SectionTwenty
JF-Expert Member
- Aug 3, 2013
- 675
- 614
SEVEN DAYS OF
KARALINA (SIKU SABA ZA
KARALINA) [1]
MTUNZI: Mysterio Hamic
CONTACT: 0714 499248
EMAIL:
mysteriohamic@gmail.
com
Twitter: mysterioHamic
Ilikua ni mishale ya saa
saba za usiku tulivu
ndani ya jiji la dar es
salaam. Nyota pamoja
na mbalamwezi zilikua
ziking'arisha anga na
kuifanyia iwe ya kuvutia.
Hali ya hewa ya baridi
kiasi na upepo ilizidi
kuleta raha miongoni
mwa wakazi wa jiji hilo.
Katika maeneo ya
mikocheni kulikua na
mwanamke mmoja
alikua akitembea
kuelekea mahali ilipo
nyumba yao. Mwanamke
huyo alikua ni karalina
Mustafa, karalina
msichana wa miaka 22
alikua ni msichana
mrembo aliyechanganya
damu ya kiarabu na
kiswahili. Baba yake
alikua ni mtu mwenye
asili ya taifa la azebaijan
mwenye uraia wa
tanzania wakati mama
yake alikua ni msambaa
wa kutoka Tanga
Usiku huo alikua
akitokea katika birthday
ya rafiki yake Janeth
iliyofanyika maeneo ya
magomeni.
Alipoangalia saa yake
katika simu yake ya
mkononi aligundua
ishatimu saa saba na
nusu za usiku,hakika
alikua amechelewa
kurudi kwao na jambo
hilo lilimtia hofu kwani
alifahamu fika jinsi
wazazi wake
wasivyopenda tabia ya
kuchelewa kurudi
nyumbani. Kwao yeye
ndio alikua mtoto pekee
hivyo alikua anaangaliwa
kwa umakini sana.
Baada ya kutembea kwa
muda kidogo hatimae
alifika nje ya geti la
nyumba yao. Kitu kimoja
kilichomshangaza ni
kukuta geti la nyumbani
kwao lipo wazi hadi
usiku huo!!! Jambo hilo
lilimshangaza sana.
Akaingia taratibu na
akaanza kuangaza huku
na huko ili kuona kama
anaweza kumuona
mlinzi wa nyumbani
kwao lakini aliambulia
patupu,Mlinzi
hakuwepo!!
Moja kwa moja akaanza
kupiga hatua kuelekea
mlango wa kuingia
sebuleni kwao,lakini
alishangaa kuona taa za
sebuleni kwao zikiwa
bado zinawaka. Hofu
ikazidi kumpanda
karalina, lakini akazidi
kusogea taratibu.
"Paaah Paaah" milio ya
risasi ilisikika kutoka
ndani ya nyumba
yao,milio hiyo ilimfanya
karalina kushtuka na
mapigo ya moyo
kumuenda kasi zaidi.
Alihisi hatari,na kwa
kuwa alikua bado
hajaingia sebuleni
aliamua kujisogeza
kwenye dirisha lilikua
karibu na mlango wa
kuingilia sebuleni kwao
ili aweze kuangalia
kinachotokea. Akiwa
hapo hakuamini macho
yake kile alichoshuhudia
ndani....
Endelea kuisoma sehemu yote ya kwanza ya hadithi hii katik http://robinvanmysterio.blogspot.com/2014/03/seven-days-of-karalina-isiku-saba-za.html?m=1
KARALINA (SIKU SABA ZA
KARALINA) [1]
MTUNZI: Mysterio Hamic
CONTACT: 0714 499248
EMAIL:
mysteriohamic@gmail.
com
Twitter: mysterioHamic
Ilikua ni mishale ya saa
saba za usiku tulivu
ndani ya jiji la dar es
salaam. Nyota pamoja
na mbalamwezi zilikua
ziking'arisha anga na
kuifanyia iwe ya kuvutia.
Hali ya hewa ya baridi
kiasi na upepo ilizidi
kuleta raha miongoni
mwa wakazi wa jiji hilo.
Katika maeneo ya
mikocheni kulikua na
mwanamke mmoja
alikua akitembea
kuelekea mahali ilipo
nyumba yao. Mwanamke
huyo alikua ni karalina
Mustafa, karalina
msichana wa miaka 22
alikua ni msichana
mrembo aliyechanganya
damu ya kiarabu na
kiswahili. Baba yake
alikua ni mtu mwenye
asili ya taifa la azebaijan
mwenye uraia wa
tanzania wakati mama
yake alikua ni msambaa
wa kutoka Tanga
Usiku huo alikua
akitokea katika birthday
ya rafiki yake Janeth
iliyofanyika maeneo ya
magomeni.
Alipoangalia saa yake
katika simu yake ya
mkononi aligundua
ishatimu saa saba na
nusu za usiku,hakika
alikua amechelewa
kurudi kwao na jambo
hilo lilimtia hofu kwani
alifahamu fika jinsi
wazazi wake
wasivyopenda tabia ya
kuchelewa kurudi
nyumbani. Kwao yeye
ndio alikua mtoto pekee
hivyo alikua anaangaliwa
kwa umakini sana.
Baada ya kutembea kwa
muda kidogo hatimae
alifika nje ya geti la
nyumba yao. Kitu kimoja
kilichomshangaza ni
kukuta geti la nyumbani
kwao lipo wazi hadi
usiku huo!!! Jambo hilo
lilimshangaza sana.
Akaingia taratibu na
akaanza kuangaza huku
na huko ili kuona kama
anaweza kumuona
mlinzi wa nyumbani
kwao lakini aliambulia
patupu,Mlinzi
hakuwepo!!
Moja kwa moja akaanza
kupiga hatua kuelekea
mlango wa kuingia
sebuleni kwao,lakini
alishangaa kuona taa za
sebuleni kwao zikiwa
bado zinawaka. Hofu
ikazidi kumpanda
karalina, lakini akazidi
kusogea taratibu.
"Paaah Paaah" milio ya
risasi ilisikika kutoka
ndani ya nyumba
yao,milio hiyo ilimfanya
karalina kushtuka na
mapigo ya moyo
kumuenda kasi zaidi.
Alihisi hatari,na kwa
kuwa alikua bado
hajaingia sebuleni
aliamua kujisogeza
kwenye dirisha lilikua
karibu na mlango wa
kuingilia sebuleni kwao
ili aweze kuangalia
kinachotokea. Akiwa
hapo hakuamini macho
yake kile alichoshuhudia
ndani....
Endelea kuisoma sehemu yote ya kwanza ya hadithi hii katik http://robinvanmysterio.blogspot.com/2014/03/seven-days-of-karalina-isiku-saba-za.html?m=1
Last edited by a moderator: