Hadithi ya Buddha. Back to Basics | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hadithi ya Buddha. Back to Basics

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andrew Nyerere, Nov 30, 2009.

 1. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #1
  Nov 30, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Miaka elfu mbili na mia tano iliyopita watu wa India walikuwa disillusioned na dini yao,mapadre wa Kihindu walikuwa degenerate,wanafikiria raha za Dunia tu,wanafikiria jinsi tu ya kujinufaisha binafsi. Watu ambao walikuwa wanapaswa kuwasaidia walianza kujitenga na imani zao za zamani,na kuegukia chochote kile ambacho kingine kingeweza kuwaletea matumaini angalau kidogo. Manabii na watabiri,walipita katika nchi wakitabiri adhabu na mateso.
  Watu waliokuwa wanapenda wanyama waliamua kwamba wanyama ni bora kuliko wanadamu,kwa hiyo wakawaabudu wanyama kama miungu.

  Wale Wahindi ambao waliokuwa wanajali utamaduni,wale waliokuwa wanafikiri sana ,waliokuwa wanahofu kwa kwa nchi yao,waliiacha dini yao ya jadi na wakatafakari sana kuhusu hali mbaya ya roho ya Binadamu. Mmoja wao wa watu kama hawa alikuwa mfalme tajri,mwenye nguvu. Alikuwa ana wasiwasi sana kuhusu mustakabali wa mtoto wake wa pekee Gautama,ambaye alikuwa amezaliwa karibuni,katika dunia yenye matatizo.

  Baba na familia walikuwa na hamu kubwa sana kwamba Gautama akue kama mtoto wa mfalme mpiganaji,halafu baadaye aurithi ufalme wa baba yake.Mtabiri mzee aliyeletwa kutabiri alisema kwamba huyo kijana atakuwa nabii mkubwa. Kwa huyo baba hiyo ilikuwa ni ''hatma mbaya kuliko kifo'' Aliona mifano mingi ya vijana wa tabaka la juu ambao waliacha maisha ya starehe na kuondoka kama wasafiri na wahujaji,bila viatu huku wamevaa matambara,kwenda kutafuta maisha ya kiroho. Baba alijitahidi kutumia kila njia kuuzuia huu utabiri wa yule mtabiri usitokee,akapanga mipango yake......


  Gautama alikuwa ni kijana mwenye akili makini,ambayo ilikuwa inaweza kuondoa utandu,na kwenda moja kwa moja kwenye moyo wa jambo. Ingawa alikuwa mtawala katika kuzaliwa kwake na katika malezi yake,aliwajali watu wa chini yake. Maoni yake yalikuwa kwamba,alikuwa anaongozwa kwa uangalifu,anakingwa,na anaruhusiwa kukutana na wale tu ambao walikuwa watumishi wake binafsi au na wale wa tabaka moja na yeye.


  Baada ya yule mtabiri kutoa utabiri,baba alitoa amri kwamba mtoto wake wakati wote akingwe kutokana na maovu na huzuni zilizopo nje ya maeneo ya Kasri. Mtoto hakuruhusiwa kutoka nje peke yake;matembezi yake yalipaswa kuongozwa,na hakuruhusiwa kukutana na yeyote aliyekuwa maskini au mwenye mateso. Raha na raha ndio ilpaswa kuwa maisha yake. Kila kitu ambacho kilikuwa kibaya kiliondolewa kwa ukatili mkubwa

  Lakini maisha hayawezi kuendlea namna hii. Gautama alikuwa kijana mwenye ari isiyokuwa ya kawaida. Siku moja,bila wazazi wake kufahamu,bila walimu wake kufahamu,alichomoka kutoka kwenye Kasri pamoja na mtumishi aliyemchagua kwa uangalifu,na akaenda matemebezi na gari lake nje ya maeneo ya Kasri.Kwa mara ya kwanza katika maisha yake aliona jinsi matabaka mengine yanavyoishi. Mambo manne aliyoyaona yalimletea mawazo mengi na yakabadilisha mwenendo wa historia ya dini.
  .
  Alipoanza tu safari yake akamuona mtu mmoja mzee,mzee sana,anatetemeka kwa umri na ugonjwa,ameegemea magongo mawili ya kutembelea na kujikokota mbele kwa maumivu makali,kibogoyo,hana akili za kutosha kwa ajili ya uzee ,yule mzee akamgeukia Gautama na kumtazama na macho ambayo hayaoni vizuri. Kwa mara ya kwanza Gautama akafahamu kwamba uzee unamfika kila mtu,na kwamba mzigo wa miaka unapomuelemea mtu,vitendo vyake vinakuwa vizito.
  Huku Gautama akiwa ameshtushwa sana na jambo hili,aliedelea na safari yake. Lakini kulikuwa na mshtuko mwingine unamsubiri;wakati farasi walipopunguza mwendo kwenye kona kali,Gautama akaona mtu mwenye huzuni,amekaa kando ya barabara,anatikisika kwa na kulia kwa uchungu,mwili wake umejaa madonda,amekondeana na amejaa magonjwa,analia huku akitoa wadudu kutoka kwenye mwili wake.

  Kijana Gautama alishtuwa sana na hili. Mgonjwa moyoni-na labda katika mwili pia-alilifikiria swala alipokuwa anaendeshwa. Ni lazima mtu ateseke? Mateso yanawaijia wote? Je mateso hayaepukiki? Alimtazama mtumishi wake. Kwa nini alikuwa mtulivu namna hiyo,yule kijana wa kifalme alijshangaa. Yule dreva alikuwa hasumbuliwi na jambo hili ,kama vile mambo kama haya yalikuwa ni mambo ya kawaida kabisa. Hii,basi,ndio sababu baba yake alikuwa anamkinga.


  Wakaendelea na matembezi yao,Gautama alikuwa ameshtushwa sana kutoa amri vingine. Destiny au jaala ilikuwa haijamalizana naye. Baada ya Gautama kutoa sauti ya mshangao farasi wakaendeshwa polepole zaidi;wakasimamishwa. Kando ya barabara kulikuwa na maiti ambayo ilikuwa iko uchi,imeharibika na kuvimba kwa ajili ya joto kali la jua. Dereva alipopiga mejeledi wake,nzi wengi waliokuwa juu ya mwili,wakainuka ghafla. Alipotazama,nzi akaruka juu ya mdomo,na kutua tena.
  “ Kwa mara ya kwanza katika maisha yake Gautama aliona kifo,akafahamu kwamba kulikuwa na kifo mwisho wa maisha. Kwa udhaifu mkubwa,kijana akamuamuru dereva arudi,... akakaa anafikiri jinsi ambavyo maisha hayadumu,akakaa kufikria juu ya uzuri wa mwili ambao kumbe baadaye unaoza. Je uzuri ulikuwa ni kitu cha muda tu namna hiyo,akawa anajiuliza?
  Magurudumu yakaendelea kuzunguka,vumbi ikawa inatimka nyuma. Kijana wa kifalme alikaa anawaza mambo mengi,yanamtatiza. Kwa bahati au jaala,destiny,akatazama na kumwona mtawa amevaa vizuri,mtulivu,anatembea kando ya barabara. Yule mtawa,mtulivu na mwenye na shwari,alitoa mionzi ya amani moyoni,na roho ya fadhila,na upendo kwa watu wengine. Gautama aliyekuwa amestuhswa na yale mambo aliyayaona, sasa alimpata mshtuko mwingine tena. Je amani,kutosheka,utulivu,na thawabu nyingine zote,zinapatikana mtu akijiondoa tu katika maisha ya Kasri na kuishi maisha ya utawa wa aina fulani? Atajiondoa kutoka kwenye maisha ya Kasri,maisha peke yake ambayo alikuwa anayafahamu.

  .
  Baba yake aligomba sana,mama yake akalia na kuomba. Yule mtumishi alifukuzwa kabisa kutoka katika eneo la Ufalme. Gautama alikaa peke yake chumbani kwake,anafikiri,anafikiri,anafikiri. Anafikiri tena na tena kuhusu yale mambo aliyayaona.-akawa anafikiria kwamba kama aliona mambo mengi kama hayo katika safari moja fupi,safari yake moja pekee aliyoifanya-lazima kutakuwepo mateso mengi na machungu mengi ambayo hakuyaona. Akakataa chakula,akwa anahuzunika tu,anafikiria afanye nini,anafikiria jinsi ya kutoroka kutoka kwenye Kasri,anafikiria jinsi ya kuwa mtawa.

  Baba yake alijaribu kila njia aliyojua kuundoa mzigo wa huzuni wa huyu kijana. Wanamuziki mahiri kuliko wote waliamriwa kucheza wakati wote ili kijana asipate muda wa kukaa kimya na kufikiri.Wacheza sarakasi waliletwa,na michezo ya sarakasi ya kila aina,na wasanii wa kila aina walijaribiwa. Wasichana wazuri kuliko wote walitafutwa katika Ufalme,wasichana hodari katika mapenzi,ili Gautama ashawishiwe na huzuni yake iishe.

  Wanamuziki walicheza mpaka wakaanguka chini kwa uchovu. Wasichana walicheza dansi za mahaba mpaka wao pia wakaanguka chini,na kuzimia kwa uchovu. Hapo tu ndipo Gautama alipowaona.Alitazama kwa mshangao mkao wao walivyoanguka ovyo,wamechujuka kwa ajili ya uchovu,na manukato yao yanajitokeza kwa hali ya kuchukiza baada ya afya yao kupungua.

  Kwa mara nyingine tena akafikiria jinsi ammabvyo uzuri haudumu,ni kitu cha kupita tu,kitu ambacho kinatoroka upesi. Maisha yalikuwa ya huzuni na ya kuchukiza. Wanawake waliopakwa rangi walikuwa wanachukiza baada ya shughuli yao kuisha. Akaamua kuondoka,akaamua kuyaacha mambo yote aliyokuwa anayafahamu,na kuutafuta utulivu kokote unakoweza kupatikana.


