Hadithi: Mbio za sakafuni huishia ukingoni

Hadithi: Mbio za sakafuni huishia ukingoni

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,637
MBIO ZA SAKAFUNI HUISHIA UKINGONI 1

Ulikuwa ni wakati wa chakula cha usiku. Waziri Mkuu Dastan Lazaro na familia yake ya watoto watatu Vero, Monica na Sofia pamoja mke wake Vicky walikuwa katika chumba cha kulia chakula nyumbani kwa Waziri Mkuu, Msasani jijini Dar.

Walikuwa wanakula chakula.

Upande mmoja wa meza aliketi Waziri Mkuu mwenyewe na mke wake Vicky. Upande mwingine walikuwa wamekaa mabinti zao Vero, Monica na Sofia.

Akiwa mtoto wa kwanza wa mheshimiwa Dastan Lazaro, Veronica alikuwa mrefu na mweupe kama alivyokuwa baba yake. Lakini urefu wake haukuchusha kwa vile alikuwa na maungo yaliyojaa na yaliyoumbika vizuri.

Alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo Kikuu cha mlimani akichukua masomo ya sheria. Alikuwa mchangamfu na aliyependa sana mzaha

Monica ndiye aliyefuatia kwa kuzaliwa. Yeye alimshabihi mama yake kwa sura na kwa umbo. Alikuwa mfupi wa rangi ya maji ya kunde. Uso wake mpana na wa duara ulionekana kama unaotabasamu wakati wote.

Alikuwa akisoma kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wanafunzi wenye vipaji maalum. Licha ya kushabihiana sana na mama yake, alikuwa kipenzi mkubwa wa baba yake.

Sofia ndiye aliyekuwa kitinda mimba wao na aliyeonekana kuwa mzuri zaidi. Alikuwa na urefu wa wastani. Hakuwa mnene wala mwembamba. Alikuwa na umbo la katikati.

Akiwa mwanafunzi wa kidato cha nne, alikuwa na tabia ya kiburi na hasira za haraka haraka lakini ndiye aliyekuwa akisikilizwa zaidi na wazazi wake.

Alikuwa akipenda sana kikolezo cha pilipili. Alipoona chupa ya pilipili haikuwekwa mezani, aliondoka kwenye kiti na kuelekea jikoni.

Mke wa Waziri Mkuu akamtazama mume wake.

“Unajua mwanao anakwenda wapi?” akamuuliza.

Dastan Lazaro akabeua mabega yake.

“Sijui”

“Amekwenda kuchukua pilipili jikoni. Mwanao anapenda sana pilipili”

“Pilipili si nzuri sana. Unatakiwa umkataze asipendelee sana pilipili”

“Nimeshamkataza mara nyingi lakini hasikii. Si unamjua Sofia alivyo mbishi!”

“Subiri arudi”

“Yaani anaweza kuacha chakula ukimwambia aache pilipili”

“Pilipili ya nini msichana mdogo!”

Zikapita karibu dakika kumi kabla ya Sofia kutokea.

“Mbona haji?” Dastan Lazaro akauliza.

“Labda amesikia tulivyosema amechukia” Vicky akasema.

“Monica hebu kamtazame Sofia, anafanya nini jikoni” Lazaro akamwambia Monica.

Monica akanyanyuka na kuelekea jikoni. Alipoingia kwenye chumba cha jiko alitoa sauti ya kimako iliyosikika. Alitoa sauti hiyo mara tu alipomuona Pili, mpishi wa nyumbani kwao amelala chini huku akiwa na michirizi ya damu iliyoganda kwenye shingo yake.

Nguo aliyokuwa amevaa ilikuwa imechanwa kwenye bega. Kiatu kimoja cha Pili kilikuwa karibu yake.

“Baba!” Monica akaita kwa sauti ya kugutusha.

“Kitu gani?” Lazaro akauliza kwa taharuki.

“Njoo baba!”

Hakuondoka Lazaro peke yake, waliondoka wote. Walikwenda jikoni na kumuona mpishi aliyekuwa amelala chini.

“Nini?” Lazaro akauliza.

“Nimemkuta mpishi ameanguka, sijui ana nini?”

Lazaro akainama na kumtazama, akaiona ile michirizi ya damu kwenye shingo yake.

“Pili! Pili!” akajaribu kumuita.

Pili alikuwa kimya huku macho yake yakiwa wazi lakini yalikuwa hayaangalii chochote hali iliyoonesha kutokuwa na dalili yoyote ya uhai.

Ilimchukua dakika moja tu Dastan Lazaro kugundua kuwa Pili alikuwa amekufa!.

Akainuka.

“Kuna kila dalili zinazoonesha kuwa huyu msichana ameshakufa” akasema.

“Sasa amepatwa na nini?” Vicky akauliza kwa hofu.

“Hatujui lakini kwenye shingo yake kuna michirizi ya damu na kwenye bega lake nguo yake imechanwa”

“Kwani Sofia yuko wapi?”

“Sijui, sikumkuta huku jikoni. Kuna kiatu chake kimoja tu hapa” Monica akajibu.

“Au amekwenda juu” aliuliza Lazaro.

Nyumba ya Waziri Mkuu ilikuwa ina ghorofa moja. Vyumba vya mabinti hao vilikuwa juu.

Waziri mkuu akatoka jikoni haraka akapanda ngazi kuelekea ghorofani. Alikuta kiatu kingine cha Sofia kikiwa kwenye ngazi kitu ambacho kilimpa imani kuwa Sofia alikuwa ghorofani.

Alipomaliza kupanda ngazi alitembea kwenye korido kuelekea kwenye chumba cha Sofia.

Alipofika kwenye chumba hicho alifungua mlango na kuchungulia ndani. Alimkuta Sofia akiwa amelala kwenye kitanda.

‘Sofia!” akamuita.

Alipoona Sofia hakuitika aliingia na kusogea kando ya kitanda.

“Sofia!” akamuita tena.

Sofia alikuwa amelala kimya kifudifudi, uso wake ukiwa ameeelekeza kwenye mlango. Macho yake yalikuwa yamefumba kama aliyekuwa kwenye usingizi lakini midomo yake ilikuwa wazi ikivuja damu.

Kwenye kiganja cha mkono wake wa kulia alikuwa amefumbata kitu. Waziri Mkuu alipokiangalia aligundua kilikuwa kipande cha kitambara kilichochanwa begani mwa nguo aliyokuwa amevaa Pili.

Wakati Lazaro akimtazama binti yake, mke wake na na mabinti zao wengine wakaingia mle chumbani.

“Nini tena?” Mke wa Waziri Mkuu akauliza kwa mshangao.

Hali ile waliyomkuta nayo Sofia ilikuwa imewashitua wote.

“Sijui!” Dastan Lazaro alisema akionekana kuduwaa. Akaongeza.

“Mdomoni kwake kunatoka damu na anaonekana amelala usingizi”

Vicky alisogea kwenye kitanda na kumuamsha.

“Sofia! Sofia!”

Sofia akazinduka na kufumbua macho. Akawatazama kwa zamu baba yake, mama yake na ndugu zake.

Macho yake yalikuwa mekundu kama aliyekuwa amelala mchana kutwa.

“Una nini?” Mama yake akamuuliza.

Sofia akajitazama kama aliyekuwa akijishangaa. Alikunjua kile kiganja chake alichokuwa amekifumba. Akakitazama kwa mshangao kile kipande cha nguo alichokuwa amekishika kabla ya kukiachia.

Akajiinua na kuketi kitandani. Kama vile alihisi ladha ya damu midomoni aliupitisha mkono wake kujifuta midomo kisha akaitazama damu aliyoipangusa mkononi.

“Sofia una nini?” Mama yake alimuuliza tena.

Sofia akainua uso na kumtazama mama yake.

“Mbona nina damu midomoni?” akauliza kwa mshangao.

Waziri Mkuu na mke wake wakatazamana.

“Hujui ni kwanini una damu midomoni?” Lazaro akamuuliza.

“Sijui, naona damu tu iko midomoni mwangu!”

Sofia aliendelea kuifuta ile damu na kuitazama.

“Na hicho kipande cha kitambaa ulichokuwa umeshika ni cha nini?”

Sofia alikitazama kile kipande cha kitambaa kabla ya kuuliza.

“Hiki?’

“Ndiyo, hicho”

“Sijui”

“Unajisikia kuumwa?” Lazaro akaendelea kumuuliza.

“Nasikia kichwa kinagonga kwa mbali”

“Hukuuma mtu?”

Sofia akatikisa kichwa.

“Sijauma mtu”

“Wewe si ulikuwa umekwenda jikoni baada ya kuondoka kwenye chakula?”

Sofia alifikiri kisha akajibu

“Ndiyo nilikwenda jikoni kuchukua pilipili”

“Ulimkuta Pili?”

“Ndiyo nilimkuta”

“Halafu nini kilitokea?’

Sofia alivuta kumbukumbu kisha akatikisa kichwa.

Je nini kilitokea?
 
SEHEMU YA 02


ILIPOISHIA



“Unajisikia kuumwa?” Lazaro akaendelea kumuuliza.



“Nasikia kichwa kinagonga kwa mbali”



“Hukuuma mtu?”



Sofia akatikisa kichwa.



“Sijauma mtu”



“Wewe si ulikuwa umekwenda jikoni baada ya kuondoka kwenye chakula?”



Sofia alifikiri kisha akajibu.



“Ndiyo nilikwenda jikoni kuchukua pilipili”



“Ulimkuta Pili?”



“Ndiyo nilimkuta”



“Halafu nini kilitokea?’



Sofia alivuta kumbukumbu kisha akatikisa kichwa.



SASA ENDELEA



“Sikumbuki. Kichwa kinaniuma sasa”



Lazaro akashusha pumzi ndefu. Akamtazama mke wake.



“Inawezekana ana malaria na imepanda kichwani” alimwambia mke wake.



“Inawezekana” Vicky alisema huku hofu na wasiwasi vikisomeka wazi usoni kwake.



“Sijui yule msichana amemfanya nini. Mwenyewe hakumbuki kitu”



“Naona kama amemng’ata”



Wakati Waziri Mkuu Dastan Lazaro na mke wake Vicky wakisemeshana, Sofia alikuwa akiwasikiliza na kuwatazama kwa mshangao.



“Nimemng’ata nani?” akawauliza.



“Pili, mpishi wetu” Lazaro akamjibu.



Sofia akatikisa kichwa.



“Hapana, sijang’ata mtu”



“Umemng’ata na ndio sababu una damu midomoni”



Mama yake naye akaongeza.



“Hicho kipande cha kitambaa ulichokuwa umeshika ni cha nguo aliyovaa. Ulikichana wakati umemshika lakini mwenyewe ulikuwa hujijui”



Mshangao wa Sofia sasa ulionekana waziwazi usoni kwake.



Lazaro alimshika mkono mke ake wakatoka mle chumbani.



“Unadhani kitu gani kimesababisha kifo cha yule msichana?” Lazaro akamuuliza mke wake.



Walikuwa wamesimama kando ya mlango.



“Labda alimkaba koo”



“Sidhani”



Sofia akawafuta kusikiliza walichokuwa wanazungumza. Wakaliona tumbo lake, lilikuwa limejaa kama mja mzito. Wakati akiondoka kwenye meza ya chakula, tumbo lake halikuwa hivyo.



“Mbona tumbo limejaa Sofia?” Mama yake akamuuliza.



Sofia akalitazama tumbo lake na kulishika.



“Limejaa kweli mama, na nateuka ladha ya damu tupu”



Lazaro na mke wake wakatambua kwamba Sofia alikuwa amemfyonza damu yule msichana na ndiyo iliyokuwa imejaa kwenye tumbo lake.



“Subiri upelekwe hospitali mwanangu” Lazaro akamwambia.



“Nitakuwa nina malaria baba?”



“Bila shaka”



Lazaro alitoa simu yake akampigia dereva wa mke wake ambaye muda ule alikuwa amesharudi nyumbani.



“Hebu njoo, kuna tatizo kidogo” Lazaro alimwambia dereva huyo kwenye simu.



“Sawa, mzee ninakuja”



“Unaweza kukodi teksi ikulete mara moja, tutailipia”



“Sawa mheshimiwa”



Lazaro akakata simu.



“Mtayarishe mwanao, dereva anakuja umpeleke hospitali”



Mke wa Waziri Mkuu akamtazama Sofia.



“Nenda chumbani mwako ubadili nguo kisha usukutue mdomo wako” alimwambia.



“Sawa mama”



Sofia akaondoka.



“Sofia ndio amemuua yule mpishi wetu” Lazaro akamnong’oneza mke wake.



“Sasa tutafanyaje” Vicky akauliza kwa tashiwishi.



“Sijui mke wangu. Kuliripoti tukio hili ni sawa na kumwaga petroli kwenye moto, linaweza kumpa matatizo Sofia na kuniweka mimi katika wakati mgumu japokuwa najua Sofia alifanya hivyo akiwa hajitambui lakini haitaonekana hivyo”



“Ninajua. Kuna mambo mengi yataangaliwa na kusemwa”



“Ninaweza pia kutakiwa kujiuzulu uwaziri mkuu kwa sababu tukio limetokea nyumbani kwangu na itaonekana nimeshindwa kulizuia’



“Sasa tutafanyaje” Viccky alirudia swali lake.



“Ile maiti tuihifadhi kwanza, tungoje vipimo vya Sofia”



“Sawa. Ngoja nikamuandae. Dereva akija twende naye”



Mke wa Waziri Mkuu akamfuata Sofia. Lazaro akawaita wanawe wengine Vero na Monica.



“Nataka tukio hili liwe siri ya humu ndani, lisitoke nje. Mmenielewa?”



Wasichana hao walikubali kuwa wamemuelewa.



“Sofia ana malaria na imempanda kichwani, bila kujielewa amemng’ata yule msichana mpishi wetu na kumfyonza damu hadi amemuua. Kwa sasa sitaki habari hii ifike kwenye vyombo vya dola wala uraiani”



“Sasa ile maiti tutaipeleka wapi?’ Vero akamuuliza baba yake.



“Tutaihifadhi humu humu ndani tukisubri Sofia apelekwe hospitali. Nimeshamuita dereva. Sasa twendeni tukasaidiane kuiondoa kule jikoni’



Lazaro na wanawe wakashuka ngazi na kuingia jikoni.



“Tumbebe tukamuweke stoo kwa muda” Lazaro akawambia wanawe.



Waliubeba mwili wa Pili na kwenda kuulaza stoo. Baada ya kumlaza, Lazaro aliichunguza ile sehemu ya shingoni iliyokuwa inatoka damu. Akagundua kuwa ilikuwa imepigwa meno na ilikuwa na tundu mbili za meno.



Wakati Waziri na wanawe wanatoka stoo, mke wa Waziri na

Sofia walikuwa wanashuka ngazi. Sofia alikuwa ameshabadili nguo.



“Sisi tuko tayari” Mke wa waziri alimwambia mume wake.



Waziri Dastan alimtazama Sofia. Safari hii alimuona tofauti kidogo. Alikuwa amechangamka na alionekana wa kawaida.



“Mumsubiri dereva awapeleke”



“Sijui atakuja saa ngapi?”



Hapo hapo mlinzi akampigia simu waziri. Waziri alipoipokea aliambiwa.



“Dereva ameshafika”



“Mwambie asubiri afunguliwe geti”



Waziri akakata simu na kumwambia mke wake.



“Dereva ameshafika, yuko nje”



“Ngoja nikamfungulie geti” Alikuwa Vero ambaye alitoka kwenda kufungua geti. Dereva akaingia.



Waziri na mke wake pamoja na Sofia walikuwa wametoka na kusimama karibu na banda la gari.



“Wapeleke hospitali, Sofia anaumwa” Waziri akamwambia dereva huyo.



“Nichukue gari lipi?’



“Chukua gari langu binafsi” Waziri alimwambia huku akimpa funguo.



Dereva alizipokea funguo za gari akaingia ndani ya gari hilo na kuliwasha.



Alilitoa kwenye banda akalisimamisha. Mke wa waziri na Sofia wakajipakia katika siti za nyuma. Walipofunga milango gari likaondoka. Lilitoka kwenye geti na kukamata barabara.



“Tunakwenda hospitali gani?” dereva akauliza.



“Tupeleke hospitali ya H.B.M” mke wa waziri akamjibu.





Fuatilia hadithi
 
SEHEMU YA 03


ILIPOISHIA



Hospitali yenyewe ilikuwa Masaki. Ilikuwa hospitali kubwa ya binafsi iliyokuwa ikiendeshwa na mzalendo wa Kitanzania. Ilikuwa ikitumiwa zaidi na mawaziri na waheshimiwa wengine ndani ya serikali.



Baada ya uchunguzi uliochukua dakika kadhaa kutoka katika sampuli ya damu ya binti wa Waziri Mkuu, iligunduliwa kuwa binti huyo hakuwa akisumbuliwa na malaria.



Madakatari walichukua vipimo vingine ambavyo navyo vilionesha kuwa Sofia hakuwa na tatizo lolote la kiafya.



Matokeo hayo licha ya kuutuliza moyo wa Sofia, yalimshangaza mama yake. Sofia alipoulizwa anajisikiaje alijibu kuwa alikuwa anajisikia vizuri.



“Alisema kichwa kilikuwa kinamuuma sana” Mama yake akawambia madaktari.



“Lakini sasa hivi hakiumi tena” Sofia akadakia.



“Anaonekana kuwa na afya njema. Uchovu pia unaweza kusababisha kuumwa kichwa. Hili si tatizo kubwa hasa kama linatokea kwa mara moja” Daktari alimwambia mama yake Sofia.



SASA ENDELEA



Sofia hakupata matibabu yoyote akarudishwa nyumbani. Dereva alipewa shilingi elfu hamsini na waziri kwa ajili ya usafiri wake kabla ya kuondoka.





“Ninashanga kusikia kuwa Sofia hana malaria” Waziri alimwambia mke wake akiwa chumbani.



“Hata mimi nimeshangaa na mwenyewe anasema anajisikia vizuri”



“Sasa amepatwa na tatizo gani?”



‘Inabidi tuendelee kumfanyia uchunguzi zaidi”



“Okey, sasa hili suala jingine tutalitatua vipi?”



“Sijui wewe mwenzangu umewaza nini?”



“Kusema kweli kichwa changu kimevurugika sana. Ni afadhali ingegundulika kuwa Sofia ana malaria”



“Itaonekana kwamba aliua kwa kukusudia”



“Lakini ni lazima kutakuwa na tatizo, Sofia hawezi kumtoboa mtu na kumfyonza damu hadi kumuua”



“Na inaonekana alifanya hivyo bila kujielewa”



“Kwa hiyo ni lazima kuna tatizo”



**************



“Ninashangaa kusikia kuwa Sofia hana malaria” Waziri alimwambia mke wake wakiwa chumbani.



“Hata mimi nimeshangaa na mwenyewe anasema anajisikia vizuri”



“Sasa amepatwa na tatizo gani?”



‘Inabidi tuendelee kumfanyia uchunguzi zaidi”



“Okey, sasa hili suala jingine tutalitatua vipi?”



“Sijui wewe mwenzangu umewaza nini?”



“Kusema kweli kichwa changu kimevurugika sana. Ni afadhali ingegundulika kuwa Sofia ana malaria”



“Itaonekana kwamba aliua kwa kukusudia”



“Lakini ni lazima kutakuwa na tatizo, Sofia hawezi kumtoboa mtu na kumfyonza damu hadi kumuua”



“Na inaonekana alifanya hivyo bila kujielewa”



“Kwa hiyo ni lazima kuna tatizo”



“Sasa tatizo limezaa tatizo na tunatakiwa tulishughulikie usiku huu huu”



“Sikiliza mke wangu, siwezi kumtia binti yangu kwenye matatizo ya kiserikali, si unajua tuhuma za mauaji ni kubwa. Na pia siwezi kujitia mimi mwenyewe katika matatizo ya kiserikali, bado ninahitaji niwe waziri mkuu kama nilivyo, nisingependa nipate kashfa yoyote”



“Umekusudia kufanya nini”



“Hili tatizo limetokea kwa bahati mbaya na linaweza likatuweka mahali pabaya sisi sote. Kwa hiyo nimeona nifanye kitu kimoja”



“Kitu gani?”



“Si kitu kizuri lakini ni lazima nikifanye haraka iwezekanavyo ili kuokoa jahazi”



“Ningependa kukisikia ili tushauriane”



“Nataka niuchukue huu mwili wa Pili nikautupe sehemu nyingine usiku huu”



“Ukishautupa itakuwaje?’



”Ninataka ionekane kuwa Pili hakuuawa nyumbani kwangu”



“Ni wazo zuri…”



“Mwili wake utakapoonekana asubuhi nitaeleza kuwa Pili aliondoka nyumbani kwangu saa moja usiku. Alituambia kuwa anaumwa na kichwa na alitumia usafiri wake mwenyewe”



“Ni sawa. Katika kujinusuru mpango huo unafaa”



“Sidhani kama kuna mtu atatushutumu”



“Si rahisi”



“Polisi watachunguza na wataona ameuawa na watu wengine”



“Mimi nakubaliana na wazo hilo”



“Sasa kama tumekubaliana acha nibadili nguo, niubebe ule mwili niutie kwenye gari langu. Nitaendesha mwenyewe. Ile gari yangu binafsi haijulikani sana, hakuna atakayeweza kunitambua”



“Halafu utakwenda kumtupa wapi?”



“Nitatafuta sehemu yenye kiza mitaa ya uswahilini. Hakuna atakayeniona usiku huu’



“Kwani hivi sasa ni saa ngapi?”



Waziri aliitazama saa yake ya mkononi.



“Sasa ni saa tano, inakaribia kuwa na robo”



“Bado ni mapema mno, ungesubiri angalau ifike saa saba. Kutakuwa kimya sana”



“Kusubiri hadi saa saba ni kupoteza muda, huu mwili tunatakiwa tuuondoe haraka humu ndani. Sidhani kama nitakosa sehemu nzuri muda huu”



“Sawa, basi wahi”



Waziri akabadili nguo. Alivaa jinzi na tisheti. Kichwani alivaa pama ili kuficha uso wake.



“Umebadilika sana” mke wake alimwambia na kuongeza.



“Si rahisi mtu kukutambua”



“Na kwa vile nitatumia gari langu binafsi ndio sitatambulika kabisa”



“Sasa twende tukasaidiane kumbeba”



Wakatoka chumbani. Walikwenda stoo wakauchukua mwili wa msichana huyo na kutoka nao. Waliupakia kwenye gari la waziri katika siti ya nyuma.



Waziri akafungua mlango wa dereva akajipakia na kuliwasha gari.



“Ngoja niende” alimwambia mke wake na kulitoa gari.



Kwa saa kadhaa Waziri Mkuu alikuwa akizunguka na gari lake katika mitaa ya eneo la Kinondoni ambako Pili, msichana aliyeuawa na mwanawe alikuwa anaishi.



Waziri Mkuu hakuwa akijua Pili alikuwa akiishi katika mtaa gani lakini hilo halikuwa tatizo kwake. Mradi alikuwa akijua kuwa alikuwa akiishi katika eneo hilo alitaka kuuacha mwili wake mahali popote tu ili iwe rahisi kutambuliwa na ndugu na jamaa zake.



Ingawa ulikuwa usiku mwingi baadhi ya mitaa ya eneo hilo ilikuwa bado ina harakati za watu. Baadhi ya mitaa mengine iliyokuwa iko kimya ilikuwa imeng’arishwa na taa za barabarani pamoja na taa za majumbani, hali iliyosababisha waziri ashindwe kuutelekeza mwili huo aliokuwa ameupakia kwnye gari.



Katika kuzunguka zunguka kutafuta sehemu tulivu iliyo kimya na yenye kiza alitokea katika eneo la shule moja ya msingi ambayo ilikuwa na kiwanja cha mpira.



Kiwanja hicho kilikuwa kama jangwa lililoachwa pekee. Karibu na kiwanja hicho kulikuwa na majengo ya shule yaliyokuwa kiza na kimya.



Waziri akaona mahali hapo palikuwa muafaka kuuacha mwili wa Pili kwani hapakuwa na nyumba za watu karibu na palikuwa kiza. Aliliingiza gari ndani ya eneo la kiwanja hicho akavipita kidogo vyuma vya magoli ya upande mmoja kisha akalisimamaisha gari.



Alibaki kwenye siti kwa dakika kadhaa kuangalia kama kutatokea mtu yeyote. Alipoona hakukuwa na mtu yeyote aliyejitokeza akafungua mlango wa gari na kushuka.



Alikwenda kwenye mlango wa siti ya nyuma akaufungua. Aliuvuta mwili wa Pili akautoa kwenye gari. Akiwa ameushikilia mikononi alikwenda pembeni mwa goli, mahala ambapo palikuwa na mti wa mwembe.



Alitaka auweke mwili huo chini ya mwembe uliokuwa hapo lakini ghafla akashitushwa na mwanga wa tochi uliokuwa ukimmulika. Mwanga huo ulitokea sambamba na mlio wa mabuti uliosikika kutoka nyuma yake.



Ule mshituko uliufanya mwili wake usisimke. Akiwa bado ameushikilia mwili wa Pili aligeuka haraka na kutazama nyuma.



“Wewe nani na unafanya nini mahali hapo?” Sauti nzito ya mtu aliyekuwa akija kwa haraka nyuma yake ilimtatanisha.



Akagundua mara moja kuwa alikuwa mlinzi wa ile shule. Alikuwa amevaa kama askari wa makampuni ya ulinzi akiwa na kofia na mabuti.



Mkono mmoja alikuwa ameshika tochi iliyokuwa ikimmulika na mkono mwingine alishika sime ambayo tayari alikuwa ameipunga juu.



Alikuwa kama hatua kumi na tano hivi nyuma ya waziri.



Ule mwanga wa tochi sasa ulikuwa ukimpiga waziri usoni.



Kile kitendo cha kufumwa akiwa katika hatua ya kuutupa mwili huo kilimfanya ababaike na kutaharuki. Kadhalika ule mwanga wa tochi uliokuwa ukimmulika usoni ulimchanganya zaidi.



“Nimekuuliza wewe ni nani na unataka kufanya nini katika eneo hili?’ Mlinzi huyo alimuuliza tena waziri huku akikaza mwendo kumfuata.



Alikuwa amemkaribia sana.



Itaendelea
 
SEHEMU YA 04


ILIPOISHIA



Waziri alijiambia hatua aliyochukua ambayo aliiona ilikuwa ya maana ya kuutupa mwili huo mahali hapo, ilikuwa ya kipumbavu. Hakuwa amefanya uchunguzi sahihi na kugundua kuwa mahali hapo palikuwa salama.



Wazo la kuwa eneo hilo litakuwa na mlinzi halikuwemo katika akili yake.



Waziri alijuta. Alijiambia siku ya kuumbuka na kukatwa katwa mapanga ndiyo ile.



Wakati mlinzi akiendelea kumfuata kwa mwendo wa haraka akiwa ameipunga sime yake, waziri alimrushia ule mwili ukaanguka karibu yake kwa kishindo.



Mlinzi akasita na kukitazama kitu kilichokuwa kimetupwa mbele yake. Alipourudisha uso wake kwa waziri, waziri hakuwepo.



Alikuwa ametimua mbio kuelekea kwenye gari lake. Kwa vile mlango aliuacha wazi alikaa kwenye siti haraka. Alishukuru kwamba gari hakuwa amelizima moto. Akatia gea ya kwanza na kuliondoa.



Mlinzi alikuwa kikimbia kulifuata gari hilo.



“Simama wewe, umetupa nini pale?” Mlinzi huyo alimwambia waziri akiwa ametinga mbele ya gari hilo.



SASA ENDELEA



Waziri alimkwepa. Ilibaki kidogo tu angemgonga. Mlinzi mwenyewe pia aliruka kando kulikwepa gari hilo. Gari likampita na kutokea barabarani.



Waziri aliposhika barabara alikanyaga mafuta. Gari lilikimbia kwa kasi!



Mlinzi alikuwa ametaharuki baada ya kukoswa kuswa na gari la waziri. Alikuwa amesimama akilitazama gari hilo likikata mbuga!



Hakuweza kujua gari hilo lilikuwa likiendeshwa na nani na kile kiu alichorushiwa kilikuwa kitu gani. Akarudi sasa kiukiangalia vizuri.



Aliumwilika tochi mwili wa Pili. Mlinzi akashituka alipogundua kuwa ni mtu tena wa jinsia ya kike. Aligeuza tena uso akatazama upande ule lilikoelekea gari la waziri kisha akachutama na kuutazama vizuri mwili huo.



Kwanza alihisi mwanamke huyo alikuwa amelewa chakari kiasi kwamba hakuwa akijiweza lakini akajiuliza aliyelewa hapumui na macho yake hayapepesi?



Akaguna kisha akanyanyuka. Akaanza kutimua mbio kuelekea kituo kidogo cha polisi kilichokuwa jirani na pale. Alipofika aliwakuta polisi wawili waliokuwa wakisinzia. Akawaamsha.



“Kitu gani?” Polisi mmoja akamuuliza kwa kutaharuki baada ya kuamshwa usingizini.



“Mimi ni mlinzi wa ile shule ya msingi pale. Kuna mtu alikuja na gari akatupa mtu tena mwanamke…” Mlinzi huyo aliwambia.



“Hebu tueleze vizuri, ni mtu gani aliyetupwa hapo?” Polisi mmoja akamuuliza.



“Sijui. Hebu twendeni mkamuone”



“Huyo mtu yuko katika hali gani?”



“Sijui amekufa…sijui ni mzima…kwa maana hapumui!”



“Ni mwanamme au mwanamke?”



“Ni mwanamke”



Polisi mmoja akamwambia mwenzake afuatane na yule mlinzi akamuone huyo mtu.



Polisi na mlinzi huyo walipofika mahali hapo, mlinzi aliumulika tochi mwili wa Pili.







Polisi huyo baada ya kuutazama mwili huo alisema.



“Sijui amepigwa au amebakwa. Kwenye shingo yake kuna damu”



“Unaona tairi za gari lenyewe hizi hapa” Mlinzi alimwambia polisi huyo huku akizimulika alama za tairi za gari la waziri zilizokuwa kwenye michanga.



“Lilitokea upande gani?”



“Lilitokea upande huu, mimi nilikuwa nimekaa pale ninaangalia tu. Gari hilo lilipofika hapa ndipo mtu mmoja akashuka, nikaona anatoa kitu. Mimi nikaja haraka. Aliponiona akanitupia huu mwili na kukimbia kwenye gari…”



“Walikuwa watu wangapi?”



“Mimi niliona mtu mmoja tu labda wenzake walikuwa kwenye gari”



“Ina maana walikuja kuutupa huu mwili?”



“Labda”



Polisi huyo akatoa simu ya mkononi na kumpigia mwenzake aliyemuacha kituoni.



“Aisee kuna mtu hapa…sijui ameuawa au amezimia…ametupwa katika uwanja wa shule” Polisi huyo alimwambia mwenzake alipopokea simu.



“Anaonekanaje…amepigwa au…?” Sauti ya mwenzake ilisikika ikiuliza.



“Katika shingo yake kuna damu iliyoganda…sasa sijui amenyongwa shingo au vipi…!”



“Ni mwanamke au mwanaume?”



“Ni mwanamke. Inawezekana walimbaka kwanza ndio wakaamua kuja kumtupa hapa”



“Sasa kata simu niwapigie polisi wa kituo kikuu walete gari”



“Sawa”



Polisi huyo akakata simu.



Polisi aliyekuwa kituoni akawapigia simu polisi wa kituo cha Kinondoni.



“Nini kimetokea hapo?” Inspekta Alex aliyekuwa katika zamu ya usiku kiuoni hapo alimuuliza.



“Kuna tukio limetokea sasa hivi. Mlinzi wa shule ya msingi ya Kinondoni ametuletea taarifa kwamba kuna mwanamke ametupwa karibu na eneo la shule”



“Nyinyi mmefika kumuona?”



“Aliyekwenda ni constebo Faustus na amenipigia smu”



“Amesemaje?’



“Amemuona huyo mwanamke na hana uhakika kwamba ameuawa au yuko hai”



“Hao waliomtupa ni kina nani?”



“Ni watu waliofika na gari. Walimshusha wakamtupa na kukimbia na gari”



“Kuna watu walioliona hilo gari?”



“Mlinzi aliliona”



“Sawa. Subiri tunakuja”



*************



Waziri Mkuu alipofika nyumbani kwake aliliingiza gari ndani ya geti akaliegesha katika banda la kuegesha magari. Alipolizima gari aligundua kuwa alikuwa akihema kama aliyekuwa akikimbia kwa miguu.



ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 05


ILIPOISHIA



Kwa mtu mwenye uzoevu mdogo tu wa vitendo vya uhalifu ilikuwa kazi ndogo tu kuutupa mwili wa Pili na kukimbiza gari kuondoka mahali hapo. Lakini kwa afisa wa serikali aliyezoea kukaa ofisini na kutoa amri kwa maneno, ilikuwa kazi kubwa sana.



Kitendo kile cha kufumwa na mlinzi kilimfanya ataharuki na kuamsha mapigo yake ya moyo. Ingawa alifanikiwa kufika nyumbani kwake salama hakuamini kwamba ilikuwa salama. Alijiambia huenda mlinzi aliziona namba za gari lake wakati akikimbia na atawatajia polisi.



Karibu njia nzima alikuwa akilaani na kujiona alikuwa amefanya kitendo cha kizembe.



Wakati analizima moto gari hilo alishusha pumzi ndefu kisha akafungua mlango na kushuka. Mke wake alikuwa amesimama kwenye mlango wa nyumba yake akimsubiri.



“Vipi?” akamuuliza.



Waziri Mkuu hakumjibu kitu, aliingia ndani. Aliketi sebuleni akauweka mguu wake juu ya mwingine. Kitendo hicho kilikuwa ni cha mazoea ya ukwasi tu, hakikuwa cha kujinafasi katika muda ule wa taharuki.



SASA ENDELEA



“Umefanikiwa?” mke wake alimuuliza tena alipomuona yuko kimya.



“Nimefanikiwa lakini…”



Mke wake akashituka kidogo.



“Kumetokea nini?”



“Unajua nilikwenda kumtupa kinondoni karibu na eneo la shule. Nikadhani hapakuwa na mtu”



Vicky alianza kutikisa kichwa.



“Enhe. Nini kilitokea?”



“Wakati nataka kuuweka chini ule mwili, mlinzi wa ile shule aliniona akaja haraka na kunimulika tochi.



Mke wa Waziri Mkuu akapiga mluzi.



“Alikuona?”



“Sijui lakini nadhani hakunitambua. Nikautupa ule mwili chini na kukimbilia kwenye gari ili asinitambue. Alikuwa ameshika sime…”



“Enhe..?’



“Sasa sijui huko nyuma nini kilitokea. Mimi niliondoka na gari haraka”



“Lakini nadhani hakukutambua”



“Ndiyo imani yangu”



“Habari zaidi tutazipata hapo asubuhi”



*******************



Land Rover ya polisi wa kituo cha Kinondoni ilisimama pembeni mwa barabara karibu na uwanja wa shule ya msingi.



Polisi aliyekuwa amesimama na mlinzi alilifuata gari hilo kwa hatua za hima.



Polisi wemzake walipomuona walishuka kwenye gari. Walikuwa polisi wanne akiwemo Inspekta Alex.



Alimpigia saluti Inspekta Alex kisha akamwambia.



“Tukio limetokea sehemu ile”



Alimuonesha kwa kidole mahali hapo.



Dereva wa gari hilo alilielekeza gari mahali walipooneshwa na kumulika taa. Mwili wa msichana ulionekana waziwazi pamoja na mlinzi wa shule aliyekuwa amesimama kando yake.



Walikwenda mahali hapo na kuukagua mwili huo.



“Hebu tueleze nini kilitokea?” Inspekta Alex akamuuliza mlinzi wa shule.



“Nilikuwa nimekaa mbele ya jengo la shule nikiendelea na shughuli zangu za ulinzi, nikaona gari linasimama hapa…” Mlinzi alieleza huku akionesha mahali liliposimama gari hilo.



“Lilikuwa gari la aina gani”



“Ni hizi Toyota Land Cruiser”



“La rangi gani?”



“Nyeupe”



“Namba zake za usajili uliziona?”



“Namba sikuwahi kuziona”



“Enhe. Gari hilo liliposimama hapa nini kilitokea?”



“Niliona mtu mmoja akishuka akafungua mlango wa nyuma na kumtoa huyu mtu. Alikuwa amemmbeba kwenye mikono yake. Hapo nikashituka na kumfuata haraka. Aliponiona akanirushia huyu mtu, akaanguka kando yangu. Yeye mwenyewe akaimbilia kwenye gari na kulipiga moto”



Mlinzi alisita kidogo akavuta pumzi kisha akaendelea.



“Ilikuwa kidogo anikanyage kwa sababu nilikuwa namfuata ili anieleze ni kwanini amemtupa huyu mtu hapa”



“Nadhani atakuwa ameshakufa. Vaeni gloves zenu mumpakie kwenye gari” Inpekta Alex aliwambia polisi wenzake.



Polisi hao walitoa mipira ya kuvaa mikononi kutoka mifukoni mwao na kuivaa mikononi kisha wakaubeba mwili wa Pili na kwenda kuupakia kwenye gari.



“Na wewe utakuja asubuhi kituoni uandikishe maelezo yako. Wewe ndiye shahidi pekee uliyeona tukio hili” Inpekta Alex alimwabia mlinzi.



“Sawa. Nitafika kituoni asubuhi”



Alex alitoa notibuku yake mfukoni na kalamu.



“Unaitwa nani?” alimuuliza mlinzi.



“Naitwa Mrisho Rajab”



“Shule unayolinda inaitwaje?”



“Ni shule ya msingi ya Kinondoni”



“Okey”



Alex aliirudisha notibuku yake mfukoni.



“Tuonane hapo kesho” alimwambia mlinzi huyo.



“Sawa afande”



Inspekta Alex alilifuata gari la polisi lilipokuwa limesimama akajipakia na gari hilo likaondoka. Kwanza walikwenda kituo cha polisi cha Kinondoni.



Mwili wa Pili ulipekuliwa, ulikutwa na simu moja ya bei mbaya na saa ya mkononi iliyokuwa imevunjika kioo.



Vitu hivyo vilihifadhiwa mikononi mwa polisi kisha mwili huo ukapelekwa hospitali ya Muhimbili.



Daktari aliyeupokea mwili huo baada ya kuuchunguza kwa dakika chache alimwambia Inspekta Alex.



“Huyu ameshakufa”



“Labda utueleze alikufaje, aliuawa? Na kama aliuawa aliuawa kwa kitu gani? Na pia utueleze kama aliwahi kubakwa”



“Tutatoa majibu kesho baada ya uchunguzi kamili”



“Kwa hiyo tuje kesho kufuatia majibu”



“Ndiyo mje kesho majira ya saa nne, tutakuwa tumekamilisha uchunguzi wetu”



“Sawa dokta, kwaheri”



Alex na polisi wenzake wakaondoka.



Walirudi kituoni. Alex akaingia ofisini kwake na kuanza kuipekua simu ya Pili.



Ilikuwa imeseviwa majina ya watu wengi. Majina mengine yaliwekwa kwa herufi moja au mbili. Alex akazingatia jina moja lililokuwa na herufi mbili za ML. Jina hilo lilionekana katika meseji nyingi za mapenzi zilizokuwa ndani ya simu hiyo.



Alex akahisi kwamba aliyewakilishwa kwa herufi hizo ndiye aliyekuwa mpenzi wa marehemu na kwamba kama atapatikana ataweza kuwaeleza, msichana aliyeuwa alikuwa nani, alikuwa anaishi wapi na pia kuisaidia polisi katika uchunguzi.



Alex akampigia simu kwa kutumia simu ileile.



Simu ikaita kwa muda mrefu kisha ikapokelewa. Sauti nzito ya mtu aliyetoka usingizini ikauliza.



“Unanipigia saa hizi, ulikuwa wapi?”



Kauli ile peke yake ilitosha kumpa imani Alex kuwa mtu huyo aliyempigia hakuwa akifahamu chochote kuhusiana na tukio lililomtokea marehemu.



“Kuna tatizo limetokea hapa” Alex akamwambia.



“Na wewe ni nani?”



“Mimi ni afisa wa polisi, niko kituo cha Kinondoni. Kuna tatizo limemtokea huyu msichana. Tunakuomba ufike mara moja”



“Mh! Tatizo gani tena?”



“Huyu msichana ameshambuliwa na watu wasiofahamika. Tumekuta namba yako kwenye simu yake, tunajua mnafahamiana”



“Ndiyo tunafahamiana”



“Sasa hebu njoo mara moja hapa kituoni”



“Umeniambia ameshambuliwa, ameshambuliwa na nani?”



“Nimekwambia kwamba ameshambuliwa na watu wasiojulikana”



“Hebu mpe simu nizungumze naye”



“Hawezi kuzungumza, ndio sababu nimekupigia mimi”



“Loh! Aisee umenishitua sana. Subiri nakuja”



“Tunakusubiri.”



Alex akakata simu.



Baada ya nusu saa tu teksi ilisimama nje ya kituo cha polisi. Kijana mmoja mtanashati aliyekuwa amevaa vizuri alishuka kwenye teksi na kuingia katika kituo hicho cha polisi.



Alijitambulisha kaunta akapelekwa katika ofisi aliyokuwemo Inspekta Alex.



Alex akamtazama kabla ya kumwambia.



“Kaa kwenye kiti?”





Itaendelea kesho
 
Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi @Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad @Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya Lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO @multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij @addenbwii ONTARIO Kobe The Vein mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya SITAKI ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo @shedede kamtu33 SteveMollel Ngushi DONALD stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 Ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny @Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj Gide MK Mmanyema mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer Heavy Metal KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche kikale DullahTza Goodluck Mshana julius Darcy Denis Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed Shaban middle east SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa gambada ynwa ney kush mossad 03 white wizard xtaper Mzigua90 Ollachuga Oc Gidbang Mateja M.G Yango jipu abaa4all DIBAJI Agenda1 Grahnman The MaskmaN Slim5 Xubzero agprogrammer JoJiPoJi @Architectus blance86 Mamtolo monde arabe Ngao Ya Imani stardust JK naiman64 Dharra seledunga ABB SHAMMA Richard Waziri wa Kaskazini Mwinjuma1 Kanungila Karim baracuda Mwamba028 besaro Pyepyepye Bilionea Asigwa ibn Kiti Chema Tugas Royal Warrior mederii mmangO manzi james LIKUD adrenaline Royal Son Mhadzabe salaniatz Natasha Ismail jiwe jeusi chibalangunamchezo
John Mloy conjuget Van Pauser great G Mtoto wa nzi Zeus1 hindustan Sci-Fi MAN OF PEACE kashata emnly danny baraka bb MTOTELA kbosho TEMLO DA VINCA
 
Hahaha unapokopy na kupaste rekebisha space, huu uandishi gani sasa?
 
SEHEMU YA 06

ILIPOISHIA



Kijana huyo aliyeonekana kuwa na wasiwasi alikaa kwenye kiti taratibu kama vile aliogopa kukiumiza.



“Unaitwa nani?”



“Naitwa Ramadhani Stambuli”



“Unaishi wapi?”



“Ninaishi Mbezi, hivi unavyoniona ninatoka Mbezi. Nilikodi teksi”



“Msichana mwenye namba niliyokupigia ni nani wako?”



“Ni rafiki yangu au niseme ni mpenzi wangu kwa muda mrefu”



“Sawa. Anaitwa nani?”



“Anaitwa Pili”



“Pili nani?”



“Pili Amrani”



“Anaishi wapi?”



“Anaishi hapa hapa Kinondoni”



SASA ENDELEA



“Mliwahi kukutana kwa siku ya leo?”



“Tulikutana jana usiku. Leo hatukuwahi kukutana”



“Kwanini msikutane, si umesema ni mpenzi wako?”



“Tuwapenzi, sawa lakini kila mmoja anaishi sehemu yake. Yeye anaishi Kinondoni, mimi ninaishi Mbezi. Mara nyingi tunakutana usiku kwa sababu mchana tunakuwa makazini. Na kwa usiku wa leo hatukukutana. Sikujua alikuwa amekwenda wapi na hakujibu sms zangu”



“Yeye anafanya kazi wapi?”



“Ni mpishi wa Waziri Mkuu”



Inspekta Alex akagutuka.



“Ala kumbe yule msichana ni mpishi wa Waziri Mkuu!”



“Ndiyo”



“Alitoka kazini muda gani?”



“Sijui kwa leo alitoka muda gani”



“Kwani kwa kawaida anatoka kazini saa ngapi?”



“Hana muda maalum. Wakati mwingine anatoka mapema, wakati mwingine anachelewa hadi saa tatu usiku”



“Sasa nikwambie kitu…”



“Ndiyo”



“Kama masaa mawili hivi yaliyopita tuliarifiwa kuwa kuna msichana ametupwa katika eneo la shule ya msingi ya Kinondoni…” Alex alimueleza mkasa mzima uliotokea.



Kijana huyo alishituka na kutikisa kichwa. Kwa sekunde kadhaa akawa ameduwaa akimtazama Inspekta Alex mdomo wake ukiwa wazi.



“Sikutaka kukueleza ukweli huo kwenye simu, nilitaka ufike hapa ndio nikueleze” Alex alimwambia.



“Pili ameuawa?” Kijana huyo akauliza kama aliyekuwa akiiuliza nafsi yake mwenyewe.



“Ndiyo ameuawa”



“Moyo wangu hautaki kukubali mpaka nisadikishe kwa macho yangu. Naomba kama inawezekana nikamuone mwenyewe huko hospitali” Kijana huyo akasema kwa unyonge.



“Utakwenda kumuona asubuhi. Unadhani ni kina nani waliofanya kitendo hiki?”



“Kwa kweli siwezi kujua, sikuwa naye wakati huo” Kijana huyo alijibu kwa kusikitika.



“Unaweza kukisia au kutueleza watu unaowashuku”



Kijana huyo akatikisa kichwa.



“Kwa kweli sina mtu yeyote ninayemfikiria kuwa anaweza kufanya kitendo hicho”



“Sawa. Sasa kuna kitu kingine ambacho wewe ndio utatusaidia, kuipata familia yake”



“Mimi nitawaonesha nyumbani kwao”



“Basi tunakutaka ufike hapa kituoni kesho asubuhi ili utupe ushirikiano wako”



“Sawa. Nitafika hapo kesho asubuhi”



Siku iliyofuata Ramadhani Stambuli aliwasili kituoni hapo saa moja na nusu asubuhi. Macho yake yalikuwa mekundu yaliyovimba, hali iliyoonesha kuwa hakuwa amelala usiku uliopita.



Alipoondoka kituo cha polisi usiku alirudi nyumbani kwake ambako alikesha akiwaza huku akiomboleza hadi kunakucha.



Licha ya kufika mapema kituoni hapo alikutana na Inspekta Alex saa mbili na nusu asubuhi. Alikuwa amesubiri kwa saa nzima hadi inpekta huyo alipotokea.



Walipokutana, Stambuli aliambiwa asuburi. Alisubiri hadi saa tatu ambapo Inspekta Alex alimpakia kwenye gari.



“Sasa tunakwenda hospitali ya Muhimbili”



“Sawa”



Wakati gari likiwa katika mwendo Alex alimuuliza Stambuli.



“Mpaka sasa hujaweza kuwafikiria watu ambao wanaweza kuwa wamemuua Pili?”



“Sidhani kama watakuwa watu ninaowafahamu. Nadhani watakuwa ni wahuni tu”



“Ndio sababu polisi tunahimiza sana juu ya ulinzi shirikishi jamii katika maeneo yetu. Ulinzi huu unasaidia sana kuzuia uhalifu mdogo mdogo na hata uhalifu mkubwa”



Stambuli akanyamaza kimya. Mawazo yake yalikuwa mbali sana.



“Unajua ni kwanini ninasema hivyo, ni kwa sababu uhalifu kama huu wa mauaji utazuilika kwa vile maeneo yetu yatakuwa na ulinzi wa wana jamii wenyewe. Na kama kwa bahati mbaya tukio kama hili linatokea basi ni rahisi wahalifu hao kujulikana au kukamatwa” Alex aliendelea kumueleza Stambuli.



“Ni kweli” Stambuli alimkubalia bila kuzingatia alichoambiwa.



Alex alipoona mwenzake alikuwa amefadhaika akanyamaza hadi alipolisimamisha gari kwenye maegesho ya hospitali ya Muhimbili.



Walishuka wakaingia ndani ya majengo ya hospitali hiyo. Dakika chache baadaye Mganga Mkuu alimpa Alex taarifa ya uchunguzi wa mwili wa maremu Pili iliyokuwa imetiwa kwenye bahasha.



Alex hakuisoma hapo hapo, aliomba kuuona mwili wa marehemu. Yeye na Stambuli wakapelekwa mochwari.



Walioneshwa mwili wa Pili ambao mara tu baada ya Stambuli kuuona aliangua kilio hapo hapo.



“Nyamaza bwana, wewe mwanaume!” Alex alimwambia akimpiga piga mabegani.



Stambuli aliendelea kulia.



“Jikaze rafiki yangu”



Walitoka hapo hospitali huku Stambuli akiendelea kulia. Lakini alinyamaza baadaye walipoingia kwenye gari.



“Najua inatia uchungu sana kwa sababu marehemu alikuwa mpenzi wako lakini jikaze kiume uweze kutusaidia” Alex alimwambia wakati akiliondoa gari.



Stambuli alijifuta machozi yake kwa kitambaa kabla ya kushukuru.



“Uhalifu umekuwa ni mwingi sana siku hizi katika jiji hili. Tunazidiwa kwa sababu polisi ni wachache”



Baada ya hapo hawakuzungumza chochote hadi walipofika kituoni.



Wakiwa ofisini mwa Alex ndipo inspekta huyo alipoisoma taarifa ya uchunguzi wa mauaji hayo.



Taarifa hiyo ilieleza kuwa uchunguzi wa madaktari katika mwili wa marehemu umebaini chembe chembe za mate ya binaadamu katika eneo la shingo mahali ambapo unapita mshipa wa damu. Kuna kijaraha cha kung’atwa na meno katika mshipa huo ambapo damu ilifyonzwa mwilini kupitia mshipa huo na kusababisha kifo cha marehemu.



Taarifa hiyo ilikuwa ndefu iliyoandikwa kitaalamu. Alex alipomaliza kuisoma aliiweka karatasi hiyo kwenye meza. Akamtazama Stambuli.



“Taarifa ya uchunguzi wa madaktari inaeleza kuwa marehemu aling’atwa katika mshpa wa shingo na kufyonzwa damu jambo ambalo limesababisha kifo chake” Alex akamwambia Stambuli.



“Alifyonzwa damu na binaadamu au mnyama?” Stambuli akamuuliza.



“Madaktari wamegundua chembe chembe za mate ya binaadamu, itakuwa aling’atwa na kufyonzwa damu na binaadamu”



“Ah! Binaadamu anamfyonza damu binaadamu mwenzake?”



“Ndio uchunguzi ulivyoonesha”



“Hakuuawa?’



“Ameuawa lakini ameuawa kwa njia hiyo”



Stambuli akatikisa kichwa kisha akawa kama anajiuliza peke yake.



“Sasa ni nani aliyefanya unyama huu?”



Alex akamjibu.



itaendelea
 
SEHEMU YA 07

ILIPOISHIA



“Ni kazi yetu sisi polisi kuchunguza na kujua ni nani aliyefanya unyama huo. Kwa vile tumeshapata taarifa hii tutaifanyia kazi”



“Mtaweza kuwakamata hao watu?”



“Kama tutafanikiwa kuwagundua tutawakamata tu”



“Ninawaomba mjitahidi kufanya hivyo ili watu hao wafikishwe mahakamani wapate adhabu inayostahili kwa kosa lao”



“Nimekuelewa. Sasa ninakuomba unifikishe kwa ndugu na jamaa wa marehemu”



***************



Kwa upande wa Waziri Mkuu, saa tatu kamili asubuhi Waziri Mkuu alikuwa ofisini kwake. Kabla ya kuondoka nyumbani kwake alimwambia mke wake ikifika saa nne aijaribu namba ya marehemu Pili aone kama inaita. Kama inaita na kama itapokelewa aulize ni kwanini Pili hajafika kazini hadi muda huu.



Wakati Waziri Mkuu yuko ofisini kwake, mke wake akampigia simu kwa kutumia namba za simu za mikononi.



“Kuna taarifa yoyote uliyoipata huko?’ akamuuliza.



“Sijapata taarifa yoyote, je wewe umesikia lolote?”



“Sijasikia kitu ndio maana nimekuuliza wewe”



“Mimi pia sijapata taarifa yoyote”



“Umefanya vile nilivyokwambia?”



“Ndiyo nataka nipige ile namba”



“Piga sasa hivi”



“Sawa”



SASA ENDELEA



Vicky akakata simu na kuipiga namba ya Pili. Simu ya Pili ikawa inaita. Vicky alishituka. Wakati ule Inspekta Alex ndio alikuwa anataka kutoka ofisini na Stambuli.



Simu ya Pili ilikuwa mezani kwa Inspekta Alex. Alex alipoona simu hiyo inaita akaishika na kutazama namba iliyokuwa inapiga.



Namba ilikuwa imehifadhiwa kwa jina la “Mama Lazaro”. Wakati anaipokea Alex hakutambua kuwa jina hilo lilimaanisha mke wa Waziri Mkuu Dastan Lazaro.



“Halloh!” Akasema baada ya kuipokea simu hiyo.



Mke wa Waziri Mkuu aliposikia sauti ya kiume akauliza.



“Wewe nani?”



“Ungejitambulisha wewe kwanza”



“Mimi ni mke wa Waziri Mkuu, hii namba ni ya mpishi wa nyumbani ambaye hajafika kazini hadi sasa”



Inspekta Alex akagwaya.



“Samahani mama Lazaro, sikukufahamu. Kuna tatizo limetokea?”



“Tatizo gani?”



“Hapa unaongea na Inpekta Alex wa kituo cha polisi cha Kinondoni….” Alex akamueleza tukio zima lililokuwa limetokea.



Mke wa Waziri Mkuu akajifanya anashituka.



“Pili ameuawa? Ameuawa wakati gani?”



“Ndio tunaendelea na uchunguzi ili tujue aliuawa na kina nani na aliuawa wakati gani?”



“Madaktari wameshaufanyia uchunguzi mwili wa marehemu?”



“Wameufanyia uchunguzi na wameshatupa taarifa ya uchunguzi wao”



“Wamegundua marehemu ameuawa kwa kitu gani?”



“Taarifa yao inatatiza kidogo. Wanasema alifyonzwa damu kupitia mshipa wake wa shingo”



Mke wa Waziri Mkuu aligutuka akaikumbuka ile damu waliyoikuta midomoni mwa mwanawe.



“Yaani kufyonzwa damu ndio kumesababisha kifo chake?”



“Ndiyo uchunguzi wa madaktari ulivyoonesha”



“Sasa hiyo damu alifyonzwa na mnyama au binaadamu?”



“Taarifa imesema alifyonzwa na binaadamu”



“Wana uhakika gani?”



“Wamegundua chembechembe za mate ya binaadamu kwenye shingo yake”



“Sasa nyinyi polisi mtafanya nini?”



“Ndio tunawatafuta waliohusika na tukio hilo”



“Kweli mtaweza kumgundua mtu aliyefanya hivyo”



“Anaweza kugundulika”



“Kwa namna gani?’



“Mtu ambaye tutamshuku tutampeleka hospitali ili mate yake yafanyiwe uchunguzi, kama zitapatikana chembechembe za mate aliyokutwa nayo marehemu, atakuwa ndiye huyo huyo”



Mke wa Waziri Mkuu akashusha pumzi.



“Sasa ngoja nimfahamishe mheshimiwa kwa sababu hadi sasa hana taarifa yoyote”



“Sawa mama Lazaro”



Mke wa Waziri Mkuu akakata simu.



Alipokata akampigia mheshimiwa wake Dastan Lazaro.



Akamueleza kila kitu alichoelezwa na Inspekta Alex. Kilichomshitua mheshimiwa Waziri Mkuu ni maneno ya mke wake alipomwambia ameelezwa kuwa muuaji anaweza kugunduliwa kutokana na chembechembe za mate yake endapo yatafanyiwa uchunguzi.



Waziri Mkuu akajiambia kama polisi watataka kuja kufanya uchunguzi nyumbani kwake na kumtilia shaka mwanawe Sofia, itakuwa kazi ndogo kugundua kuwa ndiye yeye aliyemfyonza damu marehemu. Ni kiasi cha kumpeleka hospitali ya Muhimbili tu!



“Nitakuja nyumbani mchana tuongee vizuri” Waziri Mkuu akamwambia mke wake kwa sauti iliyofadhaika.



Alipoiweka simu juu ya meza aliinamisha kichwa chake na kuanza kujiwazia. Alikuwa na muda mfupi tu toka ashike wadhifa huo wa Waziri Mkuu.



Chama cha Rais Isaac Mosha kilipotwaa madaraka mwaka mmoja uliopita kufuatia uchaguzi wa vyama vingi, Rais Mosha alimteua yeye kushika wadhifa huo wa Waziri Mkuu. Alikuwa mmoja kati ya wabunge watatu wa chama chake waliofikiriwa kuwa wangeweza kutwaa wadhifa huo.



Alijiambia endapo itajulikana kuwa ni mwanawe aliyemuua mpishi wao, tukio hilo linaweza kuwa kashfa kubwa kwa upande wake na atalazimika kuwajibika.



Atapoteza kazi, atapoteza heshima na atapoteza madaraka yake ambayo mwenyewe alijua hakuyapata kirahisi kama watu wengi walivyokuwa wakidhani.



Hivyo alikuwa na kila sababu ya kufadhaika na kupata hofu.



**********



Mara baada ya kuzungumza na mke wa Waziri Mkuu, Inspekta Alex alitoa taarifa ya kuzungumza na mama Lazaro kwa mkuu wake kisha akamtaka Stambuli ampeleke kwa wazazi wa marehemu Pili.



Stambuli ambaye katika muda wote alikuwa akihuzunika kutokana na kuuawa mpenzi wake, alimpeleka mpelelezi huyo katika mtaa mmoja walikokuwa wakiishi wazazi wa marehemu Pili.



Alex alikutana na baba yake Pili, mzee Amrani na mama Amrani na kuwauliza kama wana binti anayeitwa Pili Amrani ambaye ni mpishi wa Wairi Mkuu.



Wazee hao walikubali kuwa wana binti huyo.



“Je mna taarifa zake zozote?”



“Taarifa kama zipi?” mzee Amrani alimuuliza akiwa ameshituka.



“Inaonekana kama hamna taarifa ya tukio lililotokea”



“Labda hatuna, hebu tufahamishe”



“Nasikitika kuwambia kuwa binti yenu ameuawa”



Inspekta Alex alishuhudia uso wa mzee Amrani na wa mke wake ukitepeta.



“Unasemaje. Binti yetu ameuawa?” mzee Amrani akamuuliza Alex kwa taharuki.



Alex akawaeleza mkasa mzima uliotokea.



“Upelelezi bado unaendelea na mwili wa marehemu upo hospitali ya Muhimbili”



Tayari machozi yalikuwa yakimtoka mama Amrani.



“Ni nani aliyemfanyia mwanangu unyama huo jamani?” alihoji kwa uchungu.



“Kama nilivyowambia tupo kwenye uchunguzi, ni imani yetu kuwa mtu huyo au watu hao watapatikana” Alex aliwambia.



*************



Alex alirudi kituoni akiwa ameshamuacha Stambuli. Aliporudi tu alikutana na mlinzi wa shule ya msingi ya Kinondoni akimsubiri.



“Nilikuwa nimetoka kidogo” alimwambia baada ya kushuka kwenye gari.



“Niliambiwa kuwa umetoka nikaona nikusubiri” Mlinzi huyo aliyefika akiwa na mavazi yake ya kiulinzi alisema.



“Sawa. Tuingie ofisini”



Waliingia ofisini mwa Inspekta Alex.



“Kaa kwenye kiti”



Mlinzi huyo alikaa kuielekea meza iliyokuwemo ofisini humo.



Baada ya Alex kuketi alifungua faili lililokuwa juu ya meza yake kisha akamtazama mlinzi huyo.



“Madaktari wametuambia yule msichana alifyonzwa damu pale shingoni kisha maiti yake ikaja kutupwa kule shuleni” akamueleza.



“Alifyonzwa damu?” Mlinzi alishituka.



“Ndio uchunguzi wa madaktari umeonesha kuwa alifyonzwa damu”



“Alifyonzwa damu kwa wapi?”



Itaendelea
 
SEHEMU YA 08

ILIPOISHIA



“Aling’atwa kwenye mshipa wa shingo na alifyonzwa damu kupitia mshipa huo”



“Sasa alifyonzwa na nani?”



“Haijajulikana bado, ndio tuko kwenye uchunguzi”



“Katika akili yangu mimi nadhani aliuawa na binaadamu, ndio akaja kumtupa pale”



“Huyo aliyemfyonza na kumuua ni binaadamu si mnyama”



“Binaadamu anaweza kumfyonza damu mwenzake hadi kumuua?’



“Ndio uchunguzi ulivyoonesha. Ni uchunguzi wa kitaalamu, hatuwezi kuupinga”



“Ni nani huyo anayefyonza watu damu?”



“Ndio tunamtafuta sasa. Unaweza kutusaidia nini?”



Mlinzi akaguna.



“Ndio kwanza ninasikia mauaji ya aina hiyo. Sijui kama kuna watu wanafyonza damu wenzao!”



SASA ENDELEA



“Inawezekana ni kwa sababu za kishirikina. Hujawahi kusikia watu wanachuna ngozi za walemavu wa ngozi au kuwakata mikono na wakati mwingine kuwaua kabisa?”



“Nimeshawasikia”



“Sasa hao ndio mfano wa hao wafyonza damu. Kila siku kunaibuka vitendo vipya vya uhalifu. Mimi sishangai kusikia habari kama hii. Kuna watu ni wapumbavu sana. Mtu anamuua ndugu yake kwa sababu ni albino ili apate utajiri”



“Kwa hiyo sasa hivi ndio kumeibuka huu mtindo wa kufyonza damu ya binaadamu kama mashetani!”



“Tunahitaji maelezo yako. Hebu nieleze nini kilitokea jana usiku ulipokuwa kaika lindo lako lakini kwanza nitajie tena jina lako na umri wako”



“Naitwa Mrisho Rajab, umri wangu ni miaka arobaini na miwili”



“Unaishi wapi?”



Niko Mwananyamala B”



“Kazi yako ni mlinzi sio?”



“Ndio, kazi yangu ni ya ulinzi”



“Ile shule unayolinda inaitwaje?”



“Ile ni shule ya msingi ya Kinondoni”



Inspekta Alex aliandika. Alipomaliza akamtazama tena Mrisho Rajab.



“Sasa nieleze nini kilitokea jana usiku?”



“Kilichotokea nadhni unakifahamu”



“Hilo sio jibu. Nataka niandike maelezo yako kwa sababu wewe ndiye shahidi pekee uliyeshuhudia tukio hilo. Ilikuwa ni muda gani ulipoona hilo gari?”



“Ilikuwa ni mjira ya saa nane au saa nane na nusu usiku”



“Enhe…nini kilitokea?”



“Lilitokea hilo gari kunako kiwanja cha shule. Mimi nilikuwa nimekaa nje ya darasa moja”



“Lilikuwa gari la aina gani?”



“Ni Toyota Land Cruisser la rangi nyeupe”



“Gari hilo lilipotokea lilifanya nini?”



“Lilisimama karibu na miti ya magoli ya upande mmoja wa kiwanja hicho. Lilisimama kwa karibu dakika tano bila mtu yeyote kufungua mlango. Wakati nainuka ili niende nikamuulize aliyesimamisha gari lile pale, nikaona mlango unafunguliwa”



“Mlango uliofunguliwa ulikuwa wa mbele au nyuma?”



“Ulikuwa mlango wa dereva”



“Sawa, endelea”



“Akashuka mtu mmoja. Alikuwa amevaa pama, akafu….”



“Subiri. Mbali ya pama, alikuwa amevaa nini au nguo za rangi gani?”



“Alikuwa amevaa shati na suruali, sikuweza kuona vizuri zilikuwa za rangi gani”



“Alikuwa mtu mrefu, mfupi, mwembamba au mnene…?”



“Alikuwa mrefu kiasi lakini hakuwa mnene wala hakuwa mwembamba sana”



“Mtu huyo alifanya nini baada ya kushuka kwenye gari?”



“Alifungua mlango wa gari wa nyuma wa upande ule ule alioshuka yeye akautoa ule mwili wa msichana lakini muda ule niliona kama gunia hivi”



“Akaufanya nini?”



“Ndio pale nikawa ninamfuata, aliponioana alinirushia ule mwili ukaanguka chini miguuni mwangu. Wakati nutazama vizuri, yule mtu aliwahi kupanda kwenye gari lake. Hata hivyo nilimfuata akataka kunigonga na gari”



“Alitaka kukugonga kivipi?”



“Nilitinga mbele ya gari lake”



“Uliweza kuona ndani ya gari hilo kama kulikuwa na watu wengine?”



“Sikuweza kuona. Gari hilo liliondoka kwa haraka”



“Baada ya hapo ulifanya nini?”



“Nilipiga simu polisi”



“Ulipotupiwa huo mwili wa msichana miguuni mwako alikuwa bado yuko hai au alikuwa ameshakufa?”



“Alikuwa ameshakufa”



“Je kama utamuona tena yule mtu unaweza kumtambua?”



“Naweza kumtambua kwa sababu nilimmulika tochi usoni na nilimuona vizuri”



“Jana usiku nilipokuuliza uliniamabia kuwa namba za usajili za gari hilo hukuziona?”



“Sikuwahi kuziona”



“Sawa. Soma maelezo yako halafu weka sahihi”



Alex alimpa mlinzi huyo ile karatasi aliyokuwa anaiandika ili aisome.



Mlinzi aliichukua na kuisoma. Alipomaliza kuisoma Alex alimuuliza.



“Maelezo yako ni sahihi?”



“Ni sahihi”



“Sasa weka sahihi yako hapo chini”



Mlinzi aliweka sahihi yake chini ya maelezo yake.



“Tuachie namba yako ya simu”



Mlinzi huyo alitaja namba yake ya simu. Alex akaiandika chini ya maelezo yake.



“Kuna kingine?” Mlinzi huyo akauliza akionesha haraka ya kutaka kuondoka. Hakuna anayependa kukaa kituo cha polisi kwa muda mrefu.



“Unaweza kwenda, tutakapokuhitaji tutakujulisha kupitia simu yako”



“Sawa, asante sana”



Mlinzi akanyanyuka na kutoka.



Hakuna anayefurahia kuhojiwa kituo cha polisi hata kama ni kwa ajili ya kutoa ushahidi. Mlinzi huyo alipoondoka kituoni hapo shati lake lilikuwa limeloa kwa jasho. Dakika zile za kuhojiwa maswali zilikuwa kama dakika za jinamizi. Aliporuhusiwa kuondoka alijisikia amepata ahueni kubwa.



Dakika ile ile Waziri Mkuu alimpigia simu Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri huyo alipopokea simu ya bosi wake alisema.



“Hello mheshimiwa…habari ya asubuhi?”



“Habari ya subuhi si nzuri, nimepata taarifa sasa hivi kuwa mpishi wangu ameuawa”



Waziri wa Mambo ya ndani akashituka.



“Ameuawa wapi?”



“Sijapata taarifa kamili. Mke wangu alimpigia simu alipoona hatokei, ile simu ikapokelewa kituo cha polisi ambako alielezwa kuwa msichana huyo ameuawa”



“Polisi wameeleza ameuawa wapi na aliyemuua ni nani?”



“Wamesema maiti ya msichana huyo iliokotwa jana usiku katika eneo la shule ya Kinondoni ikiwa na jeraha shingoni kwake”



“Sasa acha niwasiliane na kamanda wa polisi anieleze nini kimetokea na nini kinaendelea”



“Sawa, wasiliana naye’



Waziri Mkuu akakata simu.



Waziri wa Mambo ya Ndani Jackson Maro akampigia simu Kamanda wa polisi wa mkoa wa Dar.



Kwa vile kamanda wa polisi alikuwa amemzidi kiumri waziri wa Mambo ya Ndani, alipopokea simu yake Maro alimwamkia.



“Shikamoo”



“Marahaba, habari ya kazi” Kamanda wa polisi alimuitikia.



“Ni nzuri. Umepata taarifa ya mauaji yaliyotokea jana usiku huko Kinondoni?’



ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 9

ILIPOISHIA



Kamanda wa polisi alianza kubabaika. Alibabaika kutokana na ukweli kuwa hakuwa amepata taarifa yoyote wakati alikuwa ndiye kamanda wa polisi wa mkoa huo.



“Sijapata bado” akasema kwa sauti ya wasiwasi.



“Kwanini?”



“Leo wamenicheleweshea taarifa”



“Eh! Mpishi wa Waziri Mkuu ameuawa jana usiku, wewe huna taarifa. Sasa sisi tumuulize nani?”



Kamanda wa polisi alionesha kuhuzunika waziwazi.



“Hawa jamaa wananicheleweshea taarifa na nilikwisha waeleza taaarifa za mauaji waniwasilishie haraka. Sasa acha niwaulize halafu nitakupigia”



“Inaonekana katika ofisi yako mambo hayaendi sawa!”



“Tatizo ni ucheleweshwaji tu wa taarifa. Hilo tatizo nitalirekebisha lisitokee tena”



SASA ENDELEA



Waziri wa Mambo ya Ndani alikuwa ameshakata simu.



Kamanda wa polisi alipogundua simu ilikuwa imeshakatwa alimpigia haraka afisa wa chini yake ambaye ni afisa upelelezi wa mkoa.



“Nini kinaendelea hapo ofisini kwako?” akamuuliza. Sauti yake ilikuwa tulivu lakini ilikuwa ya hasira.



“Afande nimepata taarifa za mauaji sasa hivi kutoka kwa OCD wa Kinondoni” Sauti ya afisa upelelezi ilisikikika kutoka simu ya upande wa pili.



“Ulikuwa unasubiri nikupigie ndio uniarifu?”



“Hapana afande, taarifa yenyewe nimeipata muda huu”



“Ni mauaji ya nani?”



“Nimeelezwa kwamba ni ya msichana mwenye umri wa miaka ishirini na tisa anayeitwa Pili, mkazi wa Kinondoni na ni mpishi wa Waziri mkuu”



“Aliuawa saa ngapi, aliuawa na nani na tukio lilitokea wapi?”



“Nimeelezwa kwamba aliuawa mahali pasipojulikana lakini maiti yake ilikwenda kuachwa katika kiwanja cha shule ya Msingi ya Kinondoni saa nane usiku”



“Ameuawa kwa kitu gani?”



“Taarifa ya uchunguzi wa mwili wa marehemu imeonesha kuwa marehemu alifyonzwa damu kupitia mshipa wake wa shingo na kusababisha kifo chake”



“Mh! Alifyonzwa na nani?”



“Uchunguzi umeonesha kuwa amefyonzwa na binaadamu lakini hajajulikana ni nani, kwa hiyo polisi ndio wanaendelea na uchunguzi”



“Ni nani ambaye aliuoana mwili wa marehemu ulipoachwa hapo kiwanjani?”



“Ni mlinzi wa ile shule”



“Ninahitaji kupata taarifa kamili”



“Ninakuja nayo ofisini kwako afande”



“Niletee sasa hivi”



Baada ya robo saa hivi, afisa upelelezi akaingia ofisini mwa kamanda wa polisi akiwa ameshika jalada.



Aliketi kwenye kiti kisha akampa jalada hilo kamanda wa polisi.



“Taarifa kamili niliyoletewa imo humu, unaweza kuisoma” Afisa upelelezi huyo akamwambia kamanda wa polisi.



Kamanda alipolitwaa jalada hilo alilifungua na kulisoma. Zilimchukua dakika kumi hivi kuyapitia maelezo yote haraka haraka. Akauinua uso wake na kumtazama Afisa upelelezi.



“Hilo gari mtalipataje?”



“Tatizo ni kuwa magari aina ya Toyota Land Cruisser ya rangi nyeupe ni mengi hapa Dar, ni afadhali kama yule mlinzi angeona namba zake za usajili. Tungeweza kulipata kwa urahisi”



“Unadhani ni akina nani watakuwa wamefanya unyama huu?”



“Ni mapema mno kudhani, upelelezi wetu ndio utatoa jibu. Tukio kama hili ndio mara ya kwanza kutokea hapa Dar”



“Sasa ni lazima vijana wako wachunguze kujua huyu msichana jana alitoka kazini saa ngapi na alipotoka kazini alikwenda wapi. Kama alirudi nyumbani kwake, alitoka tena saa ngapi na alikwenda wapi. Vile vile ni muhimu kujua kwa mara ya mwisho alikuwa na nani”



“Sawa afande, nitalishughulikia hilo suala”



Afisa upelelezi akainuka kwenye kiti na kutoka.



Alipotoka tu, kamanda wa polisi akainua simu na kumpigia Waziri wa Mambo ya ndani.



Baada ya kumueleza tukio zima, waziri alimuuliza.



“Ni uchunguzi gani ambao umefanyika hadi sasa?”



“Kitu cha kwanza kilikuwa ni kupata taarifa ya uchunguzi wa mwili wa marehemu. Hatua ya pili ilikuwa ni kuwapata jamaa wa marehemu ambao pia hawakuwa na taarifa yotote.



“Hatua ya tatu itakuwa kutuma vijana kwenda nyumbani kwa mheshimiwa Waziri Mkuu kujua marehemu aliondoka kazini saa ngapi jana na pia kwenda nyumbani kwake kujua kama alirudi nyumbani alipotoka kazini na kama alirudi aliondoka saa ngapi na alikwenda wapi”



“Ninachowaomba ni kwamba chochote ambacho mtagundua mnifahamishe haraka” Waziri akamwambia kamanda huyo wa polisi.



“Tutakufahamisha”



“Sawa”



Waziri alitangulia kukata simu kabla ya kamanda wa polisi.aliyekuwa amempigia.



Haikutimia hata dakika moja Mkuu wa Jeshi la Polisi akampigia kamanda wa polisi kumuulizia kuhusu tukio hilo.



“Ni kweli tukio hilo limetokea, polisi wanaendelea na uchunguzi” Kamanda huyo alimjibu.



“Uchunguzi huo umefikia wapi?”



“Kwa sasa hivi sina maelezo ya kutosha lakini mpaka saa kumi jioni nitakuwa na taarifa kamili’



“Utanijulisha”



“Sawa afande”



Mkuu wa Jeshi la polisi akakata simu na kamanda wa polisi akaurudisha mkono wa simu mahali pake.



Waziri Mkuu alirudi nyumbani kwake saa saba mchana. Alimkuta mke wake akiwa na fadhaa.



“Karibu” Mwanamke huyo alimkaribishaWaziri Mkuu huyo sebuleni. Sauti yake haikuwa na uchangamfu wa kawaida.



Dastan Lazaro aliketi kwenye kochi. Kama kawaida yake aliuweka mguu mmoja juu ya mwingine akamtazama mke wake.



Vicky alipoona mume wake anamtazama akamuuliza.



“Je?”



“Nimekuwa nikijiuliza swali lakini sipati jibu, Sofia amepatwa na tatizo gani?” Waziri Mkuu akamuuliza mke wake.



“Si rahisi kujua. Kama vipimo vya hospitali vinasema ni mzima, sisi tutawezaje kujua kilichompata”



“Mimi kwanza nilidhani ni malaria imempanda kichwani lakini malaria yenyewe haikuonekana”



“Mimi nimeogopa sana yule polisi niliyezungumza naye kwenye simu aliponiambia sababu ya kifo cha Pili ni kufyonzwa damu. Ina maana Sofia alimfyonza damu nyingi”



“Halafu ile nguvu ya kumdhibiti yule mwanamke aliipata wapi. Ukiwatazama Pili na Sofia, Pili ana nguvu zaidi. Alimzidi vipi mpaka akaweza kumfyonza damu na kumuua?”



“Kisha unajua kuwa mpaka muda huu Sofia hajui alichotenda. Ina maana kwamba jana usiku alikuwa amerukwa na akili!”



“Inabidi tuendelee kumfanyia uhunguzi zaidi wa akili yake…”



Waziri Mkuu akakatizwa na mlio wa simu yake ya mkononi iliyokuwa kwenye mfuko wa koti lake. Hakuwa na tabia ya kutoa simu kwa haraka inapoita lakini siku ile aliitoa haraka ili kujua ni nani aliyekuwa akimpigia.



Akaona jina la waziri wa Mambo ya Ndani Jackson Maro.



Akapokea simu.



“Hello Maro…!”



“Mheshimiwa nilitaka kukufahamisha kuwa uchunguzi wa mauaji ya mpishi wa nyumbani kwako Pili Amrani unaendelea. Nimearifiwa kuwa polisi wanataka kuja nyumbni kwako kuchukua maelezo”





ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 10

ILIPOISHIA



“Mimi nimeogopa sana yule polisi niliyezungumza naye kwenye simu aliponiambia sababu ya kifo cha Pili ni kufyonzwa damu. Ina maana Sofia alimfyonza damu nyingi”



“Halafu ile nguvu ya kumdhibiti yule mwanamke aliipata wapi. Ukiwatazama Pili na Sofia, Pili ana nguvu zaidi. Alimzidi vipi mpaka akaweza kumfyonza damu na kumuua?”



“Kisha unajua kuwa mpaka muda huu Sofia hajui alichotenda. Ina maana kwamba jana usiku alikuwa amerukwa na akili!”



“Inabidi tuendelee kumfanyia uchunguzi zaidi wa akili yake…”



Waziri Mkuu akakatizwa na mlio wa simu yake ya mkononi iliyokuwa kwenye mfuko wa koti lake. Hakuwa na tabia ya kutoa simu kwa haraka inapoita lakini siku ile aliitoa haraka ili kujua ni nani aliyekuwa akimpigia.



SASA ENDELEA



Akaona jina la waziri wa Mambo ya Ndani Jackson Maro.



Akapokea simu.



“Hello Maro…!”



“Mheshimiwa nilitaka kukufahamisha kuwa uchunguzi wa mauaji ya mpishi wa nyumbani kwako Pili Amrani unaendelea. Nimearifiwa kuwa polisi wanataka kuja nyumbni kwako kuchukua maelezo”



Waziri Mkuu alishituka.



“Ni maelezo gani wanayoyataka?”



“Ni malezo yanayohusiana na uchunguzi wao”



“Sidhani kama tuna maelezo yanayoweza kuwasaidia kwa sababu Pili aliondoka hapa nyumbani mapema. Alituambia alikuwa anajisikia kuumwa. Sasa kilichoendelea huko alikokwenda hatukijui”



“Sawa. Mtawaeleza hali halisi. Kuna maswali ambayo watawahoji”



“Watakuja saa ngapi?”



“Watakuja muda huu”



Baada ya kusita kidogo Waziri Mkuu alisema.



“Sawa waache waje?”



“Nashukuru mheshimiwa”



Waziri Mkuu akaiweka simu juu ya stuli ndogo ya kioo iliyokuwa mbele yake.



“Ni nani?” Mke wake akamuuliza akiwa amekunja uso.



“Ni Jackson Maro Waziri wa Mambo ya Ndani”



“Anataka nini?”



“Ameniambia kuna askari watakuja hapa kwa ajili ya uchunguzi wa mauaji ya Pili”



“Wanashuku kwamba ameuliwa hapa?”



“Hapana. Wanakuja kutuhoji tu kwa sababu inaonekana Pili aliuawa baada ya kuondoka hapa”



‘Sasa tutawaeleza nini hao polisi?”



“Itabidi tupange jinsi ya kuwaeleza”



Waziri Mkuu akajiweka sawa na kumuelekea mke wake.



“Sasa sikiliza, hawa jamaa wakija tuwe na kauli moja. Kwanza tusiwahusishe wale watoto. Tuwambie hawakuweko. Mimi na wewe ndio tutazungumza. Umenielewa?”



“Ndio”



“Kwa hiyo tutawambia kuwa Pili aliondoka saa kumi na moja jioni baada ya kudai kuwa kichwa kinamuuma, tukamruhusu aende hospitali”



“Labda wanaweza kuuliza aliondoka kwa usafiri gani kama alikuwa anaumwa?’



“Hatujui. Tutawambia kwamba hatujui. Hapa nyumbani aliondoka kwa miguu yake. Sasa huko nje hatujui alitumia usafiri gani”



“Sawa. Tutawambia hivyo. Sidhani kama watakuwa na maswali mengine”



“Wanaweza kuwa nayo lakini tutatumia akili kuyajibu”



Mke wa Waziri Mkuu akabaki kimya.



Ilikuwa ni baada ya saa moja Waziri Mkuu alipofahamishwa na mlinzi wa nyumbani kwake kuwa kulikuwa na makachero watatu waliokuwa wakihitaji kuonana naye.



Waziri Mkuu akatoa ruhusa makachero hao waingie ndani. Sekunde chache baadaye makachero hao wakakakaribishwa sebuleni na Waziri Mkuu mwenyewe.



Hawakupoteza muda. Mrakibu wa polisi kutoka idara ya upelelezi makao ya polisi Thabit Kombo alijitambulisha na kuwatambulisha wenzake Inspekta Alex na mwenzake Inspekta Temba.



“Mheshimiwa kuna hili tukio la mauaji ya Pili Amrani yaliyotokea Kinondoni jana usiku, ndio limetuleta hapa” Thabit Kombo alianza kumwambia Waziri Mkuu.



“Nimeshaarifiwa kuwa mtakuja. Hili tukio kwa kweli limenisikitisha sana” Waziri Mkuu alijidai kusikitika.



“Vile vile ni tukio ambalo limetushangaza polisi. Mara kwa mara mauaji yanatokea lakini si ya aina hii ya kuuawa kwa kufyonzwa damu”



“Inawezekana labda ni mnyama amemfyonza baada ya kuuawa”



“Hapana. Uchunguzi wa madaktari umebainisha kuwa aliuawa kwa kufyonzwa damu na aliyemfyonza ni binaadamu”



Waziri Mkuu akajifanya anatikisa kichwa kusikitika.



“Sijui huu ulimwengu hivi sasa unaelekea wapi!” alisema.



“Sasa mheshimiwa tumekuja kukusumbua kidogo. Tunahitaji maelezo kutoka hapa nyumbani kwako ambako yule msichana alikuwa anafanya kazi”



“Maelezo ya aina gani?”



“Kwanza tungependa kujua huyu marehemu jana aliondoka hapa saa ngapi?”



Waziri Mkuu akajifanya anafikiria.



“Kwa kweli jana aliondoka majira ya saa kumi na moja jioni”



Kombo alikuwa amefungua jalada alilokuwa ameliweka mapajani. Akaanza kuandika maelezo ya Waziri Mkuu.



“Alikuwa amewahi au ndio muda wake wa kawaida?”



“Yeye alikuwa ni mpishi wetu. Sasa kazi ya upishi si kama kazi ya ofisini, ikifika saa kumi unaondoka. Yeye kuondoka kwake ni mpaka amalize kazi. Wakati mwingine anaondoka usiku, wakati mwingine anawahi kuondoka”



“Anapotoka kazini anatumia usafiri gani kurudi nyumbani?’



“Usafiri unakuwa ni juu yake mwenyewe isipokuwa kuna siku tunamrudisha nyumbani kama ni usiku na kuna siku tunamfuata nyumbani kwake na gari”



“Kwa hiyo anapoondoka anatumia usafiri wake?’



“Hapa nyumbani anaondoka kwa miguu, sasa huko nje anajua yeye mwenyewe atapanda nini. Siku hizi kuna usafiri mwingi, kuna bodaboda, kuna teksi, kuna daladala”



“Mheshimiwa imeelezwa kuwa mwili wa marehemu ulitupwa katika eneo la shule usiku wa jana kutoka katika gari aina ya Toyota Land Cruisser ya rangi nyeupe…”



Waziri Mkuu alishituka.



Akanyamaza kimya kumsikiliza kachero huyo ili ajue angesema nini.



“Katika upelelezi wetu pia tunataka kulitambua hili gari ili liweze kukamatwa, je hapa nyumbani kwako kuna gari la aina hiyo?” Thabit Kombo akamuuliza.



Moyo wa Waziri Mkuu ukaanza kwenda mbio.



Kwanza alishukuru kwamba gari hilo halikuwepo pale nyumbani muda ule. Kama lingekuwepo na makachero hao wangeliona wangelitilia mashaka.



Alitumia kama sekunde tatu kujiuliza ajibu nini. Akubali kwamba analo gari hilo au akatae. Akajiambia endapo atakubali anaweza kuingia katika kashifa ya mauaji itakayopelekea sio tu kujiuzulu cheo chake bali pia kukabiliwa na mashitaka ya mauaji.



Akaona ni bora akatae kwamba hana gari hilo. Aliendelea kujiambia kwamba hata kama gari hilo litaonekana barabarani lisingeweza kushukiwa kwa vile jiji hilo lilikuwa na maelfu ya magari ya aina hiyo yenye rangi nyeupe.



Waziri Mkuu baada ya kuwaza alitikisa kichwa.



“Hapa nyumbani hatuna gari hilo” akasema.



Kachero Kombo aliandika kwenye jalada. Alipomaliza kuandika alimwambia Waziri Mkuu.



“Tunakupa pole kutokana na msiba huu. Tutaendelea kulitafuta hili gari na waliohusika katika tukio hili, ili wafikishwe katika vyombo vya sheria”



“Na mimi ninawaomba mjitahidi kuhakikisha kuwa watu hao wanakamatwa”



“Asante sana mheshimiwa. Tutajitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu”



Makachero hao walimuaga Waziri Mkuu na kunyanyuka. Waziri Mkuu aliwasindikiza hadi nje ya nyumba yake. Makachero hao wakajipakia kwenye gari na kuondoka.



Mara tu Waziri Mkuu aliporudi ndani mke wake alimuuliza.



“Umesema huna gari hilo, je kama watalikamata barabarani na dereva akasema ni la kwako, huoni kama umejitia mwenyewe katika hatia”



“Na ni kwanini likamatwe gari langu wakati jiji hili lina maelefu ya magari ya aina ile ya rangi nyeupe?”



“Polisi wanaweza kufanya msako wa kuyakamata”



“Watakamata magari mangapi na watakwenda kuyaweka wapi. Mimi nikisikia kuna msako huo nitawazuia. Nitawambia zoezi hilo litasumbua wananchi”



“Si itaonekana unazuia upelelezi?”



“Hapana. Sasa tujiandae twende huko kwenye msiba tuwape pole na pia tutoe ubani wetu”



“Sawa”



Baada ya kumaliza kula chakula cha mchana Waziri Mkuu na mke wake walikuwa kwenye magari mawili tofauti huku wakiongozwa na gari la polisi lililokuwa na kimulimuli.



Walifika Kinondoni nyumbani kwa wazazi wa Pili ambako tayari watu walikuwa wamejaa na vilio vilikuwa vimetawala.





ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 11

ILIPOISHIA





“Na ni kwanini likamatwe gari langu wakati jiji hili lina maelefu ya magari ya aina ile ya rangi nyeupe?”



“Polisi wanaweza kufanya msako wa kuyakamata”



“Watakamata magari mangapi na watakwenda kuyaweka wapi. Mimi nikisikia kuna msako huo nitawazuia. Nitawambia zoezi hilo litasumbua wananchi”



“Si itaonekana unazuia upelelezi?”



“Hapana. Sasa tujiandae twende huko kwenye msiba tuwape pole na pia tutoe ubani wetu”



“Sawa”



Baada ya kumaliza kula chakula cha mchana Waziri Mkuu na mke wake walikuwa kwenye magari mawili tofauti huku wakiongozwa na gari la polisi lililokuwa na kimulimuli.



Walifika Kinondoni nyumbani kwa wazazi wa Pili ambako tayari watu walikuwa wamejaa na vilio vilikuwa vimetawala.





SASA ENDELEA



Walishuka kwenye gari na kupokelewa na mzee Amrani, baba yake Pili ambaye aliwakaribisha ndani. Wakati Waziri Mkuu alipelekwa upande wa wanaume, mke wake alipelekwa upande wa wanawake.



Baada ya Waziri Mkuu kumpa pole baba wa marehemu na mama wa marehemu pamoja na ndugu wengine, alieleza jinsi alivyoshitushwa na kusikitishwa na mauaji ya mfanyakazi wake huyo.



“Marehemu alikuwa mtumishi mwenye bidii na muaminifu ambaye alikuwa kama sehemu ya familia yangu kutokana na ukaribu wetu. Nasema kwamba tumesikitishwa na kuhuzunishwa kutokana na kifo chake cha ghafla wakati tukiwa bado tunampenda na kumuhitaji. Lakini tuishie tu kusema kwamba bwana ametoa na bwana ametwaa…” Waziri Mkuu alisema akionesha kusikitika.



Baada ya maelezo yake marefu alitoa shilingi milioni moja ambazo alimwambia baba wa marehemu zilikuwa za ubani wake pamoja na mke wake.



“Tunakushukuru sana mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kuungana na sisi katika msiba huu wa binti wetu” Mzee Amrani alimshukuru baada ya kupokea pesa hizo.



Mazishi yatakuwa lini?”



“Tumepanga mazishi yawe kesho saa saba mchana”



“Basi nitafika tumsindikize mwenzetu”



“Tutashukuru sana”



Waziri Mkuu na mke wake hawakukaa sana wakaondoka.



Wakati wanaondoka tu, Thabit Kombo na Inspekt Alex wakawasili kwa gari. Walisimamisha gari mbele ya nyumba ya mzee Amrani kisha wakashuka.



Mzee Amrani alikuwa bado yuko nje akizungumza na watu, Alex akamuona.



“Mtu tunayemtaka yule pale” akamwambia kachero Kombo akimuonesha mzee huyo aliyekuwa amesimama akiwatazama.



“Karibuni” aliwambia huku akimkumbuka Inspekta Alex ambaye ndiye aliyefika kwake mapema na kumpa taarifa ya kifo cha binti yao.



“Tumekuja tena mzee” Alex alimwambia walipomkaribia.



“Ndio. Habari za kazi?”



“Nzuri. Nimekuja na afande wangu kutoka makao ya polisi. Alitaka kukuona na kuzungumza na wewe”



“Nipo tayari kuzungumza naye”



“Tunaweza kwenda nyumba ya pili tukae barazani tuzungumze” Kombo alimwmbia.



“Hakuna shaka, karibuni sana”



Mzee Amrani aliwapeleka nyumba ya pili wakakaa barazani.



“Kwanza nakupa pole sana kutokana na msiba uliotokea’ Kombo alimwambia huku akimpa mkono.



“Asante. Nawashukuru sana vijana wangu”



“Kwa Mungu ndiko tutokeako na ndiko tunakorudi”



“Ni kweli. Kila nafsi itayaonja mauti”



“Sasa mzee wangu nilitaka kukuhoji maswali mawili matatu kuhusiana na marehemu”



“Uliza”



“Mrehemu alikuwa akiishi wapi?”



“Alikuwa akiishi hapa hapa Kinondoni mtaa mwingine. Alikuwa amepanga nyumba”



“Alikuwa anaishi na nani?”



“Katika ile nyumba walipanga watu wawili, yeye na mwanamke mwenzake. Kila mmoja alikuwa na upande wake’



“Nazungumzia kwa yeye, alikuwa anaishi na nani?”



“Alikuwa akiishi peke yake”



“Kwa kadiri unvyofahamu binti yako hakuwa na rafiki wa kiume au wa kike?”



“Marafiki zake siwezi kuwajua isipokuwa binti yangu alikuwa na mchumba’



“Anaitwa nani?”



“Anaitwa Stambuli”



“Mara yako ya mwisho kukutana na binti yako ilikuwa lini?”



“Kila baada ya siku mbili ni lazima aje nyumbani kutujulia hali. Kama sikosei juzi usiku alikuja nyumbani alipotoka kazini kwake”



‘Mara nyingi akitoka kazini anapendelea kutembelea sehemu gani”



Mzee Amrani akatikisa kichwa.



“Kwa kweli siwezi kujua”



“Hilo ndilo swali la msingi lililotuleta hapa kutaka kujua alipotoka kazini jana alikwenda wapi. Tuliambiwa kwamba alikuwa anaumwa na kichwa na aliondoka kazini mapema”



“Jana mpaka saa moja na nusu usiku alikuwa yuko kazini kwake. Nilimtumia meseji kumuuliza kama ametoka kazini, nilikuwa na shida ya kuonana naye, akaniambia bado yuko kazini na hakuniambia kwamba alikuwa anaumwa…”



Kombo alishituka. Waziri Mkuu alimwambia Pili aliondoka kazini saa kumi na moja jioni baada ya kujihisi kuumwa na kichwa.



“Una uhakika na unachokisema mzee wangu?” Kombo akamuuliza Mzee Amrani kwa uso wa mashaka.



“Nina uhakika. Meseji aliyonitumia hii hapa, sijaifuta baado”



Mzee Amrani alitoa simu yake akaingia eneo la meseji na kumuonesha Kombo meseji hiyo aliyotumiwa na mwanawe.



Kombo aliiona.



“Alikutumia meseji hii saa moja na nusu usiku!”



“Ndiyo. Kama ulivyoona mwenyewe, ameniambia hadi muda huo alikuwa bado yuko kazini”



“Na hakukwambia kwamba alikuwa anaumwa?”



“Hapana. Hakuniambia. Kama angekuwa anaumwa angenijulisha”



Kombo akashusha pumzi ndefu. Aliona ulikuwepo utata, tena utata mkubwa.



“Baada ya kutumiana naye meseji, hukuweza kuonana naye tena?”



“Sikukutana naye tena hadi nilipopata taarifa ya kifo chake”



“Kwa hiyo huwezi kujua alirudi saa ngapi nyumbani?”



“Siwezi kujua”



“Sasa ningetaka utupeleke katika hiyo nyumba aliyokuwa anaishi ili huyo mwenzake anayeishi naye upande wa pili atueleze kama alimuona aliporudi”



“Sawa, naweza kuwapeleka”



Dakika chache baadaye makachero hao wakawa wamempakia mzee huyo kwenye gari wakielekea katika nyumba aliyokuwa akiishi Pili.



Nyumba hiyo ilikuwa mtaa wa tatu kutoka mtaa aliokuwa akiishi mzee Amrani.



Walipofika Mzee Amrani aliwaonesha upande aliokuwa akiishi Pili na upande aliokuwa akiishi mwenzake. Kombo akabisha mlango wa upande wa pili. Baada ya muda kidogo akatoka msichana mmoja aliyekuwa amejifunga khanga mabegani na kiunoni.



“Karibuni” akasema kwa sauti ya wasiwasi, uso wake ukionesha huzuni.



Alipomuona mzee Amrani alijaribu kutabasamu.



“Baba tumekutana tena. Naweza kuwasaidia, mna tatizo gani?”



“Sisi ni polisi wa upelelezi, tulikuwa tunachunguza kuhusu mauaji ya Pili” Kombo alimwambia na kuongeza.



“Tumekuja kwako ili uweze kutusaidia lolote unalolijua kuhusu marehemu”



“Marehemu nilikuwa ninaishi naye nyumba moja lakini kila mmoja alikuwa na upande wake. Mimi ninaishi upande huu mwenzangu alikuwa anaishi upande mwingine” Msichana huyo alijibu haraka kama vile alihisi maneno hayo yangewasaidia sana polisi hao.



“Lakini ni watu mliokuwa mko karibu” Kombo alimwambia.



“Ndio. Tulikuwa tuko karibu. Karibuni ndani”



Msichana huyo aliyeonekana kuwa mchangamfu aliwakaribisha sebuleni. Sebule yake ilikuwa ndogo lakini ilipambwa vizuri.



“Karibuni mkae” aliwambia huku naye akiketi.



Baada ya watu wote kukaa kitako Kombo aliendelea na maswali.



“Kwa kifupi tulichotaka kujua, Pili alirudi saa ngapi jana kutoka kazini kwake?”



