HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)

HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,662
Image may contain: 1 person, hat and text



HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)
SEHEMU: 01
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
SIMU: 0713 646500

REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)

Waumini wa kanisa wote walikuwa kimya wakiendelea kumsikiliza msichana Rebeka aliyekuwa akitoa ushuhuda kwa yale yote aliyoyafanya ambayo yaliyomfanya kila mmoja abakie kinywa wazi wengine bila kutegamea walibubujikwa na machozi.
Baada ya ushuhuda wake wengi waliangua kilio kilichomshtua kila mmoja aliyekuwa mule kanisani wengi wao walikuwa wake za watu walisikika wakisema:
"Oooh! Masikini tumekwisha."
Wengi wao waligaagaa chini kwa kilio cha majuto kwa kweli ulikuwa msiba mkubwa uliokuwa ndani ya kanisa uliompa kazi mchungaji amnyamazishe yupi nani amuache.
Hata waliokuwemo kanisani ilibidi wafanye kazi ya ziada kuwatuliza kina mama waliokuwa wakilia kwa kujitupa chini wengine kufikia hatua ya kujiumiza na kutokwa na damu na wengine kupoteza fahamu.
Ilikuwa ni vigumu kujua nini mahusiano ya ushuhuda wa Rebeka na wale kina mama. Rebeka ambaye alikuwa kama mtu aliyepagawa mikono kichwani machozi yalimwagika kama chemchem ya maji, alijutia kile alichokifanya pale alipojijua..... Ni swali zito kwa msomaji ili kuyajua yote tuungane na mtunzi mahili Ally Mbettu kwenye riwaya hii itakayo kusisimua muda wote na kukupa mafundisho.
*****
Ilikuwa siku ya jumapili Msichana Rebeka alipotumwa na mama yake aende akasanye kuni kwa ajili ya kupikia chakula cha mchana. Hali ya hewa ilitishia kwani kulikuwa na hali ya mawingu iliyoashilia muda wowote mvua itanyesha.
Rebeka alikwenda msituni kuokota kuni huku akimuomba mwenyezi Mungu mvua imuchie kwanza ili aokote kuni kwanza ndio inyeshe. Kutoka kwao hadi msituni ni mwendo wa dakika kumi hadi robo saa.
Akiwa ameshikilia panga mkononi kipande cha kamba na kanga chakavu kwa ajili ya kuwekea ngata ya kubebea kuni. Kila hatua aliyopiga ndivyo wingu lilivyozidi kuwa zito mpaka kuanza kuweka kiza. Lakini hali ile haikumzuia Rebeka kwenda kuokota kuni.
Alifanikiwa kufika msituni bila mvua kudondosha tone la maji na kuanza kuokota kuni ambazo zilikuwa na chache kitu kilichomfanya aingie ndani zaidi ya msitu. Kuni zenyewe zilikuwa moja moja hivyo ilimpa kazi sana kupata mzigo mkubwa.
Akiwa bado anaendelea kutafuta kuni ghafla iliteremka mvua nzito iliyoambatana na upepo mkali. Ukali wa upepo ulimfanya Rebeka ajibanze nyuma ya mti mkubwa ili kusubiri mvua ipungue.
Mvua iliendelea kwa muda wa masaa mawili bila kukatika hata ilipokatika muda ulikuwa umeisha kwenda sana.
Rebeka alikusanya zile kuni zake chache alizookota, lakini zilikuwa zimetota maji ya mvua. Alikuwa hana jinsi alizibeba hivyohivyo na kurudi nazo nyumbani akiwa anatetemeka kwa baridi kali kutokana na nguo zake kulowa na mvua.
Alirudi huku akiwa na hasira za kunyeshewa na mvua na kuni alizozifuata hakuzipata na chache alizopata zilikuwa zimeloweshwa na mvua ambazo zilikuwa hazifai kwa kupikia siku ile. Kibaya zaidi ndani hapakuwa na kuni za ziada za kupikia siku ile.
Alirudi nyumbani akiwa amefura kwa hasira hasa akizingatia asubuhi kifungua kinywa alichokipata kilikuwa cha mkono mmoja alitegemea mchana angalau angedanganya tumbo.
Taratibu aliliacha poli na kuingia sehemu za makazi ya watu huku akiwa amebeba kuni zake chake huku akitetemeka kwa baridi aliona amecheza pata potea kuni hakupata na mvua imemnyeshea.
Akiwa anaelekea maeneo ya nyumbani kwao kabakiza kama nyumba kumi afike kwao alishangaa kusikia jina lake likitajwa tena lile la utani ambalo alikuwa akitaniwa shuleni. Ilimshangaza kwani ilikuwa imeishapita miaka mitatu toka amalize elimu yake ya darasa la saba.
Jina lile lilifia shuleni kibaya zaidi shule aliyokuwa akisoma ni ya kijiji cha sita toka kijijini kwao. Elimu ya msingi aliomea kwa baba yake mkubwa ambaye alimchukua kwa wazazi wake akiwa na miaka sita. Alikuwa na imani pale kijijini hakuna aliyekuwa akilijua jina lake la utani alilokuwa nalo shuleni.
Jina lake la utani aliitwa mama maua kutokana na kupenda kupanda maua kitu kilichopelekea kupewa cheo cha bibi afya. Kabla ya kujibu aligeuka akiwa na kuni zake kichwani kuangalia nani anaye mwita ilikuwa baada ya kumwita midomo minne bila kumjibu mpaka pale alipomtaja jina lake halisi la Rebeka.
Alipogeuka alikutana na mtu ambaye waliachana miaka minne iliyopita ni mmoja wa wanafunzi wenzie lakini alikuwa amemzidi darasa moja. Kabla ya kumaliza yule kijana alikuwa ni kaka mkuu wa shule, alipomfahamu ni nani alitabasamu kwa kumtaja jina lake.
"Aaaah Mabogo!" Rebeka alisema huku akishika mdomo.
"Siamini ni wewe Rebeka mama maua!" Mabogo alisema huku akimchanulia tabasamu pana.
"Ni mimi Mabogo za siku?"
"Nzuri."
"Mmh, na huku unafanya nini?"
"Nikuulize wewe?"
"Mimi huku ndipo kwa wazazi wangu na ndipo nilipozaliwa."
"Hata mimi ni kwetu ila sikukulia huku."
"Umenenepa upo wapi mbona sijakuona hapa kijijini?"
"Nipo mjini tunaganga maisha."
"Hata mimi naona shepu za mjini zinaonekana, shavu dodo!"
"Aaaah kawaida...kwanza pole na mvua ina maana mvua yote imekuishia mwilini?" Mabogo alimuuliza kwa sauti ya huruma.
"Mabogo iishie wapi haya ndio maisha yetu ya kijijini kama mbuzi mbele kamba nyuma kiboko."
"Pole sana."
"Mabogo siwezi kusema asante kwa sababu bado hali hii naendelea nayo wala sina daliliza kujikomboa."
"Samahani Rebeka umeolewa?"
"Niolewe wapi maisha yenyewe kama haya ukimbilie kuolewa si ndio ungekutana na mimi na kunipa shikamoo....Umeisha muona Zawadi?"
"Bado."
"Ukimuona utamsahau mpaka sasa ana watoto wawili na mimba juu ukimuona kama gari zetu za shamba za spilingi kufungia mti wa muhigo najua utajua ni jinsi gani alivyochoka mdomoni kabakia na meno mawili yote yameisha kwa kipigo mumewe mlevi mbwa."
"Una mpango gani na maisha yako?"
"Nikipata nakula nikikosa na lala."
"Sasa Rebeka nisikuweke sana najua kibaridi kinakichonyota nenda nyumbani ila jioni baada ya shughuli zako zote naomba tuonane."
"Nikipata muda, hapa najua siwezi kwenda popote kwa kuwa kuni za kupikia hakuna hivyo lazima nikitoka nitaulizwa ingekuwanimeisha maliza kazi zote na wazazi wangu kwenda kwenye kinywaji hapo huwa na uhuru mkubwa."
"Unataka kuniambia kuni hizi ndizo za kupikia?"
"Nikwambie mara ngapi Mabogo yaani mvua leo imejua kunitenda."
"Basi usihofu nitakusaidia kuni maana jana kama tulijua kulikusanya kuni nyingi kwa ajili ya kuziuza si unajua mdogo wangu ana miradi yake."
"Sasa Mabogo si kuni za biashara?"
"Ndio za biashara lakini nitakulipia mimi."
"Acha tu Mabogo sipendi uhalibu bajeti yako."
"Bajeti nitakuwa nayo mimi na serikali watasemaje...Kwanza Rebeka leo nimefurahi sana kukuona, pokea msaada wangu ili leo mpate kupika chakula cha mchana msaada wangu si kwako tu hata kwa wote walio nyumbani."
"Sawa Mabogo nitashukuru kumbe roho yako ya upendo na huruma ujaiacha."
"Hata wewe msimamo wako haujauacha kweli nimeamini u mwanamke wa shoka imeonyesha jinsi gani pamoja na elimu yako ya msigi lakini amekuwa na upeo wa kuona mbele."
Mabogo aliingia ndani na kutoka na mzigo wa kuni aliomkabidhi, Rebeka alishukuru na kuondoka huku akimuahidi kurudi baadaye.
 
HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)
SEHEMU: 02
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
SIMU: 0713 646500

ILIPOISHIA:
"Bajeti nitakuwa nayo mimi na serikali watasemaje...Kwanza Rebeka leo nimefurahi sana kukuona, pokea msaada wangu ili leo mpate kupika chakula cha mchana msaada wangu si kwako tu hata kwa wote walio nyumbani."
"Sawa Mabogo nitashukuru kumbe roho yako ya upendo na huruma ujaiacha."
"Hata wewe msimamo wako haujauacha kweli nimeamini u mwanamke wa shoka imeonyesha jinsi gani pamoja na elimu yako ya msigi lakini amekuwa na upeo wa kuona mbele."
Mabogo aliingia ndani na kutoka na mzigo wa kuni aliomkabidhi, Rebeka alishukuru na kuondoka huku akimuahidi kurudi baadaye.
SASA ENDELEA…
****
Rebeka baada ya kazi zake zote alizopangiwa kuzifanya alizifanya kwa haraka na kwa umakini ili asije ulizwa kwa nini hakumaliza kazi. Muda wa wazazi wake ulipotimu wa kuelekea kilabuni alimuuliza mama yake:
"Mama kuna kazi gani nyingine?"
"Leo mwanangu umenifurahisha pumzika na chakula cha usiku nitakusaidia."
"Asante mama."
Baada ya wazazi wake kuondoka Rebeka alisubiri kwa muda wa robo saa ndipo alipo anza safari ya kwenda kwa Mabogo ili akajue amemwita amweleze nini au ndio anataka kumtafutia kazi ya utumishi wa ndani. Kwake ilikuwa sawa kwa vile maisha ya kijijini yalikuwa yamemchosha kila siku alikuwa hana mapumziko kuamka asubuhi na kulala mtu wa mwisho japo kuna siku huwahi kulala lakini sio kuaka.
Alichepua mwendo jua lilikuwa ndio linaanza kuzama aliitafuta ile nyumba ili asipotee kwa sababu hakuinakili sana akilini. Bahati nzuri nyumba zilikuwa hazifanani alikumbuka eneo alilofika asubuhi na kuitwa na Mabogo na nyumba aliyotoka.
Alikwenda hadi kwenye ile nyumba huku akijiuliza maswali mawilimawili kama akitoka mzazi wake atamwambia anamtafutia nini, kwa kuwa yeye ni msichana na Mabogo ni mvulana kibaya zaidi huenda hajazoeleka pale kijijini.
Akiwa amesimama mlangoni akihema huku akijiuliza agonge au asigonge alishtushwa na mlango uliokuwa ukifunguliwa, kwa haraka alirudi nyuma na kujibanza nyuma ya nyumba na kusikilizia ni nani aliyetoka.
Alisikia watu wakiongea:
"Sasa Lyasi wacha mimi niende kwa shangazi si unajua nina siku moja nirudi mjini."
"Si ulisema una mgeni?"
"Ni kweli nimemsubiri lakini naona shughuli zimemzidi ila kama nisipoonana naye au akija asipo nikuta mwambie tutaonana nitakaporudi tena kijijini si unajua nina ahadi ya kujenga kaburi la bibi."
"Hilo nalielewa lakini kwa nini usimsubiri...unajua nini Mabogo?"
"Nitajuaje bila kuniambia."
"Yaani nashangaa yule msichana mpaka kusimama na kukusikiliza naona ajabu."
"Ajabu ya nini kwangu si mgeni vilevile sina nia naye mbaya najua ninyi labda kila mkikutana naye mnatanguliza mapenzi atakubali wangapi?"
"Kwa hiyo humsubiri?"
"Kama nilivyo kwambia nadhani unajua vizuri kelele za shangazi nikiondoka bila kumuaga atasema kwa vile baba amekufa na yeye hatumjali."
"Kweli Bro nenda."
Mabogo alianza msafara kwenda kijiji cha pili kwenda kumuaga shangazi yake. Rebeka aliyekuwa nyuma ya nyumba aliyasikia yote moyoni alijiuliza.
"Ina maana Mabogo anaondoka kesho atakuwa amekuja muda mrefu au ndio wa mjini hawapendi kukaa sana kijijini?"
Hakutaka kumshtua haraka alimwacha atangulie kidogo na mdogo wake Lyasi kuingia ndani ndipo alipomfuata kwa nyuma kwa kuchepua mwendo mpaka alipoakaribia alimponda na kipande cha udongo. Mabogo alishtuka na kugeuka nyuma alipigwa na butwaa kumkuta Rebeka.
"Ha! Rebeka ndio unafika?"
"Nimefika muda toka unaaga kuwa unakwenda kwa shangazi kuaga unaondoka kesho ina maana umekuja muda mrefu?"
"Mmh! Rebeka mbona siamini wewe hukuwepo niliyoyasema umeyajuaje, kama kuelezwa na Lyasi si rahisi kukueleza na kuniwahi hapa umejuaje?"
"Niamini Mabogo nimefika kipindi," ndipo Rebeka alipo mweleza alivyokuja na kujificha nyuma ya nyumba na yote aliyo yaongea
"Kumbe Rebeka kama ningekuwa nakusema vibaya ningeumbuka."
"Siku zote mwanadamu anatakiwa achunge ulimi wake."
"Na kweli nimeamini...Sasa Rebeka itakuwaje sasa hivi nimepanga kwenda kumuaga shangazi na nisipokwenda itakuwa tatizo shangazi yetu mtata sana."
"Kwani shangazi yako anakaa kijiji gani?"
"Kijiji cha jirani."
"Kuna ubaya tukienda wote?"
"Hakuna ubaya wasiwasi wangu kukuchelewesha."
"Nina imani ulichoniitia ni muhimu kuliko kuchelewa kwangu."
"Sipendi ukosane na wazazi wako."
"Mabogooo ina maana utachelewa sana?"
"Sidhani ni kumuaga tu na kuondoka kama nilikwenda kumjulia hali siku niliyofika na siku ya kuondoka ni vizuri nimjulishe."
"Hamna tabu tutakwenda pamoja wazazi wangu kwa muda huu hawana shida na mimi pia hata nikichelewa chakula cha usiku anapika mama zile kuni ulizonipa zimenisaidia mpaka mama kanipunguzia kazi."
"Itakuwa vizuri...tena safari yangu itakuwa nzuri isiyo na uchovu."
Safari ilianza ya kuelekea kijiji cha jirani huku kila mmoja akitafuta njia ya kuanza mazungumzo, lakini Rebeka alikuwa wa kwanza kuanzisha:
"Mabogo hujanijibu umekuja lini?"
"Leo ni siku ya tatu."
"Yaani siku tatu tu unarudi mjini?"
"Nimekuja ghafla hata kazini nimeaga siku mbili yaani alhamisi na ijumaa kwa vile jumamosi huwa hatuendi ndio maana nimepata siku nne."
"Kwani mjini unafanyakazi gani?"
"Nipo kwenye shirika la umma."
"Mmh, wenzetu mnafaidi sio sisi kila kukicha afadhali ya jana."
"Mbona kawaida tu."
"Tusidanganyane Mabogo hali ya kijijini inatisha kila kukicha wimbi la vijana kukimbilia mjni linaongezeka maisha ni magumu, kwa vile mi’ mwanamke lakini ningekuwa mwanaume na mimi ningekwisha timkia mjini."
"Usemayo ni kweli yote hii ni serikali kusahau kuboresha vijiji na kuvisahau kila kitu wao wanatazama mjini."
"Kumbe hilo unajua ulitaka kunipima akili?" Rebeka aulimuuliza huku akimtazama usoni.
"Samahani Rebeka umeolewa?"
"Mabogo ina maana wewe ni msahaulifu sana?"
"Kwa nini?"
"Asubuhi nilikujibu swali lako."
"Ooh, sorry nilipitiwa nilitaka kukuuliza una mpango gani?"
"Vile vile nilikujibu kuwa mpango wangu nikipata nakula na nikikosa nalala."
"Ni hivi nia yangu kwako sio mbaya ni nzuri tu."
"Ni gani hiyo?"
"Unaonesha ni mwanamke mwenye msimamo pia mwenye uelewa mpana japo uko kijijini, umenivutia na kukuona unanifaa katika maisha yangu."
"Utani huo Mabogo ina maana hujaoa?"
"Yaani kazi ndio mwaka wa kwanza lazima uwe makini na chaguo lako la kwanza usije lamba garasa."
"Kwa mana hiyo unataka kuniambia huna rafiki wa kike au mchumba?"
"Jibu nimeisha kujibu sitegemei kuomba kazi wakati nina kazi."
"Inategemea masirahi zaidi."
"Nina fikiri kazi ya mtu makini huwa hakurupuki kuanza kazi mpaka awe na uhakika wa masirahi mazuri."
"Tuachane na hayo ulikuwa una maana gani?"
"Nia yangu uwe mke wangu."
"Ni jambo zuri mwanamke yoyote duniani uliomba usiku na mchana, ni kweli usemayo au ndio kutaka kuuchezea mwili wangu kwa kisingizio cha kunioa lakini ukitapa ulichokitaka uniache kama wasemavyo mjini kwenye mataa."
"Nimekuelewa nia yangu ni mke si ngono suala la ngono liondoe akilini mwako tutakutana kimwili baada ya kuwa mke wangu wa halali."
"Siamini maneno yako, kweli wewe ni mwanaume wa kwanza kutotanguliza ngono mpaka siku ya ndoa yetu."

Nini Kitaendelea?
 
HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)
SEHEMU: 03
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
SIMU: 0713 646500

ILIPOISHIA:
"Ni jambo zuri mwanamke yoyote duniani uliomba usiku na mchana, ni kweli usemayo au ndio kutaka kuuchezea mwili wangu kwa kisingizio cha kunioa lakini ukitapa ulichokitaka uniache kama wasemavyo mjini kwenye mataa."
"Nimekuelewa nia yangu ni mke si ngono suala la ngono liondoe akilini mwako tutakutana kimwili baada ya kuwa mke wangu wa halali."
"Siamini maneno yako, kweli wewe ni mwanaume wa kwanza kutotanguliza ngono mpaka siku ya ndoa yetu."
SASA ENDELEA…

"Kuku wangu mwenyewe kwa nini nimshikie manati au nidokoe finyago ya nyama kwenye chungu wakati nyama ipo kwa ajili yangu."
Walijikuta wamefika kijiji cha pili bila kujijua Mabogo alimkalibisha Rebeka kwa shangazi yake.
"Ooh, baba! Karibu sana mbona usiku?"
"Shangazi si unajua siku zangu zimeisha kesho narudi mjini."
"Na kweli...Oooh samahani nimesahau kumkaribisha mgeni, karibu mama."
"Asante shangazi."
"Mabogo na huyu ni nani?"
"Mkweo mtalajiwa."
"Ooh! Karibu mkamwana wangu tena wewe mwenyewe kamkamatie kuku umchinjie nimpikie mkamwana wangu."
"Shangazi muda umekwenda tutachelewa."
"Hapana ulijua unakuja na mkamwana wangu ilikuwaje ukaja naye usiku hawezi kuondoka mpaka nimempatia heshima yake asijesema mkwe mchoyo au unataka nije kwako aninyime chakula?"
Mabogo hakuwa na jibu ilibidi akamate kuku na kumchinja kisha shangazi yake amtengeneze kwa ajuli ya chakula cha mgeni. Japo alijua Rebeka anaweza kuchelewa lakini hakuwa na jinsi, waliondoka kurudi kijijini kwao kiza kikiwa kimeingia.
Shangazi yake aliompa Rebeka zawadi ya kuku ili awapelekee wazazi wake kama ishara ya kukubalika. Rebeka aliipokea kitu kilichompa faraja moyoni kwa kujua hata kama akiingia nyumbani saa ngapi anacho cha kujitetea na muongeaji wake mkubwa atakuwa Mabogo.
Waliwasiri kijijini majira ya usiku, kijiji kilikuwa kimya wengi walikuwa wameisha lala. Kama kawaida vijijini majira ya saa tatu nyumba nyingi huwa wameisha lala. Rebeka na Mabogo waliwasiri nyumbani kwao na kukuta wameisha jifungia ndani lakini aliwasikia wazazi wake wakizozana juu ya Rebeka kutokuonekana.
Baba yake alimshtumu mkewe kwa kitendo cha kumkataza asipike labda walikuwa na lao jambo.
"Mume wangu kuna ubaya gani kumpumzisha mtoto kwani yeye ni punda?"
"Siku zote mtoto wa kike hatakiwi kudekezwa atakuja kututia aibu akiolewa ataonekana goigoi."
"Kama kumpumzisha mwanangu nimefanya kosa basi sikatai lakini bila yeye leo tusingekula."
Rebeka hakutaka waendelee kubishana alijua kama atachelewa wanaweza kushikana bila sababu za msingi siku zote mama Rebeka huwa hakubali kuonewa. Aliamua kugonga mlango sauti kutoka ndani iliuliza ni nani anayegonga Rebeka alijibu.
"Ni mimi."
"Wewe nani?" baba yake aliuliza.
"Mimi Rebeka."
"Unatoka wapi?"
"Baba Rebeka sasa hivi tulikuwa tunataka kukatana masikio kwa ajili ya Rebeka badala ya kumfungulia unamuuliza maswali kama anafukuzwa?"
Mama Rebeka alisema yale huku akitoka sebuleni na kwenda kufungua mlango
"Ooh! Mwanangu ulikuwa wapi mama? He! na kuku umemtoa wapi usiku huu na huyu ni nani?" mama Rebeka aliuliza.
Rebeka kabla hajamjibu mama yake wakati huo na baba yake alikuwa ameisha toka nje alimkaribisha Mabogo.
"Mabogo karibu japo ni usiku hapa ndipo kwetu na walio mbele yako ni wazazi wangu baba na mama."
"Asante sana... samahani sana wazazi wangu kwa kumrudisha mwenenu usiku mkubwa kama huu, najua sio tabia yake naomba kwanza mnisamehe kwa hilo."
"Sawa baba, lakini wewe ni nani?"
"Naomba nimwache Rebeka azungumze kwanza, mimi nitakuwa mjibuji wa maswali mtakayo niuliza."
Rebeka alieleza habari zote kuanzia kufahamiana na Mabogo kuanzia shule ya msingi na asubuhi alivyo msaidia kuni na jioni walipokutana na maongezi waliyo yaongea na kuku yule alipomtoa.
"Baada ya maelezo hayo wazazi wangu napenda kuwaomba radhi kwa kitendo nilichokifanya cha utovu wa nidhamu kwa kuondoka kwenda kijiji cha jirani bila ruksa yenu," Rebeka aliwaomba radhi wazazi wake.
"Mwanangu Rebeka nakujua vizuri siwezi kukuhukumu ila nakusameheni wote...sasa wewe na mwenzio mmefikia hatua gani?"
"Hakuna hatua yoyote zaidi ya nyinyi wazazi wangu mtambue kuna kitu gani mbele yangu ni nyinyi kusikiliza na kutoa maamuzi."
"Hakuna anayepinga jambo la heri la muhimu kijana walete wazazi wako kwanza wewe ni mtoto wa nani hapa kijijini?"
"Mtoto wa marehemu Mkama Mabogo."
"Acha utani na wewe ndiye nani?"
"Naitwa Mabogo."
"Ooh! Kijana kumbe ni mtoto wa rafiki yangu marehemu Mkama wa Mabogo, wewe ni mwanangu hakuna kitakacho badilika kamilisha vitu vyote kulingana na mila zetu.”
Mabogo aliagana na wazazi wa Rebeka na kurudi kwao kulala ili asubuhi aondoke tayari kurudi na kukamilisha mipango yote ya harusi jukumu kubwa alimuachia shangazi yake na mdogo wake Lyasi.
Rebeka kwa upande wake usiku ulikuwa mfupi kwake muda mwingi aliwaza juu ya ndoa yake, aliona kama miujiza kuolewa mjini kitu alichokiomba usiku na mchana aliogopa kuolewa kijijini kwa kuogopa kuchakazwa na kuzalishwa bila mpangilio miaka kumi kwenye ndoa na watoto kumi kila mtoto na mimba juu hupumziki.
*****
Mipango ilikwenda kama ilivyo pangwa hatimaye Rebeka aliolewa na Mabogo kwa sherehe kubwa iliyokuwa simulizi pale kijijini na kuhamia mjini na mumewe. Baada ya harusi aliyaanza maisha mapya mjini kama mke wa mtu na kufanya mabadiliko makubwa na maisha yake.
Hali ya maisha ya mumewe ilikuwa ya kawaida kipato cha kawaida lakini kilikidhi mahitaji yote muhimu. Ndani mwake hakuna kilichopungua yalikuwa ni maisha ya kati ambayo mtu huwa halali na njaa na kula anachokitaka sio anachokipata.
Mumewe alionyesha mapenzi ya dhati kwa mkewe naye Rebeka alionyesha mapenzi ya dhati kwa mumewe. Ilikuwa ndoa iliyojaa neema na Baraka, katika miezi miwili Rebeka alishika ujauzito hapo mapenzi kwa mumewe yaliongezeka na alipo karibia kijifungua kama zilivyo mila nyingi za kiafrika alirudi nyumbani kwao kujifungua.
Mungu alimjalia kujifungua salama mtoto wa kike waliomwita Nyangeta jina la mama yake Mabogo.
Baada ya arobaini kuisha alirudi mjini kuendelea na maisha yake. Maisha waliyoishi Rebeka na mumewe yaliwaumiza wengi waliojiuliza wanasiri gani ya kuishi muda wote huo bila kukosana.
Siku zote palipo na neema hapakosi fitina watu walitafuta kila njia ya kutafuta urafiki na Rebeka mpaka wakafanikiwa jambo ambalo mumewe alimuonya kuwa asipende mashoga wa mjini wengi wao ni wahalibifu wa ndoa za watu zilizotulia.
Mwanzo aliweza kumsikiliza mumewe lakini hawakuchoka alifikia hatua ya kukubali kuongea nao. Mwanzo walianza kama marafiki wema ambao walimfundisha mambo mengi ya maisha ambayo aliyaona kama kufunguka macho angejuaje bila kumkaidi mumewe.
Mawazo waliyompa ni mwanake kujishughulisha asiwe golikipa kuna leo na kesho mumewe anaweza kufariki ghafla atashindwa aanzie wapi pia walitaka kujua maisha yake ya kijijini. Rebeka bila kuficha alianika mambo yake hadharani hapo ndipo walipo mwambia:
"Ona shoga kama ulivyosema familia yako ni hohehahe kwa nini uendelee kumtegemea mumeo?" wa kwanza alisema na wa pili aliongezea:
"Hivi kama ukifanya kazi ukipata pesa zako ambazo hazitahusiana na mumeo unaweza kusaidia wazazi wako hata kumpunguzia mzigo mumeo hata kukunyanyasa hawezi."
"Mimi ningejuaje?" Rebeka alisema kwa unyonge.

