JIMAMA LA SUPU YA PWEZA-12
ILIPOISHIA
Mh! huyu mama mi simuelewi, hivi
vitu anakwendaga navyo wapi?
SASA ENDELEA
TOA na vile vitabu pale
anavyosomaga baba, vitoe kumi na
tano.
Jema alitii lakini alikuwa hajijui
kiakili, aliamini kwamba kuna
biashara anayofanya huyo
mwanamke lakini anashindwa
kusema kwa uwazi.
Mama kwani unakwenda wapi?
Wewe maswali ya nini sasa?
Basi mama, nisamehe.
Weka na
aaa
naaa
weka na ngoja
nikachukue mwenyewe kibegi chake
anapendaga kubebea vikaratasi
vidogo vidogo.
Mama Sabinamu mwenyewe
alizama ndani, alipotoka alibeba
kibegi hadi nje, wakaweka vitu vyote
hapo
Unachukua Bajaj? aliuliza Jema
Ndiyo! He! Nimesahau, nenda
chumbani ukaniletee kadi ya
kununulia luku na ile
tunayonunuliaga muda wa
kingamuzi.
Ile yenye rangi rangi?
Ndiyo.
Jema aliingia ndani, aliporudi na vitu
hivyo alikuta dereva Bajaj
ameshapakia mizigo yote alikuwa
anasubiriwa yeye tu.
Haya, hakikisha geti halikai wazi,
sawa?
Sawa mama.
Wapi mama? suka alimuuliza
mwanamke huyo.
Mwananyamala.
Bajaj ilitoka kasi, ikakata kona na
kutokea barabarani, ikaingia
kwingine mwishowe ikafika
Mwananyamala, tena nje ya gesti
hiyo.
Alisaidiwa na dereva kuvipakua vitu
vyote
Mama unahamia hapa gesti au kwa
muda tu? suka alimuuliza.
Hayakuhusu, tena hayakuhusu
kabisa.
Nisamehe sana anti.
Tena ukome.
Ukimya ulitawala, baada ya mizigo
yote kushushwa na kuingizwa ndani,
mama Sabinamu alimpigia simu
Sudi.
Uje hapa jirani na kituo cha daladala
cha Komakoma, nitakuelekeza
nilipo.
Sawa, sasa hivi?
Ndiyo, unataka uue usiku?
Nakuja mama nakuja.
Umekunywa supu ya pweza lakini?
mama Sabinamu aliuliza kama kwa
utani huku akiachia kicheko cha
nguvu. Ikabidi na Sudi naye kucheka
sana
Nimekunywa, alisema Sudi huku
kicheko kikiendelea.
Palepale aliwasha pikipiki yake,
lakini kabla hajaondoka, wenzake
walimuuliza anakokwenda
Nakwenda kwa jimama.
Lipi? aliuliza yule kijana aliyelala
na mwanamke huyo mara mbili
kwenye gesti hiyo
La supu ya pweza.
La supu ya pweza? Ndiyo lipi hilo?
Iko siku utalijua.
Baada ya Sudi kuondoka, yule kijana
alihisi jimama la supu ya pweza
linaweza kuwa jimama lake pia.
Akampigia simu
Mama vipi?
Salama, hujambo kijana wangu?
Sijambo mama, uko wapi?
Leo siyo zamu yako, nitakutafuta
kesho.
Si nimekuuliza ulipo lakini mama!
Nimesema leo siyo zamu yako
kijana wangu, nitakutafuta.
Sawa, maana leo nilikunywa mchuzi
mmoja hivi, haufai mama.
Mchuzi wa samaki? Maana ndiyo
una shombo sana.
Hapana, wa pweza.
Wa pweza?
Ndiyo, wa pweza. Basi daaa! Mwili
wote unasisimka, natamani kama
tungekuwa kitandani. Na kama
ingekuwa hivyo leo ingekuwa asubuhi
mpaka jioni, acha kabisa
maana
ningekubinua, ningekupindua,
ningekubeba mpaka ungesema basi.
Mh! We kijana, kweli?
Khaa! Unajua nilipeleka wateja pale
Shekilango, kwa pembeni karibu na
kituo ndiyo nikaona supu ya pweza,
si nikanywa, weee!
Kwa hiyo hapo ungekuwa na mimi
ningekoma leo?
Usingekoma, ningekukomesha.
Mama Sabinamu alijikuta akisisimka
mwili kwa maneno ya kijana huyo
kiasi kwamba aliamini Sudi hana
kitu, kwanza wala hajanywa supu ya
pweza
Huyu wala sijamuuliza kasema
mwenyewe, yule mpaka
nimemuuliza, itakuwa kweli, aliwaza
mwanamke huyo huku akiendelea
kuongea na kijana huyo.
Hebu subiri, nipe dakika sifuri
nakupigia sasa hivi.
Sawa mama.
Baada ya kuzungumza na kijana
huyo, mama Sabinamu alimtwangia
Sudi
Mama nimekaribia.
Subiri wewe, achana na kukaribia
kwanza. Hivi umekunywa supu kweli
au maneno tu?
Nimekunywa mama.
Utaniweza?
Aaa, sana! Kwa nini nikushindwe?
Haya njoo.
Mama Sabinamu akakata simu ya
Sudi, akampigia kijana
Sasa sikia, eeee
.fanya hivi, we njoo
hadi kwenye kona ya Hospitali ya
Mwananyamala, nisubiri hapo, kaa
sehemu, kunywa hata soda
nitakupigia kukuita.
Sawa mama. Maana da! Hii supu ya
pweza leo ni balaa humu mwilini
mwangu.
Usijali kijana wangu, ee!
mwanamke huyo akakata simu,
akapokea ya Sudi...
Nimefika hapa Komakoma mama.
Nenda mbele, kata kulia, uliza mtu
yeyote ilipo gesti.
Sawa.
Ndani ya dakika tano, Sudi aligonga
mlango wa chumba alichokuwemo
mama Sabinamu
Nani kakwambia nipo humu?
Mhudumu. Ulimuulizaje?
Kuna jimama limeingia humu?
Akaniuliza si yule mama mpenda
vijana? Nikamwambia mimi sijui
kama anawapenda au anawachukia.
Akasema ni huyohuyo, ingia chumba
namba nane.
Mh! Hana adabu.
Kwani anajua kama mimi mpenzi
wako?
Hajui.
Sasa kwa nini ameongea hivyo?
Akili zake mbovu.
Na kweli. Sasa mbona humu ndani
kuna mizigo mingi, ni ya mpangaji
mwingine au?
Kabla mama Sabinamu hajajibu,
simu yake iliita
Subiri subiri, usiongee
ngoja
nipokee simu ya mume wangu.
Sudi alimkubalia kwa kutingisha
kichwa juu chini
Haloo
Upo nyumbani?
Ndiyo mume wangu.
Hebu angalia dayari yangu hapo juu
ya kabati, ndani kuna sehemu
nimeandika kiasi cha pesa
nilichonunulia kile kiwanja cha
Kimbiji. Fanya haraka, nasubiri na
sikati simu.