  Baba yake akapiga makelele,akaongeza mara mbili,halafu mara tatu ulinzi katika Kasri . Mama yake akapiga mayowe na kuingia wasisiwasi mkubwa. Mke wake,maskini,akaanguka chini,na wanawake wote katika Kasri wakalia kwa pamoja.Mtoto mdogo wa kiume wa Gautama,ambaye alikuwa mdogo sana kuelewa kilichokuwa kinaendelea,naye akapiga makelele mengi kufuatia vurugu zilizomzunguka. Washauri wa Kasri wakanyoosha mikono yao na kuongea maneno mengi,bila mafaniko yoyote.

  Kwa siku nyingi akafikiria mbinu za kuondoka. Walinzi wa Kasri walikuwa wanamfahamu sana. Watu huko nje katika Ufalme walikuwa hawamfahamu hata kidogo-kwa sababu alitoka nje mara chache sana.Mwishowe,baada ya kuwa karibu akate tamaa,wazo likamjia kwamba anahitaji kuwapiga chenga walinzi wake wa karibu tu. Gautama akatafuta nguo zilizochakaa kama wanazovaa maskini. Usiku mmoja,jioni baada ya jua kuzama,kabla milango ya Kasri haijafungwa,akavaa hizo nguo zake nzee,akazitimua nywele zake,na akaondoka na maskini waliokuwa wanatolewa ndani ya Kasri usiku.
  Akaenda msituni,mbali na njia kuu na watu,kwa kuhofu kwamba kutofahamu mambo ya maisha ya kila siku kutafanya agundulike.Usiku kucha alisafiri,akijaribu kufika ukingoni wa Ufalme wa baba yake.Hakuwa na woga kuhusu wanyama wakali kama chui na wengine waliokuwa mawindoni usiku;maisha yake yalikuwa yamekingwa sana kiasi kwamba alikuwa haifahamu hiyo hatari.

  Huku nyuma katika Kasri kuotoroka kwake kuligundulika. Jengo lote lilisachiwa,majengo yaliyozunguka,viwanjani. Mfalme alihangaika huku na huko anatoa amri,watu wenye silaha walikaa tayari. Halafu kila mtu akaenda kulala kusubiri alfajiri ambapo msako ungeweza kuanza. Katika majengo ya wanawake kulikuwa na kilio na huzuni kwa ajili ya ghadhabu ya mfalme.

  Gautama aliendelea kutembea msituni,akijitahidi kukwepa kukutana na watu kila ilipowezekana,na kukaa kimya anapoulizwa swali wakati haikuwezekana.Alichukua chakula kutoka katika vyakula vilivyopandwa,alichukua nafaka na matunda,akanywa maji kutoka katika visima vya maji safi,baridi. Lakini hadithi ya msafiri wa ajabu ambaye mwenendo wake ulikuwa siyo sawa na wasafiri wengine ,hatimaye ikafika kwenye Kasri. Watu wa mfalme wakafanya msako kwa nguvu kubwa,lakini hawakumpata mtoro,kwa vile kila mara alikuwa anajificha kwenye vichaka ambapo farasi walikuwa hawawezi kupita.


  Hatimaye mfalme akatoa agizo wanawake wote wacheza dansi wapelekwe porini,na wamfuate Gautama na wajaribu kumshawishi arudi. Kwa siku nyingi wakajipenyeza kila pahali katika msitu , kwenye maeneo yaliyo wazi kidogo katika msitu,mahali ambapo Gautama anaweza kuwaona na wakacheza dansi zao za kumshawishi. Halafu,walipofika karibu na mpaka wa Ufalme wa baba yake,Gautama akasema kwamba anakwenda nje katika dunia kutafuta mambo ya kiroho,na hatarudi. Mke wake akamfuata,na mtoto mikononi mwake,lakini Gautama hakumsiliza maombi yake,ila akageuka na kuendelea na safari yake.

  Yule mwalimu wa Kihindi alipofika hapa katika hii hadithi,ambayo tulikuwa tunaifahamu kama yeye alivyokuwa anaifahamu akasema,''Kutoka kwenye Dini iliyofilisika ya Kihindi,Imani mpya ilianzishwa wakati ule,Imani ambayo ingeleta faraja na matumaini kwa wengi. Kwa asubuhi hii tutamalizia hapa. Leo mchana tutaedelea.. Dismiss''
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  May all beings attain enlightenment.
   
 3. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #3
  Dec 1, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  ''May all beings attain enlightenment'',hiyo ni sala ya Mahayana Buddhsim.
  Lakini mafundisho haya,hilo somo hapo juu,ni Hinayana Buddhism,ambayo lengo lake siyo kuokoa watu wengine,ila ni kujiokoa mwenyewe. Na haya ni mafundisho ya historical Buddha,yaani Hinayana.
  Mafundisho ya Mahayana yanakuja baadaye,miaka mingi baada ya kifo cha Buddha.
   
Loading...