Hadithi nzuri yenye mafundisho

ng'ombo

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
418
619
Wanandoa wapya waliooana muda si mrefu waliishi maisha ya kimasikini sana. Siku moja mume akamuita mke wake akamwambia, "mke wangu naondoka naenda safari ya mbali kwenda kutafuta mali ili tuje tuishi maisha ya furaha na raha ila sijui nikiondoka nitakaa huko miaka mingapi. Nakuomba mke wangu uwe mwaminifu usinisaliti na mimi pia huko niendako nitakuwa mwaminifu sitakusaliti".

Mke alikubali na mume akaondoka akaanza kutembea. Alitembea kwa siku nyingi sana hatimaye akafika kwa mkulima mmoja aliyekuwa anatafuta mtu wa kumsaidia kufanya kazi katika shamba lake. Yule kijana akaomba kazi akapata ila akamwambia yule mkulima "nitafanya kazi ila mshahara wangu utakuwa unanitunzia mpaka siku nikitaka kuondoka nitakuambia unipe hizo pesa zangu zote nilizofanya kazi kwako."

Yule mkulima akakubali ombi la yule kijana. Kijana akafanya ile kazi kwa miaka ishirini na siku moja akamwambiaboss wake kwamba ataondoka hivyo ampe pesa zake zote.Yule mkulima akasema sawa ila nitakupa mambo mawili uchague moja. Mkulima akasema 1.Nikupe pesa zako zote uondoke au 2. Nikupe ushauri wa aina tatu afu nisikupe pesa zako zote ulizofanya kazi kwangu kwa kipindi chote cha miaka ishirini. Lakini sitaki unipe jibu sasa hivi katafakari halafu kesho utanipa jibu umechagua kipi.

Yule Jamaa akakaa akatafakari, kesho yake akaja na jibu. Boss akauliza unataka kipi? Yule jamaa akasema nipe huo ushauri wa aina tatu. Boss akarudia tena, "nikikupa huo ushauri ujue sitakupa pesa zako ulizofanya kazi kwangu. Yule jamaa akasema sawa wewe nipe huo ushauri. Yule Boss mkulima akasema, i. Usifanye mambo kimkato na usipende njia za mkato. ii. Usipende kudadisidadisi na kushangashangaa mambo yasiyokuhusu maana kuna mambo mengine ni mabaya ukiyadadisi na kuyashangaa sana yatakupelekea kifo. iii. Usifanye maamuzi wakati una hasira au una uchungu.

Baada ya hayo yule Boss akamwambia haya kijana wangu unaweza kuondoka, shika hii mikate mitatu, hii miwili utakula wewe mwenyewe ukiwa njiani kurudi nyumbani na huu mmoja utakula na mke wako siku ukifika nyumbani. Jamaa akachukua ile mikate akaanza safari. Mara akakutana na mzee mmoja akamwambia, "kijana umepitia hii njia? Hii njia ni ndefu sana unaweza kumaliza mwezi hujafika hivyo pitia hii njia ya mkato utafika haraka. Jamaa akakubali akaanza kutembea kupitia ile njia ya mkato, mara akakumbuka ushauri wa kwanza aliopewa. Akaamua kurudi tena kwenye njia ya awali ile ndefu Baadae akaja kugundua ile njia ya mkato ilikuwa na waasi waliokuwa wanaua yeyote na kumteka akipitia hiyo njia.

Akatembea kwa muda mrefu akachoka akaona nyumba ya wageni akalipia pesa akaoga halafu akalala. Usiku akasikia makelele sana akaamka ili akaangalie kuna nini, wakati anataka kufungua mlango akakumbuka ushauri wa pili, jamaa akarudi akalala zake. Asubuhi mwenye gest akamuuliza vipi hukusikia makelele usiku? Jamaa akasema alisikia ila sikutaka kufatilia sana yasiyonihusu. Mwenye nyumba akasema wewe ni mtu wa pekee kutoka salama maana hapa huwa kuna mtu anatoka usiku anapiga kelele na yeyote anayetoka nje kushangaa na kutaka kujua nini kinaendelea huwa anauawa na yule mtu na kuzikwa kwenye uwanja ule.

Jamaa akaendelea na safari na baada ya safari ya siku nyingi usiku na mchana akafika nyumbani kwake usiku na mke wake alikuwa amelala. Alipochungulia kwenye ufa akaona kuna mtu mwingine wa kiume amelala pembeni. Jamaa alipatwa na hasira na ghadhabu akataka aingie awaue mke wake pamoja na yule mwanaume mwingine aliyekuwepo ndani halafu yeye arudi akafanye kazi kwa boss wake. Lakini kabla hajafanya hivyo akakumbuka ushauri wa tatu akaamua kwanza. Akagonga mlango mke wake akafungua, mke alifurahi sana akamkumbatia mume wake. Lakini mume alimsukuma yule mwanamke na kumwambia, "kwanini umenisaliti?" Mke akasema, "sijakusaliti mume wangu toka uondoke. Jamaa akasema vipi na yule mwanaume ndani ni nani? Mke akasema huyo ni mtoto wako, ulipoondoka nilikuja kugundua kuwa nina ujauzito ndio nikamzaa huyu mtoto.

Wote walifurahi sana na baadae mke akaandaa chai ndipo mume akauchukua ule mkate wa tatu aliopewa na boss. Baada ya sala aliumega mara akakuta kitita cha pesa nyingi sana, zilizidi hata zile alizostahili kulipwa baada ya kufanya kazi miaka ishirini.

MUNGU WETU YUKO KAMA HUYU BOSS. WAKATI MWINGINE ANAPOTAKA KUJITOA SADAKA, ANATAKA ATUPE VITU ZAIDI YA VILE TUNAVYOJITOA, ANATAKA TUWE NA HEKIMA ZA KIMUNGU PAMOJA NA BARAKA ZA MWILINI.MUNGU ANATUWAZIA MEMA SIKU ZOTE.
FB_IMG_1488941452016.jpg
 
story yako ni nzuri na inafunzo ndani yake mkuu.

Ubarikiwe kwa kushare nasi.
 
:) :) ni hadithi mkuu, chukua funzo tembea, usitake scientific proof, maana utauliza alitembea siku nyingi kwanini mkate haukuoza!? :) :)
Alisafiri siku nyingi usiku na mchana,ila njiani alikula mikate miwili tu.
 
huyo angekuwa daudi wa kolomije mbona angedai pesa kwanza ushauri mpka nipate vyeti og
 
Back
Top Bottom