HAI: Mwalimu awekwa rumande kwa kushindwa kuandika jina la Mkuu wa Wilaya

Mungu niepushe maana akiniletea mtu hizo habari kazini ntaliamsha dude hataamini. Kama mbwai iwe tu DC anipigishe pushapu? Si anifukuze kazi tu nikalime huko Rais atanisamehe maana nitamtukana mwakilishi wake hadi asahau njia.
 
hahahahahah , ma D C Mnamamlaka ya kuweka mtu yeyote ndani masaa 48. walishapewa hiyo amri . sasa huyo nadhani mwezi ulikaribia kuisha aka amua walau atafte wa kumweka ndaniili mwezi huu nao uonekane kaweka mtu ndani .
 
Hakuna sheria inayomhukumu mwalimu endapo watoto watafeli. Kosa la mwalimu kubwa ni pale atakaposhindwa kuandalia, kuazimia na kazi za watoto.
Nawapongeza walimu wote wa shule hiyo kwa ujasiri wao wameonesha ukomavu mkubwa.
Hata aliyegoma kupiga push up kwa kisingizio cha afya bado ni jasiri maana alitumia busara tu.
Mwisho wa utawala huu uko mwishoni na utakuwa wa aibu. Ninaona kaibia madc wengi akili zao ni za kushikiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HUYU ASIPOTUMBULIWA BASI KUNA TATIZO

NIMEMKUMBUKA DC ALIYEWACHAPA VIBOKO WALIMU, ILA ALITUMBULIWA NA JAKAYA.

MIMI NINGEKUWA MWALIMU NINGEMSHITAKI HUYO DC.. MAMLAKA YA DC YAMETUMIKA VIBAYA NA PIA NI UNYANYASAJI.
 
Katika ziara ya kutembelea shule za sekondari,Mkuu wa wilaya ya Hai,Mh.Gelasius Byakanwa alifika shule moja iliyopo ukanda wa chini mwa wilaya ya hiyo akiambatana na afisa elimu msaidizi ndugu Jafari na mwandishi wa habari wa Redio Boma-Hai FM ndugu Davis Minja.

Dc alifanya kikao na walim hao,alianza kwa kuwauliza wangapi wanamfahamu kwa majina,walim walikaa kimya,dc akawaamuru waandike majina yake kwny karatasi aliyowapa.Baadhi ya walim walishindwa na kuwaita WANAFIKI.kosa ni kushindwa kuandika majina yake.
Baada ya mda akawataka waalimu waandike nafasi ya shule mwaka 2015 katika mtihani wa NECTA,mwalim mmoja alishindwa kuandika na alipomfata akimwamuru aandike,mwalim alimjibu hawezi kuandika uongo kwani hakumbiki.Jibu hilo lilimfanya DC apige simu Polisi na kuagiza polisi waje.

Kabla gari la polisi kuja,dc alimwita mwl pembeni na kumwambia achague kati ya kwenda rumande au kupiga push-up 20,lakini mwl alimjibu hawez kupiga push-up kwani anamatatizo ya kiafya.Basi gari lilipokuja mwalim alipandishwa na kupelekwa kituo cha polisi Bomang'ombe.

Dc aliwaambia walimu wakitaka wakashitaki kokote na hata kwny chama chao cha CWT.
Kisha aliwaamuru kupiga picha ya pamoja kama kumbukumbu...

Baada Ya KiKaO hicho.
Dc amekuwa aliwapigia sim walim hao na kutaka kujua kinachoendelea.

Taarifa ilifikishwa chama cha waalim CWT-wilaya na kisha kuja kufanya kikao na waalimu ilikupata uhalisia wa tukio,ndio mwalim mmoja wa kike kuongeza kuwa baada ya kikao kwisha DC alimpigia simu saa zisizo za kazi ikiwa ni pamoja na usiku akimtala waonane.Mwalim alitoa vielelezo vya sms na muda aliopigiwa (screen shoot) zake na kumkabidhi katibu wa cwt mkoa wa kilimanjaro...

Swali.
Je huu ndio uwajibikaji na utawala bora?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nafasi za uongozi hazipaswi kupewa wahuni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom