Hadithi: Kosa ni Langu (part 1)

Hadithi: Kosa ni Langu (part 1)

Bob swagger

Member
Joined
Jan 16, 2020
Posts
48
Reaction score
56
Ilikuwa ni wiki tuu mimi na familia yetu tukiwa tumeamia katika makazi mapya kwakua sikua na rafiki wa kuongea nae basi nilipenda kwenda kukaa mbele ya nyumba yetu kwani kulikua na mti wenye kivuli ambapo chini ya mti huo kulikuwa na gogo la mnazi, basi mimi nilipenda sana kwenda kukaa kwasababu nilikua nasubiria wazazi wangu wapate fedha ili niweze kwenda shule.

Basi baada ya siku kama mbili kupita nikiwa natoka nyumbani naelekea kukaa pale kwenye gogo chini ya mti nilikuta watoto wadogo wawili wanacheza, basi mimi nikaenda kukaa, ile nimekaa tu nikasikia nasalimiwa shikamoo nikaitia kisha nikaendelea na kufikiria mambo yangu ya shule.

Ilipita kama dakika kumi nikashituka kwani usingizi ulikua umenipitia kuangalia mbele nikaona kabaki mtoto mmoja alikuwa anacheza peke yake kwani alikuwa ana chora picha za maua kwa kuandika kwenye ardhi, mara nikasikia sauti inaita Vivian, nikaona yule mtoto kakulupuka kwa kushituka kisha akaitikia abeeeeee akasimama kisha akaanza kutembea kuelekea sauti ilipokua inatokea.

Alipo nikaribia tu akaniaga kwa kuniambia kwaheri nami nikamjibu aya msalimie dada kwani sauti niliyohisikia inamwita ilikua ya kike kwani sauti iliyokua inamuita ilikua inatokea nyuma ya mgogo wangu nami sikugeuka kuangalia.

Itaendelea..
 
Mmeipenda niweke muendelezo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom