Ngwananzengo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2012
- 1,911
- 1,320
Othmani anajilaza kitandani akiwa na lengo la kumsubiri rafiki yake Shukuru. Taratibu mawazo yanamrudisha nyuma miaka miwili iliyopita. Wakati akija kuanza masomo yake ya shahada ya Soshologi katika church cha MT. Augustino. Hakutegemea kama Muda ungeenda kwa kasi kiasi kile kiasi cha kufumba na kufumbua tayari yupo mwaka wa Tatu.
Mawazo yake yanakubaliana na ile methali ya wahenga, "Ukiona nyani Mzee porini basi jua kakwepa mikuki mingi". Ni mengi yametokea, yapo ya kutia moyo na kukatisha tamaa. Lakini kama ilivyo Ada ni wajibu wa kila mmoja kuyakabiri. Othmani akiwa katika kuwaza taratibu usingizi unampitia.
******* ******** *********
Ni siku nyingine inayowakutanisha Othmani, Shukuru na Rahabu. Wote hawa wapi mwaka wa Tatu wakisoma shahada ya Soshologi. Wamekaa kikao ili kupanga jinsi gani ya kuukabiri mwaka wao wa mwisho wa masomo. Pamoja na kwamba wote wanasoma pamoja Kuna kingine cha zaidi kinachowaunganisha wawe karibu. Othmani na Shukuru night marafiki wa dhati. Kwa sababu ya tabia zao kuendana urafiki wao uliongezeka na kuwa mithili ya ndugu.
Rahabu ambae ni mrembo kwa maana halisi ya urembo. Yeye ni mpenzi wa Shukuru. Rahabu ni binti mwenye sifa tele, macho yake mithili ya goroli, mwanya wa kishikaji bila kusahau "deenpose", umbo zuri lenye mvuto wa mahaba na nywele zake. Vyote kwa ujumla vimekuwa vikiwatia kiwewe wanaume na vijana wakwale.
Rahabu pamoja na uzuri ambao amejaaliwa anaamini elimu ndiyo inayoweza kumpa heshima. Anajituma kadri awezavyo ili aweze kufanikiwa.
******* ********* ********
Muafaka wa kikao chao ni kuongeza juhudi zaidi. Hii ni upande mmoja wa shilingi, upande wa pili Othmani ni mnyonge na hakuwa na amani rohoni. Aliwaza na kuwazua bila kupata jibu. Mapenzi ya Shukuru na Rahabu yalimfanya na yeye atamani kuwa na mpenzi. Amejitahidi kumpata ampendae lakini maskini hana bahati. Kila anapojaribu huwa anaangukia pua "Jamani nina mkosi gani mie". Kila Mara Othmani hujiuliza bila kupata jibu.
Tatizo hili ni kama kidonda ndugu katika moyo wa Othmani. Lakini nini Tatizo? Othmani amezaliwa na kukulia Kinondoni mtaa wa Mwinjuma karibu na Mango Garden. Fujo zote anazijua. Anajishangaa iweje aangukie pua kila Mara.
Mawazo yanamkumbusha jinsi Rhoda yule binti anaesoma sheria mwaka wa pili alivyomfanyia. Alianza vizuri kwa kupewa namba za simu, lakini cha kusikitisha na kushangaza alipoanza mashambulizi hakuamini yaliyomkuta. Yote tisa lakini kumi ni ule ujumbe aliotumiwa na Rhoda baada ya kuwa amefunguka. Ujumbe ule ulimtia simanzi na unyonge mwingi. Ndani ya ujumbe huo Rhoda aliamua kumpa za uso. Ujumbe ulikuwa hivi, "Wewe ni mtu wa aina gani usiejua kukataliwa. For me to be with you is a shame because I'm in next level"
Ilibidi akubaliane na hali halisi japo aliona kadharauliwa pakubwa. Hata hivyo hakuyumba katika masomo yake. Hasira zake alizimalizia katika kusoma.
******* ITAENDELEA.