Elia
JF-Expert Member
- Dec 30, 2009
- 3,425
- 568
Hii ni Hadithi ya ukweli iliyo nitokea mimi ila majina ya wahusika sio halisi nimependa kuiandika ili tushirikiane katika uzoefu na changamoto mbalimbali tunazopitia!
INTRO
Niliendelea kumuangalia kwa Muda mrefu nikiwa sijui nianzie wapi au nianze na neno gani, alinikazia macho nikainama chini kitu ambacho kilikua ni tofauti sana kwa mwanaume kukifanya. Nilimuangalia tena usoni safari hii nikiwa na wazo jipya ………
SEHEMU YA KWANZA
Mimi nafahamika kiasi kwenye hii bar, wahudumu hupenda kuniita anko sababu nazoeleka kirahisi na siko mgumu sana kuwatoa siku moja moja, kwa kweli huwa wanatumia hela yangu kwa vibia bia
Kuna muhudumu mgeni alikuja hapo bar ni mzuri sana kabla sijaonana naye kuna muhudumu kanitania, Eti wanakifaa sichomoi, mpaka wenzake wanamuonea wivu.
Na mimi bila kumuona huyo dada, nikaagiza apelekewe kinywaji atakacho kihitaji hukoaliko bili niletewe mimi, ikafanyika kama nilivyo agiza.
Nikalipa baadae nikiwa nacheza pool table akaja yule mdada kunishukuru kwa kinywaji na mimi nikamwambia poa bila hata kugeuka na kumuangalia. Huyo dada akaenda kumbe alijisikia vibaya maana amezowea kubabaikiwa.
Baadae nikaondoka bila hata kumuona na kumuaga (ndio nilivyo zowea sikumfanyia makusudi).
Kesho yake nikiwa ofisini nikapigiwa simu na namba ngeni na sauti ya kike
Nikauliza wewe nani? nikaambiwa anaitwa Maua (sio jina halisi)
Nikamwambia nikumbushe akaniambia mimi niyule dada uliye ninunulia kinywaji jana
Nikamuuliza Unasemaje? Ninadaiwa?
Akasema hapana, nimepiga nikushukuru tu!
Nikamuuliza ni hilo tu? Mbona jana ulinishukuru!
Akajibu aah, niliona upo bize sana! Nikaona ni bora nikutafute leo.
Nikamwambia jana sikuwa bize ila leo niko bize ofisini. Halafu Nikamuuliza nani amekupa namba yangu ya simu? (maana sikuwahi kutoa namba yangu pale). Akaniambia ameitafuta akapewa nilipata mshituko kidogo! Nikamjibu haya kazinjema (maana kweli nilikua bize). Kabla sijakata simu akaniuliza leo utakuja?
Itaendelea sehemu ya pili…….
SEHEMU YA PILI
Nikamjibu siwezi kwenda hapo kwa siku hiyo maana ilikua ni jumatatu, nisiku ambayo kwangu sio siku ya kupumzika. Akaniomba niende kwaajili yake, sikukubali maana haikuwa kwenye mpangilio wangu. Alisisitiza sana lakini nilianza kuudhika kwa alivyokua king'ang'anizi. Nilijisikia kufoka na kwamba ananipotezea muda, ila kwa mazingira ya ofisini kwangu nilijizuia nikakata simu, kilicho nifanya nijisikie vibaya sajazowea kubembelezwamaranyingi nikisema ndio ni ndio na no ni no. Niliendelea na kazi zangu kama kawaida nikiwa nimesahau tukio lililopita muda mfupi.
Baada ya siku mbili mchana nikiwa kazini simu iliita tena alikuwa ni Yule Yule mdada ila namba yake sikuisevu nilipo muuliza wewe nani alisita kidogo akakata simu niliendelea na kazi zangu kama kawaida baada ya kazi wakati narudi nyumbani nilikumbuka kuangalia simuyangu ili nijibu kama kuna kitu nilitakiwa kujibu, nikakumbuka simu ya mchana. Nikaipiga akapokea nikamuomba samahani na kumuuliza wewe ni nani? Akanijibu yeye ni Maua na kuniuliza inamaana ulifuta namba yangu? Nikamwambia hata sikuisevu (ambayo ilikua ndio kweli) akakakata simu nikapiga tena ikaita bila kupokelewa nikapiga tena akapokea akaniuliza unasemaje? Nikamuuliza mbona umenikatia simu? Akanijibu ‘aaah basi tu sijisikii'. Sijawahi ambiwa hivyo na mwanamke ilinikera sana. Nikamwambia sawa ila mimi nakuja huko leo maana ilikua ni jumatano siku ambayo huwa napenda kufika pale Pub. Akaniambia ‘utatukuta'. Moyoni mwangu nikajisemea huyu mwanamke ananini hasa? Mbona anajiamini kiasi hicho! hatujaonana kwa sura halafu hatuna urafiki wowote zaidi ya ileofa niliyo mpa? Nikaingiwa na hamu ya kumuona. Nilitamani nifike haraka pale Pub ila kifoleni cha Dar es salaam kilinifanya niwe mpole na siku hiyo kulikua na foleni sana, sikupenda giza liingie kabla sijamuona, kwakweli hamu ilikua juu sana hasa nilipokumbuka maneno ya Yule dada kwamba Maua ni mzuri sana, kwakweli alinichukua mawazo yangu yoote kwa wakati huo, nakumbuka nilikua sitoi hata nafasi gari nyingine kuingia barabarani yaani nilikua nawabania sana. Foleni ilianza kutembea na ilikua ni saa kumi na mbili kasoro kama ishirini hivi.