Nini Kitaendelea?
 
ADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)
SEHEMU: 04
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
SIMU: 0713 646500

ILIPOISHIA:
"Ona shoga kama ulivyosema familia yako ni hohehahe kwa nini uendelee kumtegemea mumeo?" wa kwanza alisema na wa pili aliongezea:
"Hivi kama ukifanya kazi ukipata pesa zako ambazo hazitahusiana na mumeo unaweza kusaidia wazazi wako hata kumpunguzia mzigo mumeo hata kukunyanyasa hawezi."
"Mimi ningejuaje?" Rebeka alisema kwa unyonge.
SASA ENDELEA...

"Si wewe na ndani ndani na wewe alitaka hata akikunyanyasa utakosa pa kukimbilia lakini ukiwa na pesa zako hawezi kukunyanyasa siku hizi wanawake tumeamka."
"Nilikuwa sijui kumbe ndiyo maana alinikataza nisiwe karibu na nyinyi alijua hili."
"Sasa kazi kwako muombe mumeo mtaji ukipata tu njoo tukuonyesha biashara tena tunakuhakikishia utanunua hata gari utakuwa na kipato hata kumzidi mumeo."
"Aiiiih jamaniii," Rebeka alisema kwa sauti ya aibu.
"Utabakia ‘aiii jamani’ fanyia kazi yote tuliyo kueleza."
"Nitayafanyia kazi nipeni wiki bila hivyo nyumba itawaka moto hawezi kunifanya golikipa kila siku kusubili tonge," Rebeka alijitutumua.
Rebeka aliagana na majirani zake na kurudi ndani akiwa na wazo la kumuomba mtaji mumewe kwa nguvu kwa hiyari alijiona anauweka usiku kwa kumtegemea mumewe kila kukicha kumbe anaweza kufanya kazi na kuwa na pesa nyingi.
Mumewe aliporudi alishangaa kumkuta mkewe akiwa hayupo kwenye hali yake ya kawaida aliyoizoea lakini hakutaka kumuuliza mapema alisubiri mpaka muda wakiwa kitandani ndipo alipomuuliza:
"Rebeka mke wangu una tatizo gani?"
"Sina," alijibu kwa sauti ya chini.
"Hapana mke wangu nakujua vizuri una tatizo gani?"
"Sina nimesema," alikataa.
"Hapana bado sijakuelewa mimi ni nani?"
"Mume wangu."
"Yanapotokea mabadiliko ndani nani wa kumwambia?"
"Wewe."
"Haya niambie una tatizo gani?"
"Hivi mume wangu tutaendelea na maisha haya mpaka lini?" Rebeka alimuuliza mumewe huku akikaa kitako.
"Maisha gani?"
"Yaani kama huyaoni hivi kwa bahati mbaya siombei ila kwa mapenzi ya Mungu wewe afariki ghafla mimi nitasimama upande gani?"
"Bado sijakuelewa una maana gani?"
"Unajua dunia ya leo maisha kusaidiana si kufa tu hata magonjwa hivi leo wewe uugue si tutakuwa wote tumeugua nani wa kutusaidia."
"Hakuna."
"Sasa hii hali wewe unaipenda?"
"Siipendi...wewe ulikuwa unatakaje?"
"Mimi nilikuwa na wazo la kutafuta biashara kwa ajili ya kuongeza kipato kidogo chako na changu tunapata kitu kamili tunaweza kupiga hatua kimaisha."
"Mke wangu ni wazo zuri lakini biashara yataka mtaji mkubwa vilevile ufahamu wa kuifanya biashara hiyo?"
"Mpaka nakwambia hili jambo nimelifanyia kazi kwa kipindi kirefu ninachosubiri ni kutekeleza tu."
"Mmh! Haya unataka kufanya biashara gani na mtaji wake kiasi gani?"
"La muhimu ni mtaji biashara nitakujulisha ni biashara gani."
"Haya mama kiasi gani?"
"Laki saba."
"Laki saba mke wangu mbona nyingi."
"Na biashara yake ni kubwa ambayo wewe mwenyewe utafurahi faida yake lazima utajilaumu kwa kuchelewa kukueleza."
"Haya mama nipe wiki mbili nitakukamilishia hizo hela."
"Mume wangu wiki mbili mbona nyingi wewe benki si una hela nilitegemea kuniambia kesho unanipa hizo hela."
"Mke wangu mbona umenibana hivyo huniachii nipumue?"
"Linaloweza kufanyika leo lisingoje kesho na mchuzi wa mbwa unywe ungali moto."
"Haya kesho asubuhi tutaongozana hadi benki na kukuchukulia hizo hela sawa mpenzi?"
"Hayo ndio maneno ya kiume," Rebeka alitabasamu.
Rebeka aliuona utajiri ukiwa mbele yake alijiona ndani ya miezi miwili atakuwa na pesa nyingi sana na kuweza kuwasaidia familia yake bila kumtegemea mumewe.
****
Siku ya pili Mabogo aliondoka na mkewe hadi benki na kumpatia mkewe kiasi alichotaka na kuacha akiba elfu hamsini. Alimuomba Mungu hela yake isipotee bure atakuwa ameadhirika kwa kuwa muda huo hakuwa na akiba nyingine.
Rebeka alipozipata zile hela breki ya kwanza kwa shoga zake na kuwaonyesha zile pesa alizopewa na mumewe kwanza walimpongeza kwa ushupavu aliouonyesha kwa mumewe na kuweza kuzipata zile pesa tofauti na wao wapo waliodiriki kutoa hata miili yao ili wapate pesa za biashara.
"Sasa shoga mambo mazuri, sasa unatakiwa kuomba ruhusa ya kufuata biashara na mama Stera mkoani na safari yake kesho."
"Mmh! Atanikubalia mbona haraka hivyo?" Rebeka alishtuka.
"Asikukubalie kivipi hela atoe akukataze usisafiri sasa hiyo biashara utaifanyaje?"
"Mmh! Wacha nijaribu."
"Usijaribu, fanya kweli ukimlegezea utakuzuia biashara ya kusafiri ndio yenye pesa au unataka biashara ya kukopesha kanga mtu kukulipa mpaka mwezi na hela yenyewe haulipwi yote."
"Hilo tena halina mjadala akipenda asipopenda nitasafiri," Rebeka alisema kwa kujiamini.
Rebeka aliagana na shoga zake na kurudi nyumbani kumsubiri mumewe kwa hamu ili kumuaga tayari kwenda safari akubali asikubali lazima ataondoka. Siku hiyo mumewe alichelewa kurudi alirudi saa tano usiku lakini alishangaa kumkuta mkewe akiwa bado yuko macho si kawaida yake.
Mabogo alishtuka kumkuta mkewe akiwa bado hajalala akimgojea, kabla ya kuoga na kula alihoji kulikoni kumkuta bado hajalala kitu siyo kawaida yake. Rebeka alimjulisha kilichomfanya achelewe kulala.
"Sawa mke wangu sikukatalii lakini mbona haraka hili jambo lilitakiwa mapema pia nani atakayebakia na mtoto?"
"Mtoto kesho utampeleka nyumbani nikirudi nitamfuata."
"Sasa mama Nyangeta unaelewa kabisa mimi ni mtumishi wa serekali huo muda wa kumpeleka mtoto nitautoa wapi?"
"Hiyo mimi sijui ila elewa mimi kesho alfajiri nakwenda safari unafikili maendelo yanamsubiri mtu."
Siku zote Mabogo hakutaka kubishana sana na mkewe alimkubalia shingo upande ile hali haikumshtua Rebeka akili yake iliyokuwa imeelekea kwenye utajiri. Walilala mpaka alifajiri alipopitiwa na shoga yake kwenda mkoa kwa ajili ya biashara.
****
Rebeka alirudi baada ya siku tatu akiwa amekuja na biashara ya mchele aliouuza kwa jumla na kujikuta akitoa hela ya manunuzi na usafiri alijikuwa amepata faida laki tatu.Vile vile alileta mchele mwingi kwa ajili ya matumizi ya ndani.
Kwa mara ya kwanza mumewe alimuona mkewe ni mwanamke anayeona mbali mwenye wivu wa kimaendeleo. Tokea siku ile hakuwa na shaka naye na maisha yalizidi kuwa mazuri ndani ya mwezi mmoja Rebeka aliweza kurudisha hela ya mumewe na kuweka pesa ndani shilingi milioni moja na laki tano taslimu.
Pamoja na kupata pesa zile aliendelea kumheshimu mumewe na upendo uliongezeka mara dufu. Rebeka alipanga kama biashara itaenda vizuri basi watafute kiwanja ambacho wataanza kujenga polepole.
Lilikuwa wazo zuri ambalo mumewe aliliunga mkono, familia ilizidi kuongezeka upendo kila mmoja limheshimu mwenzie kwa heshima ya mke na mume. Rebeka aliweza kufuta ile dhana ya kuwa mwanamke akiwa na kipato kikubwa zaidi ya mumewe huwa na dharau.

Nini kitaendelea?
 
HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)
SEHEMU: 05
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
SIMU: 0713 646500

ILIPOISHIA:
Lilikuwa wazo zuri ambalo mumewe aliliunga mkono, familia ilizidi kuongezeka upendo kila mmoja limheshimu mwenzie kwa heshima ya mke na mume. Rebeka aliweza kufuta ile dhana ya kuwa mwanamke akiwa na kipato kikubwa zaidi ya mumewe huwa na dharau.
SASA ENDELEA...

Siku zote shetani ni mshirika mzuri penye neema, penye upendo kupenyeza ushawishi wake kuhakikisha mwanadamu anapotea. Siku zote wakiwa katika biashara zao shoga zake hupata kinywaji kidogo pia wapo waliokuwa si waaminifu kwa ndoa zao.
Yote hayo aliyaona lakini alijisemea kila mtu anajua anachokifanya na kilichomtoa nyumbani na kumpeleka kule. Tatizo likaja kila akifuata mzigo anapata nusu kitu kilichomfanya aharibu malengo yake. Hakujua kumbe ulikuwa mtego ambao bila kutegemea ulimnasa.
Sehemu aliyokuwa akichukua mzigo alipojitokeza kijana mmoja ambaye ndiye aliyekuwa msanyaji mkuu wa mizigo toka shamba na kuwauzia wafanya biashara. Kila alipojaribu kumtongoza alimtolea nje kitu kilichomnyima raha hata alipowatumia mashoga zake aliwatolea nje.
Lakini hali ya kuyumba kwa biashara yake ilibidi aombe msaada wa shoga zake ambao ndiyo wazoefu wa kazi ile jibu alilopewa lilimkata maini.
"Shoga siku hizi toa kitu upate kitu."
“Mna maana gani?”
"Usione sisi tupo hapa ni wake za watu lakini tunapozidiwa hutumia tulichonacho ili kurekebisha mambo, kwani ukitembea naye ukirudi nyumbani mumeo atajua au sisi hatupo na waume zetu hata hao matajiri wapo walioua. Pia wapo wanaume waliokubali kugeuzwa wanawake, utajiri hauji kwa maji yanayotililika mlimani.”
"Shoga toa, harua haina makombo kwanza bwana mwenyewe unakutana naye unapokuja kwenye biashara hata mzigo mwingine utapata bure na zile gharama za kutoa mzigo shamba atazilipa yeye. Apate bahati gani shoga mpe wewe si mtoto siku zote harua haina makombo," mwingine aliunga mkono.
Yalikuwa maneno mazito yaliyotaka maamuzi ya kina sio kukurupuka, Rebeka alijifikiria kwa muda, wakati huo shetani naye aliongeza ushauri wake pale alipomshauri:
"Kwani mara moja ina nini utapungukiwa na nini kwani umefunga safari kutafuta mali na mali inapatikana kwa njia nyingi moja wapo ni hii...Hata huyo mumeo si muaminifu lakini hakuna kilichopungua mwilini mwake nawe pia hivyohivyo."
Bila kutalajia Rebeka alianzisha mahusiano na kijana aliyekuwa na pesa sana kwa kumiliki mashamba mengi ya mpunga na vilevile ndiye mufuataji mkubwa wa mazao yote yanayotoka shambani.
Kijana Kurukuchu vilevile ndiye aliyekuwa na magari yanayobeba mizigo kutoka shamba na kuleta gulioni. Rebeka siku ya kwanza kukutana kimwili na Kurukuchu au kama wengi wapendavyo kumwita tajiri mtoto Kuchu alipewa laki tano taslimu.
Rebeka aliona kama miujiza kupata pesa nyingi kiasi kile kwa starehe ya muda mfupi. Alirudi nyumbani na mchele mwingi ambao alipata kwa gharama ndogo sana.
Pesa aliyo hongwa na ya mauzo aliyopata alimpa mume wake anunue kiwanja na kuanza jenzi wa nyumba mara moja. Yeye aliendelea na kazi kama kawaida, muda wa kurudi mwanzo ulikuwa baada ya siku tatu ulibadilika na kuwa wiki mwishoe ukawa mwezi mumewe alipohoji alizibwa macho na pesa alizopewa na mkeo kwa kisingizio siku hizi biashara wanazifuata mbali.
Penzi la Kuchu na Rebeka lilizidi kukuwa kila siku mpaka pale Kuchu alipomshawishi Rebeka aachane na mumewe ili wawe mke na mume. Pamoja kwenda nje ya ndoa yake Rebeka hakuwa tayari kuivunja ndoa yake kwa kuwa mumewe alikuwa bado anampenda penzi la nje lilikuwa kwa ajili ya pesa.
Kuchu alipoona Rebeka ana msimamo alipomuahidi kumjengea kwao nyumba ya kisasa pia yeye mwenyewe kumjengea nyumba ya kifahari pamoja na kumnunulia gari la kifahari. Siku zote pesa shetani ilisababisha Yuda kumsaliti Yesu.
Rebeka kwa mara nyingine ngome iliyokuwa kwenye moyo wake ilibomoka na kukubali kulivunja penzi lake kwa Mabogo na kuivunja ndoa yake. Kuchu alimuahidi ahadi yake angeitimiza ndani ya miezi mitatu hapo ndipo Rebeka atakapovunja penzi lake na Mabogo.
Ndani ya miezi mitatu Kuchu alitimiza ahadi yake kwa kuwajengea wazazi wa Rebeka nyumba ya kisasa na kumjengea Rebeka jumba la kifahari na kumnunulia gari la kifahari aina ya Morano ya kutembelea.
Baada ya kutimiziwa ahadi zile ikabakia kazi ya Rebeka kuvunja ndoa yake na mumewe. Ilikuwa baada ya kufanya mizunguko yake kuhakikisha kile alicho ahidiwa na Kuchu. Alisimamisha gari lake kwenye nyumba yao mpya.
Alirudi nyumbani huko akiwa katika wakati mgumu katika maisha yake kwenda kuivunja ndoa yake ambayo aliahidi hataisaliti na kutenganishwa na kifo lakini pesa zilivunja nguzo za moyo wake.
Alikwenda hadi ndani na kumkuta mumewe akiwa na mwanaye na mfanyakazi wa ndani wakiwa wanacheza sebleni. Alipoingia Mabogo alinyanyuka kumlaki mkewe kwa furaha.
"Ooh! Mpenzi yaani hufi haraka tena sasa hivi mwanao alikuwa akiuliza mama atarudi lini?"
Mabogo alimlaki mkewe kwa kumkumbatia kitu kilichomfanya Rebeka aanze kulia mumewe anampenda lakini kile alichoahidiwa katimiziwa. Alimuangalia mumewe kisha alimwangalia mwanaye machozi yalianza kumtoka kitu kilichomfanya Mabogo ahoji mkewe akupatwa na nini.
"Mpenzi, mama watoto.. mama Nyangeta una tatizo gani laazizi wangu?"
Maneno yale yalikuwa kama mshale wa sumu kwenye moyo wa Rebeka uliosababisha maumivu makali ya moyo yaliyomfanya aangue kilio cha sauti.
"Basii inatosha baba Nyangeta....oooh maskini nimekuwasaliti mume wangu sina jinsi utanisamehe mume wangu....nimekusaliti nimemsaliti mtoto wetu kipenzi....oooh Mungu wangu nisamehe kwa maamuzi ya hatari niliyoyaamua sina jinsi..."
Maneno ya Rebeka, mumewe aliyasikia lakini hakuyaelewa alijiuliza mkewe amekubwa na nini na kipi alichomsaliti. Lakini moyoni mwake aliapa kumsamehe mkewe kwa lolote atakalo lifanya hasa kulingana na biashara zake.
"Mke wangu hata kama ulitoka nje ya ndoa yetu najua ni shetani mbaya aliyekupitia lakini hilo nililijua na kuuapia moyo wangu nitakusamehe kwa majaribu yoyote."
"Sio hivyo mume wangu hili ni kubwa kuliko unalolifikiria...Nina dhambi kubwa mbele ya Mungu nimekukosea mume wangu nimekuwa nyoka uliyenifuga nimeota meno nakuuma mume wangu, eeeeh Mungu wangu mimi ni kiumbe gani?" Rebeka alisema kwa uchungu huku akili.
"Mbona sikuelewi mke wangu una nini leo?"
"Sina jinsi lakini ndio hivyo mume wangu maamuzi niliyoyamua siwezi kuyabadili japo moyo unaniuma nakupenda mume wangu..."
"Hilo nalijua ndio maana nipo tayari kukusamehe kwa kosa lolote hata kama umeisaliti ndoa yetu."
"Kila neno lako mume wangu ni kama mshale wenye maumivu makali moyoni mwangu nayajutia maamuzi yangu lakini sina jinsi imekuwa hivyo utanisamehe sana najua nitakuweka kwenye wakati mgumu nakuomba vumilia Mungu atakupatia mke mwema ambaye atayapoza maumivu yako."
Rebeka aliongea yale huku akilia alikuwa amekaa chini ya zuria mbele ya mumewe wake kitu kilicho mweka mumewe kwenye mtihani mzito uliokuwa na majibu magumu. Mabogo alimnyanyua mkewe na kumkalisha juu ya kochi wakati huo mwanaye Nyangeta alikuwa akilia.
Mtumishi wa ndani alimchukua na kutoka naye nje kumbembeleza na kuwaacha tajiri zake waongee. Baada ya kutoka Mabogo alimsogelea mkewe na kumwinamia akiwa amepitisha mkono kwenye shingo yake aliutembeza shingoni kwa Rebeka taratibu huku akiongea kwa sauti ya upole iliyochanganyikana na majonzi yenye kitetemeshi cha kilio.
"Mke wangu ni nini kilichokusibu hebu nidadavulie ili nami nielewe, elewa mimi ndiye mwenzio hata kanisani unakumbuka walituhusia kuwa wewe ni mwili wangu wa pili na wewe mimi ni mwili wako wa pili hivyo kuunda mwili mmoja....
"Rebeka mke wangu kwa nini unaniacha gizani hebu niweke kwenye mwanga ili nijue nini kilichokusibu mke wangu ni muda mfupi nilikuwa nakuwaza lakini kwa bahati na wewe ukatokea moyo wangu ulijaa furaha kukuona wewe furaha ya moyo wangu joto la baridi kwenye baridi kali kato la kiu yangu pumbazo la moyo wangu....." maneno ya Mabogo yalikuwa mwiba mkali kwa mkewe kitu kilicho fanya amkatishe kwa sauti ya kilio kikali
"Basiii..basi mume wangu asiendelee kusema kila neno lako laweza kuchukua uhai wangu, ukweli wangu ni maumivu ya moyo wako ni sawa na kuupasua kwa kisu butu bila ganzi, najua maumivu yake yanaweza kukuathili kiakili na kimwili."
"Usiogope Rebeka siku zote kweli huwa chungu lakini dawa..vilevile maumivu ya kweli huwahi kupoa kuliko maumivu ya uongo niambie ukweli nipo radhi kwa lolote ulilokuja nalo kwa siku ya leo," Mabogo alimtoa hofu mkewe.

Nini kitaendelea?
 
HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)
SEHEMU: 06
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
SIMU: 0713 646500.

ILIPOISHIA:
"Basiii..basi mume wangu asiendelee kusema kila neno lako laweza kuchukua uhai wangu, ukweli wangu ni maumivu ya moyo wako ni sawa na kuupasua kwa kisu butu bila ganzi, najua maumivu yake yanaweza kukuathili kiakili na kimwili."
"Usiogope Rebeka siku zote kweli huwa chungu lakini dawa..vilevile maumivu ya kweli huwahi kupoa kuliko maumivu ya uongo niambie ukweli nipo radhi kwa lolote ulilokuja nalo kwa siku ya leo," Mabogo alimtoa hofu mkewe.
SASA ENDELEA...

