Hadithi tamu - ahadi ya ndotoni

Me370

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
985
293
Hii inabidi nitoe full credit kwa GPL ila mi nimeisoma nkaona sio mbaya nikishare.

Ahadi ya Ndotoni

AHADI YA NDOTONI



Jeska alitembea kwa mwendo wa taratibu akiwa amepoteza muelekeo wa maisha yake, alijiona ni kiumbe asiye na thamani. Pamoja na uzuri aliojaaliwa na Muumba, bado alikuwa kiumbe chenye mikosi. Hakuamini uzuri aliojaaliwa na Mungu amekuwa kiumbe wa kuchezewa na wanaume.

Wazo lake lote lilikuwa kujiua ili kujiepusha na walimwengu ambao wamekuwa hawaoneshi ushirikiano naye. Alikuwa ameisha kaa na wanaume zaidi sita ambao wote walimuahidi kumuoa, lakini mwisho wa siku ilikuwa kutendwa na kushindwa kuelewa tatizo ni nini.

Katika mitihani ya maisha Jeska amejikuta akibakwa kila alipokuwa akijaribu kutoka ili kutuliza mawazo, mara ya mwisho alibakwa na wanaume zaidi ya sita ambao hawakutumia kinga. Kwa hali ile aliamini anaweza kuwa ameambukizwa virusi vya ukimwi.

Kupima aliogopa kwani aliamini angekufa kwa presha, kimuonekano alijikatia tamaa akawa si mtu wa kujiheshimu tena. Mawazoni mwake alijua huenda Mungu alimuumba ili aje amtese, tokea ajali mbaya ya moto iliyochukua uhai wa wazazi wake wote pamoja na ndugu zake akiwa na umri wa miaka saba.

Baada ya vifo vya wazazi wake waliofia ndani ya nyumba, Jeska alichukuliwa na ndugu wa baba yake na kumlea, huku wazazi wake wakiwa wamemuachia mali nyingi. Lakini kwa bahati mbaya walioachiwa kumlea walihodhi mali yote na mwisho wa siku alifukuzwa kama mbwa baada ya kuhoji mali za baba yake.

Tokea hapo Jeska alianza kuonja adha ya maisha, pamoja na kufukuzwa na ndugu wa baba yake na kutishiwa kuuawa kama atataka kujua mengi zaidi. Siku zote Mungu hamtupi mja wake aliangukia katika mikono ya wazazi wa shoga yake. Ambao walimchukua na kumuahidi kumsomesha mpaka mwisho wa elimu yake.

Jeska alishukuru Mungu na kuwaza kusomea sheria akifika chuo kikuu ili siku moja alirudishe mali iliyochuliwa na ndugu wa baba yake. Maisha kwake yalikuwa mazuri yaliyomfanya asahau mateso ya ndugu wa baba yake, aliweza kumaliza vizuri kidato cha nne kwa kupata matokeo mazuri na kumuwezesha kujiunga na kidato cha tano. Akiwa kidato cha tano huku umbile alilojaaliwa na Mungu likizidi kupendeza na kutamanisha wanaume wakwale.

Siku moja hakuamini aliposhtuka usingizini na kumkuta baba wa shoga yake aliyemuheshimu kama wazazi wake akiwa juu ya mwili wake akimbaka. Jeska aliumia sana na kulia kwa uchungu. Lakini baba wa shoga yake alimbembeleza na kumuomba aifiche siri ile yupo tayari kumfanyia chochote katika maisha yake hata kumnunulia gari.

Jeska hakutaka kuisambalatisha familia ile kwa kuogopa kumsema baba wa rafiki yake kwa mkewe, aliamua kufa na siri moyoni ambayo ilikuwa ikimla siku hadi siku hata kupoteza uwezo wake darasani. Kila alipomuona baba wa shoga yake moyo ulipasuka na kujikuta akikimbia chumbani kwake na kuanza kulia.

Aliona kama ni uonevu kwa upande wake, wazazi wake wote wamekufa kwa mpigo ndugu waliobaki kumlea wakidhurumu mali. Na mwisho wa siku mtu aliyemtegemea kuyaokoa maisha yake amegeuka kiumbe mbaya kumbaka bila ridhaa yake. Kitendo kile kilimla sana Jeska kiasi cha kupungua siku hadi siku huku akiwaweka wenyeji wake katika njia panda wasijue Jeska anaumwa nini.

Kila walipomuuliza aliishia kulia na kuamini kauli yake huenda ikawa bomu litakalo isambaratisha familia ile. Siku zote alimuomba Mungu ampe ujasiri ili weze kuyakabili majaribu yale, Edna shoga yake muda wote alikuwa karibu yake kumdadisi kutaka kujua shoga yake amekubwa na tatizo gani ambao linaweza kutafuliwa na familia yake.

Kila alipoulizwa alisema hana tatizo lolote bali hujikuta akikosa amani kufikilia jinsi wazazi wake walivyokufa ghafla kabla hawajamtengenezea mazingira ya kujitegemea. Mama Edna na Edna walimuweka chini na kumpa mifano mingi ambayo ni mitihani ya wanadamu, mama Edna alimueleza.

“Jeska mshukuru Mungu, usipige teke fadhira zake, ni bahati kupata sehemu salama kama hii. Ni wangapi wamefiwa na wazazi wao lakini leo hii wanahangaika na kuishiwa kubakwa na kuambukizwa ukimwi.”

Kauli ile ilimfanya Jeska aangue kilio na kuamini hata yeye katika mawazo yake aliamini walio ndani ni salama kuliko wanaozurula. Lakini akili yake ilibadilika na kuamini watu wachache wenye uwezo huwa na huruma ya mamba kukuchekea kumbe wanakutamani kukutafuna utakapoingia kwenye maji kama alivyofanya baba Edna.

Alijuliza ni wangapi wamo katika mikono inayoonekana salama kumbe kuna watu wenye roho ya mamba kuwatafuna watu huku machozi yakiwatoka, wakiamini wanawaonea huruma kumbe na furaha ya kutafuna minofu na kiumbe kisicho na hatia.

Kilio chake kilizidi kuwaweka njia pana na kuanza kumdadisi upya.
“Jeska mwanangu ni hili hili au kuna jingine, hebu tuweke wazi ili tutafute tatizo?”




Ilipoishia
Alijiuliza ni wangapi wamo katika mikono inayoonekana salama kumbe kuna watu wenye roho ya mamba kuwatafuna watu huku machozi yakiwatoka, wakiamini wanawaonea huruma kumbe wana furaha ya kutafuna minofu na kiumbe kisicho na hatia.

Kilio chake kilizidi kuwaweka njia panda na kuanza kumdadisi upya.
“Jeska mwanangu ni hili hili au kuna jingine, hebu tuweke wazi ili tutafute tatizo?”
Sasa endelea
“Hakuna mama.”
“Jeska.”

‘Abee mama.”
“Mimi ni nani yako?”
“Mama.”
“Sasa kwa nini huniambii ukweli?”

“Ukweli ni huo mama, nimewakumbuka wazazi wangu kwani hujisikia unyonge pale mwenzangu anapokuwa na wazazi wake wote.”
‘Umenyanyaswa?”
“Hapana”

“Sasa nini tatizo, Jeska wewe na Edna hamna tofauti katika familia hii. Wote ni watoto hakuna kitu alichopata Edna ukakosa wewe.”
“Ni kweli mama, basi nitajitahidi kurudia hali yangu ya zamani.”
Maswali yalipozidi Jeska ilibidi afunike kombe mwanaharamu apite.

***
Kwa kweli alijitahidi kujirudisha kwenye hali ya kawaida japo moyo wake kila kukicha ulikuwa ukisikitika na kukosa amani. Kila alipokuwa peke yake alijikuta akiwakumbuka wazazi wake. Kila alivyo yaangalia maisha ya shogaye Edna moyo ulimuuma kutokana na maelezo aliyopewa kupitia watu walioifahamu familia yake vizuri.

Walimuleza wazazi wake walikuwa watu wenye uwezo mkubwa sana tena waliompenda na kumpa kila kitu ambacho alikitaka, maneno yale yalimuumiza moyo wake.Alijiuliza nini chanzo hasa kilicho yachukua maisha ya wazazi wake wote kwa mpigo japo alijua ni ajali ya moto lakini chanzo chake hakujua, kama amri ya Mungu au mkono wa mtu. Lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kumuachia Mungu.

Aliamini kama wangekuwepo wazazi wake angesoma mpaka mwisho wa uwezo wake, alipenda asomee udaktari kwani toka akiwa o lavel alipenda sayansi. Lakini sehemu aliyoiona inamfaa imekuwa na sura mbili za wema na ukatili. Kama baba yake Edna angejua thamani ya maumivu ya yatima asingefanya unyama ule pia hata kama angejua yeye na mwanaye ni kitu kimoja asingemfanya vile.

Asingekuwa tayari kumuona mwanaye akibakwa angekuwa tayari kumfanyia kitu kibaya hata kumuua kwa risasi mtu aliyefanya hivyo. Alikumbuka maneno ya baba Edna siku moja wakiwa wamekaa sebuleni wakitazama runinga baada ya kuona msichana mmoja wa rika lao akiwa amebakwa ambapo alisema kwa ukali:
“Watu kama hawa ingekuwa amri yangu wangenyongwa hadharani kwa vile hawajui jinsi gani wazazi tunavyopoteza pesa kuwasomesha watoto wetu.”

Jeska alijikuta akitokwa machozi kila alipokumbuka kauli ya baba Edna na kitendo alicho mtendelea. Lakini alikumbuka kauli isemayo chozi la mnyonge hulipwa na Mungu. Kila moyo ulipomuuma alipiga magoti na kumuomba Mungu ampe farijiko kwa yote yaliyomkuta na yatakayomkuta na kuamini ni mitihani ya maisha kwani hakujua nini kitakachofuata katika maisha yake.

Moyo wa ujasiri ulimvaa kwa kuamini lililotokea lilikuwa limekwisha tokea halitaweza kufutika kwa machozi zaidi ya kupambana na tatizo ndipo ufumbuzi ungepatikana.

Taratibu hali yake ya zamani ilijirudia na kuweza kupambana na maisha hata afya yake nayo ilitengamaa. Hali ile ilirudisha furaha ndani ya nyumba, kila alipokutana na baba Jeska alimuomba msamaha kwa kumwambia:
“Nisamehe mwanangu, ni shetani alinipitia lakini natubu mbele yako sitarudia tena kitendo cha kinyama nilichokutendelea.”

Kauli ile kweli ilimfanya Jeska amsamehe baba Edna toka moyoni mwake na kuamini kukosea ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Na siku zote muungwana akikosa kuomba msamaha, Jeska alimhakikishia kwa mdomo wake kuwa amemsamehe toka moyoni.

Amani ndani ya nyumba ya mzee Ezekiel ilirudi kama zamani kwa familia kuwa moja hakuna aliyejua nini kilitokea ilibakia siri kati ya Jeska na baba Edna ambaye alimuahidi kumsomesha mpaka mwisho wa kikomo cha kusoma.

Jeska alimshukuru Mungu kwa kila jambo, aliamini hata jambo baya huwa lina makusudi yake. Maisha yaliendelea uwezo wa darasani ulioanza kupungua ulirudi tena kwa kasi mpya akitaka kukipata kile alichoahidiwa na baba Edna kusoma mpaka kikomo chake.


Sasa endelea...

Ndoto zake za kuwa daktari zilifutika na kuzihamishia kuwa mwanasheria mkubwa sana ambaye ataweza kuwasaidia wote waliodhulumiwa mali zao na ndugu wa mume wakiwemo yatima na wajane.

Kingine alichokifikiria ni kuanzisha NGO’S ya sheria atakayotoa huduma kwa bei ya chini hasa ikiwalenga wanyonge. Usongo aliokuwa nao na uchungu wa kudhulumiwa mali zake na kumfanya kuishi maisha ya kubahatisha kuishia kuangukia katika mikono ya wabakaji.

Mwezi wa tatu toka abakwe na baba Edna aligundua mabadiliko katika mwili wake, siku zake za hedhi hazikuonekana. Pia maumivu ya kichwa na mwili kuchoka vilimtia wasiwasi. Mabadiliko yale mama Edna aliyaona, wasiwasi wake mkubwa ulikuwa malaria.

Ilikuwa siku ambayo Jesca aliamka na kushindwa kwenda shule, kichefuchefu kilikuwa kikali sana kilichofanya atapike kila chakula alichokula asubuhi ile. Baada ya kuona dalili zote za malaria, alimpeleka hospitali, Jesca ambaye hakuwa anaelewa kilichokuwa kikiendelea, alipoulizwa na daktari alimueleza anavyojisikia.

Alichukuliwa vipimo vya malaria, majibu yalikuja hana marelia. Ilibidi kichukiliwe kipimo cha mkojo, ambacho kileleta majibu. Daktari hakutaka kumpa majibu wakiwa wote alimtoa nje Jesca ili ampe majibu mama yake.

Jesca hali ile ilimtisha japo anajua virusi vya ukimwi vinapimwa kwa damu, wasiwasi wake huenda ameathirika baada ya kubakwa na baba Edna.
Ndani daktari alimueleza majibu ya vipimo yanavyosema.
“Mama binti yako vipimo vinaonesha ni ujamzito.”
“Eeh!?” Mama Edna alishtuka kusikia vile.

“Ndiyo, binti yako anaujauzito wa miezi mitatu.”
“Mtumee, mtoto huyu!”
Mama Edna alishika mkono mdomoni na kujikuta akikumbuka miezi mitatu ya nyuma hali ya Jesca ndani ilibadilika na kuwaweka katika sifahamu. Aliamini kama Jesca amefikia hatua ya ufuska lazima atamuambukiza mwanaye Edna ambaye amekuwa naye karibu zaidi.

Wazo la kumfukuza lilikuwa gumu, kwa kuhofia jamii ingemtazama vibaya, alipanga akitoka pale amueleze mume wake, nini wafanye kutokana na tabia za chui za Jesca kujificha katika ngozi ya kondoo ya upole na ukimya.
Alitulia tuli huku akiwa amehama kimawazo na kushtuliwa na daktari.

“Mama nafikiri umenielewa?”
“Nimekulewa baba, asante.”
“Nafikiri hili swala si la kulitolea maamuzi mazito, kwani siku hizi mabinti zetu wamekuwa katika wakati mgumu kutokana na Mafataki. Wasiwasi wangu asiwe ameambukizwa ukimwi tu.”
“Mmh, hapo ndipo nachanganyikiwa.”

“Basi mama kakaeni naye chini muulizeni kwa utaratibu lazima mwenye ujauzito atamtaja. Kama kuna ushahidi mfungulieni mashtaka.”
“Nashukuru baba kwa ushauri wako.”
Mama Edna akiwa amechanganyikiwa kidogo, alitoka na kumpitia Jesca aliyekuwa hajui nini kilichokuwa kikiendelea ndani.
“Twende zetu.”

Jesca alinyanyuka na kumfuata mama yake aliyekuwa anatoka nje ya hospitali bila kuelewa nini kilichokuwa kikiendelea mule ndani.
Jioni ya siku ile baada ya kurudi baba Edna mkewe alimwita na kumueleza kilichotokea hospitali, Jesca alijisogeza kwa kujificha nyuma ya mlango ili asikie mama atamueleza nini baba na nini atakijibu juu ya kilichoelezwa hospitali.

“Za saa hizi mume wangu?”
’Nzuri, vipi za hospitali?”
‘Mmh, si nzuri,” kauli ile ilimshtua Jesca na moyo kuanza kwenda mbio na kujiuliza huenda wazo lake la kuathirika ni kweli. Mwili ulimtetemeka na kumuomba Mungu amuepushe na janga lile.

“Mbona unanitisha kuna habari gani?”
“Jesca ni mjamzito,” kauli ile ilimshtua Jesca na kushika kifuani kwa hofu huku akipiga ukelele wa chini.
“Mama yangu weee nimekwisha.”
“Eeh!?” Mzee Ezekiel alishtuka.

“Ndiyo, usishituke habari ndiyo hiyo, mtoto mbaya tunamuona mkimya kumbe ana mambo ya chini chini. Unafikiri atamfundisha nini Edna kama siyo kuwa malaya kama yeye.”
Maneno yale makali yalikuwa msumari wa moto kwenye moyo wa Jesca binti yatima asiye na kosa lolote ambaye ukimya wake ulikuwa umemponza sawa na mshumaa kuwaangazia wengine huku unateketea.


ENDELEA....

“Mke wangu taratibu, Jeska ni mtoto wetu kama Edna hivyo tumchukulie kama ni Edna amekosa na wala si mtu baki.”
“Hata angekuwa Edna nisingefurahia upuuzi huo?”
“Sifurahii na pia ningemkanya kama nitakavyo mkanya Edna, hatuwezi kuwabangua kwa vile Jeska sasa hivi ni binti yetu.Umeisha mueleza tatizo lake?”

“Bado, kwa vile nilikusubiri kwanza wewe kabla ya kumueleza mwenyewe, ili nijue tutalitatua vipi.”
“Basi kazi hiyo niachie mimi,” baba Edna aliuchukua mzigo ule kwa kuamini kabisa huenda muhusika ni yeye japo hakuwa na uhakika kamili.

Mzee Ezekiel alikubaliana na mkewe, kabla ya kubadili nguo alimtuma Edna amwite Jeska aliyekuwa nyuma ya mlango akilia kwa majuto ya ujauzito alioupata baada ya kubakwa na mzee Ezekiel. Edna alimkuta nyuma ya mlango akitokwa na machozi na macho kuvimba.
“Jeska vipi mbona kila siku umekuwa mtu wa majonzi ndugu yangu?” Edna alimuuliza kwa sauti ya huzuni.

“Basi tu, naona huu ni mwaka wangu,” Jeska alisema kwa sauti ya kilio huku machozi yakiendelea kumwagika.
“Jeska una nini tena jamani?”
“Nina imani naishi kimakosa.”
“Jeskaaa!!”

“Kila balaa linaniandama mimi, unafikiri kuna umuhimu wa kuendelea kuishi?”
“Jamani Jeska maneno gani hayo ya kusema ndugu yangu.”
“Sina mengine zaidi ya hayo, kilichobakia ni utekelezaji, likitokea usishangae ila ujumbe nitakuachia.”
“Mama yangu, Jeska unataka kufanya kitu gani Mungu wangu hebu muondoe pepo wa mauti kwenye moyo wa Jeska. Jeska usifanye hivyo hata siku moja bado una nafasi kubwa ya kuishi na kutatua matatizo yako”

“Edna, umri wangu ni mdogo lakini matatizo yanamzidi mtu aliyeishi miaka mia moja. Kama nitaendelea kuishi nafikiri kuna balaa kubwa zaidi”
“Kwani kuna nini tena Jeska”

“Ipo siku utajua”
“Basi baba anakuita naomba umueleze yanayokusumbua,” Edna naye machozi yalimtoka kwa hofu ya maamuzi mazito ya Jeska.
Jeska aliongozana na Edna mpaka sebuleni alipokuwa amekaa mzee Ezekiel, alishangaa kumuona Jeska akitokwa na machozi na macho yamemvimba.

“Jeska, una nini tena mama?”
“Basi tu baba.”
“Hebu njoo hapa binti yangu mpenzi.”
Jeska alisogea pembeni ya mzee Ezekiel, ambaye kabla ya kuzungumza naye alitoka naye nje na kwenda naye kwenye bustani. Walipofika alimuuliza kwa sauti ya upole.

“Jeska una tatizo gani?”
“Mama ameisha kwambia?”
“Una rafiki wa kiume?”
“Sina baba.”

“Una..na..taka kuniambia au una uhakika una mimba?” Mzee Ezekiel aliuliza kwa sauti ya kigugumizi.
“Mimi sijui mama ndiye aliyeambiwa majibu yangu.”
“Sasa unalia nini wakati hujajua kama una ujauzito?”
“Si mama kakwambia na hali yangu ilikuwa na kila dalili za ujauzito.”

“Mmh, unaweza kuwa wa nani?”
“Sijawahi kukutana na mwanaume hivi karibuni zaidi yako.”
“Kabla yangu umepita muda gani?”
“Mwaka wa tatu sasa.”

“Mmh, makubwa, unataka kuniambia ujauzito ni wa kwangu?”
“Labda wewe unaweza kumjua mtu mwingine zaidi yako au wa roho mtakatifu.”
“Mama yako ameisha kuuliza ujauzito wa nani?”
“Ataniuliza vipi, toka tumetoka hospitali hana habari na mimi.”

“Sasa sikiliza, nitafanya mipango kuitoa hiyo mimba ili uendelee na masomo.”
“Sawa,” Jeska alikubali.
“Akikuuliza mama yako mweleze ni ya kijana mmoja kondakta wa daladala.”
“Sawa baba.”

“Ila kesho nina safari ya kikazi kwa wiki nzima nikirudi tutaitoa, ila naomba iwe siri yako”
“Sawa baba.”
“Shika hii pesa itakusaidia kwa vitu vya hamu,” alimpa laki moja.
“Asante baba.”

Baada ya makubaliano walirudi ndani, sebuleni alikuwa Edna na mama yake. Jeska alipitiliza chumbani kwake kulala, hakuwa na hamu na kitu chochote kwa siku ile.


SASA ENDELEA....

Mzee Ezekiel na mkewe walikubaliana Jeska asiguswe kwa lolote bali apate msaada kama sehemu ya familia.
Baada ya makubalino yale, Edna alimueleza mama yake uamuzi mzito aliotaka kuuchukua. Mama Edna alishtushwa na habari zile, alimfuata Jeska aliyekuwa chumbani amejilaza akilia.

“Jeska...Jeska mwanangu amka mama.”
Jeska alinyanyuka huku macho yakiwa yamemvimba kwa kulia, mama Edna alishtuka na kuamini uamuzi mbaya wa Jeska yeye ndiye muhusika kwani alionesha kumtenga toka walipotoka hospitali bila kumpa majibu muhusika.

Mama Edna alishtuka hali aliyomkutanayo Jeska ilimshtua sana.
“Jeska mwanangu mbona hivyo mama?”
“Hapana kawaida?”
“Unaumwa?”
“Hapana.”
“Sasa nini?”
“Kawaida tu mama.”

“Hapana Jeska mwanangu najua jinsi gani nilivyokukosea.”
“Hujanikosea mama.”
“Si kweli Jeska, nakiri kufanya kosa, kwanza naomba unisamehe kwa yote yaliyotokea.”
“Mama hujafanya kosa lolote.”

“Ni vigumu kuliweka wazi lililokusibu moyoni mwako, naweza kusema baada ya kutoka hospitali mimi kama mzazi nilijikuta nachanganyikiwa na kushindwa kuamini nilichoambiwa hospitali na jinsi nilivyokuwa nakuamini.”
“Ni kweli mama, mimi ndiye mkosefu kwa tukio lililotokea wa kuomba msamaha ni mimi.”

“Hapana Jeska, napenda kukueleza kitu kimoja, sisi ni wazazi na wajibu wetu ni kuwatunza ninyi. Hivyo lazima tukasirike mnapokosea kuonesha jinsi gani tusivyokubaliana na yaliyotokea. Lakini mwisho wa yote ni kukusamehe kwa vile imeisha tokea.”

“Sawa mama nimekusikia, lakini nimeisha yatia doa maisha yangu.”
“Hapana Jeska, kukosea ni sehemu ya kujifunza. La muhimu ni kumtafuta huyo mwenye mzigo huo ili tujue nini majaliwa baada ya mtoto. Ila malezi yako na hali yako bado itabakia mikononi mwetu.”
“Sawa mama.”

“Nani mwenye mzigo huu?”
“Konda wa daladala”
“Mmh, haya...yupo wapi?”
“Siku hizi simuoni wala hajui kama siku tulipokutana aliniachia ujauzito huu.”
“Umekutana mara ngapi.”

“Mara moja ilitokea kama ajali, yaani najuta,” Jeska alisema kwa sauti ya kilio ambayo ilionesha kweli anajua. Lakini alifunika kombe mwana haramu apite.
“Sawa, basi tuliza mawazo tutailea mimba na mtoto akizaliwa vile vile tutamlea na ukijifungua tutaendelea kukusomesha.”
“Nitashukuru mama.”

“Basi mama naomba usilie na kujiona umefanya kosa kubwa, la muhimu ni kujifunza kutokana na makosa. Usifanye chochote kibaya cha kujizuru, sawa mama.”
“Sawa, nitafanya hivyo mama yangu.”
“Basi twende ukale.”

“Sijisikii kula mama.”
“Hapana nyanyuka mwanangu mzuri.” Mama Edna alimbembeleza Jeska huku alimshika mkono na kunyanyua, Jeska naye hakutaka kumbishia mama yake alinyanyuka na kutoka naye nje.

* * *
Siku zilikatika huku Jeska akiendelea kumeza mfupa wa siri nzito juu ya ujauzito aliopewa na baba Edna. Alijitahidi kuzuia hali yake kila akiwa shuleni ili wasimgundue kama mjamzito kutokana na kusinzia kila wakati na kichefuchefu.

Siku ya nne toka ingundulike mimba ya Jeska, maswali ya wanafunzi wenzake juu ya hali yake yalimnyima raha wapo waliodiliki kumwambia.
“Jeska tuna wasiwasi huenda wewe ni mjamzito.”
Maneno yale yalimchanganya na kumnyima raha, alijikuta akiona siku haziendi muda alioelezwa na baba Edna amsubiri unachelewa. Wazo la haraka lililoingia kichwani mwake , kwenda kuitoa ile mimba kwa vile pesa za kutolea alikuwa nazo.

Jeska baada ya maneno ya chini chini ya kumfikiria mjamzito, alipanga siku ya pili wakati wa mapumziko atoroke kwenda kutoa ujauzito. Siri ili ilibakia moyoni mwake kwa kuogopa kuwashirikisha watu wengine.


SASA ENDELEA..
***
Usiku ulikuwa mgumu kwa Jeska alifikiria mengi katika maisha yake, aliamini mkosi ndiyo uliokuwa sehemu kubwa ya maisha yake. Familia yake ilifariki akiwa hajui lolote, mali aliyoachiwa na wazazi wake nayo ndugu wa baba yake waliihodhi yote na mwisho walimfukuza huku wakimtishia kumuua.

Hata aliyeonekana mwokozi wake, mwisho kumbaka na kibaya kampatia ujauzito. Shuleni nako maneno ya chini chini yaliishaanza juu ya hali yake ambayo wazoefu walianza kujua ni ujauzito. Wasi wasi wake ulikuwa mwisho kuchukuliwa na kupelekwa kupimwa.

Aliamini kama angepelekwa kupimwa na kugundulika mjamzito na kusimamishwa shule. Kitendo kile kingemuathiri kisaikolojia hata shule ingemshinda kusoma baada ya kujifungua.
Aliona kumsubiri mzee Ezekiel baba yake Edna ni kuongeza tatizo juu ya tatizo.

Msimamo ulikuwa ule ule siku ya pili baada ya mapumziko atoroke na kwenda kutoa ujauzito. Kutokana na taarifa za juu juu utoaji wa mimba changa hauchukui muda mrefu, mtu wa mfano ilikuwa kwa msichana Fatuma aliyejulikana mjamzito lakini alitoa mimba siku moja na siku ya pili alikuja shuleni kama kawaida.

Usingizi ulimchukua usiku wa manane, hata alfajiri alipoamka bado kichwa kilikuwa kizito kwa kuchelewa kulala. Siku hiyo alionekana mtu mwenye mawazo mengi japo alijitahidi kuchangamka, lakini kuna muda hujisahau na kurudia mawazo yake.

Baada ya kuamka na kujiandaa na shule, Edna aliiona ile hali alijitahidi kumchangamsha shoga yake.
“Jeska vipi mbona unanitia ukiwa, si kila kitu kimekubaliwa hata kama baba wa mtoto humjui lakini wazazi si wamejitolea kukulea wewe na mtoto wako hata elimu wamesema watampa?”

“Ni kweli, lakini ujauzito huu umenivurugia kila kitu katika maisha yangu.”
“Lakini Jeska ni wewe ulikuwa mstari wa mbele kunishauri juu ya kujikinga na mapenzi kipindi hiki cha masomo au ndiyo kinyozi hajinyoi.”

Kauli ile ilimfanya Jeska atokwe na machozi huku akiamini kabisa Edna angejua kilichomsababishia kuwa katika hali ile asingesema yale. Machozi ya Jeska yalimtisha Edna na kujutia kauli yake.
“Basi samahani kwa kauli yangu sina nia mbaya kwako, naomba unisamehe sana.”

“Edna, najua hujui na ukijua utanionea huruma na kuamini kauli yangu ya kukatisha maisha yangu ungeiunga mkono.”
“Nisijue nini wakati mama alinieleza kila kitu.”

“Edna wewe na mama yako hamjui kitu, nitaumeza mfupa huu mpaka hapo Mungu atakapochukua maisha yangu.”
“Jeska, kuna nini mbona unanitisha au umeathirika?”

“Mara mia moja ningeathirika ningeshangilia kwa vile siku hizi watu wanatumia dawa ya kupunguza makali na kufuata ushauri na kuishi maisha marefu kuliko hata wasio athirika.”

“Jeska shoga yangu kuna siri gani tena ambayo hutaki niijue? Kumbuka wewe ni zaidi ya ndugu maisha yetu tumekuwa tunashirikiana kwa kila kitu. Kwa nini leo unanificha siri ambayo nina uwezo hata kuwashawishi wazazi wangu kuitatua kama mimi itanishinda.”

“Edna, nina imani ukijua ukweli ninaweza kukuharibia mudi yako ya masomo.”
“Kuhusu nini?”
‘Ujauzito huu.”

“Kwani una nini?”
“Kumjua mwenyewe.”
“Mwenyewe, si konda au kuna mwingine?”
“Yupo, wala si konda ila mwenyewe alinieleza nimueleze mama kuwa ujauzito ni wa konda.”

“Jeskaaaa! U...una...taka kuniambia konda si mwenye ujauzito huu?”
“Ni kweli ila ipo siku mwenye ujauzito utamjua au usimjue kabisa, nina imani nikimtaja mbele yenu huenda nikautua mzigo lakini huenda nikamtwisha mwingine jambo ambalo sipendi litokee.”
 
Juu kuna 1-5
Sasa endelea na 6 Hadithi sio ndefu saaana ila nzuri.

Endelea...

Baada ya kufika alikutana na daktari ambaye walikubaliana kiasi cha pesa kwa ajili ya kazi ile. Jeska alipanda kitandani kwa ajili ya kutolewa mimba, daktari alianza mara moja kufanya kazi yake ya kumsaidia Ziraili mtoa roho kutoa roho ya kiumbe kisicho cha hatia.

Katika utoaji wa mimba mambo hayakwenda kama alivyozoea damu ilimtoka nyingi sana. Mganga alichanganyikiwa hali ya Jeska ilikuwa mbaya sana, cha kwanza kukifanya kilikuwa kufanya kazi ya ziada ya kuzuia damu ambayo ilitokana na makosa ya utoaji mimba.

Baada ya kufanikiwa kuzuia damu hali bado ilikuwa mbaya sana kutokana na kupoteza damu nyingi. Daktari alimuhamishia katika chumba kingine ili kumpumzisha akipata nguvu aende kwao. Dokta alifanya siri ikiwemo kumpelekea chakula cha kumpa nguvu, Jeska alikula kwa shida baada ya kula alimdunga sindano ya usingizi ili apumzike kwa muda kabla ya kiza kuingia ili aende kwao.

Majira ya saa mbili dokta alimtoa Jeska ambaye afya yake haikuwa nzuri alitembea kama mtu aliyelewa. Alimkodia gari hadi kwao na kumueleza dereva akiisha mshusha tu asisubiri kitu atimue zake kukwepa ushahidi. Jeska alipofikishwa kwao baada ya kuteremka kwenye gari, gari liliondoka bila kujua kama amefika salama. Jeska alitembea kizunguzungu kikiwa kikubwa sana hakuweza kufika mbali alianguka chini.

Wapita njia ndiyo waliomuona amelala chini pembeni ya geti la nyumba moja. Watu walimshangaa binti mwenye nguo za shule ambaye alionekana akitokwa na damu kwenye miguu hata siketi yake nayo ilikuwa imelowa damu. Kila mmoja alisema lake wengi waliamini huenda amebakwa.

Mmoja kati ya wale watu alimtambua Jeska na kuwaeleza yule ni msichana wa nyumba iliyokuwa mbele yao. Mmoja wa watu waliokuwa pale walikimbia kwenda kugonga mlango na kuwaita waliokuwa ndani. Wa kwanza kutoka alikuwa Edna, baada ya kupewa taarifa zile alikimbilia kwenye kundi la watu waliokuwa wamemzunguka Jeska aliyekuwa hajitambui.

Hata bila ya kumtambua vizuri nguo na viatu alijua ni Jeska, aliangua kilio kilichowashtua waliokuwa ndani. Mama Edna alifika kwenye tukio na kukuta Jeska amelala chini hajitambui damu zikimtoka chini kuonesha kuna kitu kibaya kafanyiwa.

Kwa haraka walimbeba juu juu na kuchukua gari mara moja alikimbizwa hospitali.
Alipofikisha uchunguzi wa haraka ulionesha alifanyiwa zoezi la utoaji mimba uliofanyika vibaya na kusababisha kutokwa na damu nyingi sana zilizosababisha kupoteza nguvu.

Ilifanyika huduma ya haraka kuyaokoa maisha ya Jeska kwa kuongezewa damu na kutibiwa majeraha aliyopata wakati wa kutoa mimba.
Mama Edna alitaka kujua kama zoezi alilofanya Jeska la utoaji wa mimba lilifanikiwa.
"Eti baba alifanikiwa kuitoa mimba?"

"Ndiyo mama, vipimo vinaonesha mimba imetoka."
"Mungu wangu mbona mtoto huyu ana mazito hivi, nilimuonya asiitoe japo baba yake hakumjua lakini sijui shetani gani aliyemvaa na kufanya mauaji ya kiumbe kisicho na hatia."
"Poleni sana."

"Hatujapoa baba na hospitali iliyofanya hivi lazima tuishitaki."
"Nafikiri kuna umuhimu wa kufanya hivyo."

Daktari aliwaomba warudi nyumbani wakapumzike kwani hakukuwa na madhara zaidi waliamini damu atakayo ongezwa itamsaidia kumrudisha katika hali yake ya kawaida. Ila walishauriwa kumpima virusi vya Ukimwi kwa usalama zaidi wa afya yake.

Baada ya kutolewa wasiwasi mama Edna na Edna walirudi nyumbani huku wakizidi kumuombea dua ili atoke salama. Njiani Edna tukio la Jeska alilimsukasuka moyoni kiasi cha kumfanya akose raha, maneno ya Jeska kukanusha ujauzito ule siyo wa konda ina mtu ambaye hakutaka kumtaja ulimsumbua sana.
 
No 7

LIPOISHIA WIKI ILIYOPITA
Baada ya kutolewa wasiwasi mama Edna na Edna walirudi nyumbani huku wakizidi kumuombea dua ili atoke salama. Njiani Edna tukio la Jeska lilimsukasuka moyoni kiasi cha kumfanya akose raha, maneno ya Jeska kukanusha ujauzito ule siyo wa konda ila ni wa mtu ambaye hakutaka kumtaja ulimsumbua sana.

Aliamua kumueleza mama yake maneno ya Jeska kuhusiana na ujauzito ule, baada ya kukaa kimya alimwita mama yake ambaye naye alikuwa katika dimbwi la mawazo.
"Mama."
"Unasemaje Edna?"

"Unajua kuna vitu vinanichanganya."
"Vitu gani?"
"Kuhusiana na ujauzito wa Jeska."
"Kinakuchanganya nini?"

"Kuhusiana na mtu aliyempa ujauzito."
"Sasa nini kinakuchanganya?"
"Usiri wa mtu aliyempa ujauzito na inaoneka haikuwa ridhaa yake."
"Edna mbona mimi kaniambia kila kitu."

"Si kweli mama alikudanganya."
"Kanidanganya kipi?"
"Aliyempa mimba si konda?"
"Si konda! Kama si konda ni nani na kwa nini unasema si kwa ridhaa yake?"

"Mama Jeska anasiri nzito moyoni mwake, ameniambia kuwa ameamua kukudanganya kwa vile anakuheshimu sana."
"Sasa kama ananiheshimu kwa nini anidanganye?"
"Alinieleza kuwa umdhaniaye ndiye kumbe siye."

"Alikueleza maana ya usemi wake?"
"Alisema atanieleza siku moja kama kuna kitu kitashindikana na kama kikifanikiwa basi siri hiyo atakufa nayo moyoni mwake."

"Mmh, mbona mnanitisha, unataka kuniambia kuna mtu aliyempa ujauzito hataki tumjue?"
"Ndiyo, inavyoonekana na kitu alichokipanga kukifanya ni kutoa ujauzito kama sikosei, kwa vile umetoka siri itabakia moyoni mwake."

"Sasa unataka kuniambia ni nani aliyempa ujauzito kwa kukisia?"
"Mama, nimemuuliza maswali mengi ashakumu si matusi ilifikia hata kumuuliza ujauzito huo labda ni wa baba."
"Alijibu nini?"
"Alikataa."

‘Sasa mbona anatuchanganya?"
"Lakini mama naomba Jeska akitoka hospitali kaa naye na kumuuliza kwa kituo atakueleza siri iliyomoyoni mwake juu ya ujauzito kuna mengi inaonekana yamejificha."

"Mmh, haya."
Walipofika nyumbani walioga na kula chakula cha usiku ambacho hawakuwahi kula kutokana na taarifa ya kushtusha ya Jeska.

***
Jeska alizinduka hospitali majira ya saa saba usiku na kukupepesa macho yake, jicho lake lilitua kwenye chupa ya damu iliyokuwa imebakia robo kumalizika. Alivuta kumbukumbu na kukumbuka alikwenda kutoa mimba lakini tokea hapo hakukumbuka vizuri kama alitokewa na nini.

Alijiuliza pale ndipo hospitali aliyokwenda kutoa mimba au wapi, lakini taratibu alikumbuka kutokwa na damu nyingi wakati wa utoaji wa mimba kiasi cha kuhamishwa chumba kingine. Pia alikumbuka kama alipandishwa kwenye gari kwenda nyumbani lakini zaidi ya hapo hakukumbuka kitu chochote.

Mazingira ya hospitali yalimchanganya yalikuwa masafi tofauti na kule alipolazwa baada ya kutolewa mimba, kilikuwa chumba kama cha kawaida lakini pale palionekana hospitali ya ukweli. Akiwa katika kutafakari macho ametizama juu, daktari aliingia na kukuta Jeska karudiwa na fahamu. Alimsogelea hadi kitandani na kumsemesha.
"Jeska," alimwita.

"Abee."
"Pole sana."
"Asante," alijibu kwa sauti ya chini.

"Unajisikiaje?"
"Bado."
"Tatizo bado nini?"

"Kizunguzungu na uchovu wa mwili."
"Ooh, pole sana, mh, tatizo kubwa ni nini?"
Swali lilikuwa gumu kwa Jeska kusema kilichosababisha kufanya vile, alibakia bubu akikapua macho. Daktari aligundua uzito wa swali lake, alimuuliza kwa kulifumbua zaidi.

"Nini kilichosababisha utoe mimba ikiwa wazazi wako walikuwa tayari kuitunza hiyo?"
"Nimeamua kuitoa kwa vile nataka kusoma."
"Kwani ungejifungua usingesoma?"

"Nina imani nisingesoma kwa vile nisingeweza kuwatumikia mabwana wawili mtoto na elimu."
"Ungejua hivyo usingejiingiza katika mapenzi ukiwa mwanafunzi."
"Najua utasema hivyo, si kila kosa likitokea linamhusu mtendaji."
"Una maana gani?"
 
No 8
Sasa endelea....

"Hii ni siri sitaki mtu aijue bali mtendaji aliyetenda kwa tamaa za mwili wake na matokeo yake kunivurugia malengo yangu ya maisha"
"Unataka kuniambia umebakwa?"
"Sina jibu sahihi kwa vile nimekutwa na ngozi lazima niwe mwizi wa ng'ombe."

Muda wote huo Jeska alizungumza huku akitokwa na machozi ya uchungu na kumfanya akumbuke mengi. Aliendelea kuumia moyoni kwa kilio cha ndani kwa ndani. Kwa sauti ya chini iliyoambatana na kilio ambayo daktari aliisikia, Jeska alisema:

"Kama wazazi wangu wangekuwepo yote haya yasingetokea."
"Jeska mbona umekuwa mtu wa mafumbo na nahau, unataka kuniambia hasa waliokuleta si wazazi wako?"
"Nani aliyenileta?"
"Mrs Elezekiel na mama Edna"

"Anasema kanitoa wapi?"
"Amesema kakukuta umelala nje ya mlango wa kuingilia kwenu ukiwa hujitambui na kutokwa na damu iliyochafua sketi yako ya shule."
"Mmh, yule ni mama wa rafiki yangu Edna ndiyo walionichukua na kunilea, ni wazazi wangu kwa vile sina ninachokikosa zaidi ya upendo wa dhati wa wazazi wangu."

"Ooh, pole sana kwani wazazi wako walikufa kwa pamoja?"
"Ndiyo."
"Kwa ajali?"
"Ya moto."

"Na ndugu zako wote?"
"Ni mimi peke yangu ndiye niliyebakia."
"Ina maana wazazi wako hawana ndugu?"

"Heri ningekaa kwenye dimbwi la mamba wenye njaa kuliko hao ndugu wa baba, nina wasiwasi hata kifo cha wazazi wangu huenda wao wakahusika. Baada ya kifo cha wazazi wangu walinichukua lakini mwishoni walinifukuza kama mbwa na matokeo yake ni haya, kuna umuhimu wa kukatisha maisha yangu tabu hizi mpaka lini?"

Jeska alizungumza kwa uchungu mkubwa na kumfanya daktari amuonee huruma, lakini bado aliamini kuna kitu cha kumsaidia kutokana na matatizo yake.
"Jeska nina cha kukusaidia kwa matatizo yako yote?"
"Kivipi?"

"Kwanza kumtafuta aliyekubaka na pili kumjua aliyetaka kukutoa roho kwa kukutoa ujauzito ili sheria ichukue mkondo wake."
Jeska hakujibu haraka kutafakari aliyosema daktari, kabla ya kumjibu swali lake alimuuliza:

"Samahani dokta."
"Bila samahani."
"Eti mama anajua kama nilikuwa natoa mimba?"
"Ndiyo."
"Alisemaje?"

"Alilalamika kwa uamuzi wako wakati waliisha kueleza usiitoe."
"Mh!" Jeska aliguna na kuendelea kutafakari swali la daktari kumtaja aliyempa ujauzito.

Aliamini siri yake ni nguzo ya ndoa ya wazazi wa Edna na kuhusu kumtaja aliyemtoa ujauzito vile vile angekuwa amewaharibia wenzake ambao walitumia hospitali ile kutoa ujauzito kama yeye angeitaja na kukamatwa kwa muhusika lazima shoga zake watamuona hana maana hata kumtenga.

Aliamini bado siri yake ni muhimu kwa jambo lile la kutoitaja hospitali aliyotumia kutoa ujauzito. Baada ya ukimya wa muda Jeska alisema:

"Dakta najua unania nzuri na matatizo yangu, lakini mwenye utatuzi wa yaliyo mbele yangu ni yule aliye sababisha yote haya."
"Hapana Jeska, najua pengine una hofu kuwataja watu hao lakini nakuahidi kukulinda kwa kila kitu ambacho kitajitokeza hata kukuwekea wakili katika matatizo yako ikiwemo ya kudhulumiwa mali uliyoachiwa na wazazi wako."

"Nashukuru, nipe muda nitakueleza kila kitu."
"Leo huwezi?"
"Nimekueleza nitakueleza kila kitu naomba unielewe."
"Vizuri, basi kuna chakula unatakiwa kula."

"Siwezi niache nilale sijisikii labda asubuhi."
"Ngoja nikudunge sindano ili upunguze maumivu."
Daktari alimdunga sindano kisha alimwacha Jeska apumzike kwa vile usiku ulikuwa mkubwa. Baada ya daktari kuondoka hakuchukua muda mrefu naye usingizi ulimpitia.
 
No 9

Sasa endelea...

***
Majira ya saa nne Asubuhi mzee Ezekiel alikuwa wa kwanza kufika hospitali, alipofika alionana na daktari ambaye alimueleza ule si muda wa kuonana na wagonjwa. Lakini alijitetea sana.

"Sikiliza kijana naheshimu kila kitu ila nilikuwa sipo nimerudi asubuhi ya leo na leo mchana natakiwa kusafiri tena hivyo nilikuwa naomba msaada wa kuonana naye."

