donlucchese
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 17,258
- 22,140
ghafla nikakumbuka Miaka michache iliyopita kijijini kwetu chalinze. ilikua usiku mzuri sana kijijini kwetu hususan kwa kijana kama mimi kwakua kulikua na sherehe pale kijijini kwetu maarufu kama 'kigodoro'. japo sikua na. nguo za gharama kutokana na hali halisi ya maisha ya nyumbani wetu, nilijitahidi kuupara jeans langu kuukuu na tisheti yangu ya sprite ya kijani iliyofubaa na kumaliza na raba yangu aina ya Reebok iliyochakaa sana........JINA LA HADITHI= SIRI YA MAFANIKIO YANGU
MTUNZI= CHIT CHAT MEMBERS
WAZO= donlucchese
. . . . . . . . . Nilihamka na kuusogelea mlango huku nikijiuza ni nani tena ananisumbua saa hizi.
Kwa kuwa ilikuwa ni sauti ya kike hata hofu yangu ilipungua kidogo kwani mara nyingi unapofika mwisho wa mwezi,mama mwenye nyumba huwa ni msumbufu sana kwa wapangaji wake.
Nilipofungua mlango nilikutana uso kwa uso na mtoto wa mama mwenye nyumba kabla hata sijamwambia chochote aliamua kuingia ndani na kusimama bila ya kuzungumza chochote.
Moyo ulianza kunidunda kwa mbali nikihisi labda anakagua achukue kitu chochote ndani ya chumba changu ili kulipizia kodi ya mama yake.
Nilijisemea moyoni "mimi ni mwanaume sitokubali changu chochote kitoke,kama ni kupigana leo tutapigana tu mpaka kieleweke"
mtoto wa mama mwenye nyumba alinitazama huku amekunja sura na kuniambia.
"hivi wewe ni mwanaume gani,hata kodi ya kulipa mwezi mmoja unaikosa,mwanaume suruali kapura mkubwa"
huwa sipendi dharau,tena kudharauliwa na mwanamke ni kosa kubwa kwangu.
Nilijikuta nikimsogelea binti huyo kwa hasira huku nimekunja ngumi . . . . . . . . .
ghafla nikakumbuka Miaka michache iliyopita kijijini kwetu chalinze. ilikua usiku mzuri sana kijijini kwetu hususan kwa kijana kama mimi kwakua kulikua na sherehe pale kijijini kwetu maarufu kama 'kigodoro'. japo sikua na. nguo za gharama kutokana na hali halisi ya maisha ya nyumbani wetu, nilijitahidi kuupara jeans langu kuukuu na tisheti yangu ya sprite ya kijani iliyofubaa na kumaliza na raba yangu aina ya Reebok iliyochakaa sana........
............Yowe la mtoto wa mwenye nyumba lilisikika vizuri kwenye masikio ya mama mwenye nyumba aliyekua yuko ndani kwake anasikiliza radio yake kipindi cha 'mirindimo ya pwani'. Mama mwenye nyumba alitoka mkuku nakuingia chumbani kwangu bila hodi na kumkuta binti yake ameanguka chini akisijilizia maumivu ya kile kibao matatata.kichwani nikatupia kofia moja ya kepu,mi mwenyewe nilijiona bonge la handsome lakini laiti msomaji ungeniona,ungesema leo umekutana na kali ya mwaka.
Nilianza kusogea karibu kabisa na uwanja wa shule ya msingo uliokuwapo hapo kijijini kwetu.
Kwa mbali niliona bendi ya wanakigodoro ijulikanayo kama WAKUNA NAZI BEND wakiwaiingia uwanjani huku wapo ktk usafiri wa trekta,kwa sisi wa kijijini ulikuwa ni usafiri wa heshima sana.
Uwanjani watu walikuwa wengi sana na kama unavyojua masharo wa kijijini walitokelezea kwa pamba za ukweli.,wapo walivalia tshit na jeans lakin miguu wakakupigia miguu peku.
Niliangaza huku na huko nikimtafuta mpenzi wangu kalunde bila ya mafanikio yoyote.
"sasa mabibi na bwana,ladies and nanilii and gentlemen sasa hivi tunawaleta kwenu wakuna nazi band" ilikuwa ni sauti ya mc wa kijiji bwana Mlio wa paka.
Mi sikutaka kumsikiliza mc bali mawazo yote yalikuwa kwa kalunde.
Nilizunguka bila ya mafanikio,lakini ghafla nilitazama katikati ya uwanja na kumuona kalunde akisakata mangoma jamaa mmoja wa bend ya wakuna nazi.
Kalunde alikuwa msichana mrembo,rangi ya maji ya kunde,sauti akikusemesha tu tayari unapoteza dira.
Nilijikuta nipo katikati ya uwanja huku wakuna nazi wakiendelea na kutumbuiza,walishtukuona mtu wao akila kibano cha nguvu.
Muziki ulisimama ghafla na mgambo wawili wakanifuata ili wanitoe katikati ya uwanja lakin mgambo hao waliambulia ngumi za uso ziliwafanya wakimbie kama wamepigwa bomu vile.
Kila aliejaribu kuingilia alikula mkong'oto.
Nilimchukua kalunde na kuondoka.
Nilikumbuka ubabe wa zama hizo na kujisemea siwezi kudharauliwa na mtoto wa mwenye nyumba,na kuinua mkono,nilimpa kibao kimoja kilichomfanya atoe sauti kali.
"uwiii ananiua"
mtoto wa mwenye nyumba alidondoka chini. . . . . . . . . . . . .
maneno makali ya yule mama yakamuamsha binti yake mkubwa aitwaye mwajabu. huyu Mwajabu anasifika kwa ugomvi mpaka wakaamua wampatie chumba cha uani. yeye hapatani na nduguze wala wapangaji.............Yowe la mtoto wa mwenye nyumba lilisikika vizuri kwenye masikio ya mama mwenye nyumba aliyekua yuko ndani kwake anasikiliza radio yake kipindi cha 'mirindimo ya pwani'. Mama mwenye nyumba alitoka mkuku nakuingia chumbani kwangu bila hodi na kumkuta binti yake ameanguka chini akisijilizia maumivu ya kile kibao matatata.
"Mshenzi mwanaharamu wewe usiye na haya ndio unataka kumuua binti yangu sio? umeona kunizungusha kodi haitoshi sio? sasa nasema hivi, nampeleka binti yangu hospitali na nikirudi sitaki kukuta ndani ya nyumba yangu mwana kutoka kubaya wewe lasivyo nitakuletea polisi ma...na zako.........,
maneno makali ya yule mama yakamuamsha binti yake mkubwa aitwaye mwajabu. huyu Mwajabu anasifika kwa ugomvi mpaka wakaamua wampatie chumba cha uani. yeye hapatani na nduguze wala wapangaji.
haijulikani anafanya kazi gani japo hutoka jioni na kurudi asubuhi, mwenyewe husema anafanyya kazi hotelini kama receptionist.
alipofika nakuona mama yake anasema anampeleka mdogo wake hospitali alianza kufoka huku akidundadunda kama kitenesi " hivi we mama unaakili!? umpeleke hospitalii we ndiyo umempiga? unajua bei ya matibabu? hapa aitwe balozi na twende kwanza polisi".
niliposikia polisi moyo ulilia paa.........
"jamani ni bahati mbaya, nisingeweza kumpiga Aisha. mara ngapi ananitukana na sijawahi......". "huyu siyo wa kuongea naye." alinikatiza Mwajabu. "inabidi aende akapigane na kina sudi ye si mwanaume". Mwajabu alikuwa akiongea hayo huku akiingia chumbani kwake na kutoka na simu na kuanza kumpigia balozi simu. nilivyosikia jina sudi ndiyo nikajua hatari iliyokuwepo.katika vitu ambayo nilikua naviogopa maishani ni neno 'polisi'. Ni polisi ndio walisababisha marehemu baba yangu kufungwa jela maisha kwa kosa ambalo hakulifanya na hatimaye kupoteza maisha gerezani akiwa bado anatumikia kifungo cha maisha na kumwachia mama mzigo mzito wakuendesha familia bila msaada wowote. Ni polisi pia ndio walifanya nitoroke kijijini na kuja kutafuta maisha mjini. Nilihisi hatar inayonikabili mbele yangu kwa maana ukiwekwa ndani na polisi kama ni kabwela kama Mimi basi unaweza ukajikuta unaozea selo. Nikajitutumua kiume na kuongea,".....,..
"jamani ni bahati mbaya, nisingeweza kumpiga Aisha. mara ngapi ananitukana na sijawahi......". "huyu siyo wa kuongea naye." alinikatiza Mwajabu. "inabidi aende akapigane na kina sudi ye si mwanaume". Mwajabu alikuwa akiongea hayo huku akiingia chumbani kwake na kutoka na simu na kuanza kumpigia balozi simu. nilivyosikia jina sudi ndiyo nikajua hatari iliyokuwepo.
sudi alikuwa mtoto wa mwenyekiti wa mtaa. alikuwa ni pande la mtu na sifa yake kubwa mtaani ilikuwa uporaji na kuuza bangi. kwa kipindi hicho alikuwa yupo jela akitumikia kifungo cha miaka minne kwa kosa la kuibia abiria waliopata ajali.
kabla sijajua nini cha kuongea kujiokoa, mwajabu akaanza kuongea na balozi..........
sio kwamba niliogopa, la hasha. niliwaza kwamba je vijana hawa walioshindikana laiti kama wakinizulia ugomvi na nikashindwa kuzuia hasira yangu je itakuaje. Katika mambo ambayo nilirithi kwa marehemu mzee wangu jambo moja kubwa ni hasira yake. Marehemu mzee wangu alikua ni mtu mwenye hasira sana na hata kipindi alkiwa amewaka kwa hasira ilitulazimu tukae mbali. L;icha ya umbo langu dogo dogo, nilikua nimejaaliwa kipaji cha kurusha masumbwi. Naam, nilikua mrusha masumbwi hodari. Wakati ipo darasa la sita kuna mvulana mmoja wa darasa la saba alininyang'anya mfuko wangu wa madaftARI Maarufu kipindi hiko kama 'sport'. Nilimuomba kiunyenyekevu anirudishie mfuko wangu lakini aligoma kurudisha mfuko huku akitukana kwa dharau na kuonesha majigambo mbele ya wasichana wa darasa la saba. Sikukawia......
Alikuwa akiniita jina langu.
Nilimgeukia na kumtazama kwa kuhuzuni,huku nikijitahidi kudhibiti hasira zangu zisije zikanipanda na kujikuta nikifanya mambo ya ajabu na kutisha.
Wakati huo sudi na mwenzake kabaa walikuwa wamekimbia baada ya kumuona polisi na mjumbe.
Askari hakutaka maelezo mengi wala mjadala,alinifunga pingu na kunielekeza nimfuate kituo cha polisi.
Nilimuomba ruhusa ili nifunge chumba changu,askari huyo hakukataa chochote,niliingae nae ndani nikachukua kufuli na kukifunga chamba changu vizuri.
Nilimuomba mjumbe abaki na funguo yangu,mjumbe kwa kuwa alinijua vizuri basi alikubali na kuipokea funguo yangu.
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu niliingizwa kituo cha polisi.
Askari mmoja aliponiona tu alimuuliza mwenzake.
"haroo afande hiri ndio rire rijamaa rinarotongoza watoto wa watu halafu likikatariwa rinareta fujo
"
ndio afande,,,afande yule alimjibu.
Niliambiwa nivue viatu na mkanda,nami nikatii amri hiyo.
Kabla hata ya kuhojiwa chochote askari alinifungua pingu na kunipeleka chumba cha selo.
Nilitembea hatua mbili na kugeuka nyuma,nilimtazama mjumbe,mjumbe alionekana kama kunionea huruma,lakini hakunisemesha.
Niliingiza sero na mlango ukavungwa.
Nilichokiona hapo kilinishtua . . . . . . . . .
.......kwani niliona wenzangu waliokuwa selo wakiwa wametapakaa damu, nikajisemea "leo kazi ipo"
. . . . . . Nilimsogelea huku roho ikinidunda.
Hakika mtu huyo alinitisha,nilikumbuka ubabe uliokuwa ukifanyika ndani ya film ya prison break.
Nilijihisi kuwa nimeingia katika ulimwengu mpya,nilijiona kama vile nimeshafika kuzimu.
Mbabe huyo alinisogelea na kuniomba nivue shati langu na kumpatia.
Kwa kuwa jamaa alikuwa akitisha mithili ya mcheza mieleka,mwili ulijaa misuli kama mwanamashinda wa michezo ya kuinua vitu vizito.
Macho makubwa na mekundu yalizidi kuniogopesha zaidi.
Nilijikuta taratibu nikifungua shati langu na kulivua kisha nikamkabidhi.
Kama vile jamaa hakuridhika,kwa sauti ya ukali alinitaka nimpe na suruali yangu.
Nilikumbuka mkasa wa mjomba wangu alipotea miaka kumi iliyopita,mjomba aliwahi kuniambia kuwa sero huwa kuna watu wababe ambao ukiwachekea au kujifanya dhaifu basi utaumia.
Jamaa alinilazamisha nivue suruali.
Nilitafakari kichwa kwamba mtaani nimepigwa,huku nako nivuliwe nguo,hapana niliona nadhalilishwa kama siyo kujidhalilisha mwenyewe.
Nilimwambia mbabe huyo ambae badae nilikuja kugundua kuwa jina lake ni tyson,kuwa siwezi kumpa suruali yangu.
Jamaa alipandisha hasira mpaka jasho likamtoka,nilijihisi nami uwoga ukinipungua kwani niliamini mimi ni mwanaume lazima nijikaze.
Tyson alirusha ngumi moja ambayo niliidaka na kumsukumia pembeni.
Sero nzima ilihamka na kila alinitaza akijua kuwa leo lazima tyson afanye mauaji ndani ya kituo cha polisi.
Tyson alinisogelea na kurusha ngumi za haraka haraka ambazo zote zilinikosa,nilikaza mkono na kumpa tyson ngumi moja ya chembe ya moyo.
Tyson alitoa mimacho mithili ya mtu anaejinyonga.
Tyson aliishiwa nguvu na kudondoka chini,povu lilianza kumtoka mdomoni . . . . .
Balaa juu ya balaa. mahabusu wote walisogea pembeni nakuniacha peke yangu nikijaribu kumpa huduma ya kwanza lakini cha ajabu povu ndio likazidi kutoka huku macho ya mbabe yule yakianza kubadilika rangi. niko wa nimepaniki nilipiga yowe zito la kumuita afande aje kutoa msaada. La haula, nilishuhudia mbabe yule akikata roho pale chini wakati maafande wakifungua mlango wa selo....