Hai: Mwili wa Mhasibu Shule ya Sekondari Nronga waokotwa kichakani

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Wakati jana Mheshimiwa Sabaya akielezea ugumu wa Wilaya ya Hai kiuhalifu leo Gazeti la Mwananchi mtandaoni linatuambia kisa hiki cha kusikitisha.

"Mwili wa mhasibu wa Shule ya Sekondari Nronga inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Helga Lema umekutwa kichakani.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumanne Mei 12, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Amon Kakwale amethibitisha kifo hicho akibainisha kuwa kimetokea jana asubuhi katika kijiji cha Nronga wilayani Hai.

"Ni kweli kuna mwili wa mwanamke mmoja, mhasibu wa Shule ya Sekondari Nronga umekutwa pembeni mwa barabara,” amesema akibainisha kuwa uchunguzi wa kifo hicho unaendelea na kwamba mwili umehifadhiwa katika hospitali ya Machame wilayani Hai."

Chanzo: Mwananchi
 
Huyu ni wa pili sasa kwa mtindo unaoshabiiana, sehemu mbili tofauti kwa umbali wa mikoa kadhaa.

Mtangazaji wa ITV naye mwili ulitupwa sio?

Mungu awape moyo wa faraja wafiwa.

Kazi iendelee.
 
Wakati jana Mheshimiwa Sabaya akielezea ugumu wa wilaya ya Hai kiuhalifu leo Gazeti la Mwananchi mtandaoni linatuambia kisa hiki cha kusikitisha.
Funny enough, yure hooligan Sabaya atakamata wanaChadema na kuwapa kesi. Pumuzika kwa amani muhasibu
 
Funny enough, yure hooligan Sabaya atakamata wanaChadema na kuwapa kesi. Pumuzika kwa amani muhasibu
Si mnasema wanachadema ndio wengi huko Hai sasa kina nani wengine watahusika?
 
Hio kazi itakua ya Ole Sabaaya ambae ni jambazi sugu katika Wilaya ya Hai na maeneo ya jirani, pia anatambulika kama Mzee wa kuomba rushwa kwa mabavu na vitisho vya kutumia silaha za moto.
 
Mtuhumiwa namba 1 hapo ni boss wake maana ndivyo polise wetu wanaweza kufikiria
 
Back
Top Bottom