Hadithi: Joto La Mapenzi

Hadithi: Joto La Mapenzi

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,638
Image may contain: 2 people

HADITHI: .. JOTO LA MAPENZI
SEHEMU: 01
MTUNZI: Ally Mbetu ‘DrAmbe’
SIMU: 0713 646500

UTANGULIZI
Kutokana na wingi wa watu kuwaorodhesha kabla ya kuwaingiza kwenye kundi la Whatsapp mtaendelea na hadithi kwenye FB likiwa tayari tutahamia huko kila aliyetuma namba ataingia msihofu. Leo tunaanza na kitu kipya tuwe pamoja.

JASHO LA MOYO
Kutokana na maji kuingia kwa kasi katika shimo alilokuwemo kijana Ambe yalimzindua kutokana na kutereza na kudondokea humo wakati wakiwakimbia askari magereza na kupoteza fahamu. Ilikuwa katika jaribio la kutoroka kwa bahati mbaya aliangukia kwenye shimo.
Rafiki ya Aloys Mabina hakutaka kumwacha alijitahidi kumwamsha ili amtoe shimoni, lakini aligundua amepoteza fahamu hivyo asingeweza kuendelea kuwepo eneo lile kwa kuhofia askari wanaowatafutakumkuta eneo lile.
Aliona kama angeendelea kuwepo pale lazima askari wanao wakimbiza wangefika eneo lile na kumkamata. Hivyo aliendelea na safari kuwakimbia na kumwacha rafiki yake ndani ya shimo.
Ambe baada ya kuzinduka taratibu alijitoa kwenye shimo huku mvua ikiendelea kupiga kwa kasi, shimo halikuwa refu sana hiyo ilimsaidia kutoka nje kwa urahisi. Alijikuta akiwa njia panda na kushindwa afanye nini arudi gerezani au aendelee kukimbia.
Wazo la kurudi lilimtisha kidogo kutokana kuogopa kuulizwa juu ya mwenzake Mabina aliyekuwa swahibu wake mkubwa gerezani. Walikuwa wamefanya tukio baya la kutoroka na siraha baada ya kumkaba askari magereza na kukimbia na bunduki ambayo ilikuwa inakwenda kutimiza azima ya rafiki yake Mabina ya kuua ili kutimiza kisasi.
Ambe na Mabina walikuwa na matukio ya kufanana yaliyowafanya waingie gerezani na kila mmoja kufungwa miaka saba. Lakini kila mmoja alikuwa na njia yake iliyomwingiza gerezani Mabina aliapa akitoka lazima alipe kisasi kwa kuwaua wabaya wake na ndiyo sababu ya kutoroka na siraha.
Lakini ilikuwa tofauti kwa Ambe, pamoja na kufanyiwa unyama mkubwa lakini aliapa hata lipiza zaidi ya kumuachia Mungu. Mabina hakuwa hivyo hakutaka kabisa kusikia eti mtu anakutendea unyama unamshtakia Mungu wakati una uwezo wa kulipa kisasi.
Baada ya kumweleza rafiki yake sababu iliyomwingiza gerezani ambayo ilikuwa ni uonevu aliapa akitoka lazima aue tena kwa risasi. Ambe pamoja na kumsihi rafiki yake asilipe kisasi hakusikilizwa. Mabina alisema toka alipofanyiwa unyama ule na mwisho wa yote kufungwa bila kosa miaka saba. Asinge msamehe mtu aliapa lazima atalipa kisasi tena cha damu.
Ambe akiwa anatoka kwenye shimo huku mvua ikiendelea kumnyeshea. Moyoni alijikuta akijilaumu maamuzi wa rafiki yake wa kumpiga askari na kuichua bunduki ambayo alimwambia ndiyo siraha aliyoitafuta kwa muda mrefu.
Katika muda wote waliokuwa gerezani Mabina aliapa akitoka gerezani lazima aue ili anyonge na kuamini kile ndicho kitakuwa kifungo cha kweli kwake. Matatizo ya rafiki yake hayakuwa na tofauti na yake ya kutendewa unyama na familia ya rafiki yake wa kike na mwisho wa yote kufungwa gerezani miaka saba bila kosa lolote kisa mapenzi.
Tofauti ya kuingia gerezani kwa Ambe na Mabina ilitofautiana, Mabina alitangulia kuingia kwa mwezi mmoja hivyo hata muda wao wa kutoka ungepishana kwa mwezi mmoja.
Ambe akiwa bado yupo njia panda aelekee wapi kwa vile pori lile lilikuwa geni kwake japokuwa hakutaka kurudi gerezani. Alikumbuka kauli za rafiki yake baada ya kumsimulia mkasa uliomwingiza gerezani:
“Ambe nakuhakikishi siwezi kuwasamehe wote walionifanyia unyama, hawezi kutudhurumu mali yetu, wamuue baba yangu na mimi kufungwa miaka saba bila kosa kisa tu nilikuwa nikijua mengi juu ya ugomvi wa baba na jirani yake juu ya mpaka wa nyumba.
“Najua sina uwezo wa kipesa, lakini lazima nimuue kwa risasi kama alivyomuua baba yangu.”
“Atapata wapi bunduki?” Ambe alimuuliza rafiki yake.
“Hapa hapa gerezani.” Mabina alijibu kwa kujiamini.
“Hapa hapa gerezani! Utaipata vipi?” Ambe alishtuka.
“Utaona tu.”
Siku ilipofika walikuwa kwenye kazi za nje kutokana na kubakiza muda mchache wa kuwepo gerezani. Wafungwa wengi walipewa kazi za nje, yeye akiwa amebakiza miezi miwili na Mabina mwezi mmoja wa kutoka gerezani. Wakiwa eneo lililojificha walilopangiwa Ambe na Mabina kukate miti huku askari magereza akiwa mbali kidogo.
Mabina alimwambia Ambe amwite askari kwa sauti ya juu, naye alifanya hivyo kwa kupaza sauti kumwita askari. Askari alifika haraka eneo aliloitiwa alipofika alishangaa kumuona Mabina akigaagaa chini kama mtu aliyekuwa akiumwa kitu. alipomuuliza Ambe ambaye hakuwa na jibu. Alipomwinamia ili kutaka kujua anaumwa nini, Mabina alinyanyuka na kukaba askari huku Ambe akishangaa. Baada ya kumkaba mpaka kupoteza fahamu alichukua bunduki na kumlazimisha Ambe waondoke.
“Twende wapi?” Ambe aliuliza.
“Ukibaki shauri yako utaulizwa nimekwenda wapi, najua hautakuwa na jibu kwa vile sisi ni marafiki wakubwa watajua nawe unahusika hivyo itaozea gerezani.”
Ambe alijikuta akimfuata Mabina aliyeanza kukimbia kuingia porini, kwa vile hakuwa amejiandaa baada ya mwendo wa masaa matatu bila kupumzika pumzi ilikata na kujikuta akianza kuona kizunguzungu kwa bahati mbaya pembeni na sehemu aliyokuwa amesimama kulikuwa na shimo aliangukia ndani.
Mabina alijaribu kumsaidia kumtoa shimoni lakini aligundua amepoteza fahamu hakuwa na jinsi zaidi ya kumwacha ili asije kukamatwa na askari watakao kuwa wakimtafuta. Baada ya saa saba kupita mvua zilianza kunyesha, maji ya mvua yaliyokuwa yakiingia shimoni ndiyo yaliyomzindua Ambe.
Muda aliotoka shimoni ilikuwa saa usiku kiza kilianza kuimeza nuru ya mchana. Alikumbuka maneno ya Mabina kuwa kama atakamatwa atafia gerezani, aliamua kuendelea na safari yake japo hakujua anaelekea sehemu gani. Wakati huo mvua ilikuwa akiendelea kunyesha, alijiona ni kiumbe kilichoandamwa na mikosi baada ya kunyang’anywa mchumba wake na kuozwa mtu mwingine bila idhini yake bado ameishia kufungwa gerezani.
Akiamini baada ya miezi miwili atakuwa uraiani na kuuapia moyo wake pamoja na yote aliyotendewa aliusihi moyo wake usilipe kisasi. Lakini mtu aliyemtegemea kuwa rafiki na msiri wake, mwisho wa siku amemwingiza kwenye matatizo makubwa ya kutafutwa na serikali kwa makosa matatu kuua kutoroka gerezani na wizi wa siraha.
Moyo ulimuuma na kutani kulia, alijiuliza pale alipo atatokea wapi na atawezaje kuikwepa serikali ambayo ina mkono mrefu. Alijua kama rafiki yake Mabina atatimiza adhima yake ya kuua na kunyongwa atakuwa ametimiza ametimiza kile alichokipanga kwa muda mrefu.
Lakini kwa upande wake, baada ya kufungo alipanga kuishi maisha mapya.
Alizidi kutembea kuingia ndani ya msitu ambao kwa upande wake ulikuwa mgeni kwake. Ghafla alijikuta akipata wazo la kijasiri la kurudi gerezani kuwaeleza ukweli kuwa si yeye bali rafiki yake ambaye wamejuana gerezani tu.
Baada ya kutembea kwa hatua kama kumi alishangaa kuona mianga ya tochi zaidi ya nne ikisogea sehemu aliyokuwepo. Wasiwasi ulimjaa na kushindwa kuelewa wale ni kina nani na mbona kama watu wanaotafuta kitu. Mwanga ulipokuwa unakimkaribia aliamua kujificha kwa kupanda juu ya mti uliokuwa karibu.
Alitulia juu ya mti ili watu wale wapite kwa kuhofia huenda ni askari waliokuwa wakiwatafuta. Watu wale walipofika chini ya mti ule aligundua kweli walikuwa askari magereza ambao walionesha walipita kitambo kuwatafuta na kumpita alipokuwa ameangukia kwenye shimo na kupoteza fahamu.
Aliwasikia wakizungumza:
“Tumefanya kazi ya ziada bila hivyo tungekufa wote.”
“Lakini katutia hasara kifo cha mtu mmoja hakilingani na askari wetu wawili.”
“Lakini rafiki yake ndiye anaonekana amekimbia na siraha lazima tumsake kwa udi na uvumba.”
Maneno yale kidogo yamfanya Ambe aanguke juu ya mti aliokuwa amepanda, aliamini kabisa rafiki yake kipenzi Mabina ameuawa na kuwaua askari magereza wawili. Kilichomshangaza ni kauli yao kuhusu kutoonekana kwa bunduki aliyochukua Mabina. Ile ilimshtua kidogo na kujiuliza rafiki yake atakuwa ameificha wapi.
Kauli ya kwanza anatafutwa yeye ambaye ndiye anayesadikiwa ameficha siraha ilimvunja nguvu sana na kuamini kama atarudi gerezani basi atakuwa amejiingiza mwenyewe kwenye kinywa mamba.
Alitulia juu ya mti akimuomba Mungu amuepushie mbali balaa lile, askari wale walichelewa chini ya mti ule kutokana na mmoja kujisaidia haja ndogo, baada ya kumaliza aliendelea na safari yao. Twambe hakuteremka mpaka ya nusu saa na kuona hakuna haja ya kwenda kujisalimisha baada ya kuonekana kuwa ndiye aliyeficha siraha hivyo wasinge muelewa.
Kila lililokuwa mbele yake aliona ni mtihani mzito ambao kwake aliamini haukuwa na jibu la mara moja. Muda ulikuwa umekwenda na kiza kilikuwa kimeingia ambacho hakikuwa kikali sana, mwezi ulikuwa umemezwa kidogo na mawingu. Hali ile ilimfanya aone kidogo sehemu aliyokuwa akienda.
Alitembea kuelekea mbele bila kujua anakwenda wapi kutokana na eneo lote kuwa mbuga yenye miti mingi. Kwa vile hakuwa na saa hakuja muda ule ilikuwa saa ngapi , alipata ujasiri na kuamua kusonga mbele na kuwa tayari kwa lolote kwa kuamini hakufanya jambo lolote baya na Mungu angemsaidia.
Alitembea asiku kucha na kujikuta akichoka sana kutokana na kutembea kwenye baridi kali kutokana na mvua kunyesha sehemu kubwa. Sehemu moja aliyokuwa na bonde alisikia watu wakizungumza:
“Sasa jamani tutakaa mpaka saa ngapi tukitafuta mtu tusiyejua amekimbilia wapi?” Ilikuwa kauli iliyoonesha kumbe askari wengi walikuwa wamesambaa eneo kubwa la pori lile kumtafuta.
“Hivi angalie tumeisha poteza watu wawili kwa mtu asiye na siraha sasa mwenye siraha si tutakufa wote. Kama mtu ametoroka alitakiwa atafutwe kwa njia nyingine,” alimsikia askari mwingine akizungumza.
Ambe alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kugundua anatafutwa kila kona na kama atakamatwa atakufa kwa kipigo kutoka kwa askari wenye hasira hasa baada ya kuuawa askari wawili kutokana na maelezo yao. Alijiuliza kote alipopita huenda aliwapita wengine ambao walikuwa wamepitiwa na usingizi hivyo kupita bila kumuona.
Kauli za wale askari ilionesha wameisha kata tamaa wapo pale kwa kutimia wajibu lakini aliamini hawezi kumuoa. Aliachana na njia iliyokuwa na sauti ya askari na kuanza kuifuata iliyokuwa ikielekea bondeni ambako kulikuwa kunatisha sana.

