaya atakayekuja kuwalindia kura zenu kwani hiyo siyo kazi yao. Kuna wengine hapo wasingependa mabadiliko makubwa ya utawala kwani mashirika ya nchi wanazotoka yamewekeza sana hapa nchini.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.