Hadithi ya babu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hadithi ya babu

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Bushbaby, Jul 6, 2011.

 1. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Siku moja babu aliniita katika kibanda chake na kuanza kunisimulia hadithi moja. Alianza kama hivi..........

  “Hapo zamani za kale, hapa ulimwenguni waliishi viumbe wanne nao ni Punda, Mbwa, Bata na Mwanadamu. Siku moja Mungu aliwaita viumbe hawa na kuwaambia kuwa alikuwa ameamua kuwaongezea umri wa kuishi upatao miaka 20 kila mmoja. Kabla ya kuthibitisha hilo aliwauliza kama wamekubali....

  Alianza Punda kunyoosha mkono Mungu akamuuliza ana tatizo gani, punda akajibu “Mungu, mwanadamu ananifanyisha kazi ngumu sana hiyo miaka 20 unayotaka kuniongezea ni sawa na kuniongezea matatizo na mateso makubwa zaidi tafadhali miaka mitano pekee inanitosha sana“ Mungu hakutaka kubishana na Punda bali alimuuliza kuwa hiyo miaka 15 inayobaki apewe nani ndipo mwanadamu aliponyoosha mkono na kudai apewe yeye Mungu akakubali na kumpa mwanadamu basi akawa amefikisha miaka 35 baada ya kuongeza na ile 20 ya kwake basi huu unaitwa UMRI WA PUNDA,maisha ya punda ni ya mateso sana, punda ni mfanyakazi anayejituma, Punda hachoki kamwe. Basi katika umri huu mwanadamu anatakiwa kujituma sana, huu ndio umri wa kutafuta kwa nguvu zote ni wakati ambao bado nguvu zipo tele mwilini.

  Mbwa naye akadai umri ule alioongezewa ni mkubwa sana kwani anakesha kila siku anamlinda mwanadamu,a nabweka sana, hivyo hata yeye alihitaji miaka mitano peke yake, Mungu alihoji kuwa nani apewe miaka hiyo kumi na tano iliyobaki,mwanadamu akanyoosha mkono na kudai apewe yeye basi Mungu akampatia miaka ile basi akawa amefikisha miaka hamsini (50), umri huu kuanzia mika 36 hadi 50 unaitwa UMRI WA MBWA, Katika umri huu mwanadamu anakuwa mtu wa kulinda kile alichokivuna wakati wa UMRI WA PUNDA mwanadamu hubwekea wale ambao huitumia mali yake vibaya, kama hukuvuna mali yoyote hautakuwa na cha kulinda wala kubwekea.

  Bata naye kama wenzake aliomba pia kupunguziwa umri na kupewa miaka mitano pekee,mwanadamu kwa mara nyingine alichukua miaka 15 aliyoikataa bata,akafikisha jumla ya miaka 65 basi umri kuanzia umri wa miaka 50 hadi 65 ni UMRI WA BATA.Maisha ya bata ni ya hovyo hovyo hajitumi ndio maana anakula matope na kuharisha popote pale na wakati wowote,katika umri huu mwanadamu hana nguvu tena za kutafuta mali,hana akili ya kujipanga huu ni wakati wa kuhudumiwa na ndugu zake ambao watakuwa wakitumia mali alizoziacha. Kama hukuvuna na wala hukulinda basi utaishia kuwa ombaomba na kufa kabla ya wakati.

  Babu alimaliza kwa kusema kama ulishindwa kujituma katika umri wa Punda basi jiongezee miaka mitatu mbele yaani miaka 38,tofauti na hapo kamwe hauwezi kufanya lolote katika umri wa miaka 40 na kuendelea labda uwe Mwizi. Basi ni hadithi hii hunipa hamasa ya kufanya kazi kwa bidii huku mateso yakiongezeka mimi naamini kuwa kwa sasa mimi ni Punda sina haja ya kulalamika eti nateseka au maisha magumu.
   
 2. pirate

  pirate JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 367
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 60
  Mmmmh..,kweli.!
   
 3. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Nilipita tu...
   
 4. B

  Babu mchumi Member

  #4
  Jul 6, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Umenena vema!
   
 5. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Modified
   
 6. pomo

  pomo JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 265
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  acha ku burn vya wenzio, try to think big
   
 7. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  similar story kama niliisikia mahali vile
   
 8. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Story tamu na inaukweli sana. Big up.
   
Loading...