"Sawa mzee kwa muda mchache sana."
"Asante kijana wangu."
Mzee Ezekiel aliingia wodini kwenda kumuona Jeska aliyekuwa amejizala huku akitazama juu, sauti ya viatu ilimfanya Jeska ageuze shingo kuangalia aliyekuwa akiingia.

Alipomuona mzee Ezekiel alishtuka na kushika mikono kifuani, machozi yalianza kumtoka.
Mzee Ezekiel alimsogelea na kumpoza kwa sauti ya chini.
"Pole sana Jeska."
"A..a..sante."

"Kwa nini umefanya haraka wakati nilikueleza unisubiri?"
"Hali ilikuwa hairuhusu."
"Kivipi?"
"Wanafunzi wenzangu walianza kunishtukia."
"Si bora ungebaki nyumbani mpaka nikarudi."

"Wazo hilo sikuwa nalo."
"Ooh, pole sana."
"Asante."
‘Unaendeleaje?"
"Sijambo kidogo."

"Eti mama yako ulimwambia mimba si ya konda?"
"Ndiyo."
"Jeskaaa umefanya nini?"
"Sikuweza kuuweka uongo moyoni mwangu umenisumbua sana."
"Sasa umemueleza ukweli?"

"Sijamueleza lolote pamoja na kunibana."
"Sasa utamdanganya vipi naye tayari alikuwa amekubaliana na kauli yako?"
"Hata sijielewi kwa nini nimebadili kauli yangu ya mwanzo."

"Baada ya kukubana mmemalizana naye vipi?"
"Mmh, bado ila anasema nisipomtaja atajua ni wewe."
"Mimiii!?" Mzee Ezekiel alishtuka sana.
"Ndiyo."

"Mungu wangu, lakini kwa nini umebadili kauli yako ya awali ambayo aliikubali huoni unanitia mashakani?"
"Kuliko ulivyonitia."
"Si nimekueleza ni bahati mbaya shetani alinipitia."

"Sikuwa na njia moyo wangu unanituma niseme ukweli."
"Mmh," mzee Ezekiel alishusha pumzi ndefu.

Alitulia kwa muda kisha alisema kwa sauti ya chini yenye kusikika.
"Jeska naomba unisaidie jambo moja, nitakupa kiasi chochote cha fedha utakachotaka."
"Msaada gani huo?"

"Nataka nikutoroshe hapa hospitali na kwenda kukuficha sehemu ili mama yako akija asikukute."
"Ha! Baada ya kunitorosha?"
"Nitakuhudumia katika maisha yako yote ili tu mama Edna asiijue siri hii lazima itanivunjia nyumba yangu."

"Ina maana nitakaa ndani siku zote?"
"Hapana nitakuweka hotelini kwa muda kisha nitakutafutia nyumba nje ya Dar kisha nitakutafutia kila kitu."
"Mmh, sawa."

"Basi jiandae ili wakija wasikukute."
"Mmh, sawa."
Baada ya makubaliano tatizo likawa namna ya kuondoka na akiondoka lazima mtu wa mwisho kuja atajulikana.

Mzee Ezekiel aliamua kula njama na daktari juu ya mpango wake huku akiumuahidi donge nono. Alichomdanganya daktari ni kuwa mke wake mama Edna alikuwa na mpango mbaya na Jeska toka alipomchukua kukaa naye.

Na mpango mwingine ulikuwa ni mbaya zaidi hata kutoa ujauzito ni kwa ajili yake, hivyo alitaka kumtorosha ili kumsaidia katika maisha yake.
 
No 10
SASA ENDELEA...

"Alikuambia anakwenda wapi?"
"Hakuniambia"
"Afya yake?"
"Ipo sawa."

Unaikumbuka namba ya ile teksi?"
"Kwa kweli sikuitilia maanani."
"Mmh, sawa kaendelee na kazi."

Waliipokea ile barua na kuifungua kuangalia ndani kuna kitu gani, baada ya kuifungua walikutana na ujumbe ambao ulionesha kweli umeandikwa na Jeska kutokana na kuufahamu vyema mwandiko wake. Barua ilikuwa imeandikwa hivi:
Kwenu wazazi wangu, shikamooni.

Napenda kuandika waraka huu kuwatoeni wasiwasi kwa kutoweka kwangu ghafla, lakini napenda kuwatoa wasiwasi wazazi wangu pamoja na dada yangu kipenzi Edna. Najua kitendo nilichokitenda kitaonekana ni utovu wa nidhamu lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kufanya niliyoyafanya.

Kupewa ujauzito kwa kubakwa kwa kweli kuliniumiza sana kiasi cha kujikuta kiumbe nisiyetakiwa duniani. Lakini ninyi wazazi wangu pamoja na ndugu yangu kipenzi Jeska umeweza kunipa moyo na kufuta dhana mbaya moyoni mwangu ya kukatisha maisha yangu.

Nina mengi ya kuzungumza na ninyi wazazi wangu baba mama na Edna juu ya nini kilinikuta, sikutaka kulitamka hili mapema kwa vile lingeniongezea maumivu moyoni mwangu. Naamini kabisa hakuna hata mmoja angekubali kusubiri kuwaeleza kitu ambacho alikuwa na shauku kukijua.

Nimeamua kuondoka hapo nyumbani ili nipate muda wa kupumzisha maumivu makali ya moyo wangu, baada ya kuupumzisha moyo wangu nitarudi nyumbani, nakuombeni mnipokee japo mimi ni mwana mkosefu pengine kuonekana asiye na shukurani.

Ila siku ilifika kila kitu kitakuwa wazi na mtanielewa zaidi pengine kunionea huruma zaidi kama milivyonionea huruma na kunitunza mpaka leo hii. Sitaki kuwachosha kwa maneno mengi, nilitaka kuwatoa hofu tu msinitafute nipo katika mikono salama na baada ya muda nitarudi nyumbani ni mimi mwanenu Jeska.

Baada ya kuisoma alimpa Edna naye aisome kutokana na kuwa na shauku kutaka kujua kwenye karatasi ile kumeandikwa nini. Edna naye alisoma kimya kimya ile barua kisha alinyanyua macho kumtazama mama yake aliyekuwa akimfuatilia alipokuwa akisoma.

"Mama hii barua umeielewa?"
"Kilichoandikwa si umekisoma?"
"Ndiyo."
"Basi lazima tuielewe."

"Sina maana hiyo"
"Una maana gani?"
"Mama kuna fumbo zito ambalo Jeska kalificha, mmh kubakwa...na nani?"

"Tutajuaje naye amefanya siri."
"Lakini mama ulitakiwa kumuelewa Jeska kuliko kumkaripia."
"Edna usitake kuniudhi, kwani angenieleza haya aliyoandika kwenye barua nisingemuelewa?"

"Asingeweza kutokana na kauli yako ya ukali, Jeska anaamini toka apatwe na tatizo umemtenga."
"Nimemtenga kivipi Edna? Mbona unanitia lawama zisizo na msingi."

"Kweli mama umekuwa mkali kauli zako hata mimi nilijisikia vibaya, ni kweli Jeska alikuwa amefanya kosa hatukutakiwa kutumia vitisho aseme nani aliyempa ujauzito. Lazima angesema tu kama alivyosema alichanganywa na kitendo cha kubakwa, hata ningefanyiwa mimi ningeumia."

"Sasa atakuwa wapi?"
"Ni vigumu kujua la muhimu tumsubiri baba arudi atatusaidia akiisoma hii barua."
 
  • Thanks
Reactions: ram
11
Endelea...

"Mmh, mwaka huu mbona Jeska ametuchanganya akili," mama Edna alisema huku akiirudisha barua kwenye bahasha.
Mara simu ya Edna iliita alipoangalia ilikuwa namba ngeni machoni mwake, aliipokea na kusema.
"Haloo"

"Haloo Edna," sauti ya upande wa pili ilisema.
"Nani mwenzangu?"
"Mimi Jeska."
"Jeska! Jamani Jeska upo wapi ndugu yangu?"

"Kabla ya yote barua mmeipata?"
"Ndiyo, upo wapi mbona umeondoka nyumbani bado tunakuhitaji?"
"Edna sipo mbali ila baada ya muda nitarudi nyumbani, kama nilivyosema."
"Lakini ipo wapi?"

"Nimekwambia sipo mbali, akili yangu ikitulia na nikiwa tayari kuyasema mbele yenu nitarudi nyumbani, msalimie mama."
"Huyu hapa," Edna alisema huku akimpa simu mama yake.
"Haloo Jeska."

"Abee mama, shikamoo."
"Marahaba, upo wapi mama rudi nyumbani...yote yamekwisha ilikuwa ni hasira tu mwanangu."
"Najua mama, ila usiwe na wasiwasi nitarudi tu mama nakupenda sana."

"Najua mwanangu chonde chonde mwanangu rudi walimwengu hawatanielewa, hata nduguyo anasema matatizo yote chanzo ni mimi."
"Hapana mama, nitarudi."
Jeska alikata simu na kuizima kila walipompigia hakupatikana.

****
Jeska baada ya kurudi kutoka kwa mzee Ezekiel kupeleka barua kutokana na makubaliano yake na mzee Ezekiel kuwa aandike barua ya kuwatoa wasiwasi ili familia yake itulie isimtafute. Baada ya kurudi hotelini kwake alitulia na kumjulisha mzee Ezekiel kwa simu.

"Tayari baba."
"Vizuri, umempa nani?"
"Mlinzi."
"Amekuona?"

"Ndiyo."
"Amesemaje?"
"Alionesha kunishangaa lakini sikumpa muda wa kuuliza swali zaidi ya kuondoka nikimwacha akinitumbulia macho."

"Jeska umefanya kitu kizuri sana, nakuhakikishia kuyabadili maisha yako kama shukurani ya kuificha siri ambayo ingenichafua."
"Nitashukuru"

Mzee Ezekiel muda ule aliamua kurudi nyumbani ili akasikie wamepokeaje barua ya Jeska, alipofika nyumbani alikuta hali ya kawaida na yeye alijifanya hajui lolote. Baada ya mapumziko mafupi mkewe alimfuata alipokuwa amekaa kwenye kochi na kumpatia barua ya Jeska. Kabla ya kuipokea alihoji.

"Ya nini?"
"We, soma."
Aliichukua ile barua na kuisoma kiuongo na ukweli kisha alishusha pumzi ndefu na kumtupia jicho mkewe aliyekuwa akimfuatilia muda wote aliokuwa alipokuwa akiisoma.

"Umeiona?" Mkewe alimuuliza.
"Nimeiona."
"Una maoni gani?"
"Nani kaileta?"

"Yeye mwenyewe."
"Alipoileta alisemaje?"
"Sikuonana naye ila alimpa mlinzi."

"Nafikiri kuna kitu anakiamini, sidhani kuna umuhimu wa kumtafuta kwa vile amesema atarudi tumpe uhuru anaotaka. Nina imani sasa hivi Jeska ana miaka 19 ana maamuzi ambayo yanayokubalika hata kisheria."
 
12
Endelea...

"Lakini bado ni mtoto aliye chini yetu."
"Ni kweli, lakini mambo mengi amekuwa akituficha sisi walezi wake ambao tulimlea kama mtoto wetu wa kuzaa. Sidhani kama kuna siku ulimpa upendeleo Edna na kumtenga Jeska?"

"Sijawahi na wala sikuwahi kuwaza jambo hilo zaidi ya kufikiria siku moja Jeska ayazungumze mafanikio yake kupitia mikono yetu. Inaonesha jinsi gani Jeska kaumizwa na kubakwa kitendo ambacho kimechubua kovu la kufiwa na wazazi wake."

"Sasa sisi tutafanya nini ikiwa yeye mwenyewe hataki kusema ukweli ili tumchukulie hatua aliyembaka. Lakini kwa vile amesema ipo siku atarudi na kuyasema yote tumpe muda."

Baada ya makubaliano mzee Ezekiel aliaga na kuondoka, safari yake ilikuwa kwenda hotelini kwa Jeska akapange mikakati mingine baada ya kufanikiwa mpango wake wa awali wa kumtorosha Jeska. Alipofika hotelini alimkuta Jeska amejilaza akiwa hajui nini hatima ya maisha yake baada ya kukubali kuusaliti moyo wake kwa kuuficha ukweli.

Mzee Ezekiel alikumta amejilaza kitandani akiwa amejifunga taulo lililovuka magoti kidogo. Jicho lake lilitua kwenye maumbile ya mvuto ya Jeska. Alimeza funda la mate na kuingia ndani wakati huo Jeska alikuwa akijiweka vizuri.

"Karibu baba."
"Asante."
"Za huko?"
"Mmh nzuri, akili tuliyotumia itakufanya uishi bila wasiwasi."

"Nitaishi vipi ina maana maisha yangu yote yatakuwa ya hotelini?"
"Hapana, kuna nyumba nimekutafutia nitakupangia nyumba nzima ambayo utaishi huko nitakutafutia mfanyakazi wa ndani. Nitakutoa siku moja moja sehemu za starehe zilizokuwa nje ya mji ili kuhakikisha unafurahia maisha."

"Kama hivyo nitashukuru."
"Nia yangu ni kurudisha furaha yako na kuondoa maumivu yote ya kubakwa, ichukulie kama ajali. Si hayo tu nina mpango wa kukujengea nyumba na kukufungulia miradi ili usiwe tegemezi. Leo nipo kesho sipo sitaki upate tabu."

Huo ndiyo ukawa mwanzo wa Jeska kuishi mbali na familia iliyomlea huku mzee Ezekiel akiongeza mapenzi kwa Jeska ambaye bila kujielewa alikuwa amenaswa na mtego wa mzee Ezekiel na kumgeuza kuwa mpenzi wake.

Penzi lake na mzee Ezekiel lililipuka kama moto wa volkano, safari zote za ndani na nje ya nchi walikuwa pamoja, Jeska alizidi kupendeza toka umbile la kitoto na kuhamia katika umbile la mtu mzima lisilo tilia mashaka ukaribu wake na mzee Ezekiel watu waliwaona wapo sawa.

Jeska kwa muda mfupi alisahau maumivu yote ya kubakwa na mzee Ezekiel na kujikuta akifurahia penzi la mzee huyo na kutamani awe mke mdogo mwenye haki zote.

Mzee Ezekiel alimhakikishia kumuoa ndoa ya Bomani na kumpatia sehemu ya mirathi ya mali yake. Hatua ile ilimfurahisha sana Jeska na kuamini mwanzo wa maisha mapya ya kuweza kumiliki mali yake kutokana na uwezo mkubwa wa mzee Ezekiel.

Ukaribu wa mzee Ezekiel na Jeska ulianza kuyumbisha nyumba ya mzee Ezekiel kwa mapenzi yote kuhamishia kwa Jeska aliyefahamika kama mke wa pili wa mzee Ezekiel. Kutokana na tabia ya mke wa mzee Ezekiel mama Edna kutotembea mambo mengi ya nje hakuyajua.

Wakati mipango imekaribia na hatua zote muhumu za kufunga ndoa ya Bomani, siku moja baada ya kutoka kwa Jeska majira ya saa tano usiku mzee Ezekiel akiwa katika gari lake alipata ajali ya gari lake kugongwa sehemu ya mlango na kumsababishia maumivu makali sehemu za kifua na mbavu.
 
13
WASAMARIA wema walimsaidia kumkimbizia hospitali ya muhimbili kwa matibabu.
Taarifa kwa familia yake zilifika siku ya pili kwa msaada wa daktari aliyepewa maelezo na mzee Ezekiel aliyekuwa akizumgumza kwa taabu. Kutokana na tabia aliyoanzisha mzee Ezekiel kulala nje au kurudi muda mbaya familia yake iliizoea.

Taarifa ya kupata ajali iliishtua na kuifanya itaharuki, walifika hospitali walimkuta mzee Ezekiel katika hali mbaya sana. Hakuwa tena na kauli zaidi ya kujitahidi kuzungumza lakini alishindwa. Madaktari walijitahidi sana kuokoa maisha ya mzee Ezekiel.

Lakini usiku wa siku ile mzee Ezekiel aliaga dunia majira ya saa mbili na dakika ishirini na nne. Ulikuwa msiba mkubwa kwa familia yake kumpoteza mtu muhimu ambaye ameondoka bila kuwaeleza familia yake neno lolote la mwisho.

Kwa upande wa Jeska ambaye muda huo alikuwa tayari ameisha muhamishia katika nyumba aliyompangia maeneo ya Mbezi beach na kumlipia kodi ya mwaka mzima, Jeska hakuwa na taarifa zozote juu ya mzee Ezekiel mtu aliyeachana naye siku moja usiku na kumuahidi Ijumaa ijayo itakuwa siku yao ya kufunga ndoa yao kwa Mkuu wa Wilaya.

Ukimya wa siku mbili ulimshtua na simu yake kila alipopiga haikupatikana, Jeska alivumilia japo moyo haukutulia kabisa kutokana na kuzama katika penzi zito la mzee Ezekiel. Pesa alizokuwa nazo na mahitaji muhimu ya ndani yalimfanya asiwe na wasiwasi sana. Wiki ilikatika bila kumuona mzee Ezekiel kitu kilichosababisha kumtia wasiwasi.

Aliamua kwenda ofisini kwake akapate taarifa zake, wasiwasi wake labda amesafiri kikazi. Lakini hakukubaliana na wazo lile kwa kuamini kila safari ya ndani na nje ya mkoa au nje ya nchi alikuwa naye. Lakini hakutaka kuumiza kichwa aliamua kwenda ofisini kwa mzee Ezekiel kupata ukweli wa ukimya ule.

Alikodi gari hadi ofisini kwa mzee Ezekiel, alipofika aliteremka garini na kuelekea ofisini kutaka kujua habari za mzee Ezekiel. Wakati akipiga hatua kuelekea ofisini alishtushwa na mtu kumwita jina lake.
"Jeska," aligeuka bila kuitika ili amjue anayemwita.

Alijikuta akitazamana uso kwa uso na Edna shogae mtoto wa mzee Ezekiel, moyo ulimpasuka lakini alijikaza kiume na kujenga tabasamu la uongo usoni kwake.
"Ha! Edna."
"Jamani Jeska upo wapi naona maisha mazuri!"
"Mmh, kawaida."

"Hapana Jeska unaonekana mama si msichana tena, au mambo ya shemeji?"
"Edna tuachane na hayo unatoka wapi?"
"Ofisini kwa baba."
"Jamani baba yupo?" Jeska alijifanya kudanganya kuwa alikuwa hamfuati mzee Ezekiel.
"Jeska wewe upo wapi?"

"Edna nitakueleza ninapoishi na ikiwezekana siku moja uje unitembelee."
"Jeska sina maana unapoishi, bali kutoweza kusikilia yaliyomkuta baba."
"Yepi tena hayo?" Jeska alishtuka.
"Jamani Jeska baba alifariki..."

"Etiiii!?" Jeska alishtuka mpaka simu aliyokuwa ameshikilia ilimponyoka.
"Jeska unashtuka kweli au?"
"Edna unasema kweli mzee Ezekiel amefariki?" Jeska aliuliza huku akitiririkwa machozi.
"Jeska jambo zito kama hili kwa nini nikudanganye."
"Mungu wangu, lini?"

"Sasa inakimbilia wiki ya pili, alipata ajali mbaya ya kugongwa gari lake ubavuni na kumsababishia maumivu ya kifua na mbavu na damu kuvilia ndani kitu kilichosababisha mauti yake kabla ya kumfanyia upasuaji."

"Edna unasema kweli mzee Ezekiel amekufa?" Jeska hakuamini aliuliza tena, aliona kama ndoto ya mchana isiyo na ukweli wowote. Machozi yalimwagika kama maji, aliona kipande cha nguo kilichomsitiri kimemponyoka mbele ya kadamnasi na kujiona kasimama mtupu.

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA
"Edna unasema kweli mzee Ezekiel amekufa?" Jeska hakuamini aliuliza tena aliona kama ndoto ya mchana isiyo na ukweli wowote. Machozi yalimwagika kama maji aliona kipande cha nguo kilichomsitiri kimemponyoka mbele ya kadamnasi na kujiona kasimama mtupu. Endelea sasa...

"Jeska kweli baba amekufa, tumelia sana lakini hatukuwa na jinsi kwa vile kazi ya Mungu. Jeska si wewe hata mimi kifo cha baba kimenichanganya sana, lakini kilichonichanganya zaidi ni hali ya mama baada ya kifo cha baba presha ilimpanda mpaka ninavyoongea hivi mama anapumulia mashine."
"Mungu wangu, sasa unaishije?"

"Kila kitu nimemuachia Mungu, nashukuru kampuni yake wameonesha ushirikiano wa juu hasa kipindi hiki cha matatizo wapo na sisi bega kwa bega kuhakikisha tunafarijika hasa mimi niliyebakia kama kinda la ndege lililoondokewa na waazazi wake katika upepo mkali ulioezua kiota chetu."

"Du, pole sana ndugu yangu."
"Asante, ila nakuomba muda huu ni muafaka wa kurudi nyumbani, rudi ndugu yangu rudi tuwe wawili."
"Nitarudi lakini si sasa hivi."
"Kwa nini?"

"Nitakujibu siku nikirudi."
"Ina maana hata kwenda kumuona mama huendi?"
"Edna nitakuja lakini si leo amelazwa hospital gani?"
"Muhimbili VIP."

"Nitakuja kesho kumuona, kwa sasa siwezi, siamini... siamini kama kweli mzee Ezekiel amekufa. Mungu wangu huu ni mkosi gani kila siku ni mimi tu Jeska."
Jeska alizungumza huku akiondoka akiwa amechanganyikiwa na kifo cha mzee Ezekiel mtu pekee aliyekuwa akimtegemea katika maisha yake.

Kuondoka kwake kulimfanya Edna apigwe na bumbuwazi kutokana na kuchanganyikiwa kwa Jeska na kuwa nusu mwendawazi. Alimshuhudia akitembea mikono kichwani huku akizungumza peke yake na kukoswa kugonga na gari.

Dereva mmoja wa taksi aliyekosa kumgonga alipoteremka na kumsogelea aligundua yule mwanamke ana matatizo mazito kutokana na kauli zake na kilio alichokuwa akili.
"Dada una tatizo gani?"

"Sina faida ya kuendelea kuishi bora nife."
"Kwa sababu gani?"
"Kwa nini kila siku niwe miye tu?"
'Umefanya nini?"
"Wee acha tu."

‘Una kaa wapi?"
"Mbezi."
"Ya Kimara au Beach?"
"Beach."
"Ingia nikupeleke kwako."
Jeska aliingia kwenye gari na dereva aligeuza gari lilielekea Mbezi anapoishi Jeska aliyekuwa amechanganyikiwa kwa kuamini tabu za dunia ziliumbwa kwa ajili yake.

Njia nzima Jeska alikuwa akilia kitu kilichozidi kumchanganya msamalia mwema, baada ya kuvumilia ilibidi ahoji.
"Kwani dada umetokewa na nini?"
"Kaka yangu kwa nini kila siku niwe mimi tu?"
"Kwani umetokewa na nani?"

"Nimefiwa na wazazi na mtu niliyekuwa namtegemea amekufa."
"Ooh, pole sana, kwani unakaa na nani?"
"Huyo huyo aliyekufa."
"Ni mwanamke au mwanaume?"
"Mwanaume."
"Hana mke?"

"Nimekuambia nimebaki peke yangu maswali mengi ya nini?"
"Ooh, pole sana, sasa utaishi vipi?"
"Hapo ndipo ninapochanganyikiwa."
"Una mtu wa kukusaidia?"
"Kaka yangu nikuambie mara ngapi sina mtu zaidi ya kuiona dunia ikinielemea na kujiona sina thamani yoyote dunia."

"Najua inauma lakini naomba nikueleze kitu kimoja, usiyaruhusu mawazo mabaya yatawale akili yako."
"Sina jinsi hivi haya maisha nitaishi maisha gani sina kazi sina ninapopategemea, kodi ya nyumba ikiisha nitalipa nini."
Jeska alipokaribia nyumba anayoishi alimueleza dereva kuwa amefika.
Dereva alishtuka kuona Jeska anaishi kwenye jumba zuri la thamani.

"Ha! Kumbe upo hapa?"
"Eeh, kaka yangu," Jeska aliteremka na kutoa pesa kwenye pochi kumpa yule kaka. Lakini yule kaka aliikataa na kusema.
"Hii si teksi ni gari langu, nilijitolea kukusaidia tu."
"Asante kaka yangu kwa kuonesha moyo wa kibinadamu, angekuwa mwingine baada ya kukosa kunigonga ningeambulia makofi, karibu ndani kaka yangu."

Yule kaka bila kubisha aliliingiza gari ndani ya geti na kukutana na jumba ambalo kodi yake ilionesha ni kubwa sana ya mamilioni ya pesa.
"Mmh, hongera una jumba zuri."
 
14
LIPOISHIA WIKI ILIYOPITA
Yule kaka bila kubisha aliliingiza gari ndani ya geti na kukutana na jumba ambalo kodi yake ilionyesha ni kubwa ya mamilioni y pesa . "
mnh, hongera una jumba zuri"

"Asante, lakini ndivyo hivyo mwisho wa mwaka siwezi kukaa hapa tena."

"Unaishi na nani?"
"Nipo peke yangu na mfanyakazi wa ndani, kwa sasa nina pesa kidogo za matumizi zikiisha nitamlipa nini.

Na mwaka ukiisha nitalipa nini na nikifukuzwa nitakwenda wapi kama sio kuadhirika mtoto wa kike," Jeska alijikuta akitoa siri yake yote bila kujua mtu aliye mbele yake ni wa aina gani kutokana na kupagawa kutokana na kifo cha mzee Ezekiel na maisha atakayoishi.

"Hapa mjini huna ndugu?"
"Wapo lakini ni wabaya wangu."
"Kivipi?"
"Japo sikujui hunijui lakini msaada wako mkubwa unanifanya niwe muwazi kwako."

"Ni kweli mimi ni mtu mwema pia naweza kuwa msaada mkubwa katika maisha yako."
Jeska alijikuta akiitoa siri yake yote toka kifo cha familia yake mpaka alivyochukuliwa na familia ya mzee Ezekiel baba yake shogae kipenzi Edna. Lakini la mzee Ezekiel kumbaka alilificha, lakini kwa ajabu yule mgeni alimwambia.

"Mbona unaficha lingine."
"Lipi hilo?"
"La kukubaka mzee Ezekiel na kukutorosha hospitali."
"Mmh, umejuaje?" Jeska alishtuka.
"Namejua tu kwani lilikuwa siri."
"Mbona unanitisha, hakuna anayejua zaidi yangu na dokta."

"Sasa hapo siri ipo wapi, tuachane na hilo, mmhu"
"Hapana, inaonekana basi unajua mengi kuhusu mimi."
"Sijui lolote, hebu endelea kunihadithia ili niweze kukusaidia."

"Kama hivyo baada ya kubakwa na kufichwa huku lakini mkosi bado ulikuwa ukiniandama na kujikuta niliyemtegemea ndiyo hivyo amefariki."
"Lakini si mlikuwa na mpango wa kuoana?"
"Eti?" Jeska alizidi kushtuka maneno ya mgeni wake kuonekana kujua mambo mengi ambayo yeye aliamini ni siri.

"Jamani kaka wewe ni nani unayejua mambo yangu mengi?"
"Sijui mengi ila hutaki kuwa mkweli na muwazi kwangu."
"Kaka yangu mengine nayasahau kutokana na kuchanganyikiwa."

"Basi nitakuwa nakusaidia, upo tayari nikusaidie?"
"Nipo tayari, japo maneno yako yananitia wasiwasi."
"Sikiliza Jeska."

"Ha! Kaka umejuaje jina langu?"
"Jeska hayo si muhimu zaidi la lililo mbele yako."
"Sasa utanisaidia vipi?"
"Nataka mali zote zilizochukuliwa na wazazi wako zirudi kwako."

"Kwangu! Wewe ni mwana sheria?"
"Ni mtu wa kawaida ila ninajua jinsi ya kukurudishia mali zako."

"Utafanya nini?"
"Jeska, wewe shida yako mali zako au kujua zitarudi vipi?"
"Mmh, siamini naona sawa na kunipa matumaini lakini jambo hili siamini kama litawezekana ni muda mrefu sana hata hati zote wanazo wao."

"Kazi hiyo niachie mimi, sawa."
Baada ya kusema vile mgeni aliingiza mkono mfukoni na kumpatia noti mpya nne za elfu tano tano na kumueleza.
"Naomba hizi hela usizitumie leo kaziweke chini ya mto mpaka kesho kisha ruksa kuzitumia."

"Asante," Jeska alishukuru huku akipokea.
"Nilitaka kusahau na ukiamka asubuhi chukua zote usiache hata moja chini ya mto."

"Hakuna tatizo."
"Wacha nikuache niwahi kwenye shughuli zangu nikipata muda nitarudi usiku."
"Kuja kulala?"

"Utakavyotaka wewe, au nisirudi?"
"Hapana njoo tu."
"Basi wacha nikukimbie."

"Ngoja nikaweke pesa zangu ndani," Jeska alisema huku akinyanyuka kuelekea chumbani kwake.

Jeska alikwenda hadi chumbani na kuziweka pesa zake chini ya mto kisha alitoka sebuleni alipomuacha mgeni. Lakini sebule ilikuwa nyeupe mgeni hakuwepo, alipotoka nje pia hakumkuta pamoja na gari lake.
 
15

Sasa Endelea...

Alijiuliza mgeni ametoka vipi kwa muda mfupi bila kuaga wala gari lake kutoa muungurumo wakati wa kuondoka.

Hakutaka kuumiza akili yake zaidi ya kurudi sebuleni na kujitupia kwenye kochi na kujikuta akivuta taswira ya mzee Ezekiel na mipango yao kabambe ya kufunga ndoa na kuyabadili maisha yake kwa kumjengea jumba na kumnunulia gari la kifahari.

Moyo ulimuuma na kujikuta akilia peke yake kwa sauti ya chini huku akipiga mikono kwenye sofa na kusema kwa sauti.

"Haiwezekani kila baya kwa nini liwe kwangu, nimefiwa na wazazi nimedhurumiwa mali nimebakwa na mwisho niliyekuwa namtegemea amekufa kuna faida gani kuendelea kuishi bora nife.
"
Wazo la haraka lililomujia Jeska ni kujiua, alinyanyuka alipokuwa amekaa na kuelekea chumbani kwake, chini ya kitanda kulikuwa na kamba ya kuanikia nguo ndani wakati wa mvua. Aliichukua na kutoka nje ili aelekee kwenye mti ajiue.

Ajabu ya mwaka aliyokutananayo kidogo apige kelele ya woga baada ya kumuona mgeni akiwa amekaa kwenye sofa akimtazama.

"Ha!" Jeska alishika mkono kifuani kwa mshtuko.
"Mbona umeshtuka?" Mgeni alimuuliza huku ameachia tabasamu pana.
"Ha..a..a..pa..na," Jeska alijibu kwa kubabaika.
"Hiyo kamba ya nini?"
"Aa..aa. ya kawaida."
"Unajua kutaka kujiua ni kuingilia kazi ya muumba kwa vile lazima ufe."

"Umejuaje?"
"La muhimu si kujua nimejuaje zaidi ya kukuonya tena usiingilie kazi ya muumba.
"
"Lakini wewe nani?" Jeska alimuuliza.
"Jeska hata ukinijua si muhimu zaidi ya kujipanga kwa maisha mapya na si kukimbilia kujiua.
"
"Ulikuwa wapi mbona nilitoka muda mfupi hukuwepo?"
"Nilikuwa nimeondoka kwa vile nilikuwa na haraka nisingeweza kukusubiri, lakini uso wako ulionesha una dhamira mbaya moyoni mwako kitu kilichonifanya nirudi kabla hujachukua uamuzi mbaya."
"Nina faida gani ya kuendelea kuteseka kila siku."
"Nimekueleza nitakusaidia unataka msaada gani zaidi ya huo?"
"Basi nisamehe, nimechanganyikiwa na maisha."
"Nimekusamehe naomba unisindikize, ila nakuomba usirudie kufanya ujinga wowote, sawa?"
"Sawa."

Walitoka hadi nje ambapo mgeni aliingia kwenye gari lake Jeska alimfungulia geti na mgeni aliondoka na kumpungia mkono. Jeska alilisindikiza gari lile kwa macho mpaka likapotea huku akijiuliza mtu yule ni nani mbona kama anaonekana wa ajabu ajabu. Lakini aliamini yale ni mawazo yake kutokana na kuchanganyikiwa na maisha.

Jeska alirudi ndani na kwenda moja kwa moja chumbani kwake na kujilaza chali macho alitazama juu ya dali.

Kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi juu ya yule mwanaume msamaria mwema. Alijiuliza ni mtu wa aina gani, bado alipingana na akili yake pengine kuchanganyikiwa ndiko kulikomfanya hata alipotoka hakumuona. Lakini kama hakumuona sebuleni hata gari lake. Bado alibakia njia panda asijue ukweli ni upi.

Kingine kilichomchanganya mtu yule kujua mambo yake mengi, wazo la kuwa mtu yule labda jini hakuwa nalo zaidi ya kuamini mtu yule alikuwa akimjua vizuri kuliko alivyojifahamu yeye mwenyewe. Akiwa amejilaza akitazama juu kwenye dari hakuona faida ya kuendelea kuishi hata kama yule mwanaume angeamua kumsaidia bado asingeweza kuyamudu maisha.

Bado shetani mbaya hakuwa mbali naye ufumbuzi mkubwa katika maisha yake ilikuwa ni kuyakatisha maisha yake. Jeska aliamini hakuna mtu wa kumsaidia tena katika maisha yake. Wazo la kujinyonga bado halikuwa mbali naye alikurupuka na kwenda kuchukua kamba aliyoirudisha chumbani na kutoka nayo tena kwa kujiamini ili akajinyonge.

Alitoka mpaka nje kabla ya kuchukua uamuzi ule mzito alimtuma mfanyakazi wake wa ndani sehemu ambayo aliamini mpaka atakaporudi atamkuta ameisha jinyonga. Hata mlinzi vilevile alimtuma mbali ili tu awe huru kutekeleza mpango wake wa kujinyonga.

Baada ya kukagua eneo lilo na kuliona lipo katika hali ya utulivu, alichukua kamba yake na kuzunguka nyuma ya nyumba kwenye miti na kuifunga kwa kupanda kwenye mti. Alikumbuka alisahau sturi ya kupandia. Alirudi ndani kuchukua kwa haraka kabla hawajarudi wafanyakazi wake.
Alipofika ndani alichukua sturi na kuzunguka nayo nyuma ya nyumba ili atimize dhamira yake ya kujinyonga.
 
16
Sasa endelea...

Wakati anatoka ndani alikutana na mfanyakazi wake wa ndani.
"Dada mbona una kisu mkononi?"
"Wewe Sara mbona umewahi kurudi?" Jeska alimuuliza kwa hasira.

"Dada ulichonituma nimekipata hata kabla ya kufika uliponituma tena kwa bei nafuu."
"Sikiliza Sara kukutuma kule nilikuwa na maana yangu nakuomba urudi upesi kachukue pesa ndani uwahi haya mafuta siyataki," aliyapigiza mafuta ukutani kwa hasira, chupa ilipasuka na mafuta kutawanyika.

"Sasa dada mbona ni kitu kile kile tu."
"Sara siku hizi tumekuwa tunabishana?"
"Dada siwezi kurudi roho inaniuma."
"Kwa nini?"

"Kwa uamuzi unayotaka kuchukua."
"Uamuzi gani?"
"Ya kutaka kuyakatisha uhai yako."
"Wewe Sara umejuaje?" Jeska alishtuka kusikia vile.
"Nijueje? Wakati uso wako unaonesha una dhamira mbaya ya kutoa uhai wako."

"Aah!" Jeska alipigwa na bumbuwazi mpaka kisu kikamponyoka.
"Lakini dada kwa nini usimsikilize mgeni?"
"Mgeni, mgeni gani?"

"Eeh, yule kaka aliyekuleta mchana."
"Alisemaje?"
"Si alisema atakusaidia kila kitu."
"Basi Sara nimekuelewa."
Jeska alisema huku akigeuka arudi ndani, alishtuka kumuona mlinzi akiwa anatokwa machozi.

"Ha! Mnyalu umerudi saa ngapi?"
"Sijaenda popote bosi."
"Kwa nini hujaenda popote na kwa nini unalia?"
"Sijaenda kwa kuhofia nikiondoka utajiua na ninalia kwa vile ukifa nitafanya wapi tena kazi."
"Umejuaje dhamira yangu."

"Inajionesha usoni kwako."
Kauli ile ilimshtua sana Jeska na kujiuliza uso wake unaonesha vipi dhamira iliyokuwa moyoni mwake. Alipanga akienda ndani akajitazame usoni ili aione dhamira yake usoni kwake inaonekana vipi.

"Mnyalu si unajua maisha magumu unafikiri baada ya kufa mzee mimi nitawezaje kuyahimili maisha haya. Kwa sasa hivi nina uwezo lakini huko mbele mambo yatakuwa magumu sana, nitatakiwa nilipe kodi ya mwaka milioni mbili na laki nne kazi sina nitazipata wapi.

"Bado mshahara wenu kula yetu mnafikiri Jeska mimi nitafanya nini, Mnyalu wewe si mgeni kwangu nimeisha kueleza siri yangu ya maisha. Umeona jinsi mikosi inavyoniandama unafikiri mwisho wake nini?"
"Lakini mbona mgeni alisema atakusaidia?"

"Mnyalu umejuaje?"
"Ma mdogo Jeska si muhimu kujua nimejuaje ila kumsikiliza mgeni alivyokuonya asiyakatishe maisha yako pia yupo tayari kukusaidia."

Maneno ya Sara na Mnyalu yalizidi kumchanganya Jeska na kukubaliana na ombi la wafanyakazi wake kuwa asiyakatishe maisha yake. Aliamua kurudi ndani huku moyo ukimuuma kwa uamuzi wa kijinga wa kutaka kuitoa roho yake bila sababu.

Aliingia hadi chumbani kwake na kupiga magoti mbele ya kitanda kumuomba Mungu amsamehe kwa yote aliyoyataka kufanya. Baada ya kuomba toba ya majuto huku akilia alijikuta akilala kwenye zuria bila kujijua. Alishtushwa na sauti ya Sara.

"Dada...dada."
Kabla ya kuitikia alijiangalia alipokuwa amelala kwenye zuria pembeni ya kitanda. Alijinyanyua alipokuwa amekaa kwenda kufungua mlango, alikutana na Sara akitweta huku jasho likimtoka.

"Vipi Sara mbona hivyo?"
"Samahani dada nilikuta foleni kubwa.
"Ya nini?"
"Si uliponituma."
"Kukutuma nini tena?"

"Dada si ulinituma nikufuatie mafuta."
"Mafuta! Mbona sikuelewi si uliishaleta."
"Dada nimeleta saa ngapi na mimi sasa hivi ndio nafika."

"Sara mbona sikuelewi unafika vipi wakati mafuta umeishaleta."
"Dada utakuwa anachanganyikiwa, umenituma mafuta na kunieleza nisinunue popote zaidi ya uliponituma na sasa ndiyo narudi."

"Sasa haya ni maajabu, sasa Sara aliyeniletea mafuta ni Sara gani?"
"Kwani kuna mtu kakuletea mafuta?"
"Sio mtu bali wewe Sara, hebu acha kunichezea akili."
"Kweli dada mimi ndiyo nafika."

"Mmh, mbona nazidi kuchanganyikiwa aliyekuja na kunikataza nisijiue ni Sara gani?"
"Ha! Dada ulitaka kujiua?"
"Ha..ha..a..pana."

Wakati akiwa bado yupo njia panda mlinzi wake aliingia.
"Ma mdogo Jeska ulichonituma nimezunguka kila kona nimekosa."
"Mmh, Mnyalu na wewe unataka kunichezea akili kama Sara au mmepanga kunitania?"

"Kivipi Ma mdogo?"
"Wewe si uliniambia hukuondoka baada ya kugundua nataka kujiua?"
"Mungu wangu! Mamdogo ulitaka kujiua?"

"Jamani mbona unanichezea akili?"
Ni kweli Sara na Mnyalu hawakuwepo? Ili kujua yote tukutane wiki ijayo.
 
17
SASA ENDELEA...

"Dada kwani vipi mbona kama umechanganyikiwa?" Sara alimuuliza Jeska ambaye aliamini walikuwa wakimchezea akili.

"Jamani hebu acheni kunichezea akili ni kweli ndio mnafika?"
"Dada tokea lini nikakudanganya, sijui kaka Mnyalu." Sara alijitetea.

"Hata mimi sijawahi kukutania, unasema kuna mtu kama mimi alikuja kukueleza usijiue labda malaika hakutaka kuona unaukatisha uhai wako."

"Hata siamini bado hayajaniingia kichwani."
"Dada kwa upande wangu ndio nafika toka uliponituma nitawezaje kwenda kule na kisha niwepo hapa kwa wakati mmoja?"

"Sawa hamkuwepo ni nani anayefanana na wewe na mwingine na Mnyalu waje kwa wakati mmoja kwa umbile na mavazi yenu?"
"Dada labda ulikuwa umelala ukaota lakini mimi sikiwepo," Sara alizidi kujitetea.
"Hata mimi," Mnyalu naye alikana kuwepo.
"Mmh, sawa."

"Lakini dada kwa nini ulitaka kujiua?" Sara alitonesha kidonda.
"Jamani naomba mniache kwanza."
"Tutakuacha tu dada, lakini kwanini unataka kututia ukiwa?" Mnyalu naye aliuliza.

"Jamani nimechanganyikiwa mwenzenu na maisha," Jeska alijitetea baada ya kubanwa sana.

"Ma mdogo Jeska kujiua bado si suruhisho la matatizo kwa vile kila kiumbe kina haki ya kufa, kuingilia kazi ya Mungu ni kujiongezea matatizo."
"Basi jamani nimekosa nisameheni sirudii tena kuchukua uamuzi kama huo."
"Sawa dada."

Walimuacha Jeska akirudi chumbani kwake kupumzika na kila mmoja alikwenda kuendelea na kazi yake. Jeska akiwa kitandani amejilaza alijikuta akijawa na mawazo mengi juu ya kile kilichomtokea cha Sara na Mnyalu kuonekana wakimsihi asijiue na baadaye kuonekana katika sura nyingine kila mmoja akikana hakuwepo muda ule.

Bila kujielewa usingizi ulimpitia, aliposhtuka alishangaa kujikuta amelala kwenye nyumba ngeni kwake. Lakini chumba kilikuwa kizuri sana kilichokuwa na mapambo na harufu nzuri hewa yake ilikuwa nzuri sana. Pembeni yake alikuwa amelala yule bwana msamalia mwema aliyemuahidi kumsaidia.

Yule bwana alikuwa kwenye usingizi mzito, Jeska alijiuliza pale ni wapi na amefikaje. Alijikuta akiwa na shauku ya kutaka kumuamsha yule bwana amuulize pale ni wapi na amefikaje.

Kabla hajamshika upepo mwanana mzuriii wenye harufu nzuri ya manukato ulimpiga usoni na kujikuta ukipatwa na usingizi na kujilaza pembeni ya yule bwana. Jeska alishtuka siku siku ya pili na kujikuta amelala kitandani kwake.

Alikurupuka kitandani na kutoka hadi nje ya chumba chake.
Milango ilikuwa bado imefungwa kuonesha hakuna aliyeingia wala kutoka. Alitamani kuita lakini ajabu aliyetaka kumwita hakumfahamu jina. Alikwenda msalani na bafuni lakini hakumuona mtu.

Alijiuliza mtu yule aliyekuwa naye usiku yupo wapi?
Bado hakuamini alitoka hadi kwa mfanyakazi wake wa ndani kumuuliza.
"Sara."

"Abee dada."
"Mgeni umemuona?"
"Mgeni gani?"
"Si yule kaka wa jana."
"Wala sijamuona."
Hakuongeza neno aliondoka hadi getini kwa mlinzi.
"Mnyalu kuna mgeni yoyote?"
"Hataa."

"Mnyalu ina maana gari la mgeni wa jana mchana hukuliona?"?"Sijaona gari wala mtu."
"Sasa atakuwa amekwenda wapi?" aliuliza swali bila kujua anayemuuliza hajui lolote.

"Nani?"
"Ok, basi."
Jeska aligeuka kurudi ndani huku akiamini kabisa mgeni alilala naye chumba kimoja, kingine kilichomchanganya ni sehemu aliyokuwa amelala kwenye chumba chenye hewa na uzuri wa ajabu. Jeska aliamini alichokiona hakikuwa ndoto bali kitu cha kweli.

Kilichomshangaza zaidi kidoleni pete yake ya uchumba aliyovalishwa na mzee Ezekiel haikuwepo, kila dakika alijikuta akizidi kuchananyikiwa na kila kilichokuja mbele yake. Alizidi kuingiwa na wasiwasi na kujiuliza yule mgeni ni nani ni mtu wa kawaida au jini. Lakini bado hakukubaliana na mawazo yake, alijikuta akiwa na shauku kuonana na mgeni kutaka kumuuliza mambo yanayomtatiza juu yake.

Asubuhi kama alivyoelezwa na mgeni alikwenda chini ya mto na kuzitoa fedha alizopewa na mgeni za matumizi. Alifunua mto na kuzitoa zile fedha ambazo alinunua vitu muhimu kwa ajili ya chakula cha siku ile. Wazo lilikuwa kumpikia chakula mgeni kama atakuja mchana, lakini hakujua mgeni anakula chakula gani.

Baada ya kuzigawa pesa kwa ajili ya matumizi ya siku ile, alioga na kufungua kinywa kisha alifanya usafi wa kitanda. Ajabu wakati akiondoa mto ili atandike alishtuka kuzikuta tena noti mpya za elfu tano tano kama alizozitoa asubuhi zipo chini ya mto.

Alijiuliza zile pesa alichukua au vipi, alitandika na kuzirudisha chini ya mto, alipanda kitandani na usingizi haukuchelewa ulimchukua.
 
18
SASA ENDELEA....

Aliposhituka alitaka kuhakiki alichokiona ni kweli au alikuwa akiota alifunua tena mto na kuzikuta pesa zipo kweli. Alizitoa na kuzihesabu, hesabu yake ilikuwa ile ile noti mpya nne za elfu tano. Alijikuta akishtuka na kujiuliza iweje pesa zile azitoe kisha alipoangalia alizikuta zipo vilevile.

Wasiwasi ulianza kumjaa huenda kaka yule si mtu wa kawaida, lakini kilichomshangaza ni upole na ucheshi wake ambaye alionekana ni mtu mwenye huruma sana.

Alijinyanyua kitandani na kwenda bafuni kuoga alipomaliza kulirudi sebuleni kuangali vipindi kwenye runinga, kengele ya mlangoni ilimfanya ananyuke kwenda kufungua. Alipofungua mlangoni alikutana na kaka msamalia mwema ambaye hakuwahi kumuuliza jina japo yeye alikuwa akilifahamu lake.

"Ha! Karibu," Jeska aliachia tabasamu pana.
"Asante," ilikuwa tofauti na alivyomzoea akiwa mtu mwenye tabasamu na bashasha muda wote huku akizungumza kwa sauti ya chini na upole. Lakini uso wa mgeni ulikuwa imejaa hasira kitu kilichomtisha Jeska na kutaka kujua kulikoni.

"Karibu kaka mwema," Jeska alimkaribisha kwa mashaka kidogo.
Mgeni aliingia bila kujibu neno na kutembea taratibu mikono nyuma na kumpa mgongo Jeska aliyekuwa akimshangaa baada ya kuketi kwenye kochi alitembea taratibu mikono nyuma na kichwa amekiinamisha kuonekana mtu mwenye maweazo mengi.

Jeska alikosa la kusema na kuendelea kumsindikiza kwa macho huku akiwa hajui kuna nini, alikwenda kusimama mbele ya ukuta na kutazamana nao bila kugeuka alimwita Jeska.

"Jeska," sauti nzito ambayo hakuwahi kuisikia masikioni kwake ilimwita.
"A..a..be..e..e." Jeska alijibu kwa kubabaika huku mapigo ya moyo yakimwenda kwa kasi kutokana na hofu iliyomshika moyoni.
"Kwanini hunisikii?" Mgeni alimuuliza akiwa bado amempa mgongo.

"Sa..sa..sa..mahani."
"Jeska kwa nini unataka kujiua?"
"Sa..sa..mahani... kaka."
"Hujanijibu, unaniomba samahani ya nini?"
"Nina matatizo yasiyokwisha."

"Una matatizo gani?"
"Sina mtu wa kuyaongoza maisha yangu toka kifo cha baba nimebakwa na niliyekuwa namtegemea amefariki."
"Jeska."

"A..a..be."
"Nilikuambia nini?"
"Nisijiue."
"Hapana Jeska la kwanza kabla ya kukueleza hili?"
"Utanisaidia."

"Sasa kwa nini unakaidi ninachokueleza?"
"Nisamehe nimekosa sirudii tena," Jeska alimfuata mgeni na kupiga magoti nyuma yake kwa vile uso wake alikuwa ametazama ukutani.

"Nimeniomba msamaha mara ngapi?"
"Najua nimekosa mimi ni kiumbe dhaifu nahitaji kusamehewa."
"Jeska ni matatizo gani umeyapata baada ya kifo cha mzee Ezekiel?"

"Sijapata ila ni wasiwasi wa moyo tu."
"Au hupendi msaada wangu nikuache ujiue?"
"Hapana kaka, wewe ni kiumbe muhimu maishani mwangu naomba usiniache."
Mgeni aligeuka na kumnyanyua Jeska aliyekuwa amepiga magoti kuomba msamaha.

"Basi nyanyuka," ajabu sauti ile ilibadilika na kuwa sauti aliyoizoea ya chini yenye upole.
Jeska alishtuka kuuona uso wa mgeni umejaa machozi na fulana yake imelowa kwa machozi.

Mgeni alimvutia kifuani kwake huku mikono yake laini ikimpigapiga taratibu mgongoni na kumfanya Jeska asisimke.

"Pole sana Jeska najua umekata tamaa lakini nakuhakikishia kukusaidia na kukulinda kama nilivyokuahidi awali."

"Nashukuru kaka mwema , samahani lakini wewe ni nani?"
"Kwa nini ya muhimu hutaki kufanya unataka kunijua?"
"Kutokana na matukio ninayo kutananayo naomba uniweke wazi ili nijue niliyenaye si wa ndotoni bali wa kweli.

Matukioni ninayokutananayo huona kama nipo ndotoni yasiyo na ukweli."
"Kwa jina naitwa Lakashi."
"Mmh, jina zuri sana."

"Asante, ningependa nawe siku moja uitwe Lakashina."
"Jina zuri lakini mbona kama la Kihindi?"
"Kwani mimi Mhindi?"
"Ila kwa mbali kama mpemba vile?"
"Ni kweli nina asili ya arabuni, unajua maana ya majina hayo?"

"Hata."
"Lakashi ni mume mwenye huruma."
"Na Lakashina?"
"Mke msikivu."
"Kwa hiyo unataka kunioa?"

"Itabidi nifanye hivyo ili kukuondolea mawazo najua shetani wa kifo bado hachezi mbali na wewe kitu kimenifanya nisicheze mbali na wewe kuyaokoa maisha yako."

"Asante Lakashi nakuahidi sitakusaliti nakupenda sana Lakashi."
"Nashukuru Lakashina."
Walikumbatiana kwa nguvu huku kila mmoja akionesha mapenzi mazito kwa mwenzake.
 
19
SASA ENDELEA...

Siku ile Lakashi alishinda na kulala pale wakiwa kama wapenzi wa muda mrefu kwa jinsi walivyokuwa. Furaha ya Jeska ilirudi upya na kujikuta akifurahia maisha na kusahau tabu zilizomkabili.
Usiku wakiwa kitandani wamejilaza kila mmoja alilalia mto wake, Lakashi alimwita Jeska.

"Lakashina."
"Abee."
"Napenda uniitikie rabeka saidi yangu."
"Rabeka saidi yangu."
"Swadakta, ni hivi japo hatujakaa pamoja muda mrefu sikupenda tutengane kwa sasa."
"Kwa nini unasema hivyo mpenzi?"

"Muda wangu wa kukaa na wewe ulikuwa bado kwa vile nina safari ya mbali ambayo itaniweka mbali nawe kwa muda mrefu."
"Lakashi safari gani hiyo? Na unasafiri lini?"
"Usiku huu natakiwa nisafiri, kilichonifanya leo niwe karibu ni kutokana na dhamira yako mbaya. Nimerudi kukuhakikishia kuwa nipo kwa ajili yako na kila nililokuahidi kukusaidia nitafanya hivyo.

Japo sitakuwepo lakini nakuhakikishia kukurudishia vyote vilivyochukuliwa na baba zako wadogo."
"Lakashi mpenzi wangu wewe ni nani, mwanasheria au mpelelezi?"
"Mimi ni mtu wa kawaida ila ni mtetezi wa haki za watu."
"Sasa utaipataje?"

"Hiyo kazi niachie ila kuna kitu nilisahau kukuambia kuhusu mama Edna, sasa hivi hali yake ni salama."
"Lakashi umejuaje?"
"Lakashina huu si wakati wa kuulizana ni kukujulisha usichokijua, ila nakuonya kitu kimoja usiende kwa kina Edna kufanya hivyo ni kosa kubwa ambalo utalijutia maishani kwako."

"Kwa nini Lakashi?"
"Unajua vizuri kuliko mimi."
Majibu ya Lakashi yalimfanya Jeska abakie kimya asihoji lolote, Lakashi aliongeza kusema;
"Lakashina unafahamu kabisa kifo cha mzee Ezekiel kinatokana na yeye kutoka kwako, uongo?"

"Kweli."
"Sasa unataka kwenda kufanya nini? Pia unakumbuka ulipokutana na Edna alipokuelezea ukamuone mama yake alikuwa mahututi hukuonesha ushirikiano kama kweli familia ile ilikulea. Leo ukienda utawaambia nini?"
"Basi Lakashi nimekuelewa."
"Tuachane na hayo la muhimu usiku huu ni kufunga ndoa ya mimi na wewe kuwa mke na mume."

"Lakashi tutafungaje ndoa ya watu wawili bila shehe wala padri?"
"Lakashina unakubali mimi niwe mumeo?"
"Hilo halina shaka."
"Hujajibu, nakuuliza tena unakubali Lakashi kuwa mumeo?"
"Nakubali."

"Lakashina hujanijibu vizuri, ngoja nikufundishe, mimi Lakashina nakubali Lakashi kuwa mume wangu."
"Mimi Lakashina nakubali Lakashi kuwa mume wangu." Jeska alirudia kama alivyoelekezwa na Lakashi.
Lakashi alirudia kumuuliza Jeska mara tatu naye Jeska alijibu mara tatu, baada ya hapo usingizi ulimpitia Jeska.

Usiku wa manane Lakashi alimuamsha Jeska kumuaga.
"Mahabuba amka nikuage muda huu ni muafaka wa kuondoka, ila sijui lini nitarudi lakini nakuhakikishia ukiwa na shida na mimi, utaniota ndotoni nami nitatokea na kukufariji kwa lolote utakalo."

"Lakashi ndotoni utanitokea vipi nawe haupo?"
"Niamini kwa hilo, kesho kuna mtu atakuletea pesa za matumizi"
"Mmh Haya! Nakutakia safari njema."
"Asante, ila nakuomba kitu kimoja kuanzia tulipofunga ndoa jina lako ni Lakashina usikubali kuitwa Jeska na wewe sasa hivi ni Muislamu."
"Jamani nitaweza masharti ya dini?"

"Si ngumu utayaweza tu, kuanzia leo vaa nguo za heshima usinywe pombe."
"Nitajitahidi."
"Kwa heri mpenzi."
"Nikusindikize."
‘Hapana usiku ni mkubwa wee lala."
Jeska alimvutia kifuani Lakashi kwa muda machozi yalimtoka kisha alimtazama usoni na kusema;

"Kwa heri mume wangu, nakuomba uwahi kurudi nina imani wewe ndiye mwanaume wangu sahihi. Kwa nini hukusubiri urudi ili tufanye hili?"
"Ni kweli usemacho dhamira yako mbaya ndiyo iliyosababisha yote haya, la muhimu zingatia, nikirudi nakuhakikishia kukupa maisha nusu ya peponi."
"Kwa heri mpenzi wangu, nakuahidi kufanya kila ulilonieleza."

Lakashi alimuaga Jeska na kutoka nje, Jeska alibakia amekaa kitandani hata usingizi ulivyompitia hakujua. Aliota yupo kwenye harusi kubwa ambayo hakuwahi kuiona katika maisha yake yote. Yeye akiwa bibi harusi aliyepambwa na kupambika na Lakashi akiwa bwana harusi. Katika harusi hiyo alivishwa pete ya almasi na mkufu wa dhahabu wenye jina la Lakashina.

Alipozinduka asubuhi alijikuta amelala kitandani kwake shingoni kulikuwa na mkufu wa dhahabu na mkononi pete ya almasi alishtuka.
 
20
SASA ENDELEA...

Jeska aliishangaa pete ya almasi na mkufu wa dhahabu wenye jina la Kashina, alijiuliza ndoa ile kaifunga saa ngapi, mbona alikuwa kwenye njozi na kuota yupo kwenye ndoa lakini ajabu asubuhi kajiona akiwa na vitu alivyoviona ndotoni.

"Mmh, hii ina maanisha nini? Au? Hapana bwana huyu huenda ni Jini haiwezekani. Mungu wangu kama nimefunga ndoa na jini itakuwaje...Eeh Mungu nisaidie mimi." Jeska alisema kwa sauti ya chini huku mkono mmoja kashikilia kifuani.

"Mmh, kama kweli sijui nitakuwaje?...Mbona kaniaga sijui anakwenda wapi na atarudi lini? Na...na...na nini hatima ya maisha yangu...Mmh! Ngoja tuone!"

Jeska alijinyanyua kuelekea bafuni kuoga, alijimwagia maji kujitoa uchovu baada ya kuoga alisimama mbele ya kioo kikubwa kujitazama. Juu ya ziwa la kushoto alishangaa kuona kuna maandisha rangi ya dhahabu yenye kumeremeta yaliyokuwa yameandikwa Lakashina.

Ilikuwa ajabu ya mwaka kuona maandishi yakimeremeta kama ndani ya mwili wake kuna taa. Alijaribu kufuta kwa mkono sehemu iliyokuwa na maandishi, vidole navyo vilianza kumetameta na hatimaye alijiona mwili mzima ukimetameta na sehemu yenye jina likimeta zaidi.

Kwa mshtuko alijikuta akianguka chini na kupoteza fahamu, aliposhtuka alijikuta amelala kitandani. Alijishangaa na kujiuliza maswali yasiyo na majibu juu ya kilichomtokea, pete ilikuwa kidoleni na mkufu ulikuwa kwenye droo ya kitanda. Aliiangalia pete iliyokuwa na uzuri wa ajabu lakini hakujua ni madini gani.

Alipotupa jicho pembeni lilitua kwenye mkufu uliokuwa na jina lake, aliubeba na kuutazama na kulisoma jina na kuurudisha kwenye droo ya kitanda. Alikwenda tena bafuni kuoga ili aende mjini kwa sonara kuulizia ile pete ni ya madini gani na mkufu una thamani gani.

Baada ya kuoga alisimama tena mbele ya kioo kuangalia alichokiona kilikuwa kweli au ndoto. Jibu lilikuwa lile lile kwenye ziwa la kushoto kuna jina lililoandikwa kwa maandishi ya dhahabu yenye kumetameta. Hakutaka kuhangaika nayo, alirudi chumbani na kubadili nguo ili awahi mjini.

Kutokana na maandishi yale aliona aibu kuvaa nguo alizozizoea za mikanda na matiti nje. Ilibidi avae za kujistiri mwili ili kuogopa watu kumuona kituko. Alipotoka sebuleni alikutana na mfanyakazi wake wa kike akiwa katika gauni lililonakshiwa uzi wa halili.

Alipomuangalia alishtuka, lakini Sara hakuonekana kushtuka.
"Za asubuhi Sara?"
"Nzuri tu dada Lakasina."
"Wee Sara umeniitaje?"

"Lakashina au ulitaka nikuite Mrs Lakashi."
"Nani kakutajia jina hilo?"
"Dada wewe mwenyewe jana kwenye harusi ulitueleza tusikuite tena Jeska bali Lakasina."

"Mmh! Haya."
"Safari ya wapi asubuhi asubuhi?"
"Nafika mjini mara moja."
"Ni kweli shemeji amesafiri jana usiku?"

"Ni kweli wewe umejuaje?"
"Dada Lakashina mbona kila kitu kwako kigeni au jana ulikuwa unatutania si jina lako?"
"Ni kweli langu."

"Sasa tatizo nini au tuendelee kukuita ulilolizoea la Jeska?"
"Hapana, kama umeweza kulishika hili jipya ni vizuri."

Jeska wakati anajiandaa kutoka kengele ya mlango ililia, alimruhusu aingie alikuwa mlinzi wa mlangoni aliyekuwa amevaa suruali nyeupe na shati jeupe lenye maua shingoni, mikononi na pembeni.

Juu alivalia kikofia kidogo chenye maua kama ya kwenye shati na suruali, miguuni alivaa makubazi.
"Mnyalu leo umevaaje?"

"Dada si unajua tumerudi muda mbaya kutoka kwenye sherehe, nikaona niendelee na kazi zangu baadaye nitabadili."

Maneno ya Mnyalu yalizidi kumchanganya na kujiuliza hiyo harusi wao waliijuaje wakati yeye muolewaje ameifunga kwenye njozi. Hakutaka kumshangaa sana, aliona kushangaa kumemchosha kila aliposhangaa walimshangaa yeye.

"Vipi Mnyalu ulikuwa unasemaje?"
"Kuna mgeni."
"Anatoka wapi?"
"Sijamuuliza ila alitaka kukuona."

"Mwanamke au mwanaume?"
"Mwanaume."
"Mwambie apite ndani."

Mnyalu alitoka na baada ya muda alirudi na mgeni aliyekuwa amevalia nguo kama za Mnyalu zilifanana kwa kila kitu hata makubazi aliyovaa. Wazo la haraka alijua ndugu yake Mnyalu.
"Karibu."

"Asante, habari za hapa?" Mgeni alimsabahi huku akimpa mkono Lakashina (Jeska).
"Nzuri," Lakashina alimtazama mgeni aliyekuwa amekaa kwenye kochi ameshikilia mfuko mdogo.

"Pole na pilikapilika za jana usiku?"
"Nn...nn...nzuri," kauli ile ilimshtua na kujikuta ni yeye peke yake aliyehudhuria ndoa yake kwenye njozi tofauti na wote waliohudhuria kama kawaida.

"Mbona kama hujiamini?"
"Aa...aa...kawaida."
"Nina imani una taarifa yangu?"
"Ipi?"

"Kutoka kwa Lakashi"
"Yupo wapi?" Lakasina alishtuka kumsikia Lakashi.
 
21
SASA ENDELEA...

"Kivipi?"
"Mnasema jana kulikuwa na harusi yangu na Lakashi mbona mimi sijui?"
"Shemu hizi piko umechorwa kwa ajili ya nini?"
"Mmh! Tuachane na hayo, karibu."
"Asante."

Mgeni aliketi kwenye kochi na kutulia huku akipepesa macho kila kona ya nyumba ile.
"Mmh! Shemu karibu."
"Asante."
"Unatumia kinywaji gani?"

"Hapana mi si mkaaji niliagizwa nilete huu mzigo mara moja," mgeni alisema huku akikabidhi mkoba wa ngozi uliokuwa wa saizi ya kati.
"Asante, na...na...," Lakashina hakumalizia alichotaka kuuliza.
"Uliza tu shemeji."

"Lakashi kaenda wapi?"
"Shemeji wewe mke wake usijue nitajua mimi?"
"Na atarudi lini?"
"Bado hilo ni swali gumu kwangu kwa vile siri ya mtu humpa mkewe."

"Asante," Lakashina hakutaka kuuliza kitu kutokana na kumuona mgeni hajui lolote zaidi ya kuleta mzigo alioelezwa na mumewe ambaye yeye anaamini ni wa ndotoni.

"Lakashi alinieleza nikueleze kuwa, tafadhali mkoba huo usiufungue, ukitaka pesa ingiza mkono na kuchukua kiasi chochote utakacho."
"Kwani una shilingi ngapi?"

"Siwezi kujua ila kanieleza usiufungue huo mkoba wewe chukua kiasi chochote ukitakacho."
"Hata milioni?"
"Si milioni tu hata zaidi ya milioni."

"Kwa hiyo hata kununulia nyumba na gari."
"Chochote kasoro pombe na nyama ya nguruwe."a"Mmh!"
"Pia alinieleza kuwa usihame nyumba hii mpaka atakaporudi."
"Sawa nimekuelewa."

"Kingine amesema hivi haina haja ya kwenda kwa sonara kuijua thamani ya vito alivyokuvisha siku ya harusi yenu. Kwa vile vina thamani kubwa kuliko mtu utakaye mpelekea. Kibaya zaidi tamaa yao itakusababishia matatizo makubwa hata kukutoa uhai wako."
"Ha! Shemu amejuaje?"

"Amesema muhimu ni kufuata maelekezo na si kujua amejuaje."
"Sawa shemu, nimekuelewa."
"La muhimu kuzingatia yote kama utakwenda kinyume utajiingiza kwenye matatizo ya kujitakia."

"Nimekuelewa."
"Nikuache, vipi unatoka?"
"Hapana."

Mgeni aliaga na kuondoka huku Lakashina akibakia na maswali juu ya yale aliyoelezwa. Alijiona kama mtu aliyetembea uchi wakati kavaa nguo kutokana na Lakashi kumfahamu kila alilokuwa akiwaza. Alijikuta akijiuliza Lakashi ni nani. Aliubeba mkoba wake na kwenda kuuweka chumbani ndani ya kabati na safari ya kwa sonara ilikufa.
***
Maisha ya Lakashina yalibadilika ghafla ya kujikuta akiishi maisha mazuri na ya kifahari. Alinunua magari ya kifahari ya kutembelea, nyumba aliyokuwa akiishi mwenye nyumba alimuuzia na kuwa yake. Siku moja akiwa amejipumzisha sebuleni baada ya kutoka kuswali simu yake iliita alipoangalia ilikuwa namba ngeni alipokea.

"Haloo."
"Haloo Jeska."
"Mimi siitwi Jeska."
"Mbona aliyetupa namba alituambia wewe ni mtoto wetu Jeska."
"Wewe nani?"

"Mimi Zebedayo baba yake mdogo na Jeska."
"Aah, kumbe ni ninyi, mnataka nini wakati mliyofanya sikutaka kuwapeleka kokote tafadhalini achaneni na mimi. Najua mmejua nina pesa mumeanza kunifuata tena ili mnidhurumu, lakini sasa hivi nitakufa kwa mali yangu."
"Siyo hivyo Jeska."

"Siitwi Jeska naitwa Lakashina."
"Hilo jina kama la Kihindi au umebadili dini?"
"Ndiyo."

"Sasa ni hivi tunaomba utupe muda ili tuikusanye mali yako tukukabidhi."
"Muikusanye ili iweje? Nimewafuata kuwaomba?"
"Hapana mama, ile ni mali ya wazazi wako lazima tukurudishie wewe mwenyewe."

"Mliponinyang'anya si mliona ni haki yenu na kunitishia kuniua sasa mnanitaka nini tena?"
"Hapana mama tupo chini ya miguu yako, tunakuomba tukurudishie mali yako."

"Sipo tayari kuipokea nimewaachieni, endeleeni na maisha yenu nami niacheni niendelee na maisha yangu."
"Jeska, ooh, samahani Lakashina, tunaomba uipokee tupo chini ya miguu yako."

"Jamani niwaeleze mara ngapi kuwa mali hizo sina shida nazo, ni miaka mingapi imepita, hamkujua nimeishi maisha gani, hamkunionea huruma mwana yatima baada ya uchungu wa kifo cha wazazi wangu ninyi ndiyo mliotakiwa kunitunza kwa vile tayari wazazi wangu waliacha mali. Lakini kwa tamaa zenu mlinitupa na kunitishia maisha yangu.

Sikwenda polisi wala mahakamani nilimshtakia Mungu, leo hii mmekumbuka nini? Naomba muachane na mimi, " Lakashina alikumbuka mambo mengi ilikuwa sawa na kuchubua kovu lililokuwa limepona. Alijikuta akishindwa kuzungumza na kuangulia kilio.
 
22
SASA ENDELEA...

Simu ile ilimtia hofu Lakashina kuona muda si mrefu mali zake zitachukuliwa na baba zake wadogo, aliizima simu ili wasiendelee kumsumbua. Wazo la haraka lilikuwa kutoiwasha mpaka atakapobadili namba ya simu. Alijiuliza ni nani aliyempa namba yake ya simu.

Akiwa bado anatafakari kuhusiana na simu za ndugu wa baba yake watu ambao kwake aliamini ni maadui na kuapa kutowasamehe mpaka anaingia kaburini, simu yake iliita tena, alishtuka na kuamini kabisa labda hakuizima, hakuipokea mpaka ilipokata. Aliichukua ili aizime lakini cha ajabu simu ilikuwa imezimwa, aliiangalia mara mbili na kuhakikisha ameizima.

Haukupita muda simu iliita tena, alishtuka na kuitazama kwa muda akijiuliza ni kweli au anaota. Iweje simu aizime itoe mlio wa kuita huku ikitetemeka kama haikuzimwa.
Japo miujiza aliianza kuizoea lakini ule kidogo ulimtisha, hakutaka kuipokea aliitazama iite mpaka inyamaze yenyewe. Lakini simu haikunyamaza iliendelea kulia kwa muda mrefu. Kila muda mlio uliongezeka na kufanya hahisi ngoma za masikio kutaka kupasuka. Aliamua kuipokea na kusema kwa sauti ya juu.
"Nimesema sitaki."

"Sikiliza Lakashina," sauti ya upande wa pili ilikuwa nzito iliyoufanya moyo wake kwenda mbio.

"Siwezi kukusikiliza nimewaambia sizitaki hizo mali nani kawaomba?"
"Wampelekee nani?"
"Watajua wenyewe."
"Lakashina naomba ufuate maelekezo yangu," sauti ile nzito iliyokuwa ikijirudia kama kwenye mwangwi ilimchanganya na kuamini lile ni jambazi lilitumwa kuchukua mali zake. Kutokana na kutetemeka kwa hofu iliyomjaa moyoni simu ilimponyoka, lakini sauti ile iliendelea kusema na kuonekana kutawala chumba kizima;
"Lakashina hofu ya nini?"

"We...we...eee nani?" Aliuliza kwa kitetemeshi.
"La muhimu sikiliza maelekezo yangu, washa simu na kubaliana nao kuhusu kurudishiwa mali zako, ni halali yako wala usimuonee huruma mtu yeyote. Kama wao hawakukuonea huruma basi nawe usiwaonee huruma hata kidogo."
"La...la...kini...we...e...we...e nani?" Lakashina aliuliza kwa hofu.
"Lakashinaaa, nikueleze mara ngapi usipende kuuliza, fuata maelekezo yangu washa simu."

"Wewe ni nani, Lakashi?"
"Huwezi kunijua kutokana na hofu iliyokujaa moyoni, la muhimu chukua mali yako. Lakashina washa simu...washa simu."
Sauti ile ilipotea taratibu huku ikijirudiarudia ikitoka katika uzito na kuwa nyepesi iliyokuwa kama ikimbembeleza Lakashina aliyepitiwa na usingizi, mfanyakazi aliyekuwa amemtuma aliporudi alimkuta amesinzia.
"Dada...dada."

"Mmh."
"Vipi?"
"Aah, kwani vipi?"
"Naona umelala huku ukitabasamu na kutikisa mguu unaota upo kwenye muziki nini?"
Lakashina aliposhtuka, alimuangalia mfanyakazi aliyekuwa amerudi toka dukani alipomtuma.

"Dada vipi mbona kama unanishangaa?"
Kabla ya kumjibu aliitazama simu yake aliikuta imezimwa, alimtazama Sara aliyekuwa amesimama mbele yake akimtazama. Alijinyoosha na kupiga miayo kisha alimuuliza.

"Eti Sara umekuja saa ngapi?"
"Mmh, muda ila mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani ikanibidi nisubiri labda una kazi zako, baada ya muda mlango nilisikia ukifunguliwa na kujua umemaliza shughuli zako. Nilipousukuma niliukuta upo wazi, lakini cha ajabu nimekukuta umelala mkono kifuani ukitabasamu na mguu ukiuchezesha."
"Sara unasema kweli?"
"Kweli, kwani vipi?"

"Mmh, tuachane na hayo, ulipokuwa nje hukusikia sauti yoyote?"
"Mmh, palikuwa kimya kama nyumba haina watu, kama usingenituma au mtu angekuja siku ya kwanza angeamini nyumba haina mtu. Kilichonifanya niamini kuna mtu, muziki wa kiarabu unaopenda kuupiga."

Lakashina alitulia kwa muda akitafakari ya nyuma kabla hajatokewa na sauti ya ajabu ndani ya simu aliyoizima baada ya kukerwa na kauli za baba zake wadogo kutaka kumrudishia mali zake walizomdhurumu muda mrefu na kumtishia kumuua. Lakini sauti ya ajabu ilimsisitiza awashe simu.
"Dada upo sawa?" Sara alimuuliza.

"Nipo sawa, ila kuna watu wanataka kunichanganya...," alinyamaza ghafla baada ya simu kuita tena, si yeye hata Sara aliiona, lakini ilikatika. Hakusema kitu aliichukua simu ile na kuiwasha. Baada ya kuiwasha hazikupita hata sekunde kumi iliita kwa mlio aliouzoea. Aliipokea kwa unyenyekevu.

"Haloo," alisema huku akimuonesha kwa ishara Sara atoke nje, Sara alitekeleza bila kuhoji.
"Haloo Lakashina tupo chini ya miguu yako tunaomba tukurudishie mali zako, tunakuomba utuombee msamaha vitu vingine hatuna."
"Jamani mbona siwaeleweni niwaombee msamaha kwa nani?"
"Kwa mumeo."

"Mume wangu? Nitawaombea vipi naye kasafiri?"
"Atarudi lini tunateseka tuonee huruma, mateso tunayopata ni makubwa."
"Mateso gani?"

Hali inachanganya, kwa nini ndugu wa marehemu baba yake wanarudisha mali, na mateso gani wanayopata?
 
Back
Top Bottom