Sehemu ya NNE
Millan alkua chumbani kwake akipanga mizigo yake kwajiri ya safari,alihitajika kufika Arusha wiki moja kabla ya mazoezi ya kazi kuanza,akiwa kwenye shughuli yake hiyo alikutana na albam yake ndogo alokua akiitumia wakati yupo shule. Mwanzo kabisa wa ukurasa wa album akakutana na sura nzuri ilo achia tabasamu pana katka picha moja wapo,haikua sura ya MTU mwingine ila Judith millambo "wewe tena" millan alijikuta akijisemea "umekua mwepesi wa kusahau ahadi zoote ulizo nipa umeona haitoshi ukaamua kukata mawasiliano na Mimi kabisa ili nikae mbali na maisha yako,ahsante Sana Judith nimekubali kuanza maisha mapya bila wewe,mwanzo nlidhani sitaweza ila imenilazim nianze" aliyamaliza maneno hayo akiwa amelowa machozi
Ben alie kua mlangoni akimtazama rafiki ake akamfata na kumshika bega "jikaze kaka wanaume hawalii" Ben alisema
"Hujui tu kaka,huyu mwanamke amenipotezea Muda Sana na Kama nlijua huko marekani asinge dhubutu kunikumbuka ila kwa maneno alo kua akinambia na kunipa ahadi nkajikuta nashawishika kumuamini lakin amenitupilia mbali nakunisahau" Millan alilalamika,huku rafiki ake Ben akiwa anamuonea huruma "huwezi jua kaka nini kilimkuta baada ya yeye kua amefika huko jaribu kuvuta subira usimuhukumu mapema"
"Mapema!!,mwaka wa tatu sasa unasema mapema" Millan alihamaki.
Asubuhi na mapema Millan alkua ndani ya basi akielekea mkoani Arusha ,akaamua ampigie mama yake simu lakini haikupatikana akamtumia ujumbe mfupi wa maneno kua atakua kazoezini kwa Muda wa miez miwili na baada ya hapo atakwenda nyumbani kwao mkoani Iringa kwa mapumziko