Hadithi: Mmhh! Hata wewe mwanangu?

Hadithi: Mmhh! Hata wewe mwanangu?

INAENDELEA

Rashid ni kijana alieishia darasa la saba na kashindwa kuendelea na masomo kwa sababu ya wazazi kukosa uwezo. Aliamua kuondoka kwao alipofikia umri wa miaka 17. Alikimbilia kwenye machimbo ya dhahabu Geita. Enzi hizo makampuni ya uwekezaji yalikuwa hayapo. Wachimbaji wadogo ndio walikuwa wametamalaki. Ilikuwa ni kazi ngumu na yenye kila aina ya hatari. Lakini yeye dhamira yake ilimtuma siku moja atafanikiwa kupitia kazi hiyo.

Baada ya miaka miwili kupita aliacha kuchimba kwa kuingia kwenye "duara" (mashimo) na kuwa "Kota". Kota kwa lugha ya machimboni night mnunuzi wa dhahabu kutoka kwa Wachimbaji. Akiwa katika kazi ya ukota taratibu mtaji wakes ulianza kuongezeka. Kikubwa kilicho msaidia ni kutopenda dhurma. Daima huamini kama riziki ipo ipo.

Uaminifu wake ulimfanya kupewa hela na matajiri wakubwa iliyopo awanunulie dhahabu. Na kama ya hela ikipita mikononi mwa mtu lazima iache vumbi. Pesa hizi ziliongeza mzunguko wake wanakufa hela na kuwa mkubwa. Aliamua kuhamia Mwanza ili kupata changamoto mpya na kutumia fursa zingine za uwekezaji.

Kwa sasa tayari ana yard ya magari, ana mgahawa wa kisiasa uliopo katika ya jiji la Mwanza na nyumba kadhaa ambazo amepangisha. Tatizo kubwa la Rashid ni kupenda warembo. Ukifika kwake ana watoto watano ambao amezaa na wanawake tofauti. Pesa anaitumia kama silaha ya kupata warembo want nguvu. Hata laki mbili na nusu alizompa Rahabu aliamini amepanda mbegu. Ndio, mbegu itaoza lakini baadae itachipua na kumea.

******** *********** ***********

Wakiwa bado Tilapia hotel Shukuru anaamua kuwa mhubiri. Anaanza kwa kuuliza swali.
"Rahabu naomba unitajie Amri ya kwanza ya Mungu "
" Shukuru Amri za Mungu za nini? Huoni sio makala pake? "
" Mwenyezi Mungu yupo kila mahali na wakati wote. Naomba unitajie "
Kwa unyonge huku akijilazimisha akasema" Mimi ndie Bwana Mungu wako niliekuta Misri katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu wengine ila mimi. Usijifanyie Mfano wa kitu chochote kilichopo majini, juu ya ardhi au angani kwa kuwa mimi BWANA MUNGU WAKO night Mungu mwenye wivu ".
" Nashukuru umenena vyema, hongera sana"
"Je, unatambua kuwa mwanadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu? "
" Hilo nalitambua vyema, sisinzii wanadamu tu Mfano wa Mungu ". Rahabu anajibu kwa haraka ili maongezi haya yakome, maana yameanza kumboa.
" Sasa kwa kuwa sisi ni Mfano wa Mungu na kwa kuwa yeye ni Mungu mwenye wivu asie taka kuona tukiabudu miungu. Huoni kwamba mimi pia ni mwenye wivu na sitatakakukuona ukijifanyia Shukuru wa kuchonga. Mungu ana WIVU itakuwa mimi Shukuru mtoto wa mama Shukuru. "

Baada ya kuongea hivyo Shukuru anaendelea kumwambia Rahabu kuwa si vizuri kumuumiza mpenzi wake. Shukuru anapomaliza kuongea akamwomba Samahani na kumuahidi kutomkwaza kwa lolote. Kwa kuonyesha msisitizo anapomaliza anamsogelea na kumpiga busu la nguvu.. Bila kutarajia maneno yanamtoka, "I love you, your so unique. For me your a special one"

Upande wa pili wa maongezi haya badala to kumkera Rahabu anafurahi kupita maelezo. Moyoni anasema "Mapenzi wivu bila wivu hakuna mapenzi.
 
