Sehemu ya nne
Basi mweka NADHIRI alimfata yuma mwanamke, alipomkalibia alipaza sauti akimwambia "POKEA ZAWADI ITOKAYA KWA MUMEO SHETANI" yule mwanamke alikataa akiae "UNIPISHE MIMI, SINA MUME SHETANI, MUMEWANGU NIYULE PALE MLANGONI." Wapitanjia walipo sikia maneno yale walimwambia, hasa wewe unastahili kupewa pesa za shetani maana humtii mumeo. Maneno yale yalimfedhehesha yule mwanamke nae alirudi na kumuomba msamaha mumewe namume alimsamehe mkewe.
Basi mweka NADHIRI alichukia sana maana pesa zile hazikupokelewa, hivyo alirudi nyumbani nakumweleza mkewe kwamba yule mke wa shetani hakuzipokea zile pesa, mke akamwambia, usichoke mwendee tena MTABIRI WA MALIMWENGU, Huenda akakupa ushauri wanwisho kutimiza NADHIRI hii. Mweka NADHIRI alirudi tena kwa yule mtabiri alipofika alikaribishwa, mtabiri akamuuliza mweka NADHIRI, nae akamwambia mke wa shetani kazikataa zile pesa je nifanyeje..? Mtabiri akamwambia usichoke mwendee tena shetani ukamwambie mkewe kazikataa zile pesa, huenda akakupa ushauri wamwisho.
MWEKANADHIRI akarudi tena msituni akasoma ile Aya kisha akamwita shetani, nae akamuuliza kuna nini tena, mweka NADHIRI akamwambia mkeo amezikataa hizi pesa, shetani akamwambia nenda ukampe mwangu akizipokea basi NADHIRI yako irakua imekwisha, mweka NADHIRI akamuuliza mwanao anaitwaje na yupo wapi.? Lakini ilesauti haikumjibu tena japo mweka NADHIRI aliuliza. Basi alirudi nyumbani akamwambia mkewe aliojibiwa na shetani, mkwewe akamwambia arudi tena kwa mtabiri wa malimwengu, nae akaenda kisha akamwekezea talitokea msituni, mtabiri akamwambia, watoto washetani wapo wengi hapa mjuni, tembea mitaani ukikuta mtoto anae mjeuria mzazi wake huyo ndio mwana wa shetani mpe pesa hizo ukimwambua zimetoka kwa baba yake shetani, akizipokea basi NADHIRI yako imetoka. Basi mweka NADHIRI alitoka akaanza kuzunguuka mitaani, alipofika katika mtaa wa mvuleni wenye chuo cha wavulani alikuta #KUSANYILO kubwaa lawatu.