Itaendelea Ijumaa
 
HADITHI: .. JOTO LA MAPENZI
SEHEMU: 02
MTUNZI: Ally Mbetu ‘DrAmbe’
SIMU: 0713 646500

ILIPOISHIA:
Kauli za wale askari ilionesha wameisha kata tamaa wapo pale kwa kutimia wajibu lakini aliamini hawezi kumuoa. Aliachana na njia iliyokuwa na sauti ya askari na kuanza kuifuata iliyokuwa ikielekea bondeni ambako kulikuwa kunatisha sana.
SASA ENDELEA...

Lakini kwa ujasiri mkubwa aliteremka hadi bondeni ambako alikutana na mto uliokuwa ukipitisha maji. Alihofia kuvuka kwa kuingia kwa vile hakujua kina cha maji yale. Aliamua kutembea pembeni ya mto huku akizidi kupigwa na baridi kali la usiku ule, moyoni alijiuliza nini hasa chanzo cha yeye kuingia kwenye matatizo mazito kila kukicha.
Lakini alijipa moyo kwa kuamini si yeye wa kwanza kutokewa na matatizo kama yale. Pia aliamini mwanadamu hasa mwanaume ameumbwa ili kukabiliana na matatizo. Hata kama angelia machozi ya damu hakuna ambaye angemuelewa au angemsaidia.
Aliendelea kutembea huku akiwa makini akisikiliza sauti au kitu chochote kitakacho hatarisha maisha yake. Kwa mara ya kwanza alijifananisha na gaidi lililotoroka kwenye gereza la Guantanamo. Alijipa moyo ili kuhakikisha anayalinda maisha yake kwa hali yoyote ile na hakuwa tayari kukamatwa kikondoo.
Aliyakumbuka mafunzo aliyochukua JKT wakati akimaliza kidato cha sita, aliamini kabisa mafunzo yale muda ule ndiyo yatakayo msaidia.
Alivunja kipande cha mti na kukigeuza kama siraha kwa kitu chochote kitakacho mtokea mbele.
Kila hatua aliyopiga kwenda mbele ndivyo ujasiri ulivyojaa moyoni mwake. Kutokana na kutembea ambali mrefu kiu kikali kilimshika na kujikuta hana jinsi zaidi ya kunywa maji yale ya mto bila kujua yapo katika usalama gani.
Baada ya mwendo wa saa nzima alijikuta akitokea kwenye njia ya kuvukia upande wa pili iliyokuwa na daraja la mti mmoja.
Alivuka na kuendelea na safari yake ya kuwakimbia askari Magereza, kabla hajachanganya miguu baada ya kuvuka daraja alisikia mtu akimuamsha mwenzake.
“Saidi...Saidi.”
“Nini Joe? Wewe hebu niache nilale.”
“Nimesikia kama sauti ya miguu ya mtu anapita.”
“Sasa akipita sisi anatuhusu nini?”
Kauli ile ilimfanya Ambe ajifiche nyuma ya kichaka kidogo huku akishikilia sawasawa kipande chake cha mti na kuwa tayari kupambana na yeyote atakayejitokeza mbele yake. Aliamini kama atalegea naye kifo chake kitakuwa kama cha rafiki yake Mabina.
Hakuwa tayari kufa kikondoo kwa kujua akikamatwa hata akijitetea vipi hawatamwelewa kwa vile Mabina hakukutwa na siraha, lazima wangemtesa ili atoe siraha asiyoijua ipo wapi, hivyo angeweza kupewa kilema cha maisha au kuuawa kifo cha mateso makali.
Akiwa ameshikilia siraha yake tayari kupambana na atakaye kuja mbele yake, aliendelea kusikia mazungumzo ambazo alijua kabisa za askari waliotumwa kumsaka.
“Kwa hapa tunafanya nini?” Mmoja aliuliza.
“Tumekuja kumsaka Ambe baada ya Mabina aliyemkaba John na kutoroka na siraha pamoja na rafiki yake, ambaye ndiye aliyekimbia na siraha.”
“Sasa kwa nini tusifuatilie hizo sauti za miguu?”
“Wewe hujipendi, Mabina hakuwa na siraha kaua wawili huyo Ambe mwenye siraha si atatuua wote. Inaonesha wazi jamaa wale ni wazoefu kutumia siraha za moto.”
“Lakini kweli, sasa tufanyeje?”
“Kwa vile hatujamsumbua hata kama ni yeye wee tulale ili kesho tuwaeleze tumemkosa. Sisi tunateseka mvua yetu baridi ya usiku mzima yetu, wakubwa wamekumbatia wake zao. Mimi hata nikikutana naye namwambia pita baba sina ubaya na wewe.”
Kauli ile japo ilitaka kumchekesha Ambe lakini aliamini kila kiumbe kinapenda kuishi maisha marefu. Hakutaka kukubaliana na kauli yao kwa kujiamini kutembea kifua mbele. Aliamua kutembelea magoti kwenye nyasi zilizokuwa na majimaji kutokana na mvua iliyokuwa amekatika muda si mrefu kuondoka eneo lile ambalo lililonyesha huenda ndipo ulikuwa mpaka wa magereza na sehemu za wananchi wa kawaida.
Alitembea kwa magoti kwa mwendo wa dakika kumi kisha alinyanyuka na kuendelea na safari yake. Sehemu aliyoingia ilionesha wazi ni eneo tofauti na magereza kulikuwa na mashamba ya watu. Kutokana na eneo la mashamba kuwa dogo tofauti na mashamba ya magereza yenye eneo lake ni kubwa sana.
Baada ya kutembea mwendo wa dakika ishrini alianza kuona kwa mbali nyumba moja moja zilizo mbali mbali. Wakati huo mwezi ulianza kumezwa na mawingu kuonesha muda umekwenda sana. Kibaridi cha kukaribisha alfajiri kilimpuliza na kuonesha kumekaribia kupambazuka.
Japokuwa hakujua hatima yake lakini moyo wake ilipata faraja kuona nyumba za watu. Wakati akianza kuyaacha mashamba na kusogelea nyumba moja iliyokuwa karibu naye. Kutokana na kiza kilichokuwa kimetokea kwa ajili ya mwezi kumezwa na mawingu.
Hakuweza kuona anapita sehemu gani kwa kukanyaga majani ya pembeni ya shamba. Bila kujua anapita wapi alijikuta akikanyaga mwiba uliomtoboa vibaya na kumfanya ahisi maumivu makali. Alichechemea kutoka kwenye miba ambayo ilionesha ilipandwa kwenye mpaka wa shamba na kuingia kwenye barabara.
Alikaa chini ili kuutoa mwiba aliokuwa umemuingia sana mguuni kwa ajasiri mkubwa huku akiuma meno aliutoa na kufanya atokwe na damu nyingi.
Ilibidi achane chati lake na kujifunga kwenye jeraha ili kupunguza damu isitoke kwa wingi.
Alitumia kipande cha mti alichokitumia kama siraha, kama nyenzo ya kumsaidia kutembelea kutokana na kuwa na maumivu makali ya mguu. Alijikongoja kuelekea kwenye makazi ya watu huku akimuomba Mungu askari wasitokee kwani wangemuokota kwa ulaini kwa maiti ndani ya maji. Baada ya mwendo mfupi wa shida alitokea sehemu iliyokuwa na nyumba mbili zilizoezekwa na nyasi.
Kila hatua aliyojitahidi kupiga ili kuingia eneo lile hali ilizidi kuwa mbaya, maumivu ya mguu yalizidi kuwa makali sana na kumfanya ashindwe kutembea. Lakini alijitahidi kuingia eneo la nyumba ile ili hata akizidiwa apate huduma. Kizunguzungu kilikuwa kikali kutokana na njaa, uchovu na maumivu ya mguu alianguka chini na kupoteza fahamu.
*****
Ambe aliposhtuka alijikuta amelala kwenye kitanda cha kamba katika chumba chenye mwanga hafifu. Akiwa anajiuliza pale ni wapi alisikia sauti ya watu wakibisha hodi kwenye nyumba ile.
“Karibuni,” sauti kutoka mule ndani ilikaribisha.
“Shikamoo babu.”
“Marahaba, niwasaidie nini mjukuu wangu?”
“Tunaomba kuuliza, hujamuona mtu mwenye mavazi ka kifungwa akipita eneo hili?”
Kauli ile ilimshtua Ambe aliyekuwa bado amejilaza kwenye kitanda cha kamba na kujua amekwisha baada ya askari kutokata tamaa ya kumtafuta na kuamua kuingia vijiji vya karibu na gereza kumtafuta. Moyo ilimwenda mbio na kujua amekwisha lazima babu atasema ukweli kuwa yumo ndani.
“Mmh! Ametoroka lini?”
“Jana mchana.”
“Sasa toka jana mchana leo ndio mje kumtafuta huku? Hamuoni ni mzembe, jana yote mlikuwa wapi?”
“Mzee hatukuja kuulizwa maswali tueleze umemuona au la,” sauti la askari magereza ilikuwa kali.
“Si kazi yangu kuangalia watu wanaopita kijijini, sijamuona.”
Ambe hakuamini majibu ya mwenyeji wa nyumba ile kukataa hajamuona, alijiuliza kwa nini hakuwaeleza ukweli. Aliendelea kumuomba Mungu amwepushe na balaa lile zito ambalo aliamini kama ataangukia mikononi kwa chombo cha dola basi jina lake litabakia historia midomoni mwa watu.
Baada ya muda mwenyeji wake alirudi ndani na kusegea kwenye kitanda alichokuwa amelala.
“Kijana..Kijana.”
“Naam babu,” Twambe aliitikia bila kujua mwenyeji wake ana umri gani japo alisikia akiitwa babu na askari magereza.
“Umeamka?”
“Ndiyo babu.”
“Ni kweli wanakutafuta wewe?”
“Ndiyo babu,” Twambe aliogopa kumdanganya.
“Siwezi kukuhukumu lolote zaidi ya kukusaidia kwanza ndipo tuzungumze, pia siwezi kukurudisha gerezani ukitoka hapa maisha yako utayajua mwenyewe.”
“Asante babu, ila nahisi nina mikosi mingi sana, kila siku mpya kwangu imeandamwa na mikosi, dhuruma uonevu ndivyo vilivyotawala maisha yangu. Nina imani nikikamatwa naweza hata kunyongwa bila kosa,” Ambe alisema kwa uchungu.
“Inaonesha una mengi moyoni mwako ndiyo yaliyonisukuma kubeba jukumu la kuwaficha askari ili nipata kitu chochote kitakachoweza kunisaidia.”

Itaendelea Jumatatu
 
HADITHI: .. JOTO LA MAPENZI
SEHEMU: 04
MTUNZI: Ally Mbetu ‘DrAmbe’
SIMU: 0713 646500

ILIPOISHIA:
“Na familia yako?”
“Hiyo niachie mimi.”
“Je, wakikataa?”
“Waliisha kataa, lakini sasa nimeamua mwenyewe sitaki kuingiliwa maamuzi yangu na mtu.”
SASA ENDELEA...

“Ambe sasa harusi yetu haitakuwa na furaha kama tutakosa baraka za upande wa pili?”
“Baraka si muhimu kama maisha yako, siwezi kukupoteza kwa ubinafsi wa roho za watu, nilikuahidi kifo ndicho kitakachotunganisha na si kiumbe chochote.”
“Mmh! Sawa, kwa hiyo?”
“Nenda nyumbani kawaeleze nimekubali kubadili dini.”
“Nashukuru mpenzi wangu kwa kuyajali maisha yangu,” Koleta alinikumbatia kwa furaha.
“Basi mpenzi nikurudishe kwenu muda umekwenda sana.”
Nilimsindikiza hadi kwao na mimi kurudi kulala, usiku ulikuwa mrefu kuliko kawaida baada ya kuwa katika mtihani mzito juu ya uamuzi wangu wa ghafla wa kukubali kubadili dini kitu ambacho wazazi wangu walinieleza kama nataka radhi yao basi nibadili dini.
Kwa upande wangu niliamini kabisa dini ni kama taasisi ambayo ipo kwa ajili ya kumfanya mtu amjue Mungu pia kuyafuata yote mema na kuyaacha yote mabaya aliyoyakataza. Moyoni niliamini hata hiyo radhi yao itakuwa haina nguvu kwa vile nilijitolea kwa ajili ya kuokoa maisha ya mtu aliyenipenda mapenzi ya dhati.
Niliamini kutafuta ushauri kwa marafiki ingenichanganya kwa vile nilikuwa tayari nimeisha toa uamuzi, kilichotakiwa ni utekelezaji na si kupokea ushauri tena. Toka awali nilipata vikwazo toka kwa watu wa karibu pale nilipowaeleza uamuzi wangu wa kutaka kubadili dini ili nisimpoteze Koleta.
***
Siku ya pili nikiwa sebuleni baada kumaliza kupata kifungua kinywa, nilishtushwa na sauti ya mtu akibisha hodi. Sauti haikuwa ngeni masikioni mwangu, ilikuwa ya mpenzi wangu Koleta, nilishangaa kubisha hodi siku ile kwani siku zote alikuwa akiingia ndani bila hodi. Nilijua ule ulikuwa wivu wa kimapenzi kwa kuamini akiingia bila hodi anaweza kufumania.
“Karibu,” nilikaribisha bila kunyanyuka kwenye kochi kwa kujua mlango upo wazi.
“Hodi tena,” sauti ya Koleta ilisema.
“Karibu mpenzi.”
Baada ya muda aliingia Koleta akiwa ameongozana na mama yake mzazi nilishtuka na kujikuta nikishindwa kunyanyuka na kubakia nimekaa baada ya kunikuta kifua wazi.
“Karibu mama,” nilimkaribisha.
”Asante, mwanangu, samahani kwa kukuvamia.”
“Ha..ha..kuna tatizo,” niliingiwa mchecheto.
Wakati huo Koleta alipitiliza chumbani na kurudi na fulana na kunipa.
“Ambe hebu vaa fulana uzungumze na mkweo.”
Baada ya kuvaa nilimgeukia mama mkwe ambaye hakuwahi kufika kwangu toka nianze uhusiano na Koleta. Kwangu ulikuwa ugeni mzito, baada ya kimya kifupi mama Koleta aliniita.
“Baba.”
“Naam mama.”
“Najua utaushangaa ugeni huu?”
“Ni kweli mama,”nilijibu kwa unyenyekevu.
“Nina imani unajua kuna kitu gani kilichopa kati yetu juu ya uhusiano wenu?”
“Ndiyo.”
“Kwa kweli siku zote nilikuwa upande wetu kwa uamuzi wowote ambao mngeamua wewe kumfuata mwenzako au mwenzako kukufuata wewe. Mimi kwangu niliona sawa tu, lakini familia yako na baba yenu walijikuta wakiweka ligi ambayo kwangu sikuona kuna umuhimu wa kutunishiana misuli kwa jambo la maelewano.
“Siamini kati na mkristo na muislamu nani yupo sawa au aliye na uhakika kuwa ndiye yupo sahihi mbele ya Mungu. Nina amini sote tuna muabudu Mungu huyo huyo. Kwa kweli ushindani ule ulinikosesha raha hasa baada Koleta kuniapia kama atakukosa basi atajiua.
“Mwanangu, nilichanganyikiwa kila siku nilimuomba Mungu huku nikiamini ni yeye peke yake aliyekuwa na uwezo wa kuokoa uhai wa mwanangu. Taarifa zingine zilizonichanganya zilikuwa kuwa umepata mchumba mwingine tofauti na Koleta. Hapo ndipo nilipokuwa nikihesabu siku za kuishi mwanangu kwa kuamini lazima atafanya alichodhamilia cha kujitoa uhai wake.
“Huwezi kuamini taarifa zile zilinifanya nikuchukie hata kuuapia moyo wangu kulipa kisasi kama utaoa na mwanangu kuchukua jukumu la kujiua. Lakini jana usiku nikiwa nimelala niligongewa mlango, kwanza moyo ulinilipuka nikijua Koleta ameisha fanya ujinga wake.
“Nilipofungua nilikutana naye akiwa katika sura nyingine tofauti na niliyoizoea, siku zote nilizoea kuona sura ya hudhuni iliyoambatana na machozi. Lakini jana usiku uso wa mwanangu ulikuwa na tabasamu ambalo ndilo nililozoea kuliona katika uso wake.
“Nilitaka kujua kulikoni kuwa katika hali ile, kitu alichonieleza kilinichanganya sana sikuamini niliamini alikuwa akiota. Lakini alinihakikishia kuwa umetamka mwenyewe kwa mdomo wako kuwa upo tayari kubadili dini na kumuoa Koleta. “Taarifa hizi nilimfikishia baba yenu ambaye kwanza alitaka kudharau lakini nilimuhakikishia kama kweli umekubali kubadili dini ili umuoe mtoto wetu bado anaweka vikwazo vya kijinga. Nilimueleza kama Koleta atapoteza uhai baada ya kupatikana suluhu, maiti ya mwanangu ataila nyama.
“Ulikuwa ugomvi mzito ambao ulihama kwa mwanangu na kuhamia kwangu na kujifunga kibwebwe, nilikuwa tayari kwa lolote hata kuachika lakini kuokoa uhai wa mwanangu. Hajui nilivyoteseka kwa mtoto huyu leo afanye ujinga kwa sababu zisizo na msingi eti ukiisha muoa utarudi kwenye dini yako, kwani hata ukirudi kwenye dini yako tutapungukiwa nini?
“Baada ya mshike mshike wa karibia nusu saa chumba kikiwaka moto, alikubaliana na mimi na kunituma nije nipate ukweli wa kauli yako ya kukubali kubadili dini. Je , ni kweli umekubali kubadili dini?” aliniuliza akiwa amenikazia macho.
“Ndiyo mama, nampenda sana Koleta siwezi kumpoteza kwa sababu ya dini,” nilimjibu kwa utulivu kuonesha sitanii.
“Asante sana mwanangu kuokoa maisha ya kipenzi mwanangu,”majibu yangu yalimfanya mama Koleta kunyanyuka na kuja kunikumbatia.
Baada ya kukaa aliniuliza swali.
“Sasa katika familia yako uamuzi wako wameupokeaje?”
“Mama siku zote kila aliaye ushika kichwa chake, nami nimeshika changu. Uamuzi huu ni wangu wala sitamshirikisha mtu yeyote.”
“Je, wakikataa?”
“Maumivu ya moyo wangu hakuna wa kuyabeba kama nitampoteza Koleta kwa kitu cha kuamua mara moja.”
“Je, harusi itakuwaje, kama familia yako itasusa.”
“Najua itasusa lakini msimamo wangu utabakia pale pale, siwezi kumpoteza Koleta kwa habari za kusadikika, nani aliyewaambia Mungu ni wa dini fulani?” nilijijaza ujinga.
“Hilo nimekuelewa, pia baba yako amenituma kwa vile leo kanisani kwetu kuna ibada ya jioni, alitaka leo utambulishwe kwa waumini ili ukaribishwe rasmi katika dini yetu.”
“Hilo halina tatizo, nipo tayari.”
“Basi mwenzako atakufuata na gari kukuchukua.”
“Hakuna tatizo mtanikuta nimejiandaa.”
“Ambe nakuhakikishia kuyabadili maisha utakapo funga ndoa na mwanangu,” Mama Koleta aliniahidi kwa kinywa chake.
“Tumuombe mambo yaende yalivyopangwa.”
Waliniaga huku Koleta akionesha furaha ya ajabu kutokana kauli yangu mbele ya mama yake. Kabla ya kuondoka nilinifuata na kuninong’oneza:
“Ambe asante mpenzi, yaani mpaka nafika hapa nilikuwa siamini kama utaweza kuyasema ulioyosema jana mbele ya mama yangu. Nilijua ulinitoa kisiasa lakini kauli haikuwa toka moyoni mwako. Lakini ulipokubali mbele ya mama nimeamini kweli unanipenda.”
“Koleta ni wewe ndiye uliyenifanya niwe jasiri na kutoa uamuzi huu.”
“Asante mpenzi wangu nitakupenda mpaka mwisho wa pumzi zangu.”
Koleta alinipiga busu na kumuwahi mama yake aliyekuwa ametangulia nje.
****
Baada ya kuondoka nilijiandaa kwenda nyumbani kuwaeleza uamuzi wangu wa kubadili dini, kwanza walishtuka na kuniomba nirudie baada ya kunisikia bila hawakunielewa.
“Unasema?” Mama aliniuliza.
“Nimeamua kubadili dini ili nimuoe Koleta.”
“Wee mtoto umelogwa, unataka kubadili dini kwa ajili ya mwanamke sijawahi kuona, naomba ufute wazo hilo,” mama alikuja juu.
“Mama nisipofanya hivyo nitampoteza Koleta.”
“Huwezi kuzuia kifo chake bali Mungu, hebu acha kutuchefua.”
“Mama uamuzi wangu ni huo, nimekuja hapa kukuelezea uamuzi wangu kuwa ninabadili dini na muda wowote nitafunga ndoa na Koleta.”
“Hiyo ndoa yako utaifanya peke yako, nakuapia kama kweli utabadili dini basi utafute wazazi na ndugu zako, lakini kwetu utakuwa umejivua.”
“Msimamo wangu ni uko pale pale hata nitengwe na dunia nzima lakini siwezi kumpoteza Koleta kama amejitoa kwangu lazima na mimi nijitoe kwake.”
“Wee mtoto kwa nini ututie aibu, kumbuka baba yako kakutafutia mwanamke na mipango inakwenda vizuri.”
“Huyo mnayemtafuta ni wenu lakini wangu ni Koleta,” kwa mara ya kwanza nilikosa heshima kwa kipenzi mama yangu.
“Hebu nenda kajiulize tena nipo chini ya miguu yako usifanye hivyo ni aibu mwanaume kumfuata mwanamke tena ukiwa mtoto wa kiislamu.”
Pamoja na yote aliyozungumza mama sikuwa na chochote cha kukibadilisha kwenye akili yangu. Niliondoka na kurudi kwangu, nakumbuka siku hiyo ndiyo ilikuwa ya kutambulishwa kanisani kwa kumtambua Yesu ndiye Bwana na mukozi wa maisha yangu.

Itaendelea Jumatatu
 
Safi sana...

Ngoja tuone kamaa jamaa atafanikiwa kudalisha dini, na kama kweli ndoa itafungwa...

Cc: mahondaw
 
Hii story imekufilia wpi jomoni
 
Back
Top Bottom