"Japo moyo unaniuma na nafsi kunisuta na kukumbuka uliponitoa na leo nilipo nimekuwa wizi wa fadhira...mume wangu siku zote mbuzi hajichungi mwenye anaweza kutamani majani ya shamba la jirani, pengine ni kishawishi cha mwenye shamba ili amkamate mbuzi wako.
"Mume wangu mbuzi wako amekamatwa shamba la watu na huwezi kumrudisha tena."
"Rebeka kama nimekuelewa lakini sina uhakika na nikiwazacho una maana gani hebu niweke wazi."
"Mabogo mume au baba mtoto wangu baba Nyangeta kuanzia leo hii mimi si mkeo tena," Rebeka alisema huku machozi yakimmwagika kama maji.
"Atiii?" Mabogo alishtuka.
"Kama nilivyokueleza mbuzi wako amekamatwa shamba la jirani na huwezi kumrudisha tena."
"Hapana Rebeka una maanisha..au sijakuelewa una maana gani?"
"Kuanzia leo mimi si mkeo sasa hivi mimi ni mke wa mtu mwingine najua ni uamuzi wa kukushtua ambao ni wa kikatili lakini sina jinsi. Sipendi na wala nisingependa maishani mwangu kutengana na wewe mume mtu aliyenitoa tongotongo za macho lakini maisha hubadilika kila siku unazoishi unalolitazamia silo linalokuwa, naomba unipe ruksa japo moyo wako hautakuwa radhi," Rebeka alisema kwa sauti kavu huku akifuta machozi.
"Rebeka mke wangu unayosema ni kweli au leo umelewa?"
"Sijalewa ila siku hizi mume wangu nakunywa pombe najua hukutegemea mimi kuongea maneno haya maishani mwako lakini huu ndio ukweli."
"Japo siamini, Rebeka mke wangu nimekukosea nini kililofanya uchukue uamuzi mbaya kama huo sawa na kuondolewa moyo wangu sijui kama nitaendelea kuishi."
"Mabogo mume wangu kipenzi changu huwezi kuamini pamoja na leo tunatengana rasmi, lakini bado nakupenda mume wangu...na mapenzi yangu kwako hayatafutika mpaka naingia kaburini."
"Kama ni hivyo kwa nini unaniacha?"
"Imebidi sina jinsi ujanikosea wala kuniudhi wewe ni mmoja wa wanaume waelewa wanaume wenye mapenzi ya kweli wenye upendo wa dhati...Najua napoteza lulu ya maisha yangu nayapoteza mapenzi ya kweli ambayo dunia ya leo ni nadra kuyapata...kilichomshinda Yuda Sikalioti na kumsaliti Yesu ndicho kilichonishinda na kuvunja ndoa yetu si kingine penzi masirahi."
"Ni nini ulichokosa mke wangu bado nakupenda bado nakuhitaji nini hatima ya maisha yangu nini hatima ya maisha ya mtoto wetu mwenetu ataishi maisha gani atayakosa mapenzi ya baba na mama," Mabogo baada ya kuamini mkewe hatanii alipiga magoti mbele ya mkewe huku akilia.
"Yote hayo niliyafikiria kabla ya kutoa uamuzi, siku zote dawa ya jipu ni kulikamua japo linauma...kuhusu malezi ya mtoto sidhani kama yatateteleka wangapi wamelelewa na bibi zao hata watu baki lakini wameishi maisha mazuri. Kitu kizuri mtoto hata kosa malezi ya baba na mama utakaa naye nikiwa na hamu naye nitakaa naye.
"Kingine ni kwamba pesa nilizozipata kwenye biashara zangu nina imani zipo kama milioni kumi na mbili. Nsina imani zitasaidia malezi ya mtoto wetu na wewe mume wangu najua tutaachana hapahapa duniani lakini kwa Mungu wewe ni mume wangu.
"Sitachukua chochote humu ndani hata nguo zangu, nitaondoka mimi mwenyewe nyumba na vyote tulivyochuma pamoja ni mali yako na mwenetu. Ila kwa sasa masuala yote ya mtoto niachie mimi nitampatia kila aina ya huduma muhimu vile vile mhudumu nitamlipa mshahara wa miaka mitano kwa mkupuo ili usifikilie suala hilo hela zako ufanyie kazi nyingine."
"Rebeka mke wangu bora ungeninyang'anya kila kitu ndani na kuniachia moyo wako ni muhimu kuliko chochote duniani… Rebeka nimekuzoea mke wangu," Mabogo aliendelea kubembeleza huku amepiga magoti.
"Hakuna nisiloelewa yote nayajua lakini sina jinsi naomba unikubalie nina muda mchache mume mwenzio ananisubiri."
"Hapana Rebeka huondoki wewe bado mke wangu...nasema huendi kokote," Mabogo aliona kuna haja ya kutumia nguvu ya kiume.
"Mabogo acha akili za kitoto usifanye uamuzi wangu ukakuumiza zaidi naomba tuachane kwa amani ili panapo matatizo tusaidizane," Rebeka alisema kwa sauti ya upole.
"Lolote na liwe nasema huondoki kama sio nitamwaga damu ya mtu."
"Mabogo mapenzi si lazima usisababishe nikakasilika na kutoa maamuzi yatakayokuumiza mara mbili."
"Nasema sikubali...toa maamuzi yoyote kumbuka nimekutoa kijijini hata ulikuwa hujui kuvaa viatu leo hii unapendeza unaniacha watu hao walikuwa wapi mpaka niwatengenezee mimi?"
"Mabogo nasema hivi kila usemalo ni kweli tupu na una haki yoyote ya kufanya, lakini kumbuka penzi alilazimishwi nina imani umenielewa kuwa mstaarabu."
Rebeka alinyanyuka huku akipigapiga mgongoni Mabogo aliyekuwa ameinama akilia
"Sweet naomba uniitie mtumishi na Nyangeta niwaage."
Mabogo alinyanyuka kama mbogo na kumsukuma Rebeka aliyeanguka chini huku akibwata.
"Muongo mkubwa mnafiki unanipaka mafuta kwa mgongo wa chupa eti sweet!"
"Huwezi amini Mabogo nakupenda kuliko mwanaume yoyote duniani nimeisha kueleza penzi masirahi nipo radhi kukulipia mahali na kukufanyia sherehe kwa gharama zozote ili kuhakikisha unakuwa na mke atakayeziba pengo langu."
Rebeka alimjibu huku akiamka pale chini alipoanguka hakuonyesha hasira yoyote, Mabogo hakumjibu neno lolote zaidi ya kuondoka kuelekea jikoni. Wakati huo Rebeka alikuwa akimwita kwa sauti ya juu mhudumu ili amlete mtoto amuage. Alishtushwa na sauti ya Mabogo nyuma yake alipogeuka alikuta mumewe ameshika kisu kikubwa.
"Rebeka ukivuka mlango tu kutoka nje shingo yako halali yangu."
"Mabogo kwa nini unataka kujiingiza kwenye matatizo bure ukiniua utapata nini?"
"Bora wote tukose au na mimi najiua."
"Sipendi ufikie uamuzi huo Mabogo, wanawake wapo wengi kwa nini ujikatie tama?"
"Rebeka mke wangu wanawake wapo wengi lakini sio kama wewe...Oooh Rebeka mbona unanitesa hivyo kosa langu nini?"
"Mabogo huna kosa wala hujanikosea wala mapenzi yangu kwako yamefutika kama hutaki kunielewa fanya utakavyo sina jinsi wala usisubili nivuke mlango niulie hapahapa."
"Nisamehe Rebeka ni hasira tu siwezi kukudhuru bado nakupenda"Mabogo aliyasema yale huku akitupa kisu chini na yeye kumuangukia miguuni Rebeka.
"Rebeka usiondoke."
"Lazima niondoke Mabogo nina deni la watu la sivyo maisha yangu yataishia gerezani sidhani kama utakuwa na mimi."
"Rebeka tutauza kila kitu ili tulilipe hilo deni ilimradi nikubakize."
"Mabogo deni lenyewe ni kubwa hata uuze chochote ulichonacho nilichonacho hutaweza kulipa hata moja ya kumi ya deni hilo naomba uniache tu niende."
"Ha.a..aa..ya sina jinsi nimejitahidi kadili ya uwezo wangu lakini nimeshindwa uamuzi unao mwenyewe kusuka au kunyoa," Mabogo alikubali yaishe.
Mabogo alitoa kauli ya kukata tamaa ambayo alitegemea Rebeka kubadili mawazo. Machozi yalikuwa yakimtoka kama mtoto mdogo aliyekuwa akimlilia mama yake. Lakini msimamo wa Rebeka ulikuwa uleule alimshika mume wake mabegani na kumuinua alimketisha kwenye kochi na kuongea kwa sauti ya upole na ya chini:
"Baba Nyangeta najua umeumia jikaze wewe ni mwanaume siku zote wanaume ameumbwa kupambana na mitihani mingi siku zote unatakiwa kuishinda naomba uushindea na mtihani huu."

Nini kitaendelea? Endelea kufuatilia Mkasa huu.

KWA WAPENZI WA CHOMBEZO KUPITIA WHATSAPP GROUP TU

Kutokana na maombi ya wasomaji wangu wengi sasa hivi kila msomaji atalipia 2500 tu kwa mwezi , Chombezo litatoka mara tatu kwa wiki. Wapenzi wote wa machombezo yangu tunafanya usajili mpya katika group ya WhatsApp kwa namba yangu ya 0713 646500.
Nitatoa wiki moja ya usajili kabla chombezo mtalolichagua kuanza, ila sitapokea mtu katikati ya Chombezo. Asante
 
HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)
SEHEMU: 07
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
SIMU: 0713 646500.

ILIPOISHIA:
Mabogo alitoa kauli ya kukata tamaa ambayo alitegemea Rebeka kubadili mawazo. Machozi yalikuwa yakimtoka kama mtoto mdogo aliyekuwa akimlilia mama yake. Lakini msimamo wa Rebeka ulikuwa uleule alimshika mume wake mabegani na kumuinua alimketisha kwenye kochi na kuongea kwa sauti ya upole na ya chini:
"Baba Nyangeta najua umeumia jikaze wewe ni mwanaume siku zote wanaume ameumbwa kupambana na mitihani mingi siku zote unatakiwa kuishinda naomba uushindea na mtihani huu."
SASA ENDELEA...
"Sina jinsi nimekubali matokea siku zote unaweza kumlazimsha punda kumfikisha mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji, Mungu atanisaidia japo ni kazi ngumu lakini nina imani atanisaidia."
"Nashukuru kwa uamuzi wa kiume...asante sana mume wangu ubakie salama na mtoto wetu lakini muda wote tutakuwa pamoja kwa lolote usisite wala kuongopa kunitafuta hata mimi vilevile."
Maneno yale aliongea huku akiwa amemkumbatia mumewe kila mmoja machozi yalimtoka. Wakati huo mtumishi wa ndani alikuwa ameishafika baada ya kuitwa na Rebeka. Alimkumbatia mwanaye na mtumishi wa ndani huku akimsisitiza amlee kwa mapenzi yote na kumuahidi kumuongezea mshahara mnono.
"Kwani dada unakwenda wapi?"
"Nina safari kidogo tuongozane nje kwenye gari nina mzigo wako."
Waliongozana na mtumishi wa ndani hadi nje kwenye gari na kumpatia mshahara wake wa miaka mitano kisha alirudi ndani kumuaga mumewe kwa kumpiga busu na kuondoka kuelekea makazi yake mapya. Mabogo hakuwa na haja ya kumsindikiza alibakia kwenye kochi kama mtu aliyekuwa kwenye njozi ya mchana.
Mawazoni alijilaumu kwa kumruhusu mkewe kufanya biashara kutokana na wanawake wengi wanapokuwa peke yao hukosa uaminifu si kumkimbia mumewe. Alikumbuka kauli aliyosema Rebeka kuwa mbuzi aliye kuwa akijichunga kaingia shamba la watu na mwenye shamba kamrubuni na kumtaifisha kabisa kusababisha mbuzi kulikimbia zizi lake alilolizoea.
Vile vile alikumbuka maneno ya Rebeka kuwa mwanaume ameumbwa kupambana na mitihani na mmoja wa mtihani ni ule pia alimsisitiza asimame kiume aushinde. Mabogo japo alijua jeraha alilojeruhiwa ni baya lakini alikubali matokeo kwa kuwa imeisha tokea.
Alimuangalia mwanaye aliyekuwa amepakatwa na mtumishi alijikuta akipata nguvu pale wazo lilipomuijia kuwa la muhimu kwa wakati ule ni kumtunza mtoto wake kwa hali yote na kwa akili yake yote. Alijua siku zote mwanadamu ambaye hutaachana naye ni mzazi wake na mwanaye au ndugu wa damu si mwanamke au mwanaume wote hao huweza kutengana japo dini inakataza mnapooana hamtaacha mpaka kifo kiwatenganishe mnaweza kutengana na baadaye kurudiana.
Mabogo aliyahamisha macho yake kwa mwanaye na kumwangalia mtumisi ambaye alikuwa bado akimuangalia tajiri yake na kujawa na mawazo tele kichwani ni nini kilichomsibu. Kwa sababu kabla ya kuwapisha wazungumze na mkewe alikuwa mtu wa furaha lakini baada ya kurudi amemkuta akiwa mtu aliyebadilika amekuwa mnyonge tena mtu aliyevimba macho na kuwa mekundu ilionyesha alikuwa analia
Alijiuza maswali mengi juu ya hali ya tajiri yake alikuwa amejikunyata upenuni mwa kochi alijikuta akimuuliza bila kutalajia kauli ilimtoka kinywani:
"Shemeji kuna nini mbona uko hivyo?"
"Yaani we acha tu umasikini mbaya sana."
"Una maana gani?"
"Dada yako ametukimbia."
"Una maana gani kusema ametukimbia si amekwenda safari?"
"Si mara kumi angekwenda safari hata ya miaka kumi na kujua siku moja atarudi."
"Shemeji sikuelewi ina maana harudi?"
"Ndiyo maana yake."
"Amekwenda wapi?"
"Amekwenda kwa wenye pesa mimi si lolote kwake kuanzia leo si mke wangu tena."
"Utani huo shemeji na Nyangeta?"
"Kuanzia leo wewe ndiye mama yake."
"Mmh! Makubwa hata siamini."
"Kuanzia sasa amini hivyo usifikilie kuna mama wa kumlea Nyangeta zaidi yako ndiyo maana amekupa zile pesa kwa ajili hiyo."
"Shemeji nakuahidi nitamlea Nyangeta kwa moyo wangu wote kama mwanzo na kwa akili yako yote," msichana wa kazi alimuahidi bosi wake.
"Nitashukuru kwa hilo."
****
Rebeka baada ya kutoka kwa mumewe alikwenda hadi kwa shoga zake ambao hawakuamini kumuona akiendesha gari. Alipofika hakuwa na muda aliwaaga shoga zake na kuwaeleza kuwa muda wowote atawaletea kadi za harusi yake na Kuchu.
"He! Makubwa, mwenzetu wewe kiboko yaani umelamba ukaona haifai umechonga na mzinga kabisa?"
"Si nyinyi mlisema penzi masirahi."
"Kweli dada penzi masirahi...utakaaje na mwanaume wewe ndiye unaye mlisha sijui yupo kwenye hali gani mwanaume Yule? Picha yake kama naiona jinsi alivyokuwa akikupenda unaweza kumfanya ajinyonge."
"Lakini namuonea huruma yule mwanaume ni mpole sana ina maana amekuachia uondoke hivihivi?"
"Ndani palikuwa hapatoshi nusra anichinje."
"Ehe, patamu hapo ikawaje?"
"Nilimweleza penzi alilazimiswi na kumpa ruhusa ya kuniua lakini alishindwa najua mume wangu ananipenda lakini penzi masirahi. Ukiwa na huruma hujengi kila umuonaye na shida barabarani utamsaidia."
"Ni kweli wenye roho ngumu ndio mwenye maendeleo hata mimi nikipata mume kama Kuchu naachia ngazi. Ona umetukuta kwenye kazi lakini leo hii mwenzetu unaendesha gari hupigwi na baridi la usiku kama zamani kazi umetuachia sisi...sasa hivi shoga unakula kwa upole."
"Yaani shoga una bahati mimi kanichezea tu na kuniacha lakini wewe kugusa tu umepata nyumba na gari kijijini kwenu sasa hivi nao wanatanua maisha mazuri bado mumeo umemuachia maisha mazuri."
"He! shoga ina maana hata wewe umetembea na Kuchu?" Rebeka aliuliza kwa ushtuko.
"Unanishangaa mimi nani katika kundi letu ajatembea na Kuchu, kila mmoja alitembea naye kwa wakati wake yule baba samaki haachi kitu ndio maana tulifanya bidii akupate ili tutimize idadi yetu ya kutembea nje ya ndoa zetu lakini wewe mwenzetu amekuwa na bahati yako kugusa tu amenogewa na kunasa una ulimbo nini mwenzetu?"
"Basi hata sielewi toka siku ya kwanza alipagawa na kunipa laki tano."
"Ona sasa sisi wote aliyezidi alipata elfu ishirini lakini wote tulipata elfu kumi na kupunguziwa bei ya mchele."
"Bibi eeeh, kajiingiza mwenyewe hilo ndilo penzi masirahi ukisikia, wacha mumeo apagawe kama hela umemuachia aoe mwanamke."
"Sasa jamani wacha niwahi ila nina imani mkija kwenye biashara sasa mna mwenyeji wenu wa uhakika."
"Shoga nenda mbona umetukomboa."
Rebeka aliagana na shoga zake na kuingia ndani ya gari kurudi kwa mumewe mpya Kurukuchu au maarufu kwa jina la Kuchu tajiri kijana. Baada ya kwenda mwendo wa kilometa kama kumi alijikuta akiisikia sauti ya mumewe ikimuomba msamaha asiondoke kilio cha mume wake kilimfanya asimamishe gari pembeni na kuanza kulia kwa muda.
Lakini hakujutia maamuzi yake alijua ni maamuzi ya kawaida kwa mwanadamu imezoeleka anayeacha ni mwanaume lakini yeye alikuwa mmoja ya wanawake wanao fanya mapinduzi ya kifikra. Baada ya kulia kwa muda alipiga moyo konde na kuendelea na safari yake.
Nini kitaendelea?
 
HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)
SEHEMU: 08
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
SIMU: 0713 646500.

...ILIPOISHIA:
Lakini hakujutia maamuzi yake alijua ni maamuzi ya kawaida kwa mwanadamu imezoeleka anayeacha ni mwanaume lakini yeye alikuwa mmoja ya wanawake wanao fanya mapinduzi ya kifikra. Baada ya kulia kwa muda alipiga moyo konde na kuendelea na safari yake.
SASA ENDELEA...
****
Mabogo toka akimbiwe na mkewe Rebeka alikuwa mtu wa mawazo kila kukicha hata kazi zilimshinda mawazo yote yalikuwa kwa mkewe, mwanamke aliyemtegemea kwa maisha yake yote aliyekuwa muhimili wa maisha yake.
Alijua makosa aliyofanya yalikuwa ya kawaida kama mwanadamu kwa kujua wote wanadamu wana mapungufu ndiyo maana mwenyezi Mungu yupo tayari kumsamehe yoyote anaye omba msamaha kwa kulijua kosa lake. Hakuwa na wazo la kwamba siku moja Rebeka atasema kuwa waachane hasa akizingatia mtoto wao Nyangeta alikuwa bado mdogo aliyekuwa akihitaji malezi na mapenzi ya wazazi wake wote wawili kama mwenyezi Mungu hajamchukua mmoja wao.
Kila alipotoka kazini alikuwa hanakaa upenuni wa kochi na kujishika tama na machozi humtoka moyo wake ulitawaliwa na majonzi. Mtumishi wake wa ndani Bibiana alikuwa na yeye anakosa raha kila akiiangalia hali ya tajiri yake.
Alijitahidi kuonyesha mapenzi utiifu na huruma kwa bosi wake na malezi bora kwa Nyangeta ili kuhakikisha hakuna mapungufu katika malezi ya mtoto. Mtoto alikua kwa afya bora ambayo alikuwa na imani hata kwa mama yake asingeipata.
Akiwa amesimama kwenye mlango muda mfupi baada ya kutoka kumlisha Nyangeta na kumuosha kisha kumlaza kitandani na kumbembeleza mpaka alipopitiwa usingizi. Siku zote Nyangeta alijua Bibiana ndiye mama yake japo humwambia amwite dada lakini mtoto hakuwa tayari kumwita dada zaidi ya mama jambo ambalo aliliacha liendelee.
Bibiana alikuwa amesimama akimwangalia bosi wake ambaye alikuwa bado kameegemea kochi mkononi alikuwa na picha ambayo aliiangalia na kutiikisa kichwa. Bibiana alishuhudia machozi mufurizo yakimtoka bosi wake, alijiuliza hali kama ile itaendelea mpaka lini.
Miezi wa sita ilikatika toka Rebeka aondoke alitakiwa kuwa na moyo wa ujasiri afya yake ilizidi kudhoofu kwa mawazo utafikiri amefiwa lakini ni jambo la kawaida mwanadamu kutokewa na hali ile. Siku zote Bibiana alijiangalia na kujiona na yeye ni mwanamke aliye kamilika ambaye mwanaume yoyote rijali alikuwa na matamanio kwake.
Alijiuliza ni wanaume wangapi wamemtamkia kumtaka kimapenzi kila siku, watu walikuwa wakitofautiana mwanzoni alipokuja wa hali ya chini lakini siku zilivyozidi kwenda na hali yake ya kimwili kimavazi na kimaumbile kilifanya hata watu wenye wadhifa wao kumtaka kimapenzi.
Bibiana alijikuta akimheshimu Mabogo kama mume wake na Nyangeta kama mtoto wake. Hakuwa tayari kutembea nje kwa kumheshimu Mabogo vilevile mawazo yake yalivyo mpelekea huenda ndiye mwenye uwezo wa kumshawishi kumsahau Rebeka kwa kumfanyia kila alilotaka kubwa kumlelea mtoto wake kwa mapenzi mazito.
Siku zote aliamini kama uzuri alikuwa nao kama Rebeka atamzidi kidogo sana lakini alikuwa na uhakika yeye ni mzuri anayefaa kuziba pengo lile kuwa mama wa nyumba hasa akizingatia ameishi ndani ya nyumba ya Mabogo kama mke wa Mabogo na si mfanyakazi kwa kuwa amekuwa akifanya kazi zaidi ya mke wa ndani.
Alijiona anafaa kuwa mke wa mtu mwenye sifa kubwa kwanza ya usafi wa nyumba pili alijua kumlea mtoto vizuri hata kumzidi mama mwenye nyumba hata malezi ya Nyangeta yeye ndiye anayeyajua, mama yake alijua kuzaa tu.
Alijikuta akipata ujasiri wa ajabu na kumfuata pale alipokuwa amekaa tajiri yake na kukaa pembeni yake wakati huo ulikuwa ni muda mchache toka atoke kuoga. Alikuwa na kanga mbili tu. Kabla ya kwenda aliidondosha ile kanga na kumsogelea na kanga upande mmoja.
Alikaa pembeni yake na kupitisha mkono kwenye shingo ya Mabogo ambaye alichokifanya ni kuigeuza ile picha ili Bibiana asiione. Bibiana alichokifanya alipitisha mkono wake laini kwenye shingo ya Mabogo iliyosababisha joto lenye msisimko lipenye kwenye ngozi ya Mabogo na kuusisimua mwili wake.
Bibiana aliinama na kufanya joto la matiti yake yauguse mwili wa Mabogo ikifuatiwa na harufu nzuri ya manukato ambayo hayakuwa tofauti na ya mkewe Rebeka ambayo alimuachia hata alipomaliza alinunua kama yaleyale.
Kwa sauti ya chini alipenyeza sauti yake kwenye ngoma za sikio la mkono wa kulia:
"Mabogo nini tatizo...lililokwisha tokea limetokea lililopo kuganga yajayo...hivi wewe ni mtu wa aina gani mwenzio anafurahia maisha wewe kila siku unaombeleza...sipendi kuongea hili, usiwe mjinga wa mapenzi isiwe kama kipofu aliyefumbua macho na kumuona punda kila akiambiwa umemuona simba anauliza mkubwa kama punda ukimuuliza umemuona tembo anauliza mkubwa kama Punda...
“ Na wewe vilevile utafikiri Rebeka ni mwanamke wako wa kwanza, aibu mwanaume hatakiwi kuwa hivyo kama alivyoongea Rebeka kabla ya kuondoka mwanaume unatakiwa kuishinda mitiani....
“Wape wengine nafasi wapo wazuri kushinda Rebeka na wenye tabia nzuri kumheshimu mwanaume kwa shida na raha, hebu fungua ukurasa upya wa maisha yako jipe moyo utashinda bora angekuwa amekufa lakini mzima wa afya njema tena mwenzio anatumbua maisha. Usiwe kama kipofu aliyeona siku moja na kukutana na sura ya Rebeka...."
Mara Nyangeta alilia ndani kitu kilichofanya Bibiana kwenda ndani kumwangalia analilia nini. Alipita mbele ya Mabogo akiwa katika upande wa kanga tu, macho ya Mabogo yalimsindikiza na kugundua alikuwa na madini ndani yaliyohitaji kuchimbwa baada ya kunyang'anywa mgodi wake na wenye pesa.
Toka zamani alimtamani kimapenzi lakini alimheshimu kwa kumuona Bibiana ni mtu muhimu maishani mwake kwa kuogopa kumgusia suala la mapenzi kungekuwa na matokeo mawili kupata au kukosa vilevile kujivunjia heshima akizingatia Bibiana aliyemuonyesha heshima ya hali ya juu pia mtu muhimu aliyeyaangalia maisha yake na ya mwanaye.
Ndani ya nyumba yake kilichopotea ni upendo wa Rebeka lakini kila kitu kilifanyika kwa ufasaha zaidi tena kwa umakini mkubwa ambao hata Rebeka hakuweza kuufanya. Kikubwa alichomsifu Bibiana ni kumlelea mwanaye zaidi ya mkewe.
Siku zote aliogopa kumkosea Bibiana na kumkimbia na kumuacha mwanaye Nyangeta ambaye angepata shida, alikubali kufa kizungu na tai shingoni. Hakuamini alichokifanya Bibiana muda mfupi kilimfanya ahamie dunia nyingine ambayo aliitamani muda mrefu.
Alipopita mbele yake kwenda chumbani kumwangalia Nyangeta ambaye alimtunza kama mboni ya macho yake mwili ulimsisimka na kujikuta akipanda na ashki ya mapenzi ambayo alikuwa ameyakosa zaidi ya miezi tisa.
Akiwa yupo katikati ya mawazo Bibiana alirudi akiwa peke yake kwa ujasiri mkubwa Mabogo alimuuliza:
"Alikuwa analia nini?"
"Alikuwa ameshtuka tu, nimembembeleza ameendelea kulala."
Macho yao yalikutana Mabogo aligundua macho ya Bibiana yalikuwa yapo kwenye wakati mgumu yalikuwa yamelegea. Kwa upande wake aliona huo ni muda muafaka wa kuhamia ile dunia aliyoitamani muda mrefu.
Bibiana alirudi kukaa palepale alipokaa mwanzo na kupitisha mkono wake kwenye shingo ya Mabogo ambaye kitendo kile alikisubili kwa hamu kubwa. Lakini safari ile Bibiana alikuwa akihema na mwili ukimtetemeka. Aliongea kwa sauti ya muhemo kama mtu aliye maliza mbio ndefu:
"Mabogo nini kimepungua kwangu nimekataa wanaume wangapi kwa ajili ya kumlea Nyangeta naogopa kumkubali mtu kwa kuogopa kumuona akiteseka...lazima nikipata bwana nitatengana na Nyangeta nampenda na nataka akulie kwenye mikono yangu....
“Sihitaji malipo yoyote zaidi ya kunifanya niendelee kuwa karibu na Nyangeta mpaka Mungu atakapo chukua uhai wa mmoja wetu nampenda Nyangeta na wewe nakupenda vilevile nayahitaji mapenzi yako....
“ Naomba nipe nafasi nikupokee ukitoka kazini nikuite mpenzi nimekuzoea sihitaji kuwa karibu ya mwanaume yoyote zaidi yako nakupenda Mabogo nipe haki yangu niliyoiota na kuitafuta kwa muda mrefu nakuahidi nitakuwa mke mwema usinihukumu kwa kosa la Rebeka na kuona wanawake wote si waaminifu."
Mabogo hakuwa na jinsi wala hiyana alimpokea juujuu na kuhamia dunia nyingine iliyoifariji mioyo yao kila mmoja aliona ni mwenye bahati yaani riziki fil kitako kumkuta alipokaa.
Sauti ya kilio ya Nyangeta aliwakatisha katika kati ya dimbwi la huba na kumfanya Bibiana anyanyuke kukimbilia chumbani akimwacha Mabogo bado yupo chini ambaye alishtuliwa na sauti ya Bibiana
"Mpenzi twende tukaoge."
Bibiana alimfuta pale chini alipokuwa amekaa chini ya zuria na kumshika mkono na kumnyanyua. Walikumbatiana kwenye mapenzi mazito kwenda bafuni kuoga.

Nini kitaendelea?
 
HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)
SEHEMU: 09
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
SIMU: 0713 646500.
... ILIPOISHIA:
Sauti ya kilio ya Nyangeta aliwakatisha katika kati ya dimbwi la huba na kumfanya Bibiana anyanyuke kukimbilia chumbani akimwacha Mabogo bado yupo chini ambaye alishtuliwa na sauti ya Bibiana
"Mpenzi twende tukaoge."
Bibiana alimfuta pale chini alipokuwa amekaa chini ya zuria na kumshika mkono na kumnyanyua. Walikumbatiana kwenye mapenzi mazito kwenda bafuni kuoga.
SASA ENDELEA...

MWAKA MMOJA BAADAYE
Maisha ya Rebeka na bwana yake Kuchu yalishamili, yaliyojaa upendo wa hali ya juu wala hakujutia maamuzi yake ya kukubali kuolewa na Kuchu kwa mkuu wa mkoa kwa kuwa alipata alichokitaka na zaidi asichokijua.
Kuchu alimlea kama malkia kitu kilicho mfanya Rebeka awe kivutio kwenye macho ya watu wenye pesa. Kila sherehe za watu maarufu Kuchu alikwenda naye na kuonekana yeye ndiye mwenye mwanamke mzuri kuliko wote.
Wapo walio kuwa na pesa kuliko Kuchu nao walimtamani kuwa naye, walijua kwa mtoto mzuri kama yule siku zote kidume ni pesa hakuna kinachoshindikana kwa pesa hasa wakizingatia Kuchu amempata kwa kumpora mtu kwa kutumia jeuri ya pesa.
Kama kawaida yake Rebeka alikuwa akitembelea gari lake la kifahari popote alipo kwenda. Wakati huo mmoja wa matajiri wenye pesa kuliko Kuchu ambaye alionekana ni mtoto kifedha alikuwa akimfuatilia Rebeka nyendo zake.
Aliliona gari la Rebeka na kulifuatilia kwa nyuma mpaka lilipoingia eneo la maegesho ya Super Market kubwa pale jijini. Rebeka aliteremka na kuingia ndani ya super market ili anunue mahitaji muhimu.
Roja Mo alikuwa kwenye gari lake la kifahari aliliegesha karibu kabisa na gari ya Rebeka na kutulia huku akila muziki laini kutoka kwenye gari lake la kifahari aina ya Toyota Vx new model.
Macho yake aliyaelekeza kwenye mlango wa super market kumsubiri Rebeka mpaka atakapotoka. Aliogopa kumfuata ndani kwa kuogopa macho ya watu pia kwa bahati mbaya huenda Kuchu anaweza kuja ghafla anaweza kuvuruga mambo yote.
Alitega mtego wake kwa kumsubiri Rebeka kwa kujua lazima atakuja pale baada ya manunuzi. Rebeka naye ndani aliendelea na manunuzi ya vitu muhimu kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwake. Baada ya kuchukua kila alichokipata alilipia na kubebewa na mtumishi wa kwenye ile Super market mpaka kwenye gari lake.
Roja Mo alimuona akiwa ameongozana na mfanyakazi wa super market akiwa amembebea bidhaa zake alizonunua, alitoka kwenye gari lake na kuanza kujifanya anafuta vumbi kioo kwa mbele.
Yule mfanyakazi baada ya kuweka vitu kwenye boneti aliondoka na kumwacha Rebeka akifunga boneti ili aondoke. Baada ya mfanyakazi kuondoka Roja Mo aliona huo ndio wakati wake wa kurusha chambo wake kwa mwanamke mzuri kama Rebeka.
Rebeka baada ya kufunga boneti alilihakikisha kwa kulinyanyua kwa juu alipopata uhakika lipo sawa alielekea kwa mbele ili aondoke.
Roja Mo alimuona akija kwa mbele naye alikuwa kama akielekea kwenye mlango wa gari yake. Alikutana uso kwa uso na Roja Mo hakumjali alimpita kuelekea kwenye mlango wa gari yake bila kumsemesha lakini Roja Mo aliamua kumsalimia.
"Hujambo binti mrembo?"
"Sijambo shikamoo," alimjibu huku akifungua mlango wa gari lake kabla hajaingia ndani aliongeza neon.
"Samahani binti," kauli ile ilimfanya Rebeka asite kuingia ndani ya gari na kugeuka kumsikiliza Roja Mo alimtizama bila kusema neno kwa ishara nimekusikia unasemaje Roja Mo alirudia kwa kuomba msamaha tena kitu kilichomfanya Rebeka aongee.
"Nimekusikia unasemaje maana naona samahani nyingi?"
"Unajua siku zote unapotaka kuongea na binti mrembo kama wewe lazima upate idhini yake."
"Haya ongea."
"Kwanza lazima nikusifie binti umependeza."
"Asante."
"Sijui unajijua kuwa wewe ni mzuri?"
"Hapana labda uniambie wewe," Rebeka alijibu huku akimtazama usoni.
"Basi wewe ni mmoja wa wanawake wazuri."
"Asante sina budi kumshukuru Mungu kwa kunifanya nionekane mzuri machoni mwa watu."
"Kwanza sijui unanijua?" Rebeka alikaza macho na kumkumbuka.
"Mmh! Wewe si sijui Mo "
"Wengi huniita hivyo lakini jina langu naitwa Roja Mo "
"Ooh, ni bahati kukutana na watu maarufu kufikia hatua yakuongea naye uso kwa uso," Rebeka aliongea huku akiachia tabasamu pana sifa za Roja Mo alizisikia kuwa ni mmoja wa matariji wanao tikisa jiji.
"Kama sikosei unaitwa Rebeka?"
"Upo sawa kabisa."
"Basi Rebeka wewe ni uwa ridi zuri lililoota sehemu isiyo yake."
"Una maana gani?"
"Yaani maisha unayoishi bado sijaridhika nayo na hadhi uliyonayo."
"Bado sijakuelewa una maana gani?"
"Sikiliza Rebeka wewe ni hadhi ya watu kama sisi wenye pesa wenye kukufanyia kila kitu kinacholingana na hadhi yako."
"Kwani mimi nina nini kikubwa mpaka nionekane tofauti au nipewe sifa ambazo huziona ni tofauti na ninavyojiona?"
"Hujiulizi ni nini kiliochomfanya Kuchu atikise vijipesa zake kwa kuvunja ndoa yako...mpaka sasa hivi toka akuoe hajarudisha hata robo ya pesa zake na maisha mnayo ishi unamuumiza akijitahidi miaka miwili lakini nakupa mwaka mmoja utaona mabadiliko ya maisha yake. Unajua ameishauza magari yake mawili na mashamba yake baadhi?"
"Mmh! Yote hayo umeyajuaje?"
"Sisi ndiyo mji tumeuweka kiganjani tunajua kila kitu ndio maana nimeona ua kama wewe linataka udongo wenye rutuba na kumwagiliziwa maji yasiyo koma wala si ya kutegemea mvua kama Kuchu."
"Umeongea mengi bado sijakuelewa ulikuwa unataka nini?"
"Utanielewa kwa kuwa wewe ni mmoja wa wanawake wanao angalia mbele."
"Una maana gani?"
"Sipendi siku moja nikuone unatembea kwa miguu wakati ulikuwa na gari kama leo kauza zake kesho atauza yako mwisho nyumba mtarudi kupanga na hatimaye kukukimbia na kukuacha unaadhirika nitajisikia vibaya siku nitakayokukuta pekupeku mitaani...
"Amini amini Rebeka, Kuchu amebeba mzigo mzito kuliko uwezo wake."
"Mbona tunaishi maisha ya kawaida."
"Wewe unaona ya kawaida ila mwenzio maji ya shingo kusema anaona aibu labda asubiri kipindi cha mavuno.. ni leo? Mvua zisiponyesha hapo ndipo kazi ana shughuli gani zaidi ya mashamba na zile gari zake na mbili ameishauza?"
"Nimekusikia ulikuwa unasemaje?"
"Sasa tutaelewana unajua Rebeka wewe sasa hivi ni mke wa mtu siwezi kuongea kwa nafasi tutapanga siku ambayo utakuwa na nafasi ambayo nitaongea mengi ikiwa na mipango ya maisha bora mpaka kifo kitakapokuchua usiijue shida ni nini Mungu si mjinga kukupa uzuri siku zote kizuri hukaa pazuri ndiyo maana malaika wapo mbinguni wanakula raha na wewe unatakiwa uishi pepo ya duniani."
"Sawa nimekuelewa vizuri zaidi ya uliyoongea, sasa tutaongea lini?"
"Siku yako ambayo utakuwa na uhakika Kuchu hatatualibia maongezi yetu."
"Hilo halina shida nitapanga safari ya kwa mama hata siku mbili nina imani itatutosha sidhani kama una la ziada wacha niwahi."
"Sijajua lini?"
"Leo lini?"
"Jumanne."
"Alhamisi."
"Nitakuona vipi?"
"Nitatoka nyumbani saa tatu asubuhi baada ya Kuchu kuelekea shamba, ruhusa nitamuomba leo hii hawezi kunikatalia hapa ageuzi," Rebeka alijipata.
"Lazima utumie tunu aliyokupa muumba."
"Nina imani yote kwa leo tumemaliza yote tukikutana hiyo siku ambayo nina imani mtoto hatumwi dukani," Kauli ile ilimfanya Roja Mo achekelee moyoni kwa ushindi alioupata ambao alitegemea ungemtoa jasho.
Roja Mo ili aonekane sifa alizozisikia Rebeka na zake hasa alimwambia asubiri alikwenda hadi kwenye gari lake na kumuandikia cheki ya milioni ishirini na kumkabidhi huku akisema binti hizi ni lashalasha mvua kamili inakuja.
Rebeka hakuamini mambo bado milioni ishirini siku akimpa mambo ya kweli lazima atamnunua ndege.

Nini Kitaendelea ili kuyajua yote endelea kufuatulia.
 
HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)
SEHEMU: 10
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
SIMU: 0713 646500.

ILIPOISHIA:
Roja Mo ili aonekane sifa alizozisikia Rebeka na zake hasa alimwambia asubiri alikwenda hadi kwenye gari lake na kumuandikia cheki ya milioni ishirini na kumkabidhi huku akisema binti hizi ni lashalasha mvua kamili inakuja.
Rebeka hakuamini mambo bado milioni ishirini siku akimpa mambo ya kweli lazima atamnunua ndege.
SASA ENDELEA...

Rebeka aliipokea ile cheki na kushukuru huku naye akijinadi kuonyesha shukurani zake kwa vitendo.
"Nina imani Roja Mo hutazijutia pesa zako."
"Hilo sina shaka nalo na hii na lashalasha mvua kamili inakuja." Roja Mo alijigamba.
"Mmh! Mimi yangu macho."
Waliagana Roja Mo na Rebeka kila mnmoja aliingia kwenye gari lake na kwenda na safari zake Rebeka akirudi nyumani na Roja Mo akienda katika shughuli zake. Njiani Roja Mo alikuwa akijiona mshindi kati ya kundi la matajiri ni yeye atakuwa wa kwanza kutembea na msichana mrembo Rebeka.
Naye Rebeka alijiona ni msichana mwenye bahati aliye na mvuto machoni kwa wanaume. Yeye kwake mapenzi aliyaona ni masirahi wala si sitarehe tena. Kwake sitarehe ilikuwa kwenye ndoa yake ya kwanza na mzazi mwenzie Mabogo lakini hakuwa tayari tena kuona mapenzi kama sterehe hata kizazi alikuwa amefunga ili astarehe na wanaume wenye pesa.
Alirudi hadi nyumbani akiiangalia mara mbili mbili ile cheki ya milioni ishirini. Alijkwenda moja kwa moja hadi chumba cha kulala na kusimama mbele ya kioo kikubwa na kujiangalia upya kama ndio mara yake ya kwanza kusimama kwenye kioo kile cha kujipodolea.
Aliuchunguza uso wake kwa kituo na kugungua kitu fulani kilichomfanya aachie tabasamu pana lililozidisha uzuri wa sura yake alijikuta akijisemea mwenyewe kwa sauti ya chini:
"Mmmh kumbe mimi mzuri."
Hakuishia hapo alivua nguo zote na kuuangalia mwili wake kwa kituo alianzia kifuani matiti yake madogo kama hajawahi kunyonyesha yalikuwa ya muundo wa duara yaliyo jaa vyema na kumfanya mwanaume yoyote rijali apende kuyashika au kumtia ashki ya mapenzi.
Aliteremsha macho yake hadi kwenye kwenye tumbo lake dogo kama mtu asiye kula sana chini kulikuwa na kiuno chembamba kilichoingia ndani na kuyaacha makalio yatoke kwa nyuma na kumfanya kila amuonae lazima ageuze shingo.
Rebeka alijikuta akijitamani mwenyewe kwa kusema ningekuwa mwanaume ningefaidi kumpata mwanamke mwenye umbuile kama lake. Moyoni alijiona kumbe hakufaa kuwa na watu kama Kuchu bali kama Roja Mo watu wenye pesa zisizo na kikomo.
Katika maisha yake mwanaume alimuona ni mmoja ni mumewe Mabogo ambaye pamoja na kumsaliti bado alimheshimu na kumpenda lakini wengine wote ni penzi masirahi. Alivaa nguo zake na kujifunga kanga moja na kuelekea bafuni kuoga kisha aliingia jikoni kuandaa chakula cha mchana siku zote mumewe Kuchu chakula cha mchana alikuwa nyumbani.
Majira ya mchana Kuchu alirudi akiwa na mawazo mengi kitu kilichomshtua Rebeka hapo ndipo alipomsogelea na kumuuliza.
"Vipi sweetheart?"
"Aah! Mikosi kila kukicha gari langu nililokuwa nikilitegemea limepata ajari mbaya."
"Ooh, pole sana sasa itakuwaje?"
"Tatizo pesa sasa hivi sina na gari ndilo nalitegemea kipindi hiki nachosubiri mavuno," kauli ile ilimfanya Rebeka akumbuke maneno ya Roja Mo kuwa pesa za Kuchu za msimu na uchumi wake ulikuwa ukididimia kila kukicha.
"Sasa utafanyaje?" Rebeka alimuuliza bwana yake.
"Ni hivi nilikuwa naomba tuiuze gari yako ili nitengengezee gari yangu ndani ya miezi miwili nitakununulia nyingine."
"Kuchu utani huo yaani mimi nilikuwa nataka unibadilishie gari lingine wewe una wazo la kuliuza kwa taalifa yako kama umenishindwa bora uniambie mapema leo gari kesho nyumba kesho kutwa mimi mwenyewe."
"Hapana Rebeka sasa hivi mambo yamekuwa magumu nahitaji msaada wako kama mke wangu."
"Sikiliza Kuchu nimefanya dhambi kubwa ya kumkimbia mume wangu kwa ahadi zako, sasa leo imekuwa kinyume bora nirudishe kwa mume wangu."
"Hapana Rebeka bado nakupenda ugumu wa maisha usivunje pendo letu ni hali ya mpito tu."
"Kuchu mimi sikupendi kama unavyofikiria bali penzi lako lilijali masirahi zaidi."
"Hilo nalielewa lakini ni kipindi hiki tu nina imani mambo yatakuwa mazuri."
"Wewe nitakuvumilia kwa vile ndio ubinaadamu lakini mali zangu sikubali mtu aziguse tafuta ufumbuzi mwingine."
Kuchu hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali kwanza alishukuru kwa Rebeka kukubali kuendelea kuwa naye pamoja na matatizo aliyokuwa nayo. Aliingia chumbani kujilaza alishangaa kukuta pembeni ya dresing table kuna kikalatasi cheupe.
Alikiokota na kuanza kukisoma hakuamini kukuta ni cheki ya hela nyingi yenye jina la Rebeka alishangaa na kujiuliza Rebeka pesa nyingi kama zile amezipata wapi. Wakati huo Rebeka alikuwa amekumbuka kuwa cheki yake ameisahau juu ya dresing table.
Aliingia ndani mkuku na kumkutanayo Kuchu bado anaishangaa alifika na kuinyakuwa mkononi mwa Kuchu huku akibwata.
"Nani kakwambia unichukue."
"Mbona hivyo Rebeka kwani ya nani?"
"Hilo sio swali shida yako nini?"
"Rebeka ni hela nyingi umezitoa wapi?"
"Nimeuza nyumba yangu."
"Ha! kwa nini?"
"Mtu kuuza chake kuna maswali wewe mbona umeuza magari yako nani aliyekuuliza?" kauli ile ilimfanya Kuchu afunge mdomo wake.
Rebeka baada ya kuchukua ile cheki alitoka sebuleni na kwenda kukaa kwenye kochi akiwa amefura kama unga ulioumuliwa na amila. Kuchu naye alitoka nje na kumkuta kwenye hali ile ilibidi aingie kazi ya kumbembeleza.
Rebeka alijiona ni mshindi kwa kujua Kuchu hatamuulizia tena juu ya cheki ile. Kuchu alikuwa amechanganyikiwa kwa kujua alitegemea kuiuza nyumba ya Rebeka kwa siri mpango wake umegonga mwamba. Lakini alishangaa kuiza kwa bei ndogo ya milioni ishirini nyumba ambayo kwa bei ya chini angeweza kuuza kwa milioni sabini nyumba aliyojenga kwa milioni hamsini.
Nyumba aliiona chungu hata hamu ya kula hakuwa nayo aliamua kutoka nyumbani kwake ili akatafute ufumbuzi mwingine au sio ataumbuka huku akijiona pia Rebeka kumkimbia jambo ambalo hakulitaka kuliona katika maisha yake kwa kujiapia kumlinda kwa hali na mali kuhakikisha hampotezi.
Rebeka alifurahia hali ile kwa kupata nafasi ya kwenda benki alisubiri mpaka robo saa na kuwa na uhakika Kuchu hayupo ndipo alipoupara harakaharaka na kuingia kwenye gari na kuelekea benki kuchukua milioni zake ishirini.
Alipofika benki alikwenda hadi kwa keshia na kumpatia ile cheki ambayo moyoni alikuiwa bado haamini huenda amepewa cheki hewa. Lakini hakujutia sana kama atakuwa amemdanganya atakuwa amejidanganya mwenyewe kwa kuwa bado hajampata hana hasara.
Mawazo yake yalikatishwa na muhudumu wa kike wa benki kumwita
"Dada hesabu pesa zako," macho yake hayakuamini maburungutu ya pesa yakiwa mbele yake.
"waaaooo yaani siamini."
"Kwa nini dada?"
"We acha tu," Rebeka alizihesabu zile pesa huku mikono yake ikitetemeka zilikuwa pesa nyingi sana kuzishika maishani mwake. Mhudumu wa benki nusra acheke lakini aliishia kushika shavu kwa kumuonea wivu.
Pesa zote Rebeka aliziingiza benki na kurudi nyumbani akiwa njiani alichekelea moyoni na kumshukuru muumba kwa utundu wake alioupitisha juu yake na kuonekana kipusa mbele ya wanaume hasa wenye pesa. Alijiapia moyoni kumpa Roja Mo penzi ambalo hatajutia pesa alizozitoa hata kumfanya asahau nyumbani kwake.
Majira ya usiku Rebeka kama kawaida yake alijipamba kwa manukato ya kunukia na kuvaa kanga moja. Kuchu alirudi majira ya saa mbili kasoro usiku na kulakiwa na Rebeka Kama kawaida yake kwa kuonyesha uchangamfu wake wa kawada.
Naye kuchu alijitahidi kuonyesha uchangamfu lakini siku zote amuonapo Rebeka hata awe na mawazo gani mawazo yote hufutika hasa anapokumbatiwa na kulisikia joto la Rebeka hupagawa na kusahau kila kitu.

Nini Kitaendelea
 
HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)
SEHEMU: 11
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
SIMU: 0713 646500.
ILIPOISHIA:

Majira ya usiku Rebeka kama kawaida yake alijipamba kwa manukato ya kunukia na kuvaa kanga moja. Kuchu alirudi majira ya saa mbili kasoro usiku na kulakiwa na Rebeka Kama kawaida yake kwa kuonyesha uchangamfu wake wa kawada.
Naye kuchu alijitahidi kuonyesha uchangamfu lakini siku zote amuonapo Rebeka hata awe na mawazo gani mawazo yote hufutika hasa anapokumbatiwa na kulisikia joto la Rebeka hupagawa na kusahau kila kitu.
SASA ENDELEA...
Kama kawaida Rebeka alimvua nguo palepale sebuleni na kumpatia kipande cha kanga na kuelekea naye bafuni kuoga pamoja. Baada ya kuoga na kupata chakula cha usiku, siku hiyo Rebeka alimpa mapenzi mazito yaliyomrusha akili na kumfanya mwanaume mzima kutoa chozi na kumuomba msamaha Rebeka.
"Samahani mpenzi usiniache bado nakupenda ukiniacha nitachanganyikiwa."
"Nani kakwambia kuwa nakuacha bado nakupenda lakini ni makosa kuuza aseti za ndani mimi nakupenda kwa hali yoyote jisikie upo na mke muelewa."
"Asante sana Rebeka nilikuwa kwenye wakati mgumu kutafuta pesa na kukutuliza wewe."
"Usihofu mimi siyo tatizo kwako fanya mambo yako kwa utulivu nina imani mambo yatakuwa mazuri maisha kama bahari kuna kupwa na kujaa."
"Ooh! Asante Mungu kunipa mke mwelewa."
Rebeka alichekelea moyoni kwa kumuona anacheza mpaka asubiri pesa za msimu kama ndizi za kupepea. Moyoni alijiapia kumpenda mwanaume mmoja tu duniani si mwingine ni mzazi mwenzake na mumewe baba Nyangeta Mabogo lakini kwake mwanaume yeyote penzi kwake masirahi.
Rebeka aliona hiyo ndiyo sehemu muhimu ya kuombea ruhusa ya kwenda kusaliti mapenzi kwa awamu ya pili ya kwanza kuisaliti ndoa yake takatifu iliyojulikana mpaka mbele ya Mungu na hii ya pili ya kumsaliti mpenzi wake ambaye kwa sasa maisha yake yalikalia kuti kavu kuanguka si ajabu.
"Mpenzi kesho kutwa nilikuwa naomba ruhusa nikimbie mara moja nyumbani."
"Aah! Mpenzi kuna nini tena si wiki jana ulikuiwa kule?"
"Nilisahau kukueleza samahani kwa hilo nina shda na mama tuna maongezi nilijua nitakueleza lakini mambo yamekuwa mengi naomba unisamehe kwa hilo mpenzi wangu."
"Sawa lakini uwahi kurudi si unajua nyumba bila mwanamke inapooza."
"Kwa jioni sitaweza kurudi siku hiyo bali siku ya pili asubuhi na mapema si unajua maongezi mazuri usiku."
"Hakuna tatizo kwa vile na mimi mambo yangu sio mazuri utawapelekea laki moja."
"Mbona nyingi kila siku siyo lazima uwape nyingi hata kama huna usihofu kule ni kwenu sio lazima kila nikienda lazima pesa nikikosa ina maana nisiende?"
"Wengine hawajui hivyo."
"Labda wawe wanaishi peponi."
"Nashukuru kwa kulitambua hilo," Kuchu naye alikuwa anatafuta njia ya kumtoa Rebeka ili aweze kufanya upekuzi juu ya hati za nyumba na gari alikuwa haamini kama nyumba kama ile kuuzwa kwa kiasi. Kukataa ilikuwa danyanya toto lakini akili ilikua inalenga wapi. Alimshukuru Mungu kwa Rebeka kupata safari itakayo mweka mbali na nyumbani kwao ili afanya upukuzi wa kina bila wasiwasi wowote.
Rebeka alimkumbatia Kuchu kwa mahaba mazito na usingizi mororo uliwapitia.

*****
Siku ilifika kama ilivyopangwa kama Rebeka aliamka na mapema na kumwandalia mpenzi wake kifungua kinywa Kuchu tayari kwenda kwenye mihangaiko yake. Baada ya kifunguia kinywa Kuchu alimuaga Rebeka na kumuomba awasalimie wote kijijini baba na mama mkwe.
Kila mmoja alimla kisogo mwenzie kwa kujiona amefanikiwa mpango wake. Baada ya kuondoka Kuchu, Rebeka alijiandaa na saa tatu juu ya alama alitoka mwenye mlango wa geti la nyumbani kwake.
Roja Mo aliyekuwa amefika saa moja kabla ya muda waliopanga alilishuhudia gari alilokuwemo Rebeka alikuwa na uhakika lazima atakuwa peke yake. Baada ya kumshuhudia Kuchu akitoka muda si mrefu, alimwacha ampite ndipo alipomfuata kwa umbali mfupi.
Rebeka aliendesha gari lake si kwa mwendo mkubwa kwa kujua kuna mtu alikuwa akimfuata baada ya kulipita gari la Roja Mo jirani na nyumbani kwake. Roja Mo alikuja nyuma yake mpaka magari yao kuacha mji ndipo alipo ongeza mwendo baada ya kuwa na uhakika hakuna mtu aliye kuwa akiwafuata.
Alilipita kidogo na kulipigia honi naye Rebeka alijibu kwa kuwasha taa na kuzizima kuonyesha ushara amempata. Baada ya mwendo mfupi waliacha njia ya kwenda shamba na kuelekea kwenye hoteli moja ya kitalii iliyo na hadhi ya kimataifa Biski Hotel.
Waliongozana pamoja hadi hotel ya Biski na kuyaegesha magari yao sehemu salama ya kuegeshea magari pale unasimamisha gari mbele ya hoteli kisha unaliacha kuna wahudumu kazi yao kupeleka kwenye maegesho.
Ni vitu vilivyokuwa vigeni kwa Rebeka waliongozana hadi mapokezi ambako walipata chumba cha hadhi ya juu cha bei kubwa kuliko vyumba vyote vya hoteli ile. Kwa upande wa Roja Mo maeneo yale hayakuwa mageni kwake. Mara nyingi alionekana pale wengi walimjua kwa utajiri wake jina lake lilitawala akilini mwa watu wapo waliomjua kwa sura na wapo waliomjua kwa kusikia au kumuona kwenye vyombo vya habari.
Roja Mo na Rebeka waliongozana hadi kwenye chumba waliochopanga. Kilikuwa cha hadhi ya juu ambayo kwa Rebeka kilikuwa ndio mara yake ya kwanza kuingia aliona kama miujiza alijikuta akijitupa juu ya kitanda kipana kilichotandikwa maridadi.
Roja Mo alimuangalia Rebeka na kumuona jinsi alivyokishangaa chumba alijua ni ugeni wa mambo alimuuliza:
"Vipi mbona kama umeshangaa sana?"
"Siamini yaani najiona kama nipo ndotoni vitu hivi huzoea kuviona kwenye televisheni tena sio nchini nchi za watu leo hii na mimi nimekilalia siamini."
"Amini hivi vitu ndivyo hadhi yako..unataka kuniambia Kuchu hajawahi kukuleta sehemu kama hizi?"
"Utani huo Roja Mo sehemu kama hizi si za watu kama Kuchu nimeamini wewe ni matawi ya juu," Rebeka alimwaga sifa.
"Huwezi kuamini yaani kama ningepata muda niliotaka kukupeleka hoteli za Ulaya wewe Rebeka si wa kulala hooteli ya hadhi ya chini lakini baadaye tutapanga lazima na wewe upande ndege."
"Utani huo!"
"Huwezi amini hata mke wangu hajawahi kulala sehemu kama hii ni wewe peke yako mwenye hadhi ya kulala sehemu kama hizi."
"Usiniambiee!" Rebeka alikurupuka kutoka kwenye kile kitanda na kumvamia Roja Mo kwa kumrukia kama nyani na kuanguka wote kitandani.
"Rebeka ninataka kukufanyia vitu ambavyo vinafanana na hadhi yako, Kuchu anacheza tu uwezo wake haulingani na hadhi yako."
"A.a.lafu eti alitaka kuuza gari langu ili atengenezee gari lake," Rebeka alimwanga siri ya ndani.
"Kiko wapi?...hata mwezi haujafika tayari kile nilichokisema kimetokea."
"Yaani siamini."
"Haya ni madogo makubwa yanafuata."
Rebeka alijitahidi kumpa Roja Mo penzi zito liliomrusha akili na kujikuta akitangaza ndoa siku ile ile. Bila kujielewa alijikuta akimuandikia cheki ingine ya milioni hamsini.
"Rebeka amini hapa ni maji ya bahari yasiyo na mwisho wala yasiyojulikana lini yatapungua sahau kukauka."
Wakati wa kupeana raha Rebeka alitaka watumie mpira wa kiume Kondomu lakini Roja Mo alikataa kwa kusema yeye anajiamini vile vile hata Rebeka anamuamini.
"Rebeka wasiwasi wa nini wewe mke wa mtu hata mimi mume wa mtu vilevile sina tabia ya kurukaruka na siwezi kugharamikia penzi kwa kufanya mapenzi kwa mpira kuna raha gani si bora nimalize haja zangu kwa sabuni?"
"Siyo kwamba sikuamini si unajua kuna mimba zisizo tegemewa ambazo siku zote uharibu mipango ya maisha ya watu."
"Rebeka ni mipango gani itakayo halibika kama ukishika ujauzito, nini kitakachopungua kwenye maisha yako?"
"Hakuna.”
“Au Rebeka unipendi?"
"Aiii honey nisipo kupenda wewe nimpende nani?"
"Nilitaka kushangaa kwanza kama leo Mungu akijalia tukapata mtoto utakuwa mwanzo mzuri namshangaa Kuchu au jogooo lake haliwiki."
Rebeka hakujibu alimumunya midomo na kuachia tabasamu la mbali moyoni alijisemea "Angejua hapa hapendi mtu bali pochi."
Siku hiyo hakuna aliyerudi walilala pale pale hadi siku ya pili.

Nini Kitaendelea
 
HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)
SEHEMU: 12
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
SIMU: 0713 646500.

ILIPOISHIA:
"Nilitaka kushangaa kwanza kama leo Mungu akijalia tukapata mtoto utakuwa mwanzo mzuri namshangaa Kuchu au jogooo lake haliwiki."
Rebeka hakujibu alimumunya midomo na kuachia tabasamu la mbali moyoni alijisemea "Angejua hapa hapendi mtu bali pochi."
Siku hiyo hakuna aliyerudi walilala pale pale hadi siku ya pili.
SASA ENDELEA...

Wakati huo nyumbani baada ya kuondoka Rebeka, Kuchu hakuwa mbali alirudi hadi nyumbani baada ya kuliona gari la Rebeka likikamata njia ya kurudi kijijini kwao.
Alirudi hadi ndani na kwenda moja kwa moja kwenye kabati la nguo na kupekua. Ajabu hakuchukua muda mwingi kukutana na hati za nyumba na gari, alichukua ile hati ya nyumba lakini ya gari aliiacha kwa kujiua atawahi kugundulika.
Aliikumbatia kwa furaha alirudisha vitu kama vilivyo kuwa hakuwa na haja ya kupoteza muda alikwenda kwa mnunuzi wa nyumba ambaye alipatana naye kipindi kirefu. Mnunuzi kwa vile alikuwa na shida na nyumba alimuongezea milion ishirini juu yaani ikawa milioni mia.
Kuchu sasa alijiona ni mwanaume mbele ya wanaume kwa kuweza kutengeneza gari lake na kuweza kununua mengine mawili alijua mpaka anajua atakuwa na pesa ya kununua nyumba nyingine.
Siku hiyo aliingia baa kupata moja moto moja baridi kwa kweli kidogo moyo ulitulia vilevile alikuwa tayari kuliuza gari la Rebeka na kumnunulia la bei ya juu kwa kumuongeza milioni ishirini.
Kwa vile alijua Rebeka arudi usiku ile alirudi usiku wa manane akiwa chakali na kujilaza sebuleni kwenye kochi bila kuvua nguo wala viatu hata mlango alisahau kufumga bila mtumishi wa ndani nyumba ingelala wazi hata kuibiwa na vibaka.
****
Rebeka alirudi nyumbani kwake majira ya saa mbili asubuhi alishangaa kumkuta bwana yake amelala sebuleni alifika na kumshtua.
"Kuchu mume wangu umerudia pombe zake yaani kuyumba kidogo umechanganyikiwa hivyo?"
"Wala jana sijalewa sana lakini kitanda nilikioa kipana kama bahari ndio maana niliamua kulala hapa mazoea yana tabu"
"Oooh pole mpenzi wangu nimeisha rudi twende basi tukaoge"
Alimnyanyua na kuelekea bafuni baada ya kuoga na kupata kifungua kinywa Kuchu alikumbuka anatakiwa gereji kwa ajili ya kulipia vifaa vya gari ili gari litoke kesho tayali kuanmza kazi
"Vipi mpenzi mbona huna hamu na mimi wala kuulizia hali za shamba"
"Ni kweli mpenmzi utanisamehe si ujajua sasa hivi shughuli pevu mambo yamekuwa mazito lazima nihangaike ili kuhakikisha nakufurahisha wewe malkia wangu"
"Hilo nalijua lakini sipendi nmiwe tatizo kwako"
"Huwezi kuwa tatizo kwangu kwa kuwa kukutafutia nmi wajibu wangu"
"Unajua nini sweet huu ni wakati muafaka wa mimi nikusaidie kupunguza ukali wa maisha"
"Una maana gani?"
"Nataka nirudie biashara zangu za zamani ambazo kwa sasa nina zoefu nazo"
"Wewe unajua sasa hivi hali yangu ya kipesa sio nmzuri mtaji utapata wapi?"
"Suala la mtaji lisikuumize akili nina pesa za mtaji baada ya kuuza nyumba"
"Mmmh sawa"
Kauli ile ilimfanya Kuchu awe na mawazo tele kichani na kujiuliza inma maana zile milion kumi amezitoa wapi?Lakini hakutaka kumuuzi kwa kujua kukuudhi ni mwanzo wa kuachika.
Baada ya makubaliano walipanga kuanzia wiki ijajo ataanza shughuli ya biashara vile vile akutakiwa kuhoji ni biashara gani.Kuchu alijiona sawa na mbwa mkubwa asiye na meno hata akibweka ni kazi bure aliishia kunyamaza akijua lazima Rebeka ameisha ota mapembe.
Moyoni alijutia uamuzi wake wa kuishi na Rebeka maisha ya kifahari yaliyomghalimu pesa nyingi na kujikuta uchumi wake ukiyumba.Lakini alimuomba Mungu ili Rebeka asigungue upesi kama nyumba yake imeuzwa kama gari lake la milioni nane amekuwa mkali kiasi kile nyumba ya milioni sabini si patachimbika.
***
Kama ilivyo kawaida matajiri wanapokutana kila mmoja alikuwa na majingambo yake. Kikundi hiki wa matajiri sifa zao kubwa ni kushindana kupata Mwanamke mzuri hushindana kwa dau kubwa kumpata kimwana yoyote.
Kila msichana mwenye sifa hushindana kumpata atakaye fanikiwa kumpata kabla ya wenzake hupewa milioni mia moja hamsini kama zawadi ya kuwadizi kete wenzie. Mara nyingi wamekuwa wakitafuta ni msichana gani gumzo mjini au katika vyombo vya habari mamisi wote waliwanasa kwa mitindo hiyo ya kutoa pesa nyingi ambazo huzirudisha kwa mtindo huo wa kulipwa. Wao hushindana kila mtu kwa wakati wake kuhakikisha anampata na akiishampata huchukua picha za mchezo mchafu na kuziwakilisha kwa wenzake hapo hupewa kitita chake na kutoa ruksa kila mtu aonje kwa wakati wake.
Matajiri watano walikutana kama kawaida yao siku ya pili toka Roja Mo afanikiwe kumnasa Rebeka ambaye kwa kipindi kile kila mmoja alikuwa akimpigia mahesabu makali. Kikao chao kama kawaida kilihudhuriwa na Sabri, Yusuf Msumi, Mualani na Kanuth.
Kanuth kama kawaida yake haya mkuu lete utamu naona leo unafuraha isiyo kifani."
"Jamani mnakumbuka tuliweka dau kiasi gani kwa atakaye mnasa Rebeka?"
"Rebeka yupi, mke wa Kuchu?"
"Haswaaa."
"Milioni mia mbili."alisema Yusuf
"Haya wakubwa nipeni changu," alisema huku akinyoosha mkono.
"Muongo utawahi wewe mdomo wa zege" alijibu Sabri.
"Sasa hivi naitwa mdomo wa kasuku kila siku niwapeni nyinyi leo na mimi nimelamba dume la mchezo."
"Haya baba tusiandikie mate tupe vielelezo"alisema Mualami.
Roja Mo alitoa kamera yake ndogo na kuchoka waya kwenye screen kisha aliiwasha wakubwa walianza kuangalia live kwa macho yao. Hakuna aliyeamini alikuwa Rebeka kweli hawakuwa na jinsi milioni mia mbili ziliwatoka.
Roja Mo baada ya kupata kiasi kile alisema kwa lugha ambayo wengi hawakuipenda.
"Jamani huyu siyo kama mchezo wetu wa kila mtu kuonja bali huyu mmuheshimu kama shemeji yenu nina mpango wa kuoa kabisa."
"Utani huo utamuoaje mke wa mtu?" Sabri aling'aka.
"Kwani hata Kuchu naye alimpata kwa njia hii hii hakuna la ajabu," Roja Mo alijitetea.
"Hii haiwezekani mara ngapi umekula vyetu leo wewe umepata umeona kitamu cha kula peke yako?" alihoji Yusuf.
"Jamani eeeh, nimeisha sema yoyote atakaye ingiza timu tutaonana wabaya nitammwaga mtu ubongo," Roja Mo alikuwa mkali.
"Usitutishe bwana labda mzikwe kaburini lakini kama duniani lazima tutamlamba hata kwa bilioni kumi nitamtia mikononi," Sabri hakukubali.
"Si wewe, hata mimi," aliongezea Mualami.
"Si kwa mtu mmoja mmoja bali kwa watu wote"alimalizia Kanuth.
"Nimeisha sema kazi kwenu kuchezea sharubu za Simba," Roja Mo alitoa onyo.
Roja Mo alisema yale na kuondoka akiwaacha wenzake wakijadiliana juu ya kauli yake iliyokwenda ndivyo sivyo.
*****
Kitendo cha Roja Mo kula vya wenzake lakini vya kwake kuwa vigumu viliwafanya matajiri wenzake kufanya mkutano wa muda ili kumkomoa Rebeka. Walipanga kumpata kwa gharama yoyote lakini lazima wamkomoe Roja Mo na Rebeka kwa tabia zake za kugeuzwa kipusa na kuonekana yeye ni zaidi ya wanawake wote duniani.
Wakati wakipanga hivyo Roja Mo alikuwa ameandaa harusi ya siri ambayo alingeifanya kwa siri ili kuwashitukliza rafiki zake wasiweze kumchezea kwa kuwa atakuwa mke wa mtu tayali.
Ilikuwa ndoa ya mkataba walioandikishiana mbele ya wanasheria ambayo Roja Mo alimlipa Rebeka Milioni sabini nyumba ya thamani ya milioni hamsini na gari aina ya Toyota Vx new model na mkataba wandoa ya miaka mitano.
Ndoa ilifungwa na kuhudhuliwa na watu wachache wenye nyadhifa serikarini na matajiri wa mbali tofauti na rafiki zake akina Mualami,Sabri, Kanuth na Yusuf.
Ilikuwa ndoa iliyofanyika kwenye hoteli ya kifahali ya Biski Hotel iliyogharimu milioni mia moja. Baada ya ndoa Rebeka aliohamia rasmi kwenye nyumba yake iliyokuwa nje ya mji iliyokuwa na hadhi kubwa.
Kwa upande wa Kuchu alikuwa kwenye kipindi kizito cha kumtafuta mkewe ambaye alikuwa amepotea zaidi ya wiki nzima. Alipokwenda kwao walishangaa kuambiwa hawajui habali zozote za Rebeka wao wanajua yupo mjini na yupo kwake japokuwa mwanzo walipinga kitendo cha mtoto wao kumkimbia Mabogo lakini zawadi na pesa ziliwaziba mdomo na kumuona mwanaume anayefaa kuwa na mtoto wao ni Kuchu na si Mabogo.
Taarifa za kutokuwepo kulimchanganya kwa hali ya juu na kumpa presha alijua lazima amezidiwa akili na wajanja kama alivyomzidi mume wa Rebeka wa ndoa. Alijikuta akipoteza mwelekeo alirudi nyumbani na kuwa kama aliyefiwa, rafiki zake wa karibu walimuonea huruma kwa kumwambia kuwa mwanamke kama Rebeka ni hatari kwa mwanaume mwenye kipato kidogo vilevile walimwambia asiumie sana kwa kuwa hata yeye alimpata kwa mtindo ule.
Rebeka kama kawaida yake alikwenda kwa Kuchu akiwa kwenye gari aina ya toyota Vx hadi ndani. Aliteremka hadi ndani na kumkuta Kuchu akiwa na rafiki zake walipo muona wote walishtuka.
Hakuwa Rebeka yule waliomzoea alikuwa kwenye mavazi ya gharama kubwa mkononi alikuwa na simu ya milioni, kila kidole kilikuwa na pete ya dhahabu na shingoni alikuwa na mkufu wa milioni mbili na nusu.
Rebeka alionekana mwanamke wa gharama kitu kilichofanya hata marafiki wa Kuchu kukili moyoni kuwa Rebeka si hadhi ya Kuchu.

Nini Kitaendelea
 
HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)
SEHEMU: 13
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
SIMU: 0713 646500.

ILIPOISHIA:
Hakuwa Rebeka yule waliomzoea alikuwa kwenye mavazi ya gharama kubwa mkononi alikuwa na simu ya milioni, kila kidole kilikuwa na pete ya dhahabu na shingoni alikuwa na mkufu wa milioni mbili na nusu.
Rebeka alionekana mwanamke wa gharama kitu kilichofanya hata marafiki wa Kuchu kukili moyoni kuwa Rebeka si hadhi ya Kuchu.
SASA ENDELEA...

Kuchu ambaye alikuwa bado amepigwa butwaa alishtusha na salamu ya Rebeka.
"Jamani habari za saa hizi?"
"Nzuri," walijibu wote kasoro Kuchu ambaye alikuwa bado amejikunyata kwa majonzi, Rebeka ile hali aliijua lazima itatokea lakini haikuwa ngeni machoni na moyoni mwake. Mwanaume ambaye ilikuwa ni vigumu kutoa maamuzi ya kuvunja mapenzi ni mumewe Mabogo, lakini aliweza kukaza moyo na kumeza mfupa itakuwa Kuchu mtu aliyempenda penzi masilahi.
Rebeka akiongea kwa kujiamini alisema:
"Jamani naomba mnipe nafasi niongee na mpenzi wangu," wale marafiki wa Kuchu walitoka nje na kuwaacha wapenzi, wakati huo Kuchu alikuwa bado amejiegemeza upenuni mwa sofa akiwa ameangalia chini kwa hudhuni huku machozi yakimtoka.
Rebeka alimsogelea na kukaa pembeni yake na kuzifanya pua za Kuchu kupokea manukato ya bei mbaya. Rebeka aliupitisha mkono wake laini shingoni kwa Kuchu na kumpapasa kitu kilichofanya mwili wake kusisimka na kujikuta akiongea kwa sauti ya kilio.
"Lakini kwa nini mpenzi umeamua kunifanya hivyo?"
"Aaah mpenzi kukufanya nini tena?"
"Yaani umeamua kuniacha kosa langu nini?"
"Huna kosa lolote mpenzi."
"Hapana mpenzi ni wazi kuna kitu ambacho nilikuwa nakuudhi lakini hukutaka kuniambia na kuamua kunihukumu bila kujua kosa langu lakini bado nilikuwa na muda wa kujirekebisha."
"Wala siyo kama unavyofikilia basi tu kila chenye mwanzo kina mwisho wake kama nilivyotoka kwa mume wangu wa kwanza na wewe vilevile."
"Yaani umeona umenifilisi ndio unanikimbia."
"Wasiwasi wako tu mimi kwa taarifa yako naondoka kama nilivyo kuja siondoki na nyumba wala gari vyote nakuachia pia zile pesa ulizobahatika kuziona milion kumi nitakuachia sitaki uyumbe kimaisha nina imani tumeelewana," Rebeka alisema kwa sauti ya upole.
"Siyo hivyo Rebeka nimekuzoea."
"Huwezi kunizoea kama mume wangu Mabogo."
"Lakini kumbuka wewe bado mke wangu bado sijakupa talaka."
"Kuchu usinichekeshe mimi na wewe tumefunga ndoa kwa mkuu wa mkoa, lakini Mabogo tumefunga kanisani ndoa inayotambuliwa na Mungu wewe na Mabogo nani mume wangu?"
"Tuachane na hayo Rebeka bado nakupenda usiniache nitakuwa kwenye wakati mgumu," Kuchu alijitetea.
"Kuchu fanya kama mtu kufa, hufa akiwa anaipenda dunia lakini kila kitu na wakati wake na mapenzi vile vile hujivunii mapenzi yetu yamezaa faida nimekuachia kila kitu au ulitaka niondoke na vitu vyangu?"
"Hapana."
"Basi ndio hivyo nimekuja kukuaga rasmi kuwa sasa hivi ni mke wa mtu naomba upokee pete yako kwa kuwa sasa hivi haina nafasi. Ila nakuomba uwe mstaarabu kama Mabogo zaidi ya hapo utajiingiza matatani nami sipendi ifikie hatua hiyo kwa kuwa niliye naye kwa sasa uwezo wake una karibiana na nguvu za mkuu wa nchi," Rebeka alisema kwa kujiamini.
Rebeka alimkabidhi pete Kuchu ambaye hakuipokea zaidi ya kupiga magoti kumuomba Rebeka abadili mawazo.
"Kuchu kubadili mawazo ningebadili kwa mume wangu ambaye nilimuacha nikiwa nampenda na bado nampenda mpaka kufa moyoni mwenye nafasi ni yeye kwa mwingine penzi masilahi....Ila Kuchu usikate tamaa zichange kama mambo yako yatakuwa safi na mimi sijazeeka unaweza kabisa kurudisha majeshi nyumbani."
Rebeka aliangalia saa yake na kumueleza Kuchu.
"Kuchu muda niliopewa na mume wangu umeisha naomba ruksa niondoke ila kabla ya kuondoka tuongozane kwenye gari nikupe milioni zako ishirini nina imani milioni moja ina uwezo wa kukurudishia furaha yako kwa kuoa mpenzio uliyekuwa ukimpenda kabla yangu.
“Sina imani kama ulikuwa ukinipenda mapenzi ya dhati zaidi ya kuvutiwa na umbile na sura yangu kwa kuniweka ndani kama fenicha bado naamini aliyenipenda mapenzi ya kweli ni mume wangu Mabogo kwa kuwa ameniokota nikiwa sina hata viatu si ninyi mliyenipenda kwa kuniona nimeisha pendeza kabisa."
Kuchu hakuwa na la kuzungumza zaidi ya kuvuta kamasi kwa ndani huku akifuta machozi kwa mkono. Hata nguvu za kunyanyuka kutoka nje hakuwa nazo Rebeka alikwenda hadi kwenye gari na kuchukua mkoba wenye burungutu la pesa na kumpelekea Kuchu ndani aliinama na kumpiga busu kisha alisema:
"Kwa heri ya kuonana," Kuchu hakujibu hilo Rebeka hakulijali aliondoka bila kugeuka nyuma hadi kwenye gari na kuondoka zake.
******
Maisha ya Mabogo na Bibiana yalishamili kila kukicha na Bibiana alitumia uwezo wake wote kuziba pengo la Rebeka. Hakuna aliye amini kuwa Nyangeta si mtoto wa kuzaa wa Bibiana, alipata malenzi yote ya mtoto tena yenye mapenzi mazito.
Mabogo na yeye hakuwa na hiyana aliamua kumuoa kabisa Bibiana kwa mkuu wa mkoa baada ya kanisani kugomewa kwa kujua ndoa ilikuwa moja ya Mabogo na Rebeka ambayo hutenganishwa na kifo.
Harusi ilipendeza iliyohudhuliwa na watu wengi mmoja wapo aliyehudhulia lakini bila kualikwa alikuwa Rebeka ambaye alimzawadia Bibiana gari dogo aina ya LAV4. Aliyemuona Rebeka siku ya harusi hakuamini hata shoga zake walikuwa wamempotea alikuwa amebadilika kwa kiasi kikubwa kwa mwili hata mavazi na mapambo ya bei mbaya.
Wengi walimfananisha na mzungu kwa kuonyesha mapenzi ya dhati kwa mke mwenzie Bibiana msichana aliyemuacha kama mtumishi wa ndani ambaye aligeuka kuwa mke mwenzie.
Muda wote wa harusi alionekana mwenye furaha aliyekuwa mstari wa mbele kwenye shughuli zote za harusi. Hata baada ya harusi alipata muda wa kuongea na maharusi kwa kutoa nasaha zake kwa kumuomba Mabogo amtunze Bibiana na ampende kama alivyompendwa yeye.
"Nina imani moyo wa Mabogo ulikuwa na nafasi moja ya upendo kwangu lakini naomba ile nafasi yangu japo nina imani huwezi kumpa yote basi mpe hata nusu ya upendo...
“Si kwamba moyo wangu una furaha basi tu ni macho tu yanacheka na midomo kutabasamu lakini moyoni ni majuto nina imani Mungu huumba wanaume na wanadamu wenye mfano wake mmoja wapo ni wewe Mabogo.
“Mwanaume unayejua mapenzi kwa mwanamke na ni mwalimu mwema, naweza sema najutia maamuzi yangu ya kuachana na wewe vilevile naweza sema siyajutii kwa kuwa kila kitu hupangwa na Mungu ila amini bado nakupenda na upendo wangu utakoma pale roho itakapo tengana na mwili...
“Lakini upendo wangu usikufanye usimpende mke mwenzangu, Bibiana, kwanza nashukuru kwa kuweza kutuliza maumivu ya moyo ya mume wangu. sitakoma kumwita mume wangu kwa kuwa ndoa yetu tayari tuliisha iandika kwenye kitabu cha Mungu na haifutiki mpaka kifo.
“ Bibiana nakuomba umlee mume wetu kama ulivyomlea ukiwa mtumishi wa ndani, japo nipo mbali nanyi kila kizuri utakacho kifanya nitakupa zawadi ambayo itakuwa kumbukumbu maishani mwako hii ya leo ni mwanzo vilevile habari nimezipata juujuu japo hamkutaka nijue.
“Lakini Mabogo mimi na wewe ni ndugu na aliyetuunganisha ni Nyangeta. Nioneni ni mmoja ndani ya familia nakuombeni msinitenge vilevile nikiomba ushauri msisite kunipa. Mabongo sitampenda mwanaume yoyote chini ya jua zaidi yako, wewe ni zaidi ya mwanaume Mungu akulinde na akuongoze kwa kila jambo."
Baada ya nasaha zile Rebeka alimkabidhi Mabogo milioni hamsini kama mchango wake wa harusi na kuanzia maisha mapya ya kifamilia. Mabogo ambaye hakuwa na kinyongo tena na Rebeka alishukuru kwa moyo aliouonyesha na zawadi alizotoa za gari na pesa taslimu. Rebeka aliondoka na kuwaacha maharusi wapumzike na kurudi nyumbani kwake.

Nini Kitaendelea?
 
HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)
SEHEMU: 14
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
SIMU: 0713 646500.

ILIPOISHIA:
Baada ya nasaha zile Rebeka alimkabidhi Manogo milion hamsini kama mchango wake wa harusi na kuanzia maisha mapya ya kifamilia. Mabogo ambaye hakuwa na kinyongo tena na Rebeka alishukuru kwa moyo aliouonyesha na zawadi alizotoa za gari na pesa taslimu. Rebeka aliondoka na kuwaacha maharusi wapumzike na kurudi nyumbani kwake.
SASA ENDELEA...
*****
Wakati tajiri Roja Mo akitumia uwezo wa kipesa wa kumdhibiti Rebeka asiguswe na mtu kwa kumwekea walinzi ambao walikwenda nao kila kona aliyokwenda kitu kilicho mnyima raha Rebeka na kujikuta anakorofishana na Roja Mo.
"Sikiliza Roja Mo hii tabia ya kunifanya kama gaidi hatari mimi siiwezi."
"Una maana gani tena ma sweet?"
"Hivi hawa watu uliowaweka wanifuate mpaka chooni ni wa nini?"
"Ha! Ina maana wanakufuata mpaka chooni?"
"Kunisimamia nje ya choo nikiwa chooni kuna tofauti gani hata nikipumua wanasikia mimi siwezi mambo yenyewe kama ndio hivyo mimi siwezi bora tuachane nina imani huniamini ndio umeniwekea walinzi ili nisikimbie...
“Sikiliza Roja Mo nimekuvumilia sana lakini sasa naona inatosha pesa zako zote nakurudishia hata sasa hivi sina dhiki kiasi hicho. Tena tuongozane nikakupe pesa zako na liba juu hutaona nateteleka pesa ninazo nahitaji mapenzi ya kujitanua mimi mbona sikufuati unapokwenda au kumtuma mtu...
“Au huniamini bora tuachane mapenzi bila kuaminiana hayana raha na wala hayana muhimu ya kuwapo bora tuachane utakufa na presha bure."
"Nakuamini lakini nawaogopa rafiki zangu wanaweza kunipora."
"Kivipi?"
"Wanaweza kukupa pesa zaidi yangu na kukuchukua kitu ambacho sipendi kitokee maishani mwangu."
"Ha! Roja Mo ina maana ulikuwa ukinidandanya?"
"Kuhusu nini?"
"Si uliniambia kuwa pesa za rafiki zako wakizichanganya ndio zinafika robo ya za kwako sasa mbona sikuelewi?" Rebeka alikuja juu.
"Pamoja na hayo mwanamke mzuri kama wewe hutakiwi utembee hivihivi kulindwa ni haki yako kama mke wa Rais."
"Ni mke wa Rais kwangu kama unataka niwe na wewe nataka uhuru umenikuta na uhuru wangu sipendi uninyang'anye..siku zote heri maskini huru kuliko tajiri mtumwa nasema tena sitaki."
"Nimekuelewa..lakini safari za mbali basi nitakupa mtu akusindikize."
"Ina maana kwetu siku hizi nimepapotea?"
"Sina maana hiyo kwa usalama wako."
"Sasa sikiliza tuondoe mzizi wa fitina kuanzia leo kila kona nitakayo kwenda tutaambatana na wewe."
"Itakuwa vigumu si unajua mimi nina mihangaiko kuongozana na wewe kila wakati kazi zitasimama."
"Sasa unataka kuniambia mimi mwanamke nikishikwa na hamu zangu unaniruhusu kuzimalizia kwa mlinzi wako?"
"Kwa nini?"
"Ndiyo maana hutembea peke yangu nishikwapo huwahi nyumbani kukuwahi ili umalize hamu zangu au tukiwa pamoja tunaweza kunimazia kwenye gari."
"Mmh, haya."
"Mmh, haya umekubali lipi kati ya yote tuliozungumza?"
"Safari zako utakwenda peke yako," Roja Mo alikubali yaishe.
Baada ya mjadara mrefu hatimaye Rebeka aliweza kwenda safari zake akiwa peke yake bila mlinzi. Wakati huo Roja Mo alimweka mtu kwa siri afuatilie nyendo zake.
Naye Rebeka katika mizunguko yake kuna mtu alimuona zaidi ya mara zote anazokuwa kwenye mizunguko yake lakini hakumtilia maanani. Siku moja akiwa anatoka chumbani ambako aliingia kwa ajili ya kulala lakini usingizi haukupatikana na kuamua kurudi sebuleni kukaa na mpenziwe wake.
Alipotoka Sebuleni bila taarifa alimuona kijana ambaye hakuwa mgeni machoni mwake kwa kumuona maeneo mengi anayokuwepo.Yule kijana alikuwa akimpa Kamera automatic digito. Alisimama kimya mlangoni bila kusema lolote na kushuhudia tendo la kukabidhia ile kamera.
Baada ya kukabidhiana Roja Mo alimpa yule kijana pesa ambazo zilikuwa nyingi kiasi zilikuwa noti za elfu kumi kumi. Rebeka alijikuta akijiuliza zile pesa alizopewa na za nini na ile kamera ni ya kazi gani vilevile alijiuliza yule kijana kukutana naye kila sehemu alizo kwenda alikuwa na nia gani?.
Yule kijana aligeuka ili aondoke aliponyanyua macho walikutanisha na Rebeka na kumfanya kushtuka na kupoteza muelekeo wa kwenda japo hapakuwa na kitu alijikwaa na kuanguka.
Kama angekuwa peke yake angetimua mbio, alijikuta akiaga mara mbili.
"Aaaah! Mama, shikamoo, kwa heri."
Rebeka alitabasamu huku akipiga hatua kuelekea kwenye makochi alipokuwa amekaa Roja Mo. Naye Roja Mo alishikwa na butwaa kwa kitu ambacho hakuwa amekitegemea alijua Rebeka muda ule atakuwa amelala.
Aliiweka ile kamera ndogo pembeni yake ili Rebeka asiione lakini kumbe Rebeka alikuwa ameishaiona muda mrefu na yeye kujifanya hajui chochote. Alipofika karibu wakati yule kijana jasho lilikuwa likimtoka kwa hofu.
"Vipi kaka yangu mbona hivyo?"
"Aaah anasumbuliwa na maralia ndio maana anatetemeka na jasho kumtoka," aliwahi kujibu Roja Mo.
"Oooh! Basi awahi dawa si unajua kuiwahi homa ni vizuri..pole sana," Rebeka alisema kwa sauti ya upole.
"A.a.asa.ante."
Yule kijana aliondoka kabla ya kuondoka alipopiga hatua mbili Rebeka alimwita kitu kilichomfanya yule kijana kushtuka na kijikuta akilazimisha miguu yote itembee kwa wakati mmoja na kumfanya ampige mweleka mwingine.
Kitu kilichozidi kumpa wasiwasi Rebeka na kujiuliza yule kijana ana siri gani na mumewe. Mwanguko nusra umchekeshe Rebeka, Roja Mo alishangaa ni wasiwasi gani alioupata yule kijana lakini aliamini Rebeka hajui kitu.
Yule kijana baada ya kuamka pale chini alirudi huku bado hofu ipo moyoni Rebeka alimtoa hofu.
"Oooh! Pole sana kaka yangu inawezekana ni maralia kali uliiachia muda mrefu na kusababisha kukimbilia kwenye viungo," yule kijana hakujibu kitu aliangalia chini tu.
"Samahani kwa kukurudisha nilitaka kuuliza kama amempa pesa za dawa kama bado nimpatie hata elfu tano," Rebeka alisema kwa sauti ya upole.
"Nimeisha mpa elfu kumi,"alijibu Roja Mo.
"Zitamtosha au tumuongezee?"
"Nina imani zinatosha kama zitapungua nimemwambia arudi."
"Siyo mbaya wahi basi kununua dawa kaka yangu."
"Aa.asante mama," yule kijana alijibu na kugeuka kwenda zake.
Baada ya yule kijana kuondoka Roja Mo alibadili mada:
"Vipi mpenzi mbona hukulala?"
"Yaani kulala peke yangu wewe ukiwa sebuleni wala usingizi hauji ndio maana nimekufuata nilale kwenye kifua chako."
"Haya njoo ulale au twende chumbani?"
"Vyovyote vile."
"Basi twende chumbani hata mashetani yakipanda ni rahisi kuyapunga."
"Kama ulijua."
Waliponyanyuka Roja Mo aliiziba ile kamera kwa mto wa kochi tukio lote Rebeka aliliona na kujawa na maswali mengi juu ya ile kamera. Hakusema kitu waliongozana chumbani lakini kabla ya kuingia chumbani Rebeka alirudi kwenye kochi na kunyanyua mto wa kochi na kuichukua ile kamera.
Tukio lile la ghafla lilimfanya Roja Mo abakie kinywa wazi na kushindwa aongee nini. Rebeka aliichukua ile kamera na kusema:
"Mpenzi hii kamera ilikuwa wapi?"
"Aaa..aa mbona ipo."
"Oooh sawa." Rebeka aliishika ile kamera mkononi akionyesha kutokuwa na wasiwasi nayo. Kitu kilichompa imani Roja Mo kuwa hajui lolote wala hajui kinachoendelea ndani ya kamera.
Waliingia mpaka chumbani Rebeka aliiweka ile kamera juu ya droo ya kitanda na kujitupa kitandani kitu kilichozidi kumpa uhakika Roja Mo hakuna tatizo lolote na kuondoa hofu na kuendelea kufaidi mapenzi.
Rebeka mwanamke aliyekuwa amekubuhu kwenye fani ya mapenzi alitumia uwezo wake wote kumchosha Roja Mo na kumlazimisha kulala usingizi bila kupenda kwa uchovu. Baada ya kupata uhakika Roja Mo amelala aliamka na kuifungua ile kamera iliyokuwa juu ya droo ya kitanda.

Nini Kitaendelea?
 
HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)
SEHEMU: 15
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
SIMU: 0713 646500.

ILIPOISHIA:
Rebeka mwanamke aliyekuwa amekubuhu kwenye fani ya mapenzi alitumia uwezo wake wote kumchosha Roja Mo na kumlazimisha kulala usingizi bila kupenda kwa uchovu. Baada ya kupata uhakika Roja Mo amelala aliamka na kuifungua ile kamera iliyokuwa juu ya droo ya kitanda.
SASA ENDELEA...

Aliangalia picha zilizo hifadhiwa alikuta picha nyingi zote zikiwa za kwake za siku ile na kila kona aliyofika ilikuwa imepigwa picha. Lakini hakukuwa na picha mbaya pamoja na kutokuwa na picha mbaya ilionyesha ni jinsi gani asivyo muamini kitu ambacho alijua bado ni kumnyima uhuru.
Aliirudisha kama ilivyokuwa na kujilaza pembeni ya Roja Mo kwa kuwa na yeye alikuwa amechoka usingizi ulimpitia. Alipoamka walikwenda kuoga na kupata chakula cha usiku bila kuonyesha mabadiliko yoyote.
Wakiwa kitandani Rebeka ndipo alipo muuliza Roja Mo kuhusiana na picha zile
"Mpenzi nina imani bado huna imani na mimi kwa hiyo hakuna umuhimu wa mimi kuwa na wewe."
"Ha! kwa nini?" Roja Mo alishtuka.
"Nilikueleza nini na unafanya nini?"
"Lakini si nimefanya kama ulivyo niagiza."
"Hujafanya."
"Lini umefuatwa na mtu?"
"Siku zote toka tulipokubaliana haya toka utume vibaraka vyako nimefanya lipi baya?"
"Rebeka mbona sikuelewi?"
"Tatizo unanifanya mimi kama mtoto mdogo au kuwa na pesa unaweza kuwa na akili nyingi."
"Bado sijakuelewa una maana gani mbona kila dakika unanipa presha?"
"Mimi na wewe nani ampae mwenzie persha...Sikiliza Roja Mo nimechoka yaani kumbe kila niendapo nafuatwa na watu ya nini kama huniamini tukae pamoja?"
"Nisamehe Rebeka nakupenda sana."
"Anayenipenda ni mmoja."
"Nani huyo?"
"Mume wangu."
"Mbona sikuelewi mume wako nani kama sio mimi?"
"Nyinyi wote hamuwezi kuwa waume zangu bali mmoja."
"Ni kauli gani za kunidhalilisha hivyo Rebeka?"
"Aha! Mimi ndiye ninaye kudhalilisha kama sio wewe kuniwekea watu mpaka chooni sasa hivi kila ninalofanya napigwa picha mbona mwaka huu makubwa!"
"Sina maana hiyo, sipendi kukupoteza nakupenda sana."
"Usijidanganye mapenzi kama kifo siku ikifika haina ujanja hakuna aliyeweza kuzuia kifo hata mtu umpende vipi ni Mungu pekee na mapenzi vilevile na kwa mtindo huu hatufiki mbali."
"Basi nakuhakikishia lolote litakalo tokea kwa upande wangu litakalo kukwaza ruksa kutoa maamuzi yoyote."
"Mimi tena siongei ni vitendo tu vitafuata."
Kauli ile ilimuweka Roja Mo kwenye wakati mgumu sana wa kujilinda asimkosee lolote Rebeka kauli yake mwenyewe ilikuwa sawa na kitanzi alichojivisha mwenyewe.
*****
Wakati Roja Mo akiwa kwenye mtihani mzito wa kulinda vitendo vyake vya vivu wa kitoto wenzake walikuwa kwenye mkakati mzito wa kuhakikisha wanamshikisha adabu kwa kitendo chake cha kupenda kula vya wenzie lakini vya kwake vigumu.
Kikao kiliendesha chini ya Alfonsi Lemba katika mkakati wa kumchukua Rebeka binti aaliyekuwa gumzo na tishio machoni mwa wanmaume kila mwanaume mwenye pesa bila kutembea na Rebeka alijiona amepungukiwa kitu fulani maishani mwake.
Kikao kiliendelea kila mmoja alitoa maoni yake kuhakikisha wanampata Rebeka na kuhakikisha wanafanya kitu kitakachomfanya Rebeka aukimbie mji na kumtia aibu ya mwaka Roja Mo.
"Sasa wakubwa mnasemaje kwa kuwa tupo wote mimi si muongeaji peke yangu"alisema Lemba
"Vilevile kama tulivyo zungumza ni mchango kabambe kila mmoja avunje benki mkataba wa harusi ile nimesikia ni milioni mia mbili themanini"alisema Muarami
"Mm,h kweli mshikaji alipania...lakini kwa vile tumeamua kumshikisha adabu kila mmoja milioni mia moja sifa kubwa ya Rebeka penzi kwake masirahi kama atapa zaidi aliyopewa na Roja Mo tutaweza kufanikisha mpango wetu," aliongezea Kanuth.
"Jamani kwa upande wangu milioni mia moja ni nyingi labda sabini nitajitahidi kidogo japo vilevile nitakuwa nimeumia,"alisema Yusufu Msumi.
"Lakini mimi nawazo tusiwe na wazo la kuvunja mkataba bali tumteuwe mmoja wetu amtokee Rebeka kwa penzi la saa moja la malipo ya milioni mia mbili lazima atakubali mi namjua yule mwanamke anaijua pesa hawezi kukubali kuiacha milioni mia mbili kwa saa moja sijui wazo langu mnasemaje?"alisema Lemba.
"Ndiyo maana tulikuchagua mwenye kiti kwa mipango ya kuona mbali nina imani ni mpango mzuri na wenye gharama nafuu kama ukifanikiwa," alisema Kanuth.
"Nina imani mia kwa mia lazima ataingia ni mtego wa kibwege sana," alisema Yusufu.
"Siku zote ndege mjanja unaswa na mtego mbovu," aliongezea Muarami.
"Haya nani wa kumtuma kufanikisha mpango wetu," aliuliza Lemba.
"Kuna mwingine zaidi ya doctor love Kanuth," alisema Muarami.
"Basi Kanuth ndiye tuliyempa jukumu zima la kuhakikisha Rebeka anaingia anga zetu tayari kufanya kitu cha kihistoria ambacho kitachukua muda kupotea akilini mwa mwatu na wewe usitufanye kama Roja Mo tutatoana uhai ooho," walimtaadhalisha.
"Mmh, kweli Rebeka maneno mengine usipo kuwa na moyo utaganda kama ruba lakini lazima Kanuth uishinde nafsi ili tumshikishe adabu Roja Mo ," alisema Muarami.
"Mimi kwangu kitu cha kawaida nyinyi wenyewe mtanivulia kofia na kunipigia saruti."
"Mchango mpaka kesho jioni uwe umekamilika kazi iishe wiki hii hii ili tufikirie mambo mengine maana suala hili limetukosesha raha kabisa ," Lemba alifunga kikao
Kikao kilifungwa kila mmoja aliondoka tayari kwa utekelezaji wa kuleta pesa kiasi cha milioni hamsini kila mmoja tayari kufanya dhalilisho kwa mwanamke mrembo mwenye kila sifa ya uzuri binti mrembo Rebeka.
***
Baada ya kukabithiwa milioni mia mbili Kanuth alikuwa akitembea nazo kwenye gari kufuatilia nyendo za Rebeka kila kona aliyokwenda. Ilichukua wiki ndipo siku moja alibahatika kumkuta Rebeka akiwa ameharibikiwa na gari.
Kanuth alisimamisha pembeni yake wakati huo Rebeka alikuwa akijiandaa kumjulisha fundi wake aje. Ulikuwa muda mzuri kwa Kanuth kujaribu bahati yake, kipindi kile Roja Mo alikuwa amesafiri nje ya mji kwa siku moja kwa ajili ya shughuli zake.
Baada ya kusimamisha gari alimfuata Rebeka ambaye ilionyesha simu aliyopiga ilikuwa haipatikani. Sura ya Kanuth haikuwa ngeni kwa Rebeka lakini hakukumbuka aliiona wapi.
"Samahani shemeji."
"Bila samahani kaka yangu."
"Una tatizo gani?"
"Hata sielewi gari limenizimikia ghafla."
"Ngoja nijaribu bahati yangu."
"Kwani wewe ni fundi?"
"Huwa najaribu mara nyingi gari langu matatizo madogo madogo humaliza mwenyewe."
"Jaribu na hapa," Rebeka aliongea huku akiokota jani kavu chini, macho ya Kanuth yaliyua juu ya umbile la Rebeka mapigo ya moyo yakimwenda mbio alijikuta akisahau kutoa msaada na kuendelea kuyaacha macho yake yaendelee kufaidi umbile la mwanamke ambalo mwake lilikuwa adimu. Alikiri Roja Mo kuwa alikuwa na kila sababu kutotoa basi ule si mpira wa kutoa pasi lazima ufunge mwenyewe.
Hata Rebeka alipo nyanyuka baada ya kuokota jani alikutanisha macho na Kanuth, Koleta ambaye alikuwa hana habari kama kanuth alikuwa akimwangalia alimuuliza
"Vipi kaka yangu tayari?"
"Oooh..aah..mmh, ulisema imeharibika nini?" Kanuth alibabaika.

Nini Kitaendelea?
 
HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)
SEHEMU: 16
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
SIMU: 0713 646500.

ILIPOISHIA:
Alikiri Roja Mo kuwa alikuwa na kila sababu kutotoa basi ule si mpira wa kutoa pasi lazima ufunge mwenyewe.
Hata Rebeka alipo nyanyuka baada ya kuokota jani alikutanisha macho na Kanuth, Koleta ambaye alikuwa hana habari kama kanuth alikuwa akimwangalia alimuuliza
"Vipi kaka yangu tayari?"
"Oooh..aah..mmh, ulisema imeharibika nini?" Kanuth alibabaika.
SASA ENDELEA...
"Aaaah kaka yangu mbona nimekueleza mapema sijui gari imenizimikia ghafla."
Kanuth hakuongea kitu alifungua boneti na kuangalia ndani labda kuna kitu kimelegea au kuchomoka. Kwa bahati nzuri alikuta ni waya wa betrii imechomoka aliokota jiwe na kuurudisha ule waya kwa kuupigilia ambao ulikaa vizuri.
Alimuomba Rebeka aingie kwenye gari na kuliwasha kwa kunyonga ufunguo. Alipowasha gari lilikubali kitu kilichomfanya Rebeka kumshukuru Kanuth.
"Oooh kaka yangu Mungu akujalie sana."
"Akujalie wewe aliyekupa upendelea wa sura umbile sina wasiwasi na tabia yako."
"Asante," Rebeka alijibu kwa kuachia tabasamu pana lililouchanachana moyo wa Kanuth na kumpa wakati mgumu kutamka kilicho mpeleka pale.
"Sasa kaka yangu sijui nikupe kiasi gani cha ufundi?"
"Hapana msaada wangu kwa viumbe kama nyinyi ni thawabu kwa Mungu, moyo wangu ungefarijika zaidi kama ungekubali mualiko wangu japo wa ghafla wa chakula cha mchana."
"Nashukuru kwa mwaliko wako hata mimi ningejisikia faraja kuongozana na wewe kupata chakula cha mchana mwanaume mwenye moyo wea huruma lakini utanisamehe kwa leo."
"Usifanye hivyo Rebeka."
"Ha! unanifahamu?"
"Rebeka nani asiyekuja hapa jijini mwanamke mwenye kila aina na uzuri na mvuto."
"Itakuwa vizuri kama unanijua ni rahisi kunielewa."
"Kukuelewa kivipi?"
"Mimi ni mke wa mtu kwa hiyo maeneo mengine siruhusiwi kwenda na mtu tofauti na mume wangu."
"Hilo nalielewa au sina hadhi ya kufuatana na wewe?"
"Mimi ni mtu wa kawaida ila naheshimu ndoa yangu vile vile mume wangu ni mtu maarufu."
"Rebeka cha mtu uliwa na mtu chuma pekee huliwa na kutu."
"Mbona sikuelewi una maana gani maana nimeona kama maongezi yamepoteza muelekeo?" Rebeka alishtuka.
"Rebeka maongezi hayajapoteza mwelekeo bali kila kiumbe anautashi wa kuongea yale yausibuyo moyo wake na siku zote mtu huutetea moyo wake mbele ya mhusika japo mke wa mtu naomba penzi lako la siku moja hata kwa saa moja na kuligharamia kwa kiasi chochote ukitakacho."
"Mmh! Usinichekeshe kaka yangu mwanaume kuugusa mwili wangu nina imani itakubidi uuze shamba la mzee wako nyumba yako kama unayo na gari zote bado nina imani itakuwa haitoshi."
Kauli ile ilimshtua Kanuth na kujiuliza huenda dau la milion mia mbili halitoshi. Lakini bado hakuonyesha kuteteleka japo moyo ulikuwa yukivuja jasho, alijikaza kiume na kumuuliza:
"Sidhani kama pesa niliyonayo ndani ya gari langu japo hailingani na hadhi ya uwezo wangu, wengine hatuna matangazo lakini mambo yetu makubwa nina imani hata huyo anayekumiliki ana pesa za kujitangaza lakini hapa anafunga breki."
Kauli ule ilimfanya Rebeka amuangalie upya Kanuth kuanzia kichwani mpaka miguuni na kumthaminisha. Ni kweli alionyesha ni mtu mwenye pesa lakini siku zote aliamini bwana yake Roja Mo ndiye mwenye pesa kuliko tajiri yoyote pale mjini.
Lakini alijua siku zote wanaume ni watu wa majingambo japo katika maisha yake hayo aliyaona miaka mingi iliyopita akiwa kijijini. Lakini toka aingie mjini wanaume wote wanaomfuata huwa wamejiandaa vilivyo.
Akiwa amejitanua kama ndege tausi kwenye hifadhi moja wapo ya taifa Rebeka aliongea kwa kujidai kuangalia yule bwana ana dau gani la chapuchapu. Hesabu aliyoweka ni milioni mia moja hamsini.
"Kwa shepu hii utanipa kiasi gani?"
"Kwa kukuonyesha uwezo wangu wa kipesa mimi ndiye naitwa bwana bingo kufanya mapenzi na mimi ni sawa na kushinda bingo."
"Ooh sikusimama kusikiliza ukijinadi kama mgombea ubunge kinachotakiwa pesa hapa penzi masilahi."
"Kwa saa moja nitakupa milioni mia mbili."
"Etiii!?" Rebeka alishtuka.
"Ndiyo wala sijakosea kutamka milion mia mbili kwa saa moja moja kwa vile ni haraka lakini tukipanga siku nzima nitakupa bilioni moja."
"Unasema kweli bwana bingo?"
"Kwa jeuri yangu pesa yenyewe ipo kwenye gari nitakupa sasa hivi nenda kaisabie kwako jioni nijulishe tuonane wapi?"
"Siamini unanitania," tamaa ya pesa ilimuingia Rebeka na kutaka kuiona ile pesa siku zote aliuapia moyo wake kuwa hata ipisha pesa aliifananisha na samaki na chambo.
Kanuth alikwenda mpaka kwenye gari na kurudi na fuko lenye pesa milioni mia mbili taslimu. Alipomfikishia aliufungua ule mfuko na kuyafanya macho ya Rebeka kukutana na maburungutu ya pesa mpya mpya tu. Moyo ulimwenda mbio na kuzitamani zile pesa na kuwa tayari kufanya naye mapenzi hata ndani ya gari.
Lakini aliogopa kuwekewa kanyaboya ilibidi aombe kuzihakikisha.
"Siamini kama zote ni pesa halali!"
"Nakuomba tuondoke na wewe hadi benki yoyote unayo iamini kisha wakusaidie kuzihakiki kisha wakusaidie na kuhesabu ili ujue tupo duniani kwa ajili ya kustarehe na viumbe wazuri kama nyinyi."
"Basi tuongozane hadi NMB."
Waliongozana pamoja kwa mbali Rebeka akiwa mbele na Kanuth nyuma hadi NMB. Rebeka aliteremka na zigo lake na kuingia benki na kumwacha Kanuth mbali na kidogo na benki akimwangalia Rebeka akiingia benki.
Muda ule Kanuth alinyanyua simu na kuwajulisha wenzie ambao muda wote walikuwa wakisubili taarifa kama zile.
"Mm’hu, lete taarifa?"
"Ndege kaishaingia kwenye mtego."
"Kwa hiyo sasa hivi upo wapi?"
"Nipo benki amekwenda kuzihakiki akitoka kitaeleweka."
"Kwa hiyo sisi tunasubili tujua wapi mnapokwenda."
"Hiyo msiwe na wasi kila mmoja ajiandae na kisu kuja kujikatia uwezo wake."
Kwa mbali Kanuth alimuona Rebeka akitoka kwenye mlango wa benki na kuingia kwenye gari lake na kwenda moja kwa moja alipo kuwa amesimamisha gari lake Kanuth.
Alipofika aliachia tabasamu pana lililozidi kumuumiza Kanuth huku akisema:
"Sasa baba kazi kwako tafuta uwanja mechi ichezwe."
"Twende Biski Hotel."
"Hapana kule mume wangu anafahamika sana."
"Basi Lyasingo Hotel."
"Kama huko sawa."
Waligeuza magari yao na safari ya kwenda Lyasingo hotel ilianza kama kawaida yao waliachana kwa mbali kitu kilichofanya mtu yoyote asitilie wasiwasi. Wakati huo Kanuth alikuwa ameisha wajulisha washikaji wake wapi waliko elekea.
Waliwasiri kama walivyopanga na kupata chumba cha bei mbaya. Baada ya kuingia ndani Kanuth alijifanya ni mtu asiye na papara lakini angekuwa peke yake angemrukia kwa sababu uzalendo ulikuwa umeushinda kuchelewa kuvua nguo kulikuwa kama kukosa alichokifuata.
Alijichelewesha kuwasubiri rafiki zake, alipopata uhakika wameishafika ndipo alipokwenda naye kuoga kabla ya mpambano. Wakiwa bafuni wakioga aliingia Mwarami na kuweka dawa ya kulevya kwenye kinywaji cha Rebeka na kutoka nje.
Walipotoka kuoga Kanuth alimuomba Rebeka wamalizie kinywaji ili mpambano uanze Naye Rebeka alikuwa kama mbwa kwa chatu baada ya kuziona milioni mia mbili alikubali chochote alichoambiwa na Kanuth.
Walimalizia vinywaji vyao kwa Rebeka kukibugia chote naye Kanuth alifanya vilevile. Haikuchukua Muda Rebeka alizidiwa na zile dawa alilegea kilichoendelea hakujua. Kanuth aliwaita wanzie ambao walifanya tendo la udhalilishaji huku wakimpiga picha mnato na video.
Baada ya kufanya tendo lile walimdunga sindano ya kukata sumu ya dawa na kumuacha akiwa amelala. Waliondoka wakisherehekea ushindi mzito walioupata wa kumkomoa Roja Mo pia kumdhalilisha Rebeka.

Nini Kitaendelea?
 
HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)
SEHEMU: 17
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
SIMU: 0713 646500....

ILIPOISHIA:
Walimalizia vinywaji vyao kwa Rebeka kukibugia chote naye Kanuth alifanya vilevile. Haikuchukua Muda Rebeka alizidiwa na zile dawa alilegea kilichoendelea hakujua. Kanuth aliwaita wanzie ambao walifanya tendo la udhalilishaji huku wakimpiga picha mnato na video.
Baada ya kufanya tendo lile walimdunga sindano ya kukata sumu ya dawa na kumuacha akiwa amelala. Waliondoka wakisherehekea ushindi mzito walioupata wa kumkomoa Roja Mo pia kumdhalilisha Rebeka.
SASA ENDELEA...
****
Sindano aliyopigwa Rebeka ilimuwahisha kuamka, alipozinzuka usingizini alijishangaa kujikuta peke yake. Mwanaume aliyejitambulisha kwake kama bwana Bingo hakuwepo hilo hakulijali alinyanyuka kitandani na kutulia kwa muda mwili ukiwa mchovu.
Alijishangaa kwa kuzidiwa na pombe si kawaida yake kuzidiwa kiasi cha kulala, siku zote hunywa kwa kipimo kilekile. Kumbukumbu zake zilimjulisha hakunywa sana, alitulia ameinama kitandani akiwa ndani ya shuka.
Kichwa alikisikia kizito alijiuliza ametumia pombe gani ambayo kwake ni ngeni. Aliamua kunyanyuka baada kusubiri bila kumuona mtu. Aliangalia saa yake ndogo ya dhahabu ya mkononi na kukuta ni saa kumi na moja jioni.
Alijiona kumbe usingizi ulikuwa mzito wa masaa zaidi ya manne. Moyoni alishukuru kuwa bwana yake Roja Mo yupo safari bila hivyo dili lake linge bumburuka. Aliamua kwenda bafuni kuoga, lakini alipoteremsha mguu alihisi maumivu makali chini ya kinena kitu kilichomfanya arudi tena kitandani.
Pembeni alipotupa macho alikuta kuna mipira ya kiume kondomu kumi na mbili zilizokwisha tumika, alijikuta akiguna.
"Mmh! Inamaana huyu bwana kanitumia kwa mipira yote hii kweli kanikomoa."
Alijilazimisha kuamka kuelekea bafuni kuoga kila hatua aliyopiga maumivu yalikuwa makali lakini aliuma meno na kwenda hadi bafuni na kuoga akiwa kwenye maumivu makali sana sehemu za siri.
Alitembea kwa shida hadi kwenye kabati na kuchukua nguo zake alizivaa kwa shida na kuamua kuondoka huku mwili ukimuuma kama kidonda hadi kwenye gari lake. Lakini alishindwa kuendesha alipojalibu kukanyaga mafuta maumivu yalikuwa makali sana kitu kilichomfanya ajilaze juu ya uskani akiwa ameuma meno.
Aliteremsha kioo na kumwita kijana mmoja ambaye alikuwa nje ya teksi yake kwa shida kwa kuwa hata alipomwita mtu kwa sauti maumivu yalikuwa makali. Bahati nzuri yule kijana alimsikia na kuja.
"Vipi sister inaonekana una matatizo mbona machozi yanakutoka?"
"Samahani kaka yangu naomba msaada wako."
"Upi huo?"
"Wewe ni dereva?"
"Ndio na gari langu hili hapo."
"Nilikuwa naomba unisaidie kunitafutia dereva ambaye atanisaidia kuniendeshea gari langu mpaka kwangu."
"Kuna malipo?"
"Kiasi chochote atakachotaka."
"Haina haja mimi natosha kwani mbali?"
"Sio mbali sana ni mjini."
"Utanipa elfu kumi na tano."
"Haina wasi ingia twende," yule dereva alikabidhi gari lake kwa mtu na kuliendesha gari la Rebeka ambaye kila muda ulivyokuwa ukienda ndivyo hali yake ilivyozidi kuwa mbaya.
"Dereva naomba unipeleke moja kwa moja Ambe Hospital."
"Kwani dada unaumwa nini?"
"Sio muhimu sana kujua kama kunifikisha hospitali," Rebeka alijibu kwa shida.
Yule kijana aliendesha kwa mwendo wa kasi ili kumwaisha hospitali. Njia nzima Rebeka aliugulia.
"Mama nakufa sijui..sijui amenifanya nini..Oooh nakufa."
Yule kijana aliyekuwa na maswali mengi kichwani lakini aliogopa kumuuliza kwa kuogopa majibu ya yule mwanamke. Aliliingiza gari Ambe Hospital hata bila maelekezo alikimbia mapokezi na kuwaeleza kuna mgonjwa mahututi.
Walikuja na machela hadi kwenye gari na kumchukua mgonjwa ambaye muda ule hakuwa na kauli. Walimbeba kwenye machela hadi wodini, dereva alijikuta akiulizwa maswali asiyoyajua.
"Eti kaka mgonjwa anatatizo gani?"
"Kwa kweli mimi sijui aliniomba msaada niendeshe gari lake nimwahishe hospitali."
"Ina maana humjui?"
"Simjui."
"Ha! huyu si Rebeka mke wa tajiri Roja Mo," muuguzi mmoja alimfahamu.
"Aaaah kweli," mwingine alimfahamu.
"Mnamjua kumbe?"dereva aliuliza.
"Ndio ni mke wa tajiri Roja Mo."
"Basi mimi nilitoa msaada tu wacha niwahi nimeacha gari langu halina mtu."
Dereva alikwenda hadi kwenye gari siku zote alijua jungu kuu halikosi ukoko. Ndani ya gari alikuta pochi ya Rebeka alipofungua alikuta kuna pesa nyingi zilikuwa kama milioni mbili. Alichukua elfu ishirini na zingine alizirudisha kisha alifunga gari na ufunguo aliwapa wahudumu wa gari ili atakapopata nafuu wampe na kuondoka zake.
****
Rebeka alizinduka saa tano za usiku na kuweza kuelezea tatizo lake aliweza kupata huduma nzuri zilizomfanya apate nafuu kwa haraka. Lakini bado ilikuwa hawezi kutembea akiwa wima kwa maumivu ya chini ya kitovu.
Daktari alimhakikishia ndani ya siku mbili angalau ataweza kusimama na kutembea japo si umbali mrefu. Lakini alimhakikishia ndani ya wiki mbili atakuwa amepona kabisa.
Rebeka akiwa amejilaza kitandani macho yakiangalia juu ya dali alijiuliza maswali mengi juu ya kitendo kile cha jana kwanza hana kumbukumbu kama alikuwa na akili zake wakati wakifanya mapenzi pili yule bwana alikuwa na uwezo gani wa kutumia Kondomu 12 peke yake tatu kwa nini ameamua kumkomoa japo kampa pesa nyingi.
Akiwa katikati ya lindi la mawazo aliingia mhudumu na kumkabidhi bahasha kubwa ambayo ilionekana ndani ilikuwa na picha. Kabla ya kuipokea alimuuliza:
"Nani kakupa?"
"Ameniambia anaitwa bwana Bingo."
"Bwana Bingo! yupo wapi?"
"Baada ya kunipa hii bahasha ameondoka na gari lake."
"Amesemaje?"
"Ameniuliza jina lako na upo wodi gani kisha alinipa bahasha hii na kuondoka."
"Akusema kitu chochote?"
"Hapana."
"Haya asante," Rebeka aliipokea ile bahasha na muuguzi alitoka nje ya chumba na kumwacha Rebeka peke yake akiifungua ile bahasha.
Baada ya kuifungua ile bahasha alikutana na picha ambazo zilikuwa zikionyesha mwanzo wa kukutana na bwana Bingo baada ya kuhalibikiwa na gari. Nyingine zilionyesha akizipokea zile pesa. Moyoni alijiuliza zile picha zina maana gani aliendelea kuchomoa picha mojamoja.
Picha zingine zilionyesha aliingia benki na nyingine zilionyesha magari mawili yakiwa yameongozana la mbele la kwake la nyuma la bwana Bingo. Nyingine zilionyesha akiingia Lyasingo Hotel na nyingine zilionyesha wakiingia chumbani na yote waliofanya ya kuvua nguo na kwenda bafuni kuoga na baada ya kuoga wakimalizia kinywaji chao.
Zilizofuata alitamani ardhi ipasuke na immeze akiwa amelazwa kitandani kama alivyozaliwa na pembeni kulikuwa na wanaume wanne na bwana Bingo alikuwepo wote wakiwa watupu.
Zilizofuata zilikuwa za udhalilishaji mkubwa ambazo hazitizamiki machoni mwa watu ni kichefuchefu. Zilikuwa zikionyesha matukio ya udhalilishaji kitendo cha kinyama alichotendewa na wanaume wale wanne ambao walimuingilia kwa zamu kila mmoja zaidi ya mara tatu.
Rebeka alitamani kulia lakini atafanyaje ni tamaa zake ndizo zimemponza. Kwa mara ya kwanza woga ulimwingia na kujiuliza Roja Mo akijuasijui itakuwaje. Aliamua kuzificha ili wahudumu wasizione.
Akili yake ilichanganyikiwa na kujiuliza maswali mengi yasio na majibu juu ya kitendo alichofanyiwa na bwana Bingo na kundi lake kumbe kutoa pesa nyingi kiasi kile kilikuwa ni kwa ajili ya kumdhalilisha. Alijiuliza na zile picha walizompiga zilikuwa za nini na kwa nini wamempelekea pale hospitali.
Alijikuta kwenye majuto makuu na kumkumbuka mume wake Mabogo na kuona heri mara mia maisha aliyokuwa akiishi na Mabogo kuliko ya muda ule. Alijiuliza sura yake atauweka wapi akikuta na na wanaume wale ni sawa na kutembea uchi japo atakuwa amevaa nguo.
Aliapa akitoka hospitali atatoroka na kwenda sehemu yoyote asiyojulikana kukimbia aibu ile.

Nini kitaendelea?
 
HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)
SEHEMU: 18
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
SIMU: 0713 646500....
... ILIPOISHIA:
Alijikuta kwenye majuto makuu na kumkumbuka mume wake Mabogo na kuona heri mara mia maisha aliyokuwa akiishi na Mabogo kuliko ya muda ule. Alijiuliza sura yake atauweka wapi akikuta na na wanaume wale ni sawa na kutembea uchi japo atakuwa amevaa nguo.
Aliapa akitoka hospitali atatoroka na kwenda sehemu yoyote asiyojulikana kukimbia kukimbia aibu ile.
SASA ENDELEA...
***
Roja Mo aliporudi safari zake alipatwa na mshtuko kusikia mkewe yupo hospitali amelazwa. Hakuwa na haja ya kuingia ndani alikwenda moja kwa moja hospitali. Rebeka alipomuona alitamani kukimbia lakini aliificha hofu yake.
Alipogundua uso wa Roja Mo una wasiwasi walimtoa hofu kwa kumchanulia tabasamu lililo upoza moyo wa Peza na kuhoji kwa wasiwasi.
"Vipi mpenzi kulikoni?"
"Aaah ni tumbo la kike tu lilinibana gafla jana."
"Oooh afadhali..vipi hali yako kwa sasa?"
"Naendelea vizuri"
"Huduma ya hapa unaridhika nayo au tubadili hospitali?"
"Kwa kweli ni nzuri sana nawashukuru manesi na madaktari wamenipa huduma na dawa nzuri."
Rebeka alitoka hospitali baada ya siku nne na kupewa masharti ya kutokufanya kazi nzito kwa miezi miwili. Toka atoke hospitali muda mwingi alikuwa ni mtu mwenye wasiwasi juu ya kitendo cha kinyama alichofanyiwa, alimuomba Mungu Roja Mo asijue.
Zilipita wiki mbili hali ikiwa ya kawaida kitu kilichofanya moyo wa Rebeka upunguze wasiwasi kwa kujua itabakia siri kati ya watenda na mtendewa. Aliweza kutembea japo si kwa kuendesha gari zaidi ya kuendeshwa.
Siku moja akiwa amemtembelea mwanaye na mumewe Mabogo alipofika moyo ulimshtuka pale alipomkuta Bibiana mke mwenzie akiwa mjamzito wa mimba kubwa. Japokuwa mimba ni kitu cha furaha kwake kilikuwa ni kama mkuki uliomwingia moyoni mwake.
Katika mawazo yake alipanga kurudi kwa Mabogo kumuomba msamaha na Bibiana arudi kuwa mhudumu wa ndani ambaye atamlipa kiasi chochote anachotaka lakini mambo yalikwenda sivyo Bibiana alikuwa mjamzito na yeye muda si mrefu atakuwa mama wa mtoto. Alikuwa na imani baada ya kupata mtoto atasababisha Mabogo kumfuta kabisa mawazoni mwake.
Rebeka alijikuta kila muda maumivu yanadizi moyoni mwake na kuona kama ni laana ya Mungu kwa kumkimbia mumewe na sasa anamuadhibu. Hata hamu ya kwenda kijijini kuwasalimia ilitoweka na kuamua kurudi mjini ili apange mikakati mipya ya kumtoroka Roja Mo na kwenda mbali sana hata ikiwezekana bora ajiue kabisa.
Alirudi hadi nyumbani alipoingia ndani alimkuta Roja Mo akiwa sebuleni akisoma gazeti la siasa juu ya uchaguzi, alipomuona alilitupa pembeni na kumlaki kwa kumkumbatia kwa furaha.
"Yaani huwezi kuamini nilikuwa nakuwaza sasa hivi sijui mimi bila wewe itakuwaje?"
"Hata mimi nimeamua kurudi nilipokuwaza tu bila wewe sina maisha yaani uliposafiri nilipata shida sana siku moja kwangu ilikuwa mwaka."
Baada ya kupigana mabusu na kujitupia kwenye kochi wakiwa bado wamekumbatiana walishtushwa na mlio wa kengere ya mlangoni.
"Pumzika wacha nikafungue," Roja Mo alimwambia mkewe wakati huo Rebeka alikuwa akienda ndani kubadili nguo ili aende akajimwagie maji.
Roja Mo alikwenda hadi mlangoni na kufungua alikutana na mlinzi wa getini ambaye alimkabidhi bahasha kubwa aliyekuwa na maandishi makubwa ya wino wa kalamu yenye wino mzito ya rangi nyekundu ilikuwa na maandishi yaliyoandikwa MLA CHA MWENZIE NA CHAKE HULIWA.
Baada ya kuisoma alimgeukia mlinzi ambaye alijua lazima ataulizwa swali alikuwa bado amesimama mbele yake.
"Nani kakupa hii bahasha?"
"Wale rafiki zako."
"Kina nani hao?"
"Si wale ambao mara nyingi huongozana nao muda wote mmoja ni yule mfupi mweupe ulinitambulisha kama sikosei anaitwa Kanyute"
"Oooh si Kanyute ni Kanuth."
"Ndiye huyo huyo walikuwa wote wanne."
"Wameelekea wapi?"
"Mmh, sijui waliponipa tu waliingia kwenye gari na kuondoka wakati huo mimi nakuja kwako."
"Walisemaje?"
"Waliniuliza kama upo nilipowaambia upo walinipa mzigo huu na kuniambia nikuletee..tena nimekumbuka waliniuliza na mama kama yupo?"
"Uliwajibu nini?"
"Niliwajibu yupo ajabu aligonga mikono na kusema shughuli imekwisha walikumbatiana na kuondoka wakicheka kwa furaha."
"Shughuli imekwisha wana maana gani na hili neno mla cha mwenzie wana maana gani?"
"Bosi kwa kweli maswali kama hayo mimi utanionea wewe ndiye unayewajua vizuri."
"Ooh! Samahani kaendelee na shughuli zako."
Yule mlinzi aligeuka na kurudi kwenye lindo lake na kumwacha Roja Mo akiwa ameshikilia bahasha mkononi ambalo lilionekana lina picha.a Alifunga mlango na kurudi kwenye sofa na kujilaza kisha aliifungua ile bahasha ili aone kuna kitu gani.
Wakati Roja Mo anafungua bahasha Rebeka alikuwa amejifunga kanga moja na juu alikuwea ameweka taulo begani akielekea kuoga. Alipotoka chumbani alishtuka kumuona Roja Mo akifungua bahasha moyo ulimpasuka alijua huenda ni ile siri ambayo sasa inamfikia bwana yake.
Alitamani kuikimbia na kuinyakua kabla Roja Mo hajaanza kuziangalia zile picha. Miguu ilikuwa mzito alibakia amesimama kama sanamu akimwangalia Roja Mo alichambua picha moja baada ya nyingine.
Roja Mo ambaye baada ya kuanza kuziangalia zile picha hazikuwa tofauti na zile alizopewa Rebeka kote alipotazama hapakumshtua sana japo sehemu ya Rebeka kuongozana Lyasingo Hotel lilimfanya jasho limtoke alijua kazidiwa akili.
Pigo kubwa lililomfanya apige kelele na kuzirai lilikuwa ni zile picha chafu alizokuwa amepigwa Rebeka na ujumbe wa maneno unaosema:
Mheshimiwa kazi imekwisha huwezi kutuzidi akili sisi ndiye tuliyekukaribisha mjini ongea na watu uvae viatu, siku zote mla cha mwenzie na chake uliwa. Chetu chako cha kwako chako mwenyewe hii haipo ukijua kupokea ujue na kutoa.
Hii shughuli unayoiona imeghalimu milioni mia mbili hamsini kwa hiyo ili issue hii ibakie siri yetu malipo yake milion mia nne bila hivyo kona yote ya nchi hii na jirani picha za mpenzio zitazagaa kuanzia kesho tunataka hizo pesa, wewe si kiburi basi hapa ni maji marefu.
Upatapo ujumbe huu tujulishe tupo sehemu yetu ya kawaida.
Roja Mo baada ya kusoma ujumbe ule alipiga ukelele na kuzimika kwa kusema
"Oooh wamenimaliza."
Rebeka aliyekuwa akimfuatilia Roja Mo alishtuka kama mtu aliyepigwa na shoti ya umeme na kujikuta akikurupuka kumkimbilia.
Alimkuta akiwa chini ameishapoteza fahamu, alizitupia macho zile picha zilikuwa zile zile chafu. Wazola ghafla lililomuijia ni kutoroka kwa kuhofia Roja Mo alipata fahamu huenda atachukua maamuzi mabaya.
Alikumbuka kauli ya Roja Mo kuwa yupo tayari kutoa roho ya mtu ili kuhakikisha anamlinda kwa gharama yoyote tena alimuonyesha siraha kwa kusema mwenye pesa hata akiua hadharani hafungwi wanaofungwa ni masikini tu.
Hakutaka hata kumsaidia alikimbilia chumbani na kuchukua vitu vyake muhimu na kuvipaki kwenye mabegi na pesa zilizokuwepo kwenye kabati kama milion sabini na kupitia zile picha na kuviweka kwenye gari lake na kuondoka huku mlinzi alikiwa amepigwa butwaa.
Rebeka alipitia kituo cha mafuta kujaza mafuta na safari ya sehemu isiyojulikana ilianza. Pamoja na kuelezwa usifanye kazi nzito lakini aliamua liwalo na liwe. Aliendesha gari kwa kasi kufuata barabara inayotoka nje ya mji.
****
Mlinzi ile hali ya uondokaji wa tajiri wake kike Rebeka ilimtia wasiwasi maana hata mlango hakufunga. Aliamua kwenda ndani japo huwa haruhusiwi kuingia ndani bila sababu maalumu. Alipoingia ndani aliona hali imekaa sagarabagara. Alikwenda kwa mwendo wa taadhari hadi subuleni. Macho yake yalitua kwenye mwili wa mtu aliyekuwa amelala chini.

Nini kitaendelea?
 
HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)
SEHEMU: 19
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
SIMU: 0713 646500....

ILIPOISHIA:
Alijua akishafanikisha zoezi lile litakalo fuata ni kumsaka Rebeka na kumrudisha nyumbani alijua lazima kakimbilia kwao. Wakati akiwa njia kuelekea Kim hotel nako Kim Hotel matajiri wanne walikuwa wakijipongeza kwa kufanikisha zoezi lao.
Walikuwa wakinywa kwa furaha huku wakiongea maneno ya kejeri.
SASA ENDELEA...

" Roja Mo ni mshamba tu hawezi kushindana na sisi mji tumempokea wenyewe hata kutongoza tumemfundisha eti leo atuzidi akili?"alisema Lemba kwa kujigamba.
"Picha tulilocheza kama ulaya vile sasa kazi kwake alipe milioni mia nne au tuzitawanye kama tulivyo mwambia sisi ndio watoto wa mjini," aliongezea Muarami.
"Tena tumekosea si anajifanya ana pesa tungemwambia milion mia sita," alisema Yusuf.
Wakiwa katikati ya maongezi mlango ulifunguliwa na kuingia Roja Mo ambaye alionekana mpole kitu kilichomtia huruma kila mmoja aliyekuwamo mule ndani. Kwa sauti ya upole alisema:
“Kwa hiyo wakubwa mnataka kiasi gani?"
"Kama tulivyo andika milioni mia nne liba ya milioni mbili tuliyo fanyia kazi," alijibu Lemba aliyekuwa na glasi ya pombe mkononi.
"Mimi nina milioni mia tatu mtapokea?"
"Hata milioni tatu na nusu hatupokei," alijibu Yusuf.
"Basi pokeeni cheki hii ya milion tatu zingine nitaleta."
Roja Mo alipitisha mkono nyuma kama anataka kuchomoa cheki walishangaa kujikuta wakitazamana na mdomo wa bastora.
"Mmefanikiwa kumuondoa ndani mke wangu lakini na ninyi mnaondoka duniani sasa tunataka tuone mmeweza kutumia milion mia mbili kuvunja ndoa yangu nataka na sasa mtumie sijui ni kiasi gani kuokoa uhai wenu," Roja Mo alisema kwa sauti ya chini.
" Roja Mo umefika mbali usifanye hivyo, tulijua tunaonyeshana jeuri ya pesa tu na si kingine," alijitetea Muarami.
"Ya kunidhalilisha au sio?"
"Lakini ni wewe uliyevunja makubaliano yetu sasa nani mwenye kosa?"
"Ikifikia hatua ya mtu kuwa na mke ilitakiwa kuheshimu kwani mpango wetu ulikuwa umekwisha kwa vile mliniahidi kufanya uliyofanya nami sina budi kufanya niliyoyaahidi kwenu. Haya kila mmoja aombe dua yake ya mwisho sipendi muingie kwenye ufalme wa mbinguni bila kujiandaa."
"Usifanye hivyo Roja Mo " Kanuth alisema huku akimsogelea Roja Mo
"Kanuth tena wewe ndiye adui yangu namba moja usinyanyue mguu rudi nyuma," Kanuth alisuasua kurudi nyuma kitu kilichomzidisha hasira Roja Mo na kuongea kwa sauti ya juu.
"Nasema moja rudi..." Kanuth alikuwa bado anaomba msamaha.
"Mbili..rudi nyuma..tatu...moja..tatu..mbili..tatu mwisho."
Hakuongeza kauli nyingine zaidi ya milio miwili iliyotua kifuani kwa Kanuth na kumtupa kwa nyuma ikiwa imehalibu vibaya kifuani na kuyachukua maisha yake.
Yusuf alijua sasa kazi imeiva alipotaka kutoa bastora yake naye alikuwa amechelewa kwani risasi mbili zilitua kwenye kifua upande wa kushoto wa moyo na kumnyamazisha palepale.
Chumba kilikuwa kikinuka damu Lemba na Muarami walijikuwa wapo kwenye wakati mgumu wa kuokoa maisha yao, Lemba aliamua liwalo na liwe aliamua kumvaa Roja Mo lakini wakati akijirusha kumvaa alikutana na risasi iliyotua kichwani iliyomfanya amuangukia Roja Mo kama mzigo.
Kitendo cha Roja Mo kuanguka na mwili wa Lemba ambaye naye alikuwa tayari mgeni wa Mungu. Mwarami alipata nafasi ya kuitoa bastora yake na kuwa tayari kwa kujihami. Roja Mo baada ya kuanguka chini aliupindua mwili wa Lemba na kutaka kummalizia Muarami.
Walijikuta kila mmoja akiachia risasi zilizompata kila mmoja kifuani na kumtupa kwa nyuma na kuchukua uhai wa kila mmoja. Ndani ya chumba kulikuwa na maiti za watu watano. Mlio wa milipuko ya risasi iliwafanya polisi waliokuwa wakimfuatilia Roja Mo waingie ndani na kwenda moja kwa moja kwenye chumba cha tukio kwa taadhari kubwa.
Ndani ya chumba walijikuta wakipingwa na butwaa kwa kukuta maiti za watu watano warafiki wakubwa lilikuwa fumbo zito ambalo hakuna aliyelijua. Polisi walizichukua maiti zote na kuzipeleka hospitali ya mkoa na kuanza uchunguzi wa vifo vya marafiki watano mara moja.
****
Rebeka aliendesha gari kwa mwendo wa masaa sita bila kupumzika na kuvuka mikoa miwili dhamira yake ni kuvuka mikoa zaidi ya mitano aende kuanza maisha mapya mpakani mwa nchi.
Aliingia mkoani majira ya saa mbili usiku aliona muda ule unafaa kutafuta sehemu ya kupumzika ili kesho aendelee na safari yake.
Alitafuta hotel yenye hadhi na kupanga, baada ya kupata chumba alijimwagia maji na kumtuma mhudumu amletee chakula hakuwa ha haja ya kutembea mwili ulikuwa umechoka sana.
Akiwa amejiegemeza kwenye tendego la kitanda akila chips kuku na bia yake ya castel macho yakiwa kwenye Luninga akiangalia taarifa ya habari. Pamoja macho yalikuwa kwenye Luninga lakini alikuwa akisinzia kwa uchovu.
Habari za mauaji ya kutisha ilimshtua baada ya kusikia sehemu aliyotoka, alitulia bila kuweka kipande cha chipsi mdomoni wala kutafuna chakula kidogo kilichobakia mdomoni na kusikiliza, alimsikia mtangazaji akisema:
"Kumetokea mauaji ya kutisha ya matajiri watano waliouana kwenye chumba cha hotel ya Kim, mpaka sasa hakuna anayejua sababu ya mauaji yale ya kutisha majina ya matajiri hao ni Roja Mo,...."Rebeka hakutaka kusikiliza tena alijikuta akiangua kilio wakati huo miili ya marehamu na sura zao zilikuwa zikionyeshwa.
Rebeka alijutia tabia yake kama angetulia kwa mume wake yote yasingemkuta, lakini alikumbuka sehemu ile haifai watu wajue yeye ni nani. Aliamua kulilia moyoni japo maumivu yake yalikuwa sawa na kukipasua kifua kwa kisu butu bila ganzi.
Alilala pale mpaka siku ya pili asubuhi alfajiri alianza safari yake ya kuelekea mpakani mwa nchi. Alitumia masaa sita kufika mpakani mji uliokuwa umechangamka sana. Alitafuta hotel yenye hadhi na kupanga pale.
Ndani ya miezi miwili Rebeka alikuwa maarufu pale mpakani, alikuwa mgeni lakini mwanamke mwenye pesa na mrembo ambaye kila tajiri alimtaka. Lakini hakuwa tayari kurudia makosa kama yaliyomkuta na kumfanya atangetange.
Kwa miezi minne alinunua jumba kubwa la milion hamsini ambalo lilikuwa likimilikiwa na mzungu ni jumba ambalo ndilo lilokuwa la kifahari pale mpakani. Kama kawaida alirudia biashara zake kwa vile alikuwa mzoefu alitengeneza hela nyingi.
Jina lake lilikuwa midomoni mwa watu lakini hakutumia tena jina la Rebeka alijiita Eva. Kila mmoja alimpenda alikuwa mwanake mwenye roho nzuri mcheshi asiye na malingo tofauti wengine ambao hata nusu ya uzuri wake hawamfikii lakini wanachagua watu wa kuongea nao.
Rebeka au Eva akiwa kwenye duka lake kubwa ambalo lilikuwa lina kila kitu na kuajili wafanyakazi zaidi ya kumi na kuwalipa mshahara mzuri. Akiwa anasoma gazeti aliona habari za kifo picha haikuwa ngeni machoni mwake.
Ilikuwa ya bwana yake Kuchu maelezo yalisema kuwa Kuchu amejiua baada ya kugundua ana ugonjwa wa upungufu wa kinga mwilini (ukimwi). Habari zile zilimshtua na kujiuliza ina maana hata yeye huenda anao anaishi nao bila kujua.
Siku ya pili aliamua kwenda hospitali kupima damu majibu hayakuwa tofauti na mawazo yake kweli alikuwa ameathirika japo hakuwa na tatizo lolote mwilini. Kila aliyemuona hawezi kuamini hata akimwueleza ameathirika ataona anataka kumnyima tu.
Aliporudi nyumbani alikuwa na mawazo mengi juu ya taarifa zile japo alijiona anapendeza machoni mwa watu lakini alikuwa muathirika maiti inayotembea au marehemu mtarajiwa.
Kweli shetani hupenda pale mtu unapokuwa na matatizo Rebeka alipata wazo baya la kutokukubali kuondoka peke yake alitaka kuacha simulizi ya marehemu kaacha orodha ndefu. Kuanzia hapo Rebeka alipunguza safari za kujijenga kimaisha kazi nyingi aliwatuma watu.

Nini kitaendelea?
 
HADITHI: REBEKA ( Zaidi ya Mwanamke)
SEHEMU: 20
MTUNZI: Ally Mbetu ‘Dr Ambe’
SIMU: 0713 646500....

ILIPOISHIA:
Kweli shetani hupenda pale mtu unapokuwa na matatizo Rebeka alipata wazo baya la kutokukubali kuondoka peke yake alitaka kuacha simulizi ya marehemu kaacha orodha ndefu. Kuanzia hapo Rebeka alipunguza safari za kujijenga kimaisha kazi nyingi aliwatuma watu.
SASA ENDELEA...

Aliamua kuwa mtu wa kustarehe nao kina baba wakwale hawakuchoka, safari ile alikuwa mpole kila aliyemtongoza alimkubalia bila masharti kama mwanzo.
Kila aliyempata alijiona amepata kumbe amepatikana hakukubali kufanya mapenzi kwa kutumia mpira. Kila aliyempata alipolazimishwa kuvua mpira alitii amri, kila ulipoenda na mtu nyumba ya wageni alikuwa wa kwanza kuvua nguo ili uingie kichwakichwa hata wazo la kondomu linapotea.
Kila aliyegusa aliondoka nao naye aliugawa kama peremende, sifa zake mbaya ziliwanyima raha wake za watu mtu alikuwa tayari kukorofishana na mkewe ili tu ampate Rebeka.
Rebeka baada ya kumaliza waume za watu akawaanzia vijana ambao aliwahonga ili kufanya nao mapenzi wao waliona wamepata kumbe maskini walikuwa wamepatikana. Kila mmoja alimchukia pale mpakani hasa wanawake.
Siku moja akiwa peke yake amekaa dukani mwake walipita watoto wazuri wakitoka shuleni, walikuwa watoto wenye afya njema. Aliwaangalia alijikuta machozi yakimtoka moyo ulimuuma na kujiuliza nafsini hivi ataendelea kugawa maradhi yale mpaka nini nini hatma yake mbele ya Mungu.
Alijiuliza watoto wazuri kama wale wazazi wake watakapofariki lazima wataishi maisha ya kutangatanga kwa kukosa lishe bora elimu. Kilio cha mateso yao lazima kitamhukumu akiwa duniani au akiwa amekufa.
Jioni akiwa amekaa akiangalia kipindi cha mahubiri alimsikia mhubiri akisema kuwa kila mwenye mzigo wa dhambi ampelekere Bwana kwani ndiye mwenye uwezo wa kusamehe na kumfanya mtu aingie dunia mpya akiwa safi mbele ya Mungu.
Rebeka aliona hiyo ndio njia pekee iliyobakia ya kwenda kutubu mbele ya Bwana ili asamehewe makosa yake toka kumkimbia mume wake mpaka siku ile.
Jumapili Rebeka akiwa amepakatia Biblia mpya ambayo aliinunua siku alipopata wazo la kwenda kutubu madhambi yake. Hakuna aliyeamini kumuona Rebeka akiingia kanisa wapo walio mshukuru Mungu kwa kumuonyesha njia lakini wapo waliomuona shetani wa kike walitamani kutoka kanisani wamwache peke yake.
Rebeka baada ya kuingia kanisani alitafuta sehemu ya nyuma pembeni na kutulia tuli kusubiri ibada ianze. Baada ya ibada wapo waliokuja kutoa ushuhuda mbele ya kanisa. Kila mmoja alisema yale aliyoyafanya ambayo yalimchukiza Mungu.
Walikuwa wanaume na wanawake wapo waliohasi nyumba zao kwa ajili ya nyumba ndogo wapo waliotoka nje ya ndoa zao wapo waliotelekeza nyumba zao kwa ajili ulevi. Hata wachawi walitoa ushuhuda wao jinsi walivyo watesa watu kuwaua na kula nyama zao.
Ulikuwa ushuhuda wa kusisimua uliowaacha watu midomo wazi, akiwa amebakia mmoja akimalizia ushuhuda wake, Rebeka alitaka naye kwenda lakini moyo ulikuwa mzito lakini alijiuliza asipokwenda pale ambako kila mmoja alisema mabaya yake yeye anasubiri nini.
Alijilazimisha kunyanyuka na kupita katikati ya mistari miwili ya waumini walio kuwa wamekaa. Kila mmoja alimtupia jicho kutaka kujua anakwenda wapi. lakini hakujali macho ya watu alikwenda kwa mwendo wa taratibu Mchungaji alipomuona alimfuata na kumshika mkono na kumpandisha kwenye madhabahu.
"Karibu mama," Rebeka hakumjibu zaidi ya kububujikwa na machozi ilikuwa tofauti na wote waliokuja kutoa ushuhuda ni yeye tu ndiye aliyetoa machozi.
Mchungaji alimpa kipaza sauti lakini alioendelea kulia huku akiwa ameshikilia mikono kifuani ikionyesha ana maumivu makali moyoni. Mchungaji alimuinamia na kuongea naye kwa sauti ya upole.
"Najua una maumivu makali moyoni mwako na kujutia makosa yako lakini huu ndiyo wakati wako wa kuyatubu yote, kama Bwana alivyosema wote wenye mizigo mizito njooni kwake naye atakutueni haya mama ongea yaliyokusibu."
Rebeka alinyamaza na kuanza kuongea kwa sauti iliyochanganyikana na kilio maisha yake yote tokea alipotoka tumboni kwa mama yake mpaka siku ile aliyosimama pale alimalizia kwa kusema:
"Nilipojijua mimi mzuri ndio mwanzo wa kuisaliti ndoa yangu na nilipojijua nimeathirika ndipo nilipoaanza kuusambaza ugonjwa kwa wanaume wote wakware na nilipojijua namkosea Mungu ndipo nilipokuja hapa kutubu....kwa sasa hivi mimi ni muathirika wa gonjwa wa UKIMWI."
Kauli ile ilikuwa kama mshare wa moyo kwa wanawake wote waliokuwa na uhakika kuwa Rebeka alitembea na waume zao. Kanisa muda mfupi baada ya ushuhuda mzito liligeuka jumba la vilio, wengi walilia mpaka kujitupa chini huku wakisema kwa sauti:
"Ooooh Mungu wangu tumekwisha...Eva umetuuua."
Ilibidi shughuli zote za kanisa zisimamishe na kufanya kazi ya kuwahudumia kina mama na kina baba ambao wengi wao walikuwa wamepoteza fahamu. Rebeka alijutia nafsi yake lakini ndiyo hivyo maji yalikwisha mwagika.
Baada ya masaa mawili kanisa lilirudi kwenye hali yake ya utulivu na maombi mazito yalifanya kuzifariji roho za wote walioathirika na ushuhuda wa Rebeka.
Siku ileile Rebeka alitangaza pale pale kanisani kuwa mali zake zote anazikabidhi kanisani ikiwa kusaidia watoto yatima na wajane aliomba baada ya kuondoka jumba lake liuzwe na pesa ziingizwea kwenye mfuko wa kanisa.
***
Siku ya pili Rebeka alijipakia kwenye gari lake na kuamua kurudi nyumbani kwa wazazi wake hakuwa na hamu ya kuishi tena mjini. Nyumbani kwao alipokelewa na wazazi wake wote na ndugu na jamaa.
Kijijini ilikuwa furaha isiyo kifani kwa wazazi wake bahati nzuri alimkuta mwanaye ambaye alikuwa amefuatana na baba yake. Mwanaye alikuwa kwenye afya njema, wazazi wake walitaka kujua alikuwa wapi muda huo wao walijua na yeye alikuwa amekufa kwenye mauaji yale ya kutisha ambayo hayataondoka akilini mwa watu haraka.
Baada ya mapumziko na kupata chakula aliwaweka sebuleni ndugu na jamaa na kuwaelezea tamu na chungu ya maisha yake. Kila mmoja alijikuta machozi yakimtoka Rebeka naye alikuwa akiongea huku akilia kwa majuto ya kuufuata moyo wake kwa kila ulilotaka.
Wakiwa katikati ya majonzi kila mtu akitokwa na machozi Mabogo na mkewe Bibiana waliingia wakiwa na mtoto wao Mafuru. Macho yake yalitua kwenye uso wa baba mkwe alikutana na michirizi ya machozi ilibidi ajiulize kulikoni.
"Jamani kulikoni kuna habari gani?"
Kauli ile ilimfanya Rebeka anyanyue uso na kukutana na mumewe Mabogo alijikuta akisema:
"Aaah Mabogo!"
"Mungu wangu ni wewe Rebeka!?"
Rebeka bila kuongeza neno alijitupa mzimamzima kwenye miguu ya Mabogo
"Mume wangu nimekwisha kweli mshahara wa dhambi mauti."
"Rebeka una maana gani kusema hivyo?"
"Nimeathirika."
"Nini?"
"Nimeathirika nimevuna nilichopanda."
Kauli ile ilimfanya Mabogo kutokwa na machozi kama mtoto mdogo, alimnyanyua na kumkumbatia kwa mahaba mazito huku akimweleza maneno yaliyomliza kilio cha sauti Rebeka:
"Rebeka mpenzi mwanamke niliyempenda kwa moyo wangu wote na kwa nguvu na akili zangu zote najua tatizo lililokutokea si lako ni letu sote nakuahidi kauli yangu ni ileile niliyoitoa mbele ya padri siku ya kutufungisha ndoa nitakupenda kwa uzima na ugonjwa mpaka Mungu atakapomchukua mmoja wetu.
“Pamoja na yote yaliyokukuta lakini amini wewe ni mwanamke zaidi ya wanawake ni mwanamke jasiri mwenye moyo wa upendo na huruma kwa watu wote, Mungu huwa hampi vyote mwanadamu tatizo ni maamuzi bila kufikiria faida na hasara zake wewe ulifikiria faida bila kujua hasara zake ambazo ni furaha ya muda mfupi lakini majuto ya muda mrefu.
“Hilo ndilo kosa kubwa ambalo mwenyezi Mungu atakalo tuhukumiwa wanadamu ametupa akili ya kuwaza kabla ya kutenda kitu kilicho tutofautiana na wanyama ambao ni mahayawani...Lakini Nakuhakikishia Rebeka kuugua sio kufa ondoa wasiwasi moyoni mwako. Yoyote anaweza kufa sio lazima uugue kufa ni ahadi unaweza kufa bila kuumwa au kwa ajari wakati asubuhi uliamka mzima afya njema.
“Jione kiumbe uliyezaliwa upya tena sasa hivi umezaliwa kiroho ni maisha yaliyo bora mbele ya Mungu...Rebeka nakupenda sintasita kukupenda bado mke wangu mbele ya Mungu."
Rebeka alijikuta akilia kilio kilichomliza kila mmoja pale lakini Mabogo alimfariji kitu kilichomfanya moyo ulitulia. Mabogo alimuacha Rebeka kijijini kwa hakutaka tena maisha ya mjini alijenga kanisa kubwa na kituo cha kuwahudumia waathirika wa Ukimwi na kununua gari la kijiji litakalo kuwa likihudumia watu wenye matatizo.
Jina lake lilikuwa tena midomoni mwa watu mwanamke jasiri mwenye moyo wa huruma na upendo alifahamika kama dada wa kanisa. Pesa zake zote alizitumia kwa maendeleo ya kanisa. Pamoja ya yote linalomuumiza moyo wake ni upendo wa mume wake Mabogo anaamini mpaka anaingia kaburini Mabogo ni mwanaume bora mwenye sifa zote za kuwa mume wa mtu ambaye pamoja na kumfanyia yote bado upendo wake bado mbichi usioisha moyoni mwake.
Lakini ndio hivyo Bibiana ndiye mrithi wake hana jinsi amekubali yaishe. Sasa hivi Rebeka mama wa shamba mjini anakuogopa kama ukoma.
Mwisho kila mtu ameona moyo si wa kuuendekeza kila mmoja aridhike anachopata tuziheshimu ndoa zetu hata kama tunakula mara moja kwa siku. Tamaa ya mwili ni majuto ya moyo Mungu huwapenda wenye subira ya moyo ambao huwapa farijiko la milele. Hadithi hii ni tunu kwa wote waliokuwa waaminifu kwenye ndoa zao, hata kwa walio athirika nawaeleza kuugua si kufa waishi kufuta ushauri maisha yao hayatakuwa na dosari kufa kwa mtu ni ahadi.
Mwishoooooooo Kabisaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom