Episode Three
Wageni waliendelea kutiririka Ikulu, watu walikuwa wengi mno kana kwamba kulikuwa na mkutano hivi. Wapo ambao walikuja na familia yao, wapo ambao walikuwa wenyewe. Wapo ambao walikuwa ni walinzi lakini hawa wote walikuja kwa ajili ya kumpokea binti Rais ambaye aliwasili kwenye majira ya saa 11 jioni hivi.
Ilikuwa furaha kwa Baba, ilikuwa furaha kwa Mama pamoja na Rais na hata mke wake pia ambao walikuwa wanamtaza binti huyu. Nami nilipomuona sikutaka mambo mengi, nilijua sitapata muda wa kuzungumza na Mpiga mbira. Nilijitoa ufahamu.
Nikaenda kwa mmoja wa wafanyakazi wa ndani ambaye aliitwa Anna, huyu tulimzidi cheo kwahiyo ilikuwa rahisi kumtumikisha ana akanielewa.
“Unamjua yule mpiga mbira?”[emoji851]
“Ndio”[emoji2955]
“Nataka ujue wapi ambapo anaishi, ila hii iwe siri yetu”[emoji2958]
“Unanipa Tsh ngapi?”[emoji389]
“Unapenda hela, nataka unisaidie bhana”[emoji2357]
“Sawa hakuna shida” Anna alinielewa nami sikumuacha bure nilimwahidi kama atajua wapi anakaa basi ningempa kiasi cha laki mbili kama posho. Alinikubalia na nilirudi Ikulu kuzungumza na familia.
Nilikuta sehemu ambayo sherehe ya mapokezi ya Judy ikiwa imejaa, mida ya saa moja usiku ilikuwa kama saa sita usiku. Sauti ya muziki haikuacha kusikika huku wasanii mbalimbali wakiendelea kutumbuiza.
Baba, Rais, Mama, Mama Judy walikuwa wamekaa meza moja huku Judy akiwa amesimama akizungumza na Kijakazi wake. Nami nilipiga hatua hadi karibu yake, nilimsalimia kabla ya kurudisha macho kwa Mpiga Mbira ambaye alikuwa amesimama kwa pembeni akitutazama.
“Anaonekana mzuri, ngoja nikamsalimie” Nilijiambia moyoni na kumuaga Judy ambaye aliniuliza naenda wapi? Lakini nilimdanganya, akanielewa.
Nilienda hadi kwa Mpiga mbira, nikajaribu kumsemesha lakini hakujibu lolote. Nikamuuliza mbona hakunitafuta lakini alikausha tu. Alinikera mno hadi nilipayuka.[emoji3166]
“Kila siku nakuongelesha na huongei, au unapenda navyoteseka kukutafuta?”[emoji853] Nilidhani kwamba angechukia lakini hakuonesha dalili hizo.
“Ondoka, rudi sehemu yako” Sauti ya Mama kutoka nyuma yangu ilipenya kwenye masikio yangu. Niligeuka na kumtazama.
“Mama namuongelesha muda wote lakini haongei?[emoji34]
“Unaongea kwa sauti, Rais atakusikia na utamweka mwenzako sehemu mbaya Muache”[emoji120]
“Sawa”[emoji17] Nilirudisha macho kwa Mpiga mbira.
Yule binti alishika mbira yake na kuanza kupiga taratibu, sauti ambayo ilikuwa inatoka ilipoza kabisa hasira zangu. Alikuwa anafuatisha wimbo nzuri ambao sikuwahi kuusikia kabla, nilijikuta nikisimama na kugeuka. Nikamtazama, naye aliweka tabasamu huku akiendelea kupoga mbira. Nikahisi kama hakuna kitu ambacho kimetokea. Basi ilinibidi nirudi lakini sio kwamba sikuwa na hasira.
Nakumbuka siku hii nilimtazama sana huyu binti, nikataka kumchukua video lakini sikuwa na simu maana Baba aliichukua muda tu. Nikachukia kuanzia mwanzo wa shughuli hadi ilipoisha kwenye majira ya saa sita hivi.
Watu mbalimbali waliondoka katika eneo lile nami nilikuwa wa mwisho kabisa. Kutokana na kuwekeza macho kwa Mpiga mbira, kwa muda mrefu. Judy alihisi jambo maana hata muda niko naye sikuwa mtu wa kuzungumza kama ilivyokuwa kawaida yangu. Macho nilimpa yule binti na sio Judy tena. Hii ilimkera lakini alishindwa kuniambia.
Basi asubuhi ilipofika, tulitoka na Judy kuelekea kwenye hotel moja hivi ambako huko tungekutana na marafiki zake. Lakini tukiwa njiani sikuacha kuwaza kuhusu yule binti. Nilitamani kumuona mpiga mbira wangu. Nilijikuta naangaza kila sehemu ila wapi? Sikumuona.
“Unaonekana kama mtu ambaye hujafurahishwa na ujio wangu?” [emoji20]
“Kwanini?”[emoji849]
“Nimehisi hilo, tangu jana usiku hunipi muda kabisa”[emoji26]
“Hapana sio kweli, nimependezwa na Baba anasema kwamba mpango wa ndoa upo tayari”[emoji2357]
“Upo tayari kunioa?” [emoji183]
“Kwani ushapata mchumba?”[emoji12]
“Hapana ndio maana nimerudi kwa ajili yako”[emoji56]
“Nami nipo kwa ajili yako pia” Niliamua kumzuga lakini sikuwa na lamaana ambalo namaanisha.
Basi, tuliendelea na safari hadi tulipofika kwenye hotel ambako Judy alinitambulisha kwa Marafiki zake kibao ambao walinipenda na kunipa pongezi kwa kuwa na mwanamke mzuri. Licha ya pongezi zao, ila binafsi ilikuwa nikimtazama Judy namuona ni mwanamke wa hovyo na hayupo katika moyo wangu.
Tuliporudi Ikulu, muda wa chakula cha jioni. Anna alikuja na kuninong’oneza.
“Tayari nimeshajua wapi anakaa”[emoji86]
“Usiniambie..?”[emoji87]
“Ndio” Ilinibidi nitoke na Anna nje ili tuzungumze vizuri maana kwa jambo kama lile hatukupaswa kuongea mbele ya watu.
Tulitoka hadi nje ambapo tuliweka kituo kwenye bembea, kila mmoja akawa tayari kumsikiliza mwenzake.
“Umejua na jina lake?”
“Ndio, anaitwa Jane” Niliposikia jina tu, nikasawazika moyo. Nilikuwa napenda niwe na mwanamke ambaye jina lake linaanzia na J, kama ilivyokuwa kwangu.
“Woow! Naitwa Jack then ye ni Jane, kama titanic hivi”
“Kwani umempenda?”[emoji2955]
“Ndio”[emoji26]
“Jack unapendaje mwanamke kiziwi, hasikii wala aongei?”[emoji1787]
“Kiziwi?”[emoji15][emoji26]
“Ndio ni kiziwi”
“Mungu wangu[emoji2296]kwanza anaishi wapi?”
“Karibu na nane nane lakini ni mtoto wa kimaskini sana, anaokota makopo na yupo na mwanamke ambaye anaishi naye kama Mama yake lakini sio mzazi”[emoji19]
“Oh! Mama yake mzazi kafa au kamtelekesa?”[emoji26]
“Nimeambiwa kafariki muda tu lakini pia huyo mwanamke ni kipofu. Pia ana ndugu yake ni kibubu. Msaada pekee upo kwa Jane ambye anategemea mbira ili kuwalisha hao wengine”[emoji26] Nilihisi Anna ananiongopea, anataka kunipa hadithi za kale za kipofu, bubu na kiziwi. Nikajiambia, kesho nitaenda na kuhakikisha nampata ili kujithibitishia kama ni kweli ama anataka kuniongopea..... ITAENDELEA