“Jana nilikutana na Pili asubuhi tu wakati anatoka kwenda kazini kwake. Yeye huwa anawahi kutoka kabla ya mimi. Lakini sikumuona kurudi tena”



“Kwani anaporudi huwa anakutambulisha”



“Anaweza kuja kwangu au mimi nakwenda kwake, tunapiga stori hadi wakati wa kulala. Lakini jana sikumuona na hata taa hazikuwashwa”



“Kama taa hazikuwashwa inamaanisha kuwa hakurudi” Mzee Amrani akasema.



“Tulifikiri labda alirudi kisha akakuaga kuwa anakwenda sehemu fulani” Kombo akamwambia msichana huyo.





ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 12


ILIPOISHIA



“Angerudi na angeniaga kuwa anakwenda sehemu, ningewambia”



“Unadhani atakuwa amekwenda wapi?”



Msichana huyo akabetua mabega yake.



“Kwa kweli siwezi kujua. Pili alikuwa mtulivu sana, hakuwa mtu wa kutokatoka sana anaporudi nyumbani. Mimi mwenyewe nilishangaa kwa kutomuona ile jana usiku.



“Hakuwahi kukueleza kama kulikuwa na mtu ana ugomvi naye?”



“Hakuwahi kunieleza. Pili mwenyewe alikuwa mpole sana. Sidhani kama alikuwa na ugomvi na mtu yeyote”



“Hakuwa na tabia ya kwenda kwa waganga wa kienyeji ambao labda watakuwa ndio waliomfyonza damu”



“Mh!” Msichana aliguna kisha alisema.



“Sijui. Kama alikuwa anakwenda kwa waganga wa kienyeji basi ilikuwa siri yake. Mimi hakuwahi kuniambia hata siku moja”



“Kwa hiyo huna tetesi tetesi zozote ulizozipata zinazohusiana na kuuawa kwake?”



SASA ENDELEA



Msichana akatikisa kichwa.



“Kwa kweli sijapata tetesi zozote”



“Tunakushukuru sana kwa maelezo yako ambayo ingawa hayakutusadia sana lakini yametupa mwanga kidogo”



“Na mimi pia nawashukuru, karibuni tena”



Wakati huo Kombo alikuwa ameshainuka, wenzake nao wakanyanyuka.



“Haya kwaheri mama” Mzee Amrani akamuaga.



“Jamanai karibuni sana”





Msichana huyo aliwasindikiza wageni wake hadi nje. Kombo na wenzake wakajipakia kwenye gari. Walimrudisha mzee Amrani nyumbani kwake kisha wakaelekea kituo cha polisi cha Kinondoni.



“Maelezo ya Waziri Mkuu na ya baba wa marehemu yanapingana sana” Kombo alimwambia Inspekta Alex.



“Hata mimi nimepata utata kidogo”



“Waziri Mkuu ametuambia kuwa marehemu aliondoka kazini kwake saa kumi na moja jioni baada ya kujisikia kuumwa kichwa na inawezekana kuwa alielekea hospitali. Lakini baba wa marehemu anasema mwanawe aliendelea kuwa kazini hadi saa moja na nusu usiku”



“Labda urudi tena kwa Waziri Mkuu akupe ufafanuzi zaidi” Alex alimwambia Kombo.



Kombo akanyamaza kimya. Aliona kurudi kwa Waziri Mkuu ili ampe ufafanuzi ilikuwa ni kama kumtuhumu kuwa alisema uongo.



“Hatuwezi kwenda kwa Waziri Mkuu kama tunaokwenda nyumbani kwa mtu mwingine” Kombo alisema baada ya ukimya. Akaongeza.



“Suala lenyewe ni muhimu sana kueleweka”



“Ni muhimu kwa sababu kinachotakiwa ni kujua marehemu alitoka saa ngapi kazini na alipotoka alikwenda wapi”



Baada ya Alex kusema hivyo palipita ukimya mwingine. Kombo alikuwa bado akiendelea kuwaza.



Alimuamini sana Waziri Mkuu kuwa hawezi kuongopa katika suala kama hilo lakini pia alimuamini yule mzee ambaye alimuonesha ushahidi wa meseji ambayo marehemu alimtumia saa moja na nusu usiku kumjulisha kuwa bado alikuwa kazini. Sasa nani atakuwa amesema uongo kati ya Waziri Mkuu na baba wa marehemu?



“Huu uchunguzi sasa umeanza kuingia utata!” Kombo alisema na kuutanzua ukimya uliokuwepo.



“Afande mimi naona suala ni la kurudi kwa Waziri Mkuu ili atoe ufafanuzi!”



Msisitizo huo wa Alex ulimkera Thabit Kombo kwa vile mtu aliyemtaja alikuwa mheshimiwa. Lakini mbali ya kukereka huko Kombo aliona kauli ya Alex ilikuwa ya ukweli na ya maana.



“Nitajadiliana na wakubwa” Kombo alisema huku macho yake yakitazama mbele ya kioo. Uso wake ulionesha kuwa alikuwa amezama kwenye mawazo.



“Hilo pia ni wazo zuri, unaweza kwenda kumhoji mheshimiwa Waziri Mkuu ukajikuta unalaumiwa”



“Ninajua. Kazi zetu zinakwenda kwa sheria lakini pia kwa amri”



Kombo alimuacha Alex kituo cha polisi cha Kinondoni akaelekea makao ya polisi.



Alipofika alikwenda moja kwa moja kwenye ofisi ya afisa upelelezi wa mkoa.



“Afande nimekwenda nyumbani kwa Waziri Mkuu kuchukua maelezo yake na pia nimekwenda nyumbani kwa wazazi wa marehemu, nako pia nimepata maelezo kutoka kwa baba wa marehemu” Kombo alimwambia afisa upelelezi.



“Je umegundua nini katika upelelezi wako?”afisa upelelezi akamuuliza.



“Nimegundua kwamba kuna utata kati ya maelezo ya Waziri Mkuu na maelezo ya baba wa marehemu”



“Umegundua utata gani?”



“Maelezo yamepishana kidogo. Waziri Mkuu alitueleza kwamba marehemu aiondoka kazini kwake jana saa kumi na moja jioni. Aliondoka mapema kwa sababu alikuwa anaelekea hospitali baada ya kueleza kuwa kichwa kilikuwa kinamuuma”



“Ndio”



“Baba wa marehemu ametuambia kwamba aliwasiliana na mwanawe saa moja usiku akiwa bado yuko kazini. Alituonesha meseji ambayo marehemu alimtumia baba yake kumjulisha kuwa muda huo alikuwa bado yuko kazini. Na vile vile baba wa marehemu hakuwa na taarifa yoyote kuwa mwanawe alikuwa anaumwa”



“Naam. Huo utakuwa ni utata”



“Sasa tufanyeje?”



“Itabidi urudi tena nyumbani kwa waziri Mkuu ili atuweke sawa. Nitamfahamisha hilo Mkurugenzi wa Upelelezi”



“Sawa”



“Inawezekana alighafilika au inawezekana baba wa marehemu ndiye aliyeghafilika lakini vizuri umfahamishe ili atuweke sawa”



“Nimekuelewa afande”



******************



Toyota Land Cruiser la rangi nyeupe la mheshimiwa Wazirui Mkuu lilikuwa linatoka Kibaha. Dereva wa gari hilo alikuwa ametumwa na mheshimiwa kwenda kukagua shughuli zilivyokuwa zikiendelea katika shamba lake lililoko nje kidogo ya mji wa Kibaha.



Shamba hilo lililokuwa na zaidi ya hekta mia moja lilikuwa na ng’ombe mia tatu wa mheshimiwa Waziri Mkuu na lilikuwa na wafanyakazi wasiopungua thelathini.



Dereva wa gari hilo Kidas Athumani alikuwa eneo la Kimara akielekea nyumbani kwa Waziri Mkuu. Aliona lori linataka kumpita akabana kushoto. Mbele yake kulikuwa na gari jingine dogo alilokuwa amelikaribia sana.



Kwa vile gari la Waziri Mkuu lilikuwa kwenye kasi, dereva Kidasi aligusagusa breki ili kuzuia gari lisiligonge gari la mbele yake kwa nyuma. Moyo wake ulishituka alipogundua kuwa breki haikutii agizo lake. Gari lilikuwa limefei breki!



Kutahamaki akajikuta ameligonga kwa nyuma gari la mbele yake!



Kwa sababu gari hilo lilikuwa limefeli breki liliendelea kulibamiza gari hilo hadi liliposimama.



Kidasi alifungua mlango na kushuka haraka. Alikwenda mbele ya gari hilo na kulitazama gari aliloligonga. Lilikuwa limebonyea sehemu ya nyuma upande wa kushoto ambapo taa yake ilikuwa imevunjika.



Mwenye gari hilo ambalo lilikuwa limesimama, naye alikuwa ameshuka akilitazama gari lake lilivyoharibiwa.



“Unaona!” alimwambia Kidasi kwa hasira.



“Samahani. Gari langu lilifeli breki”



Watu wakaanza kumiminika katika eneo hilo. Polisi wa usalama barabarani waliokuwa karibu wakajisogeza mahali hapo. Walishaona kilichokuwa kimetokea.



“Umemgonga mwenzako kwa nyuma, ni kosa kubwa sana” Polisi mmoja alimwambia Kidasi.



“Ni kweli gari langu lilikuwa limefeli breki” Kidasi aliwambia. Uso wake tayari ulishajaa tembe za jasho. Alitoa kitambaa akajifuta.



Polisi hao walilikagua gari lake kisha wakamwambia atoe leseni yake waione.



Kidasi aliwapa leseni yake. Polisi mmoja akaikagua.



“Lete kadi ya gari lako”



Kidasi aliwatolea kadi hiyo na kuwapa.



Baada ya kuikagua kadi hiyo polisi huyo alimuuliza Kidasi.



“Gari hii ni ya nani?”



“Ni ya mheshimiwa Waziri Mkuu”



Polisi hao walishituka.



“Wewe ni dereva wake?” Polisi mmoja akamuuliza.



“Ndiyo”



Walimrudishia leseni yake na kadi ya gari.



“Umesema gari ilifeli breki?”



“Ndiyo”





itaendelea
 
SEHEMU YA 13


ILIPOISHIA



Polisi hao wakaanza kupima ajaIi hiyo na kuzuia magari mengine yapite kando. Baada ya kupima ajali polisi mmoja alimwambia dereva wa gari jingine atoe kadi ya gari lake.



“Iko nyumbani” aliwambia.



“Kwanini hutembei nayo?”



“Niliisahau”



“Leseni yako iko wapi?”



Jamaa alijipapapasa kisha akasema.



“Leseni pia nimeisahau nyumbani”





SASA ENDELEA

“Kila kitu Umesahahu nyumbani? Yaani unaendesha gari bila kuwa na leseni?”



“Sio kama sina, nimeisahau tu”



“Tutaaminije kama unayo leseni au huna?”



“Nitakwenda kuichukua”.



Kombo alikuwa yuko ofisini kwake akisubiri ruhusa ya kurudi tena nyumbani kwa Waziri Mkuu kumhoji kuhusu utata uliojitokeza kati ya maelezo yake na maelezo ya Mzee Amrani, simu yake ikaita juu ya meza.



Aliunyakua mkono wa simu na kuuweka sikioni kwake, akasema.



“Hello!”



“Kuna gari limekamatwa na polisi wa usalama barabarani limefanana na lile lililoshukiwa, ni aina ya Land Cruiser la rangi nyeupe. Nimewaambia walilete hapa” Kombo aliitambua sauti hiyo kuwa ilikuwa ya afisa upelelezi.



“Limekamatwa wapi?” Kombo akauliza.



“Limekamatwa Kimara, liligongana na gari jingine lakini limegundulika kuwa ni la waziri mkuu”



“Ni nani aliyekuwa akiliendesha?”



“Ni dereva wake”



“Ningependa nimuone”



“Hilo gari litaletwa sasa hivi pamoja na huyo dereva”



*******



Waziri Mkuu alikuwa amesharudi nymban kwake alipopigiwa simu na dereva wake Kidasi Athumani.



“Mzee nimepata ajali, gari limekamatwa na polisi” Kidasi alimwamba Wazri mkuu kwenye smu.



“Umegonga au umegongwa?”



“Nimegonga gari kwa nyuma. Gari lilifeli breki”



“Kuna aliyejeruhiwa?”



“Hakuna aliyejeruhwa”



“Ajali imetokea wapi?”



“Kmara. Nilikuwa narudi kutoka Kibaha”



“Ilikuwa ajali kubwa?”



“Si kubwa lakini gari nililoligonga limebonyea kwa nyuma”



“Polisi wamekwambia nini?”



“Wamenikamata”



“Umewambia kuwa gari hilo ni langu?”



“Nmewambia”



“Sawa. Waache wafuate taratibu zao halafu utanifahamsha”



“Sawa mzee”



Waziri Mkuu aliiweka simu yake juu ya meza kisha akamtazama mke wake.



“Kidasi amepata ajali” akamwambia.



“Wapi?”



“Kimara”



“Amegonga au amegongwa?”



“Amegonga”



Mke wa Wazir Mkuu akaguna.



“Wiki hii ni ya mkosi kwetu, sijui ni kitu gani kinataka kututokea”



“Yuko kituo cha polisi, nimemwamba anifahamishe kitakachoendelea. Kama mwenye gari atataka kulipwa tutamlipa, kama atataka tuendelee na kesi sawa”



“Vizuri ni kumlipa tu”



“Akitaka tumlipe gharama za matengenezo tutamlipa”



“Kabla ya Kidasi kukupigia simu ulikwa unataka kunieleza kitu”



“Nimearifiwa kuwa wale wapelelezi wanataka kurudi tena kutuhoji kuhusu kuuawa kwa Pili”



“Waje tena mara ya pili?“



“Ndio, na mimi nimeshangaa”



“Labda wamegndua kitu”



“Kitu gani?”



“Kitu chochote tu. Unadhani wanakuja bure”



“Nmewambia na waje tu”



“Watakuja saa ngapi?”



“Nimewambia baada ya masaa mawili nitakuwa nyumbani. Wanaweza kuja wakati wowote kutoka sasa”



*************



Kidasi alishangaa alipoona akipelekwa katika ofisi ya idara ya upelelezi makao ya polsi. Aliingizwa katika ofisi Thabit Kombo na kuanza kukabiliana na maswali ambayo hayakuhusiana na ajali iliyotokea.



“Wewe upo katika ajira ya serikali au binafsi?” Kombo alimuuliza.



“Niko katka ajira binafsi. Waziri Mkuu aliniajiri niwe dereva wa gari zake”



“Gari zake binafsi sio?”



“Ndio”



“Unamuendesha nani?”



“Zile gari ni kwa ajili ya shughuli za shamba lake lililoko Kibaba”



“Sawa. Ni wakati gani unaingia kazini, na wakati gani unatoka kazini?”



“Sina muda maalum wa kuingia au kutoka kazini. Kuna siku naingia kazini saa kumi na moja alfajir kwa ajili ya kwenda Kibaha kufuata maziwa ya ngombe. Ninakuwa kwenye gari nyengine. Siku nyngine naingia kazini saa mbili asubuhi”



“Na kutoka?”



“Pia sina muda maalum, inategemea nitakapomaliza kazi ninazotumwa”



“Unaweza kuwa na gari hilo hadi saa ngapi?”



“Wakati mwingine hadi saa nne usiku”



“Hebu niambie jana ulitoka saa ngapi kazini?”



“Nilitoka saa nne usiku”



“Ulikuwa umekwenda wapi?”



“Kibaha”



“Na uliondoka hapa jijini saa ngapi?”



“Niliondoka saa kumi”



“Hilo gari liko wapi?”



“Limeletwa hapa makao ya polisi”



“Hebu twende nikalione”



Kombo na Kidasi walitoka ofisini wakaenda lilikokuwa gari hilo.



Kombo alilikagua. Alifungua mlango wa nyuma na kulitazama ndani kisha akafunga mlango.



“Kwa hiyo jana ulikuwa na gari hili hadi saa nne usiko?”



“Hili gari nilikuwa nalo kuanzia asubuhi hadi saa kumi ambapo nilichukua gari jingine ambalo tunabebea ndoo za maziwa”



“Sio hili?”



“Hapana. Kuanzia saa kumi hadi saa nne usiku nilikuwa na gari jingine, sio hili”





itaendelea
 
SEHEMU YA 14


ILIPOISHIA



“Labda tumepishana kiswahili. Uliponiamba kwamba jana ulitoka kazini saa nne usiku nilielewa kwamba ulikuwa na gari hili”



“Hapana, ni gari jingine”



“Sawa. Nitakwenda kuzungumza zaidi na Waziri Mkuu mwenyewe”



“Naamini atakueleza vizuri”



************



Jua lilikuwa linakaribia kuchwa wakati kachero Thabit Kombo alipofika nyumbani kwa Waziri Mkuu. Safari hii alikwenda peke yake akiwa na jalada lake mkononi.



Alikaribishwa sebuleni. Waziri Mkuu akamuuliza kama alihitaji kinywaji chochote.



Kombo akatikisa kichwa.



“Asante mheshmwa. Sitahitaji kinywaji chochote. Nimerudi tena kwa sababu kumejitokeza utata kidogo, ninahitaji ufafanuzi”



SASA ENDELEA



“Utata gani uliojitokeza?’



Ingawa sauti ya Waziri Mkuu ilikuwa tulivu lakini moyo wake ulikuwa ukienda mbio.



“Kama nilikusikia vizuri uliponipa maelezo yako kwa mara ya kwanza uliniambia kwamba marehemu Pili Amrani aliondoka kazini hapa nyumbani, jana saa kumi na moja jioni baada ya kueleza kuwa kchwa kilikuwa kinamuuma”



“Sasa ni utata gani uliojtokeza?’



“Nilipokuwa namhoji baba mzazi wa marehemu aliniambia kwamba hadi saa moja usiku mwanawe alikuwa bado yuko kazini hapa nyumbani. Je mheshimiwa waziri atatoa maelezo gani kuhusiana na utata huo?”



Waziri Mkuu alishituka lakini alifanikiwa kuuzuia uso wake usioneshe taswira ya mshituko.



“Yeye ana ushahidi gani kuwa mwanawe alikuwa hapa nyumbani hadi muda huo?”



“Alituambia kuwa waliwasiliana kwa meseji. Mzee Amrani alimtumia marehemu meseji muda huo kumuuliza kama alikuwa ameshatoka kazini. Marehemu akamjibu kuwa alikuwa bado yuko kazini”



Sasa macho ya mheshimiwa Waziri Mkuu yalianza kuwa makali. Kombo aliyakwepa kwa kugeuza uso wake kando.



“Alikwambia waliwasiliana muda gani?”



“Saa moja usiku”



Waziri Mkuu alitaka kutikisa kichwa lakini alipata hoja.



“Alikuonesha hiyo meseji ambayo marehemu alimtumia?”



“Alinionesha kwenye simu yake”



“Uliiona?”



“Ndiyo”



“Sasa unadhani ni nani alikupa maelezo yasiyo sahihi?” Waziri Mkuu akauliza kwa sauti iliyoonesha kuwa ametaharuki.



“Hatuko huko mheshimiwa. Mmojawapo anaweza kuwa ameghafilika”



“Nilichokueleza mimi kilikuwa sahihi. Kama kulikuwa na tatizo lilikuwa kwa marehemu mwenyewe”



“Tatizo, kivipi?”



“Inawezekana marehemu alimdanganya baba yake kuwa yuko kazini, kumbe alikuwa kwenye shughuli zake mwenyewe lakini hapa kwangu hakuwepo muda huo”



“Nimekuelewa. Yaani ni kwamba marehemu alimwambia baba yake kuwa bado yuko kazini, kumbe hakuwepo. Alikuwa ameshaondoka”



“Na ninadhani kutokana na maelezo hayo marehemu hakuwa anaumwa kama alivyotuambia bali alisingizia tu akiwa na sababu zake. Kama alikuwa anaumwa kweli angemwambia baba yake”



“Nimekuelewa”



“Una swali jingine?”



“Sina mheshimiwa”



“Karibu sana”



Kombo alihisi Waziri Mkuu alikuwa amechukia. Wakati anajiandaa kuinuka akaisikia sauti ya Waziri Mkuu.



“Nimesikia kwamba gari langu limekamatwa”



Kombo hakutaka kulizungumzia suala la gari hilo. Alipitisha sekunde mbili hivi kabla ya kumjibu.



“Mheshimiwa gari hilo lilikamatwa na trafiki baada ya dereva wake kugonga gari la mtu mwingine”



“Hilo ni suala dogo tu, kwani kuna mtu aliyejeruhiwa”



“Hakuna aliyejeruhiwa”



“Mbona dereva wangu amecheleweshwa sana, kama trafiki wameshapima ajali iliyotokea na labda wamezuia leseni yake, basi zifuate taratibu zingine”



“Natumaini hadi sasa watakuwa wamekamilisha hizo taratibu”



Kombo akainuka. Waziri Mkuu naye aliinuka na kumuaga.



“Karibu sana”



Wakati Kombo anatoka nyumbani kwa Waziri Mkuu aliliona gari la Waziri Mkuu likiwasili. Ndani ya gari hilo alikuwamo dereva wa gari hio na msaidizi wa Waziri Mkuu.



Polisi walikuwa wameshaliachia baada ya msaidizi w wa Waziri Mkuu kukubaliana na mwenye gari lililogongwa kuwa watagharamikia matengenezo yake.



********



Baada ya mazishi ya Pili Juma, upelelezi wa kesi hiyo ukaachwa. Na Waziri Mkuu hakuulizia tena suala hilo.



Sasa suala lililokuwa linakula vichwa katika familia ya Waziri Mkuu ni kile kitendo cha binti wa Waziri Mkuu kumfyonza damu mpishi wao hadi kumuua.



Baada ya vipimo vya hospitali kuonesha kuwa Sofia hakuwa na malaria, Waziri Mkuu alihisi kwamba binti yake huyo anaweza kuwa na matatizo ya akili. Akataka kumpeleka hospitali ili akafanyiwe uchunguzi wa akili yake lakini hakutaka uchunguzi huo ufanyike hapa nchini kwani alitaka uwe wa siri. Na matokeo yake pia yawe siri.



“Mimi nafikiri tumpeleke Nairobi” Waziri Mkuu alimwambia mke wake jumapili moja walipotoka kanisani.



“Ni sawa. Akifanyiwa uchunguzi kule, habari zake hazitajulikana”



“Mimi bado nina wasiwasi kuwa ana matatizo. Kuna siku naona anakuwa mkimya sana”



“Sasa atakwenda na nani huko Nairobi?”



“Uende naye wewe”



“Lini?”



“Nataka iwe haraka iwezekanavyo. Itabidi leo nifanye mawasiliano na ile hospitai ninayoifikiria. Ikiwezekana kesho kutwa muondoke”



“Sawa”



“Ninapokagua vitabu vyake vya shule anaonekana anaendelea vizuri tu, sijui ana tatizo gani. Kama ni matatizo ya akili ni vizuri yajulikane mapema na yapatiwe tiba kabla hali haijakuwa mbaya”



“Ni kweli”



Jumapili ile ile baada ya chakula cha mchana, Sofia na Monica waliingia chumbani kupumzika. Waziri Mkuu na mke wake walikuwa wamekaa sebuleni wakiendelea kuzungumza. Vero alikuwa hayupo nyumbani.



Kwa kawaida kila inapofika saa kumi jioni siku za jumapili Sofia na Monica huenda katika masomo ya tuisheni lakini siku ile waliendelea kubaki chumbani hadi muda huo.



Ilipofika saa kumi na nusu mke wa Waziri Mkuu alipata wasiwasi baada ya kutowaona Sofia na Monica, akawafuata chumbani walimokuwa.



Alifungua mlango na kuingia ndani. Alikuta hali iliyokuwa imemshangaza. Monica alikuwa amelala chini wakati Sofia alilala kichali chali kitandani huku miguu yake ikiwa chini. Alikuwa kama mtu aliyekuwa ameketi kisha akaamua kujilaza.



Kulikuwa na michirizi ya damu kwenye shingo ya Monica. Kadhalika kwenye midomo ya Sofia pia kulikuwa na damu na tumbo lake lilionekana limejaa.



Mke wa Waziri Mkuu alimtazama Monica pale chini alipokuwa amelala. Akajiuliza maswali matatu.



Kwanini Monica alikuwa ameala chini?



Kwanini shingo yake ilikuwa na michirizi ya damu?



Damu ile ilitoka wapi?





Itaendelea
 
SEHEMU YA 15


ILIPOISHIA



Hakupata jibu. Akasogea kwenye kitanda ambako Sofia alikuwa amelala akamtazanma kwa makini. Maswali matatu yakamjia tena akilini.



Kwanini Sofia ana damu midomoni?



Damu ile imetoka wapi?



Na kwanini tumbo take limejaa?



Moyo wake ukiwa umeshituka, mke wa Waziri Mkuu alitoka haraka akashuka ngazi na kumfuata mume wake aliyekuwa chumbani.



“Hebu twende ukawaone wale watoto” alimwambia kwa sauti ya kutaharuki.



Waziri Mkuu naye alishituka.



“Wana nini?” akamuuliza.



“Hebu twende ukawaone mwenyewe”



Mke wa Waziri Mkuu alikuwa ameshatangulia kutoka. Waziri Mkuu akamfuata nyuma.



SASA ENDELEA



Walipanda ngazi na kuingia katika chumba walichokuwemo Sofia na Monica.



“Hebu watazame”



Waziri mkuu akawatumbulia macho mabinti zake wawili, mmoja akiwa kitandani na mwingine akiwa chini.



“Uliwakuta wakiwa hivi hivi?”



“Niliwakuta hivyo hivyo, Monica yuko chini ana michirizi ya damu shingoni na Sofia yuko kitandani, mdomoni ana damu na tumbo lake limejaa…!”



Waziri Mkuu akiwa ameshituka alichutama akamtazama Monica.



“Monica! Monica! Monica!” alimuita mara tatu.



Monica hakuitika wala kugeuka. Mke wake alijaribu kumshika na kumuinua. Monica alikuwa baridi na alikuwa amelegea kama mnyoo. Akamrudisha chini na kuweka mkono kifuani kwake kusikiiza mapigo ya moyo wake.



Wakati akifanya hivyo Waziri Mkuu alikuwa akimtazama.



“Moyo unapiga?” akamuuiza.



Mke wake akatikisa kichwa.



“Sina hakika kama mwanangu yuko hai” akasema.



“Isije kuwa lile tukio la mpishi wetu limejirudia kwetu?”



Waziri mkuu naye aliuweka mkono wake kwenye pua ya Monica kuona kama alikuwa anapumua, hakuhisi dalili yoyote kuwa Monica alikuwa anahema.



Hapo hapo akaguna. Uso wake ukasawijika. Alikuwa kama mtu ambaye alitaka kulia.



Akanyanyuka na kusogea kunako kitanda, akamtazama Sofia. Kwa kumtazama kwa macho tu aligundua kuwa Sofia alikuwa akipumua tena alikuwa akipumua kwa nguvu kama alikuwa anakabwa pumzi.



Tumbo lake lililokuwa limejaa kuliko kawaida lilikuwa likienda juu na kurudi chini. Tembe za jasho zilikuwa zikiendelea kutanda kwenye paji la uso wake.



Midomo yake alikuwa ameichanua. Damu nyeusi ya mtu mwenye afya njema ilionekana kwenye papi za midomo hiyo. Meno yake yalionekana. Yalikuwa mekundu kwa damu.



“Sofia!” Waziri Mkuu alimuita.



Sofia aliendelea kupumua tu kama mtu aliyekuwa kwenye usingizi mzito.



Mke wa Waziri Mkuu alisogea karibu na kitanda akamshika mkono Sofia na kumuita.



“Sofia!”



Sofia akashituka, akafumbua macho na kuwatazama mama yake na baba yake kwa macho makali. Macho yenyewe yalikuwa mekundu yakionesha kuwa alikuwa katika usingizi mzito.



Sofia alipozinduka aliduwaa kwa sekunde kadhaa kabla ya kuinuka na kujifuta midomo yake. Aliifuta ile damu kisha akaitazama damu hiyo kwenye mikono yake.



“Hii ni damu!” akasema peke yake na kuuliza.



“Imetoka wapi?”



Alijipangusa tena kisha akaitazama damu hiyo.



“Ninatoka damu midomoni” alisema kisha akateuka.



Wakati huo wote baba yake na mama yake walikuwa wakimtazama.



“Inatoka wapi hiyo damu?” Baba yake akamuuliza.



Sofia akabetua mabega.



“Sijui baba, kinywa chote kimejaa harufu ya damu. Hapa nilipoteuka nimeteuka damu halafu naona tumbo langu limejaa”



Wakati Sofia akisema hivyo Baba yake na mama yake walikuwa wakitazamana kwa mshangao.



“Monica yuko wapi?” baba yake akajaribu kumuuliza.



“Nilikuwa naye hapa kitandani tunazungumza halafu usingizi ulinipitia. Labda ameondoka”



Waziri Mkuu akamtazama mke wake.



“lazima kuna tatizo” akasema.



“Kwani mwanangu unajisikiaje?” Mke wa Waziri Mkuu akamuuliza Sofia.



“Najisikia kichwa kinaniuma” Sofia alisema.



“Hebu toka naye” Waziri Mkuu akamwambia mke wake.



Mwanamke huyo alimshika mkono Sofia akamwambia ashuke kwenye kitanda.



“Monica si huyu hapa amelala chini!” Sofia alisema alipomuona Monica, lakini hakukuwa na yeyote aliyemjibu.



Alitoka na mama yake.



Waziri Mkuu alisali kisha akaubeba mwili wa Monica na kuuingiza katika chumba cha wageni, akaulaza kwenye kitanda.



Hapo ndipo alipomchunguza Monica kwa makini. Mbali ya kuthibitisha kuwa Monica alikuwa ameshakufa aligundua pia jaraha la meno kwenye shingo ya Monica, pale pale palipokuwa na michirizi ya damu.



Akashusha pumzi ndefu. Aliketi pembeni mwa kile kitanda akawa anajiuliza, mwanawe Sofia alikuwa amepatwa na nini?



Alishagundua kuwa Sofia alikuwa amemfyonza damu mwenzake hadi kumuua. Alifahamu pia kuwa wakati Sofia akifanya hivyo hakuwa akijitambua na baada ya hapo akapitiwa na usingizi mzito kama ilivyotokea siku ile kwa Pili.



Baada ya muda kidogo mke wake aliingia mle chumbani. Alisimama mbele ya kitanda kilicholazwa mwili wa Monica na kuangua kilio.



“Hapana, usilie mke wangu. Tatizo limeshatokea tunatakiwa tupange tutafanya nini. Kwanza Sofia yuko wapi?”



Mke wake alijifuta machozi.



“Sofia nimemuacha sebuleni anaangalia tv”



“Sasa hebu keti hapa tupange”



Mke wake akaketi kwenye pembe ya kitanda karibu na mume wake.



“Monica ameshakufa na ameuawa na Sofia, amemfyonza damu kama alivyomfyonza yule mpishi wetu” Waziri Mkuu alimwambia mke wake ambaye aliposikia maneno ya mume wake alianza tena kulia.



“Nimekwambia usilie, jikaze kwanza. Sofia atakuwa na matatizo ya akili. na matatizo yake ni makubwa kuliko ya mwendawazimu anayevua nguo”



“Si ndio tulipanga tumpeleke Nairobi kesho kutwa akafanyiwe uchunguzi, sasa leo tatizo limejitokeza tena”



“Tulichelewa. Lakini si kitu. Sasa huyu binti yetu aliyekufa tutasema ameuawa na nini?”



“Tutasema alikufa mwenyewe”



“Ana jeraha kwenye shingo yake!”



“Tumfute ile damu tumuweke sawa, tusimpeleke hospitali kuchunguzwa. Mtu anapokufa si lazima apelekwe hospitali”



“Ni sawa. Labda tuseme kuwa aliumwa ghafla”



“Ndio. Tunaweza kusema alidai kuwa alikuwa anajisikia vibaya baya. Wakati tunamuandaa kumpeleka hospitali akafariki ghafla”



“Itatosha”



“Hakuna atakayetuhoji chochote. Kifo ni kitu cha kawaida”



“Tukishamzika ndio tutashughulikia suala la Sofia”





ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom