Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,638
MTUNZI : ERIC SHIGONGO
MWANZO
HALI ya hewa ilikuwa ya baridi kali, kwa kipindi hicho cha mwezi Machi, ilikuwa ni hali ya kawaida kwa eneo hilo kuwa na baridi. Watu walikuwa wengi sokoni wakiendelea na shughuli zao kama kawaida.
Soko hilo lililopo eneo la Shokoni, Marangu, mkoani Kilimanjaro ni maarufu sana kwa uuzaji wa mazao mbalimbali.
Wilson Johnson, mzungu kutoka nchini Marekani akiwa na wenzake Joel Poulsen na David Robert walikuwa kijijini hapo kwa kazi moja tu; kumtafuta msichana mrembo ambaye wangesafiri naye hadi Marekani kwa ajili ya kwenda kwenye shindano la kumsaka msichana atakayecheza sinema iitwayo Sweet Pain. Ilikuwa ni kampeni ya Afrika nzima, walisambazwa mawakala mbalimbali kwa ajili ya kutafuta wasichana ambao wangeshindanishwa na mwisho mshindi angecheza sinema hiyo.
Ilikuwa ni kazi ngumu sana kumpata msichana mwenye sifa zilizohitajika. David Robert ambaye alikuwa ni Mtanzania aliyeishi nchini Marekani, ndiye alikuwa mwenyeji wa wageni wake hao maana wote walikuwa ndio mara ya kwanza kufika nchini Tanzania.
Walianzia jijini Tanga, Mwanza kisha baadaye wakaelekea mkoani Mbeya bila mafanikio yoyote. Wakiwa jijini Dar es Salaam tayari wamekata tamaa kabisa, David ndiye aliyetoa wazo la kwenda kijijini huko Marangu ili kujaribu bahati.
Wapo sokoni wakiangaza macho huku na huko na mara nyingi wale wazungu walikuwa wakiguna, wakisema kwamba hakuna uwezekano wa kumpata msichana mwenye vigezo kijijini hapo.
“Oh! Look, can't that girl be suitable for us?”
(Oh! Angalia, yule msichana hawezi kutufaa kweli?)
Wilson Johnson alisema akisonza kidole kuonesha mahali msichana aliyevaa nguo kuu-kuu akipita na kapu lake lenye bidhaa.
“My God! I can't believe my eyes, I do not remember when I can across a beautiful girl such as this one.
I think our mission has come to the end.
We have to talk to her right away!” (Mungu wangu! Siamini macho yangu, sikumbuki kama niliwahi kukutana na msichana mrembo kama huyu.
Nadhani safari yetu inaelekea ukingoni.
Ni lazima tuongee naye sasa hivi!)
Joel Poulsen akadakia. “David make sure you talk to the girl right now!”
(David hakikisha unaongea na yule msichana sasa hivi!) Wilson alimwambia David.
“Okay sir, I will do so.” (Sawa,nitafanya hivyo.)
Mara moja David akachepuka akimkimbilia yule msichana. Kwa kumtazama alionekana mrembo sana, lakini alikuwa amevaa nguo za hadhi ya chini kabisa.
David akachanganya miguu hadi alipomfikia sehemu aliyokuwa amesimama akinunua nyanya.
Alipofika alisimama nyuma yake, akimuacha amalize alichokuwa akikifanya kisha akamgusa bega na kumwambia: “Samahani, samahani sana!”
“Unasemaje?”
“Usinifikirie vibaya binti, mimi ni mtu mwema kwako na nina jambo zuri sana nataka kukushirikisha!”
ITAENDELEA