Hadithi nzuri ila kuna kauongo kadogo hapo toka umemuacha kijijini hadi miezi 9 imepita hujui yupo kwa wazazi wako inamaanisha ulikuwa huwasiliani na wazazi wako miezi yote 9? Hebu edit hapo
Kabla hawajauigiza niliundika kwa mara ya kwanza katika Gazeti la Heko mwaka 1992 kwa jina hilihili lakini nilishangaa kuigizwa na akina Warid na Bishanga bila ya ridhaa yangu, haki nyingi zinapotea.
Kwenye Heko kulikuwa na sehemu iliyokuwa ikiitwa Darasa la Mapenzi nilitunga kisa kingine kinaitwa Toto la Tanga, nitakileta hapa pia, kuna mtu humu ndani amesema kama alishawahi kuusoma mahali ni kweli, hapo ndipo nilipoundika mkasa huu kwa mara ya kwanza.