Chilojnr
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 308
- 1,354
NYEMO CHILONGANI.
UCHAWI WA BILIONEA BAZOKA.
0718069269
Ndiyo kwanza mwanga wa asubuhi ulikuwa ukitokeza, watu waliokuwa wakifanya kazi sehemu za mbali, wakaamka na kuanza kujiandaa kwenda makazini, kwa wale waliokuwa njiani kuelekea makazini kwao, wakaongeza kasi ili kuwahi na kuanza kazi.
Wabeba mizigo waliokuwa wakifanya kazi katika masoko makubwa kama Kariakoo, Tandale na Buguruni tayari walianza kazi zao mapema kabisa, siku hiyo ilionekana kama siku nyingine na hivyo walitakiwa kufanya kazi kwa bidii.
Katika muda huohuo, kijana aliyekuwa akiishi maisha ya chini katika Mtaa wa Kwa Ally Maua, Emmanuel Bazoka ndiyo kwanza alikuwa akiamka katika usingizi mzito. Alionekana kuchoka mno, pale kitandani alipokuwa, hakutaka kuteremka, aliyafumbua macho yake na kuangalia huku na kule kama mtu aliyekuwa akimtafuta mtu fulani ndani ya chumba hicho.
Joto likaanza kumsumbua, jua lililokuwa limechomoza liliambatana na joto kali. Akashuka kutoka kitandani na kukaa sakafuni, kichwa chake kikaanza kufikiria mambo mengi, maisha aliyokuwa akipitia ambayo yalimfanya kuwa hapo siku hiyo.
Alikuwa kijana msomi kidogo aliyeishia kidato cha nne, alikuwa na cheti chake ambacho kwa kipindi hicho hakuona kama kilikuwa na kazi yoyote ile. Maisha aliyokuwa akiishi, yalikuwa ya kimasikini mno.
Hakuwa mtu wa kula milo mitatu kwa siku, kila siku alikuwa akila asubuhi na usiku kisha kulala. Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake, yalimuumiza lakini hakuwa na jinsi, ili aendelee kuishi ilikuwa ni lazima afanye kazi ndogondogo alizokuwa akizifanya.
Maisha yake yalichakaa, kila siku alimuomba Mungu kuondoka katika maisha aliyokuwa akiishi lakini ilishindikana kabisa. Aliendelea kuishi hivyohivyo na kila siku asubuhi aliondoka nyumbani kwake kuelekea katika Soko Kuu la Tandale na kubeba mizigo.
Siku hiyo hakujisikia kwenda kufanya kazi, alitamani kuendelea kulala lakini alipokumbuka kwamba kama asingetoka basi asingeweza kula, hakuwa na jinsi, akainuka na kuelekea nje, akachukua maji, akaenda kuoga na kujiandaa kwenda kazini kwake.
Maisha yake yalikuwa ya mateso sana, hakuwa na mke, hakuwa na mchumba wala mtu yeyote yule. Wazazi wake walikuwa masikini kama yeye, hawakuwepo tena duniani, walifariki miaka miwili iliyopita, katika mwaka ambao alikuwa akimaliza kidato cha nne.
Alifeli. Kufeli kwake hakukumaanisha kwamba hakuwa na akili, hapana, alikuwa na uwezo mkubwa ila msongo wa mawazo juu ya vifo vya wazazi wake vilimfanya kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yake.
Aliuchukia umasikini, katika maisha yake alipanga kuwa tajiri mkubwa hapo baadaye. Hakujua angeanza vipi, hakujua ni sehemu gani ambayo angeanzia kuupata utajiri ambao kila siku alikuwa akiufikiria kichwani mwake.
Hakutaka kuiba, aliamini kwamba kama angeendelea kupambana basi kuna siku angekuwa tajiri mkubwa na kufanikiwa kuiteka Tanzania kwa kuwa na mali nyingi.
“Kuna siku nitakuwa tajiri! Labda tajiri mkubwa kama Bakhresa,” alijisemea huku akivaa nguo zake na kuondoka.
Ni kama aliishi ndani ya ndoto kubwa iliyomfanya kuona kuna siku angekuwa tajiri mkubwa, hakujua kama ndoto hiyo aliyokuwa akiiota kila siku ingekuja kuwa kweli au alikuwa akipoteza muda wake.
Siku hiyo, akaelekea kazini kama kawaida, aliungana na wenzake na kuanza kubeba mizigo kama siku nyingine. Sokoni huko, alikuwa na rafiki yake aliyekuwa akipenda sana kufanya naye kazi, huyo aliitwa Hamisi Kibwila.
Huyo ndiye aliyekuwa akishirikiana naye kwenye kila kitu, ndiye ambaye alimwambia mambo mengi kuhusu maisha yake, ndiye ambaye alizijua siri za Bazoka kwamba leo alikula au alilala bila kula.
“Kuna siku naamini nitakuwa tajiri mkubwa,” alisema Bazoka huku akimwangalia rafiki yake huyo ambaye kabla ya kusema kitu chochote, akamwangalia, tabasamu la mbali likautawala uso wake.
Si kwamba alipingana na alichokuwa akikizungumza rafiki yake, alikubaliana nacho ila kilichokuwa kikimuumiza ni aina ya maisha waliyokuwa wakiishi.
Waliishi kwa shida, ili wale, walitakiwa kufanya kazi kwa nguvu sana, hawakuona dalili zozote za kuweza kufanikiwa kutoka katika maisha waliyokuwanayo, kwao, walijiona kuwa masikini milele, walijiona kufanya kazi ya kubeba mizigo milele, ilikuwaje Bazoka aseme kwamba kuna siku angekuwa tajiri? Jambo hilo halikuweza kukubalika kichwani mwa Hamisi hata kidogo.
“Wewe uwe tajiri?” aliuliza Hamisi huku akimwangalia rafiki yake huyo.
“Ndiyo! Unadhani inashindikana?” aliuliza Bazoka huku akimwangalia Hamisi.
“Si kwamba inashikana!”
“Kumbe?”
“Kwa Maisha haya ya kubeba mizigo unataka kuniaminisha kwamba kuna siku utakuwa bilionea! Utaanzia wapi Bazoka? Kuna wengine kama sisi, Mungu aliandika kwamba tutakuwa wabeba mizigo mpaka vifo vyetu, na hivi ndivyo inavyotokea,” alisema Hamisi, tabasamu lile likapotea, akaamua kulikalia gunia lililokuwa na mchele.
Bazoka alimwangalia kwa macho yaliyoonekana kutokukubaliana na kile alichokisema, kwake, alitamani kuwa bilionea mkubwa, alijua kabisa kwamba kuna siku maisha yangebadilika na kuendesha magari, kumiliki majumba ya kifahari na hata kusafiri huku na kule kama bilionea.
Walizungumza mambo mengi mpaka baadaye alipoamua kuendelea kufanya kazi zake. Kila siku ilikuwa ni mawazo tu, aliupenda utajiri, alikuwa tayari kufanya kitu chochote kile lakini mwisho wa siku awe tajiri mkubwa.
Katika nyumba aliyokuwa akiishi, aliishi na wapangaji wengine na mwenye nyumba aliyeitwa mzee Ramadhani Kibidu ambaye alikuwa na watoto wawili wa kike, Asha na Amina.
Asha ndiye alikuwa binti mkubwa wa mzee huyo. Alikuwa msichana mweupe, mrefu, mwembamba ambaye uso wake ulipendezeshwa na vishimo viwili maishavuni mwake.
Japokuwa alikuwa na uzuri wa ajabu na kupendwa na wanaume wengi, kwa Asha hakuwa akijali kuhusu mahusiano ya kimapenzi. Moyo wake ulikuwa umejeruhiwa baada ya kuacha na mwanaume aliyekuwa akimpenda sana.
Baada ya kuachana naye kwa takribani miaka miwili iliyopita, hakutaka kuwa na mwanaume mwingine yeyote yule. Aliamua kubaki peke yake mpaka kipindi ambacho Bazoka alihamia ndani ya nyumba hiyo.
Alikuwa kijana masikini ambaye katika kipindi cha kodi ilikuwa ni lazima kugombana na baba yake lakini huyohuyo masikini Asha alikuwa akimpenda kweli. Kila alipomwangalia Bazoka, moyo wake ulifarijika na kuona kabisa kwamba huyo ndiye mwanaume ambaye alitakiwa kuwa naye katika kipndi chote cha maisha yake.
Wakati akimpenda Bazoka, mwenzake hakuwa na habari naye, alikuwa bize na mambo yake, alikuwa akiyaangalia maisha yake yaliyokuwa yakimuendesha mno. Hakuwa na pesa, wakati mwingine Asha ndiye aliyekuwa akimpelekea chakula na kula.
Kwa Bazoka, alikuwa akijishtukia lakini hakuwa na jinsi, alichukulia kama urafiki tu kwa kuwa alikuwa mpangaji kumbe mwenzake kichwani alikuwa akifikiria mambo mengne kabisa.
Asha aliogopa kumwambia Bazoka ukweli, aliona kabisa kwamba asingekuja kukubaliwa kwa kuwa tu kijana huyo alikuwa masikini na hakuona kama angeweza kuishi na msichana huyo.
Ila hakuacha, kwake, mwanaume huyo alikuwa kila kitu katika maisha yake. Wakati mwingine alikuwa akitoka chumbani kwake usiku na kwenda katika chumba cha Bazoka na kuangalia televisheni ndogo iliyokuwa humo ndani. Bazoka hakuwa na mawazo na Asha, alimchukulia kama dada yake kitu ambacho hakikukubalika kichwani mwa msichana huyo.
Kila alipokuwa akikaa chumbani kwa Bazoka, hakuonyesha kitu chochote kile, alionekana kama gogo ambalo halikuwa na hisia zozote zile. Hilo lilimuumiza sana Asha kiasi kwamba akafikia hatua ya kumwambia ukweli.
“Bazoka..” alimuita kijana huyo.
“Naam.”
“Mbona unanitesa hivyo?” aliuliza msichana huyo kwa sauti ya chini huku uso wake ukianza kuingiwa na aibu.
“Nakutesa? Unamaanisha nini?” aliuliza Bazoka.
“Huoni kama unanitesa? Ninakupenda sana, nimejaribu kukuonyeshea kila kitu lakini naona mwenzangu huelekei kabisa,” alisema Asha kwa sauti ile ile ya chini.
Bazoka hakuzungumza kitu, alibaki akimwangalia Asha. Msichana huyo aliona haitoshi, akasimama na kumsogelea Bazoka pale alipokaa na kukaa karibu naye.
Huo ulikuwa wakati wake wa kulalamika, alimwambia jinsi alivyokuwa akijisikia kwamba kwake hakuwa akipindua, wakati akilalamika hayo yote Bazoka alikuwa kimya tu akimsikiliza.
Kichwa chake kilikuwa na mawazo tele, alishangaa, hakujua sababu iliyomfanya msichana huyo kumpenda namna hiyo na wakati hakuwa na kitu chochote kile, hakuwa na maisha mazuri, aliishi kwa kuungaunga kama masikini wengine, kama angeamua kuwa na Asha, angempa nini?
“Asha! Hivi upo siriazi kweli au unanitania?” alimuuliza msichana huyo.
“Bazoka! Ninakupenda kwa moyo wa dhati.”
“Na maisha haya?”
“Ndiyo! Ninakupenda, naomba unikubalie, naomba uupoze moyo wangu, unateseka na hakuna mtu ambaye atanipa tulizo la moyo zaidi yako,” alisema Asha huku akimwangalia Bazoka kwa macho yaliyoonyesha kumaanisha kile alichokizungumza.
Je, nini kitaendelea?