INAENDELEA

"Mapenzi wivu bila wivu hakuna mapenzi ". Rahabu anaongea ndani ya nafsi. Hata yeye alitaka kuwa na wasiwasi iweje" baby "wake ashuhudie kitendo cha pale ATM kati yake na Rashid asishituke. Ndio maana alianza kuwa mdogo baada ya" baby" kuonyesha dalili za kutoguzwa na lolote. Lakini sasa anajiona yupo juu mithili ya kisoda. Maneno aliyoambiwa anayachukulia kama ushindi unaoashiria kwa kiasi gani mpenzi wake alivyomweka rohoni.

"Shukuru Kuna umuhimu wowote wa kurudi chuo?"
"Sikuelewi?"
"Namaanisha kwa nini tusiende kupumzika kwenye hotel usiku wa Leo. Mimi naona si vyema tukakaa na hizi pesa , ni vyema tuzitumie zote ziishe "
" Hilo neno, ila jiandae tusije tukafika nikajijukulia ushindi wa mezani maana kiwanja kigeni kisije kikawa kisingizio "
" Duuuhh, siku zote wewe si ndio hupoteza mechi na kuanza kutaja jina la Bibi yako leo unasema utashinda? "
" Haya tusubiri tuone nani zaidi " Shukuru anasema.
" Haya tutaona, maana leo nitazionyesha silaha zangu za maangamizi nilizozipata 'lukuledi' "
" Mimi nitakuonyesha kwa nini Kagera watu wazima kila siku wanaanika magodoro. Nitakuonyesha "katerero" na wazimu wake.

*************** ************ *********

Othman ameteseka mno. Moyo wake umezamilia kumweleza ukweli Bhoke. Kwa nini aumie kiasi hiki wakati dawa ipo. Kabla ya kwenda kwa Bhoke anaamua kutafuta undani wa Bhoke. Anaamua kumtumia Paul na Paul anakubali sababu wanasoma kozi moja na Bhoke.

Leo ndio siku ambayo Othman kaambiwa atapewa taarifa za Bhoke ili zimsaidie katika pambano lililo mbele yake.
"Hodi " Paul anagonga mlango wa chumba.
" Karibu " Othman anaitikia.
Paul anaingia ndani huku usoni wake ukiwa na bashasha. Baada ya kusalimia anaona asipoteze Muda
" Kaka hongera sana "
" Ahsante, lakini hongera ya nini? " Othman anaipokea na kuuliza.
" Habari nilizozipata ni kwamba Bhoke mbali ya kuwa ni binti mrembo hana makuu na anajiheshimu kwa namna ambayo sina Mfano wa kukupa. Lakini habari nzuri kwako ni kwamba kwa sasa yupo single. Huenda anafanya kwa siri tena siri kubwa. Hata hivyo naamini penzi ni kikohozi watu wangekuwa wanajua. Nakutia shime huenda wewe ndie ulieandaliwa kwa ajili yake " Paul anasema.
" Kwa maelezo yako huenda nafasi ikawa finyu ".
" Huenda ni kweli, huenda si kweli kweli. Mapenzi ni upofu, anaweza asione mwingine akawa kakuona wewe "

Paul anaendelea kumfahamisha Othman kuwa kuna Makuwadi wengi wanaowatafutia wenye hela zao viburudisho kwa Bhoke wamekwama. Si tu amewakatalia bali hata maneno yake yamekuwa mwiba mkali kwao. Wengi wamekuwa wakiondoka vichwa chini. Hali hii imewajaza hasira kubwa baadhi ya vibompa kiasi cha kuwa radhi kupanda Dau na kuweka mezani ofa kubwa kubwa kama gari na safari za Dubai, China na kwingine huko ughaibuni. Sijui anajiamini nini, labda masomo anayochukua. Maana watu wenye kusoma mambo yenye kuhusiana na hesabu "automatic" hali hii huwafanya wawe watu wa misimamo kama sio kusimamia kile wanacho kiamini.

Othman anamshukuru Paul na kumweleza atajipa ili ajue anatoka vipi. Paul anaaga na kuondoka. Anamwacha Othman akitafakari. Unyonge unaanza kumwingia. Maskini mie Sijui lini nitafanikisha. Duuuhh hii ligi ni ngumu na kweli mchezo huu hauhitaji hasira. Hata hivyo kwa mbali Kuna chembe chembe za ujasiri zinamwingia. Anasikia sauti kwa mbali inamwambia, "Siku zote Jemedali wa kweli hufia kwenye uwanja wa vita, ni aibu na fedheha kusita kufika uwanja wa mpambano.
 
Mkuu Principle girl jamaa yako katekwa nini mbona kyima toka atoe epsod ya tano
 
Back
Top Bottom