Hadithi: Hirizi ya mapenzi

Hadithi: Hirizi ya mapenzi

Mdharuba

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2011
Posts
824
Reaction score
521
Na:

Mdharuba J.K.

*SEHEMU YA KWANZA*

★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Nashindwa kuelewa kwa nini nakupenda kiasi hiki Jay, nahisi kuchanganyikiwa juu ya penzi lako my” Jacqueline alisema maneno haya huku akiwa amelalia kifua changu. Tulikua katika chumba changu kidogo nilichopangisha uswahilini. Kutokana na kazi yangu ya kuuza karanga, sikuweza kumudu kupangisha katika vyumba vyenye thamani nzuri. Niliishi kwa kuungaunga.
“Mimi nadhani upendo wangu unaotoka moyoni ndio unaokufanya uzidi kunipenda kila leo, sidhani kama kuna jingine”. Nilimjibu huku nikijifanya kama sijui niyafanyayo.

“Na kweli, maana huwezi kuamini sijawahi kulala nje ya nyumbani tangu napata fahamu hadi leo, lakini tazama hii ni siku ya tatu sasa nipo hapa kwako halafu sihisi kujuta hata kidogo”. Alizidi 'kuropoka' Jacq na kunifanya nijihisi wa kipekee sana.

“Penye mapenzi ya dhati majuto wala usiyakaribishe kamwe my” Nilikazia ili kuendelea kumpa moyo Jacq ahisi niko pamoja naye kwa kila hali.

★★★★★★★★★★★★★
Jina langu naitwa Jumanne, ingawa najulikana zaidi kama 'Jay'. Nimezaliwa mkoani Tanga miaka 22 iliyopita. Kutokana na utundu pamoja na ukorofi niliokuwa nao sikubahatika kuendelea na elimu yangu ya sekondari baada ya kufika kidato cha pili. Niliona shule inanichelewesha nikaamua kuingia mtaani kutafuta maisha.

Maisha yalikua magumu sana mtaani. Nilihangaika sana hadi pale nilipoamua kujikita katika biashara ya kuuza karanga ambayo kiasi fulani ilikua ikiniingizia walau pesa kidogo za kuendeshea maisha ya kila siku.

Nilianza biashara hii nikiwa bado na umri mdogo wa miaka 17 tu, na sasa ni miaka mitano naendelea na biashara yangu nikiwa nimejizolea umaarufu sehemu mbalimbali za jiji hili la wastaarabu.

Kutokana na pirika za maisha na jinsi hali yangu ilivyo duni miaka yote hii ambayo nauza karanga, nilijikuta napitia kipindi kigumu sana katika habari za mahusiano. Nguo zangu chakavu pamoja na haiba yangu isiyovutia vilinifanya nitengwe sana na wanawake karibu wote na kutotaka kabisa kuanzisha uhusiano na mimi licha ya kujaribu 'kurusha mshipi' kwa wanawake kadhaa mara kwa mara. Hapa ndipo nilipojihisi mnyonge sana na kuamua kutafuta njia mbadala itakayonifanya nipendeke mbele ya wanawake.

Hapa ndipo nilipotafuta hirizi ya mahaba ijulikanayo kwa jina maarufu la 'ndere'.

★★★★★★★★★★★★★★★★★
Jacqueline alikuwa ni msichana aliyetokea kwenye familia yenye maisha ya kawaida sana, babaake akiwa mwajiriwa wa serikali na mamaake akijishughulisha na ujasiriamali. Sifa pekee aliyosifika nayo Jacqueline ni uzuri wake wa sura pamoja na umbo. Alikuwa mrefu mwenye umbo la wastani, lililojichonga kwa 'shape' nzuri ya kuvutia. Lipsi zake pana zilizidi kuushajihisha wajihi wake. Rangi yake ya maji ya kunde pamoja na ngozi yake ya kuvutia ilizidi kumpa 'marks' kwa amuangaliae.

Wanaume wengi wakware walishamtokea kumtongoza lakini kutokana na jinsi alivyokuwa anajichukulia, ilikua ngumu kumkamata.
Wengi wa wanaume waliishia kumnyooshea vidole tu huku yeye akijisikia furaha kila siku anavyozidi kuwakataa wanaume tofauti tofauti.

Kwa mara ya kwanza nilivyokutana nae wakati amejipumzisha katika moja ya bustani za jiji hili, huku mimi nikipita na kapu langu la karanga, moyo wangu ulishtuka sana. Hii ni kutokana na uzuri wake. Na kwakuwa kwa sasa nilishazoea kuwatokea wasichana wote warembo huku nikiwa na uhakika kuwa sikataliwi, ndipo nilipomfuata pale alipokuwa na kuamua kumuonjesha karanga. Nikabahatika kukaa nae kwa dakika chache kabla sijachukua namba yake ya simu na kuondoka.

★★★★★★★★★★★★★★★★
Nikiwa bado pale kitandani huku Jacq amelala kifuani kwangu, nilisikia simu yangu ndogo iliyokuwa katika meza ndogo iliyokuwa chumbani humo ikiita.
Nikapeleka mkono na kuikamata kwani meza haikuwa mbali na kitanda. Wakati naileta karibu niangalie nani anapiga ili nipokee, ikaniponyoka na kuanguka chini. Mpira niliokuwa nimeifunga kuishikilia isije kuachana na battery ukafunguka na kufanya battery itoke. Nikainuka pale kitandani na kuiokota kisha nikarudishia battery na ule mpira kisha nikaiwasha.

“Saa ngapi hapo?” Nilimuuliza Jacq ili niweze kurekebisha saa katika simu yangu. Jacq akaangalia saa yake ya mkononi aliyokuwa amevaa.
“Saa 4:30 baby..” Alinijibu na kubaki nimehamaki. Ni siku ya pili sasa nipo na Jacq na hata kwao hakumbuki. Na hii ilishakuwa usiku sana hawezi tena kurudi kwao usiku huu. Hii ilimaanisha kuwa nitalala nae na atatimiza siku ya tatu akiwa hapa kwangu.

Wakati narekebisha saa ya simu yangu, mlio wa 'sms' ukasikika katika simu yangu. Nikaamua kuisoma..

“Wewe kata tu simu, lakini huyo binti wa watu uliyenaye siku ya pili leo atasababisha karanga ukaziuzie jela” Ndivyo ilivyosomeka sms ile na kunifanya nimuangalie Jacq jinsi alivyojiachia pale kitandani huku nikishusha pumzi ndefu.

★★★★★★★★★★★★★★★★

Itaendelea....
 
HIRIZI YA MAPENZI

Na:

Mdharuba, J.K.

*SEHEMU YA PILI*
★★★★★★★★★★★★★★★
Nilibaki nimepigwa na butwaa huku nikiachia mdomo wazi, sijui ni nani amenitumia ile sms na amejuaje kuwa mimi niko na Jacq hapa chumbani kwangu.
Akili ya haraka iliyonijia hapa ni kumtimua Jacq arudi kwao ili aniepushe na matatizo yanayokaribia kunikuta.
Ujumbe wa ile sms ulikuwa mzito sana, nisingeweza kuupotezea hata kidogo. Ila swali nililojiuliza “Ni vipi Jacq atalipokea hilo?”. Nilikuwa na hakika kuwa hatanielewa. Na pale simu yangu ilipoanguka na kuzima, mpigaji alifikiria nimemkatia simu, hivyo akazidi kupandwa na hasira.
Nikaamua nimuonyeshe Jacq ile sms ili nijue atasema nini.
“Anko Jose huyu, achana nae..” Ndivyo alivyoniambia Jacq huku akinikabidhi simu baada ya kusoma sms ile.
“Hapana mpenzi, nawezaje kuachana nae wakati ujumbe ni mzito sana huu na wewe unajua maisha yangu tena yalivyo, na hapo pametajwa jela tayari” Nililalama ili angalau Jacq anisikilize na kunielewa, lakini ilikuwa kazi bure.
“Hawawezi kukufanya chochote, wala usiwe na wasiwasi my” Jacq alisema kwa kujiamini.
“Kama ni hivyo basi washa simu yako ili wakutafute wewe na sio mimi” Nilimkazia Jacq kwakuwa hali ilishakuwa tata upande wangu. Tangu siku ya kwanza kuja hapa kwangu Jacq alizima simu yake, hakutaka apatikane.
“Simu mimi siwezi kuwasha maana bado nataka niendelee kukaa na wewe hapa, halafu hiyo mada ibadilishe” Ndivyo alivyonijibu Jacq na kugeukia pembeni.
Nikakaa pale juu ya ile meza nikitafakari namna ya kulikabili janga lililopo mbele yangu muda huu. Sikuwa na namna ya kufanya.
★★★★★★★★★★★★★
Niliuangalia mwili wa Jacq uliokuwa umeumbika akiwa na kanga moja tu pale kitandani huku akiwa amenipa mgongo nimuone kwa nyuma. Nyuma palikuwa pamejazia vizuri kuliko maelezo, hisia za mapenzi zikapanda. Nikasahau kabisa kuwa nimepigiwa simu na watu wa kwao.
Nikaiweka simu pembeni kwenye ile meza, nikautupa mbali msuli niliokuwa nimejifunga kiunoni na kujirusha pale kitandani.
Nikaikagua vizuri ile kanga pasi na kuishika, nikafanikiwa kujua ilipoanzia. Haikuwa imefungwa, iliegeshwa tu, labda hii ilikuwa ni makusudi ili kumvutia mtazamaji. Nikaishusha taratibu na kuanza kumpapasa 'chura' wake. Akageuza uso kunitazama kisha akatabasamu. Mimi sikuongea chochote, nikajiweka 'busy' na kazi ile ambayo nimeianzisha.
Nikamgeuza na kukitazama kifua chake jinsi kilivyokaa vizuri. Hapa palikuwa na nido za wastani zilizosimama barabara. Rangi yake ya maji ya kunde ilinogesha zaidi muonekano wa hapa. Nikazamisha kichwa changu na kuanza 'kuzipiga ulimi'.
Hapa ndipo niliposikia mlango wa chumbani kwangu ukigongwa kwa nguvu sana. Nilishtuka na kuruka pale nilipokuwa. Nikarudishia msuli kiunoni kama mwanzoni na kuuendea mlango bila kutoa sauti yoyote. Mgongaji bado alikuwa anaendelea kugonga kwa nguvu. Safari hii akipiga makelele “Funguuaaaaa”. Nikakamata kitasa na kuzungusha funguo, kisha nikausukuma mlango kuelekea ndani ili kumfahamu mgongaji.
Lahaulaaa... Sikuamini macho yangu.
Alikuwa ni rafiki yangu kipenzi, Nira aliyekuwa pale mlangoni huku akitweta. Akataka kunisukuma niingie ndani nikakataa.
“Tuyamalize tu hapa hapa kaka, ndani yupo shemeji yako humu” Nilimsihi.
“Hicho ndo kilichonileta, kaka uko hatarini” Aliniambia na kunifanya nishtuke kuliko kawaida. Ni kweli nilihisi kitu si cha kawaida kwa ujio wake ule, lakini kuhatarisha maisha yangu tena?! Hii sikuitegemea.
“Eeenh.. Ni nini hicho kaka?!, tatizo nini kaka? Nambie..” Nilisema kwa sauti ya juu sana, nilihisi kuchanganyikiwa.
Nira akanishika kichwa na kunivutia kwake na kulileta sikio langu usawa wa mdomo wake kisha akaninong'oneza.
“ Kaka, kimbia haraka, wazazi wake wanakuja na polisi”.
“Jay mbona kelele, kuna nini mpenzi?” Ilikuwa ni sauti ya Jacq aliyekuja kwa nyuma na kunishika bega.
Nikamtazama kisha nikamtazama Nira bila kujua nijibu nini.
★★★★★★★★★★★★★

Itaendelea...
 
*HIRIZI YA MAPENZI*

Na:

Mdharuba, J.K.

*SEHEMU YA TATU*
★★★★★★★★★★★★★★★
Nilimpa ishara rafiki yangu, nikaingia ndani na kufunga mlango.
“Huyu rafiki yangu ana matatizo kidogo ameniomba nikamsaidie, naomba dakika tano tu nitarudi my”. Nilimdanganya Jacq huku nikiwa navaa nguo zangu harakaharaka.
“Najua unachotaka kukifanya Jay, lakini mimi nitafanya zaidi ya hivyo, wewe jaribu tu kunikimbia, kesi itakua kubwa zaidi kwako kuliko unavyofikiria”. Jacq alisema kwa kujiamini huku akionesha kukerwa na kitendo changu cha kutaka kuondoka mle ndani.
“Ina maana hunielewi au vipi? Kwahiyo nisimsaidie rafiki yangu katika tatizo lake?” Nilimhoji Jacq.
“Acha ujinga Jay, unahisi sijui unachokifanya? Najua sana”. Jacq alionekana kuamini katika hisia zake. Nikamuangalia sana kwa makini, nikaona amemaanisha kitu kutoka moyoni. Hapa nilikua nimeshamalizia kuvaa hadi 'Cap' yangu nyekundu, na raba zangu nyeupe, tayari kwa kutoka. Nikamtizama kwa makini sana kiasi cha dakika moja, kisha nikaugeukia mlango na kutokomea. ★★★★★★★★★★★★★★★
*HIRIZI YA MAHABA* Iliyokulika zaidi kwa jina la Ndere au Kindere, ndiyo iliyokuwa 'ikiniweka mjini' kwa kipindi hiki. Niliringia sana hirizi hii, kwa sababu ilinikutanisha na wanawake wengi wa aina tofauti. Hakuna mwanamke ambaye angeweza kuniringia kwa wakati huu. Kila mwanamke niliyemtaka niliweza kumpata.
Kwa muda wa miaka mitatu tu tangu nimiliki hirizi hii, nilishatembea na wanawake wasiopungua mia moja na sabini. Walikuwemo wake za watu, wachumba za watu, wanafunzi, walimu, wafanyakazi wa serikali na sekta binafsi, maaskari, madakari, manesi, wauguzi, maafisa elimu mpaka wafanyabiashara.
Sikuwa najali sana kuhusu magonjwa na kitu kingine chochote, na wala sikuchukua tahadhari yoyote katika kufanya ngono zote ambazo nimezifanya. Nilihisi kawaida sana, nilijali starehe zaidi.
Kwakweli kwa muda huu tangu nimiliki hirizi hii, karanga nauza kwa kutafuta tu wanawake warembo wa kila idara, na si kwa ajili ya pesa, kwani nilikuwa na wanawake wengi waliokuwa wakinihudumia. Sikujutia hata kidogo pesa yangu niliyoipata kwa tabu kwenda kuitoa kununulia mbuzi ambaye damu yake ndiyo iliyotumika kutengenezea hirizi hii. Kwa sasa nilihisi faraja sana.
Nilivaa na kula nilichojisikia kupitia hirizi hii. Wanawake wote warembo walikuwa wa kwangu.
Wengi wa wanawake walinitaka nihamie kwao kutokana na mazingira mabovu niliyokuwa naishi pale uswahilini, lakini nilikataa kufanya hivyo. Na hii si kwa sababu nyingine, bali lilikuwa moja ya sharti la hirizi hii.
“Usihamie kwa mwanamke hata kama umeshawishika kiasi gani, utapoteza ufalme wako”. Bado yaliendelea kunijia kichwani maneno haya ya mganga wangu.
Sikuwa na namna zaidi ya kuendelea kuishi pale. Maisha yangu yalikuwa ya namna hii, kubadilisha wanawake kila leo. Sikujua nitaishia wapi, lakini kama wasemavyo *'Ujana maji ya moto'*, sikujali sana hali ya baadae.
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Nilimwacha Jacq pale kitandani akiwa haamini kama nimeondoka, hakutegemea.
Nikatoka nje ambapo Nira alikuwa akinisubiri, tukaongozana na kutembea kuelekea kwake.
Tukatembea hatua chache sana, kwa mbali nikaona mtu ambaye nilihisi namfahamu akiwa anatembea kuja huku tunakotokea sisi. Kwahiyo tukawa tunatembea kuelekeana. Kadri tulivyozidi kumkaribia ndivyo nilivyojihakikishia kuwa ni yeye huyu ninayemfahamu mimi.
Tukatembea mpaka tukawa tumemfikia kabisa, naaam ni yeye kweli.. Rahel, mke wa mtu aliyetokea kukolea kwenye penzi langu kiasi cha kumsahau mumewe ambaye wapo kwenye ndoa kwa miaka saba sasa.
“Siku ya nne leo nakupigia simu hata hupokei simu zangu, ndo nini sasa Jay?” Aliniuliza Rahel kabla hata ya salamu.
“Ndio salamu ya kwenu hiyo?” Nilimzingua.
“Ooh samahani mpenzi, nina hasira ndo maana nimekuwa hivi” Alirudi chini. Na hiki ndicho kitu kikubwa nilichompendea Rahel, alikuwa mwepesi sana wa kurudi chini anapoona amekosea, tofauti hata na Jacq na wengineo ambao mara nyingi walijiona wako sahihi.
“Simu yangu imepotea mlemle chumbani kwangu, siku ya nne leo naitafuta siioni, na ilikuwa 'silent' nikiipiga inaita lakini sijui iko wapi”. Nilidanganya.
“Ok, haina shida, nikahisi una tatizo” Aliridhika Rahel na uongo ule.
“Ndio, tatizo ninalo” Na mimi nilisema kile ambacho hakukitegemea kukisikia.
“Eeenh? Tatizo gani tena?” Aliuliza kwa kuhamaki.
“Mambo tu ya ulimwengu” Nilimjibu haya huku nikionyesha ishara ya kutaka kuendelea na safari yangu, kwani Nira alishanifinya kwa siri kuwa nifupishe maongezi tunachelewa.
“Naomba basi twende pale kwako tukaongee kidogo, nimekuja kwa ajili yako baby, afu nina zawadi yako pia leo. Na pia nataka nkuachie ile laki 3 ulosema unahitaji kwa ajili ya mambo yako”. Rahel aliongea akijaribu kunishawishi nirudi nyumbani kwangu.
“Samahani Rahel, waweza kunipa hivyo vitu vyote hapahapa, maana nina safari muhimu kidogo” Nilipitisha ombi langu nikiashiria kuwa siwezi kurudi nyumbani kwa muda huu.
“Tangu lini nikafanya hivyo? Leo iwe ya pili? Kama safari yako ni muhimu kuliko mimi na zawadi zangu unaweza kwenda, ila kwa barabarani hapana” Aliongea kwa msisitizo Rahel pasipo kujua ugumu wa jambo linalonikabili.
★★★★★★★★★★★★★★
Je, Jay atarudi nyumbani kwa ajili ya zawadi za Rahel? Au nini kitatokea..??!!

Usikose HIRIZI YA MAPENZI SEHEMU YA 04.
 
Kwahiyo ulikuwa unamatatizo ya kiuchumi lakini bado ukaenda kutafuta dawa ya mapenzi.hahahaha anyway kimbia haraka sana jela Katanga haziuzi
 
*HIRIZI YA MAHABA*

Na:

Mdharuba, J.K.

*SEHEMU YA NNE*
“Kama utaamua kunipa hapahapa wewe nipe tu, lakini huko nyumbani mimi sirudi” Nilimjibu Rahel na kumwacha akishangaa.
“Ok, sawa, mimi narudi nyumbani, lakini leo umeniudhi sana..” Alilalama Rahel wakati anageuka kurudi alikotoka.
“Ukisema leo nimekuudhi unamaanisha siku zote nakufurahisha?” Nilimuuliza.
“Ndio, siku zote unanifurahisha, lakini leo sijui kwanini, lakini sawa, najua ni huu upendo wangu ndio unaokufanya uniringie”.
“Nyie wanawake ni wa ajabu sana, yaani siku zote nakufurahisha lakini hujaona hilo, umeona leo nilivyokukera, haya nenda salama”.
“Samahani basi Jay, naomba nikuambie kitu” Rahel alisema haya huku akiniashiria niongee nae faragha kidogo, hakutaka Nira asikie alichotaka kuongea. Nilitii huku Nira akiwa amesimama pembeni akisubiri tumalize maongezi haraka ili tuwahi kutoroka tuepukane na janga liliokua mbele yangu.
“Hizi hapa pesa ulizohitaji, najua utakua na tatizo lakini hutaki kunieleza, ila nakupenda sana..” Aliniambia Rahel huku akifungua pochi yake na kunikabidhi noti za elfu kumi kumi nyingi. Wala sikuzihesabu, nilizichimbia moja kwa moja katika mfuko wa mbele wa Jeanz yangu na kuagana na Rahel kisha nikamgeukia Nira tukaondoka kwa mwendo wa haraka.
****************************************
“Umenibeba kama mwehu yani, hata sijui naelekea wapi” Nilimhoji Nira baada ya kuona tunaenda tu, sijui mwisho wa safari yangu.
“Twende kwa yule demu wako wa pale Makorora” aliniambia Nira.
“Wa Makorora yupi? Nasra, Regina au Rukia? Maana wako watatu pale Makorora” Nilimhoji Nira.
“Regina bana, ndo ambaye ana nafasi hiyo, Nasra si mke wa mtu yule, na yule Rukia muda huu yawezekana hata kurudi hajarudi”.
“Ok, hapo sawa, nimekupata”.
Tulifika hadi nyumba anayoishi Regina, hapakuonekana dalili kuwa kulikuwa na mtu mle ndani, milango yote ilifungwa kwa nje.
“Gonga basi bro” Nira aliniambia.
“Sasa nagongaje bro wakati milango imefungwa kwa nje hii, hapa hakuna mtu” Nilibisha kwa hoja. Kisha nikaongezea.
“Kwanini tusiende kwako tu? Tatizo nini kwani?” .
“Kaka, kwanza nahofia wanaweza wakawa wanapajua na kwangu, wewe ni 'best' yangu, kwahiyo lazima watu watakuwa wanajua tu ninapoishi kwa sababu muda mwingi tuko pamoja” Alinipa maelezo ambayo sikuyaafiki moja kwa moja.
“Wewe twende tu, unafikiri tutafanyaje saa hizi, wakija kunikamata basi tu” Niliamua liwalo na liwe.
“Hapana bro, hata hivyo mi mwenyewe nina mgeni pale kwangu, sasa unafikri tutalalaje watu watatu chumba kimoja kile?” Hii hoja ndiyo iliyoninyong'onyeza zaidi, nikaona nisimbishie Nira.
“Nina pesa ya kutosha amenipa Rahel, wacha nikalale gesti, kesho tutajua cha kufanya.” Maelezo haya yalionekana kueleweka mbele ya Nira, pasi na kuongeza neno alinisindikiza hadi gesti ya karibu na kuniacha pale yeye akaondoka.
****************************************
Nikiwa pale gesti ndipo nilipopata wazo la kumpigia Jacq nimueleze hali halisi, halafu nione kama anaweza kuja kubadili makazi na kuja hapa gesti. Simu iliita bila kupokelewa, nilipojaribu mara ya pili, ilipokelewa na kusikia sauti ya upepo kama mtu aliye katika pikipiki inayoendeshwa kwa kasi sana.
“Haloo, nipo kwenye bodaboda, naelekea nyumbani” Alinambia kabla ya kumwambia chochote.
“No, kuna gesti ya karibu nipo hapa, njoo bana, usiende nyumbani..” Nilijaribu kumsihi.
“Hapana, wamekufuatilia na wameshafika hapo gesti, acha mimi niwahi nyumbani, wewe enjoy usaliti wako, yaani uliona unikimbie uniache pale, looh.. Mfyuuu”. Jacq alimaliza kwa msonyo.
Nilipigwa na taharuki, nikachomoka pale ndani na kufungua mlango, nikaangalia kulia na kushoto, nikaanza kutimua mbio kuelekea geti la ile gesti.
Kabla sijalifikia, geti lilifunguliwa na kuingia askari watatu pamoja na mamaake Jacq (huyu namfahamu vizuri ingawa yeye hanifahamu) na mtu mwingine wa makamo.
Nikanyong'onyea sana., nikainama na kushika magoti yangu huku nikihema kwa nguvu sana..
“Nimekwisha, Mungu niokoe...” Nilijisemea moyoni.
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Itaendelea...
 
*HIRIZI YA MAHABA*

Na:

Mdharuba, J.K. & Saire, N.M.
0718274130
0653686008
*SEHEMU YA TANO*
Wale askari wawili walionekana kunigundua mara moja na kuongeza mwendo kuelekea pale nilipokuwa nimesimama.
“Bwana Jay uko chini ya ulinzi, tuelekee kituoni kwa mahojiano”. Alisema askari mmoja huku yule mwenzake akinikamata mkono wangu wa kushoto kwa nguvu sana kama vile nilimwambia nina mpango wa kuwakimbia. Akatoa pingu kwa mkono wake mwingine na kutaka kunifunga. Nilishituka zaidi baada ya kuonana uso kwa uso na pingu ile maana sikuwahi kufungwa pingu kabla, na mama yangu anasemaga kufungwa pingu ni mkosi. Hivyo, nikaanza kujitetea nikikwepesha mikono yangu kukutana na pingu ile.
“Hebu ngoja kwanza afande, nimefaya nini kwani?” niliuliza swali wakati huu mama Jacq na yule mzee ambaye sikumjua walikuwa wametufikia. Mama Jacq akadakia kujibu lile swali.
“Unajifanya hujui ulichofanya?? mimi nahangaika kusomesha mtoto, wewe unakazana kumuharibu? Mwisho wako umefika mbwa weeeh!!”. Mama Jacq alikuwa na jazba sana, hata alipokuwa anaongea alionekana kama alikuwa akitaka kunivamia ila yule mzee alikuwa akimzuia.
“Nionesheni basi nyaraka za kuhalalisha kukamatwa kwangu” niliamua kujaribu kuwaonesha mapolisi wale kuwa ninajua haki zangu, polisi mmoja akatoa karatasi na kunikabidhi. Nikaipokea na kuisoma kisha nikagundua kukamtwa kule ni halali kabisa, nikaishiwa nguvu na kukubali kuvishwa pingu ile na mwendo wa kuelekea kituoni ukaanza.
Mara mama Jacq akamponyoka yule mzee na kunichapa kofi zito mno ambalo lilitua moja kwa moja kwenye macho yangu, niliumia sana hata nikashindwa kuona kwa muda. Askari mmoja akamdhibiti vizuri mama Jacq akimtaka apunguze hasira na kuacha sheria ichukue mkondo wake.
Tulipofika kituoni askari wale wakanitaka kukabidhi vitu vyangu vyote, wakanivua na mkanda kisha wakawa wananipeleka selo.
“Afande naomba kumpigia mtu wa kuniwekea dhamana” nilitoa ombi huku nikijua fika kuwa ni haki yangu. Hivyo, wakanipa simu yangu, nikaipokea na kuamua kumpigia rafiki yangu Nira.
“simu ya mteja unayempigia haipatikani, tafadhali jaribu tena baadae” nilichanganyikiwa baada ya kukutana maneno haya, Nira alikuwa amezima simu.
Akili ikanambia mtu pekee ambaye naweza kumtaka msaada sasa ni mjomba Mwinyi, hivyo nikaamua kujaribu na namba yake huku nikomba asiwe amezima simu. Kwa bahati nzuri mjomba Mwinyi akapokea, nikamweleza kinachoendelea kwa kifupi na kumuomba aje kunidhamini. Mjomba akanijibu kuwa yuko tayari kunidhamini ila sio usiku huu, hivyo akaahidi kudamkia kituoni asubuhi.
“Duuuh! Leo nimeshalala hapa, hakuna namna nyingine” nilikubali kinyonge kabisa nikamrudishia simu yule askari akaitunza na kuendelea kunisindikiza selo.
Miongoni mwa askari waliokuwepo pale kituoni, ni msichana wa kama miaka 28 hivi ambaye pamoja na kuwa kwenye matatizo niliweza kuuona urembo wake bila kificho.
Msichana yule alionekana kuniangalia kwa huruma wakati wote, tukamuacha pale na kuelekea selo, nikafungiwa na askari yule akaondoka.
Ndani ya chumba kile cha mahabusu kulikuwa na mtu mmoja ambaye sikuhitaji kuambiwa alikuwa mlevi kutokana na harufu kali ya pombe iliyokuwemo kwenye kile chumba. Mtu yule alikuwa amelala usingizi fofofo. Alikuwa na majeraha mwilini ikionekana alikuwa amechezea kichapo kizuri muda mfupi uliopita. Nikampuuza na kuchagua kaeneo kangu nikakaa chini nikiendelea kuwaza namna ya kulitoka kasheshe hili.

Nilikuwa nimepitiwa na usingizi. Nadhani ulikuwa ni usiku mwingi sana wakati ule niliposikia sauti ya kike ikiniita “Jay... Jay....we Jay”. Nikashituka na kufumbua macho yangu na kuonana na uso wa mwanadada yule askari .
“Naaaam” Nikaitika huku nikiwa nimekaa palepale chini nikijinyoosha shingo yangu ambayo ilikuwa na maumivu kutokana na mazingira yale ya kulala nikiwa nimekaa.
“Njoo” alinitaka kusogea pale alipokuwa amesimama nami nikatekeleza.
Nikiwa nimesimama mbele yake tukitenganishwa na nondo za mahabusu ile.
“Sasa mvulana handsome kama wewe unahangaika na watoto wa shule wa nini Jay? Unaona ulivyojieletea matatizo?” Aliongea dada yule ambaye inaelekea alikuwa amekwishafutilia vizuri taarifa zangu.
“Matatizo ni sehemu ya maisha afande, ndo imeshatokea hivyo”. Nilijibu kumtoa njiani tu maana hata sikuwa na namna ya kujitetea.
“Usiniite afande bwana mi sipendi hilo jina” aliongea dada yule kwa sauti ya mitego huku akirembua macho kimahaba. Bila shaka ndere yangu ilikuwa imeshamteka dada wa watu.
“Sasa nikuite nani jamani? Dada polisi?” niliuliza kiutani akacheka na kujibu..
“Niite Mwantumu, au ungependa kuniita mpenzi?”. Kufikia hapo, nikajua kuna kitu anataka huyu dada ambaye alikuwa anavutia sana ndani ya sare ya polisi. Nikajiuliza tena swali ambalo huwa najiuliza mara nyingi “Hivi hawa askari wetu wa kike wanaweza kweli kumdhibiti muhalifu na hivi visketi vyao vya kubana na vifupi?”
“Haya my love Mwantumu, nambie” nilijaribu kumuelekeza zaidi huko ambako alitaka kuelekea.
“Inamaana Jay wanawake wakubwa hujatuona mpaka unaaamua kutembea na vitoto vya shule jamani?” aliuliza Mwantumu kwa sauti ya kimahaba.
“Wanawake warembo kama nyie hamna muda na watu choka mbaya kama mimi”.
Nikashangaa kuona Mwantumu anatoa funguo na kuanza kufungua lango lile la mahabusu.
“Njoo tuongelee huku bwana, hapa mlevi kachafua hali ya hewa na mapombe yake” alisema Mwantumu huku akitangulia na kutaka nimfuate. Kichwani mwangu nilikuwa nikijiuliza wale polisi wa kiume walikuwa wapi mpaka binti yule anaamua kufanya mambo kama yale??!!.
Tulikwenda mpaka chumba kimoja kidogo ambacho hakikuwa na kitu zaidi ya godoro dogo pale chini, hapa nikaamua kuuliza lile swali langu “Kwani wale polisi wengine wako wapi? Tusije tukaingia matatizoni”. Mwantumu akaniangalia, akatabasamu kisha akanijibu “wale ni walevi, mida hii huwa wananiacha pekeyangu, wanaenda kulewa halafu alfajiri wanarudi”. Nikashusha pumzi ya usalama. Tukakaa kwenye kale kagodoro na kuanza kuongea..
“Sasa utafanyaje Jay? Unajua ukishindwa kesi hii utafungwa miaka mingi sana?” aliuliza Mwantumu ambaye macho yake yalionesha waziwazi kuwa hakunileta huku kuongelea kesi yangu. Hivyo, nikakamata shingo yake na kumvutia kwangu. Kinywa changu kikapokea chake kisha ndimi zetu zikaanza kutambuana, mikono yangu ikipapasa mwili wake.
Mwantumu alionekana kama alikuwa na uhitaji wa muda mrefu kutokana na sauti alizokuwa akizitoa. Nikaona mavazi yake yalikuwa yananichelewesha kula kwa uhuru tunda lile ambalo lilikuwa limeiva tayari. Nikaanza kumvua kwa kasi huku na yeye akinisaidia kwa kasi ileile. Tulipomaliza kuvua ya kwake tukahamia kwenye ya kwangu. Sote tukawa watupu kisha nikaanzia pale tulipoishia.
Kifua cha Mwantumu kilikuwa kinashawishi kulimaliza zoezi lile palepale lakini nilijikaza nikaamua kumpagawisha kwanza. Ulimi wangu ukapita eneo moja baada ya jingine la mwili wake. Hatimaye ukajikuta chumvini, hapa Mwantumu alisahau tuko wapi!! Akawa anapiga kelele kama tuko nyumbani kwake, huku akikibana kichwa changu kwa mapaja yake kama vile anataka kukipasua, “baby ambaaaaa!!.. utaniua mpenzi... please naombaaa”.
Mwantumu alikuwa amechoka mateso sasa akitaka niumalize mchezo, hata mimi nilikuwa na matakwa kama yake hivyo nikateleza ndani polepole Mwantumu akinipokea vizuri na ndani-nje ikaanza.
Nilivutiwa sana na namna Mwantumu alivyokuwa anajua kujituma hivyo nikaona nimuweke juu ili nimpe uhuru zaidi ya kunionesha ujuzi wake. Mwantumu alinipa burudani ambayo sikuwahi kuipata ingawa nimetembea na wanawake wengi sana.
Ikafikia muda nikajisikia kama nakaribia kufika kileleni lakini Mwantumu akanizuia...
“usikijoe baby... ningojee kidogo” Nami nikasitisha lakini ndani ya muda mfupi tu nikajikuta nafika tena, ila Mwantumu akanizuia tena nami nikaacha kwanza, Mwantumu akaendelea kuutawala mchezo na mara yeye akataka sasa tumalize...
“tukojoe mpenziiiiii... siwezi tennaa!!”alisema Mwantumu huku akiongeza speed nami nikajiachia na tukajikuta tukifika pamoja.
Miili yetu ilikuwa ikitoka jasho tukaanza kujipepea kwa zile nguo zetu.
“Asante sana Jay, wewe ni mtamu sana” alisema Mwantumu huku akinisogelea na kujilaza kifuani kwangu.
“Wewe ndo mtamu zaidi Mwantumu, sijawahi kupata shoo ya maana kama hii” Nami nikaamua kumsifia, maana kwakweli alinipa burudani ya hali ya juu.
“Utapata wapi wakati wewe unahangaika na vitoto vya shule?” alitania Mwantumu. Tukaendelea kusifiana mpaka tukapitiwa na usingizi.

“MWANTUMUUUUUU.... MWANTUMUUUUUUU” tulishtushwa usingizini na sauti ikiita huku ikizidi kusogea karibu na chumba hiki tulichopo. “Mungu wangu, tumelala mpaka wamerudi” alisema Mwantumu.


*Story ndo kwanza inaanza, usikose sehemu ya Sita*
 
*HIRIZI YA MAHABA*

Na:

Mdharuba, J.K & Saire, N.M.
0718274130
0653686008

*SEHEMU YA SITA*
Kabla sauti ile haijafika mlango wa chumba tulichokuwepo, niliruka kutoka pale nilipokuwa nimelala. Nikanyanyua shati langu na kuanza kuvaa haraka haraka. Nikawa nimesimama pembeni. Mwantumu alikua amehamaki sana. Akakosa cha kufanya kwa muda huu mchache ambao tulijaaliwa kabla ya kufumwa rasmi.
“Hee Afande vipi tena?! Mbona sielewi??!! Alihamaki afande mmoja baada ya kutukuta pale, ambaye baadae nilimtambua kwa jina la Zassor. Muda huu Mwantumu alikua amesimama, akiwa anaiweka sawa sketi yake, huku ameshikilia shati lake la sare ya askari kwa mkono wa kushoto. Sehemu ya kifuani pakiwa wazi huku maziwa yakiwa yameshikiliwa na sidiria ya rangi ya pink.
Afande Zassor alisogelea hadi pale tulipokuwa, huku akiachia mdomo wake wazi. Haamini anachokiona. Mimi pale nilipokuwa dua zangu zote zilikuwa nimezielekeza kwa Mungu kuomba kitu kimoja tu.. Niliomba Afande Zassor asije akaona chupi ya Mwantumu iliyokuwa pembeni mwa kile kigodoro pale chini.
Lakini nahisi dua zangu hazikupokelewa, kwani katika kupitapita na kutuchunguza vizuri, Afande Zassor alifanikiwa kuikanyaga ile chupi ya Mwantumu.. Akazama na kuiokota na kuanza kuiangalia kwa umakini. Akaigusa sehemu ya mbele, ilionekana kama imelowa ingawa si sana. Mwantumu baada ya kuona hivi, akaruka na kuikwapua ile chupi kutoka kwa Afande Zassor.
“Siwezi kuamini Afande kama wewe ndo umefanya mambo haya” Zassor aliongea kisha akanigeukia mimi. Akanishika mkono na kunivuta kuelekea nje..
“Twende huku wewe falaa...”
Akanikokota mpaka nje kabisa ya kituo. Nilishangazwa na hali ya Afande Zassor baada ya kufika nje ya kile kituo. Ni tofauti na alivyokuwa pale ndani. Aliachia tabasamu huku akinifutafuta vumbi kama vile mtu anayenithamini sana. Tofauti na hapo awali.
Nje kulishapambazuka ingawa bado ilikuwa ni saa 11 kasoro alfajiri. Kama yalivyo maeneo mengi ya mikoa ya Pwani, jua huwahi sana kuchomoza.
“Kaka, hebu nambie, umewezaje kumla yule Mwantumu? Yaani siamini ujue, umewezaje wezaje?” aliniuliza Zassor tukiwa pale nje. Baada ya swali hili, nikaona ndio nafasi pekee ya mimi kutoka pale selo kwa kesi ile iliyonikabili. Cha kufanya ni kumueleza tu Afande Zassor ukweli, nikiamini ni lazima atanisaidia tu.
“Hakuna jipya kaka, ni yeye mwenyewe tu kaka” Nilimjibu jibu jepesi ili kuona kama kweli ni muhitaji wa kiasi kikubwa ama laa.
“Hapana kaka, yule demu mimi nimeshamuhangaikia sana, na bado alinitosa, na tupo wengi.. Yaani anajisikia sana” Aliweka nukta ndogo Afande Zassor kisha akaendelea..
“Sasa huwezi kuniambia eti amekutamani yeye mwenyewe, si kweli!! Maana ana dharau kwa sisi askari wenzake halafu akutake wewe Mhalifu uliye mahabusu? Wewe nambie tu, umetumia nini kumnasa, basi!!” Hapa sasa nikapata kumsoma vizuri Zassor na kumuona kweli alikuwa na shida haswa..
“Afande, sio siri, mimi natumia Ndere, kuwanasa hawa warembo”.
“Ndere?! Ni nini hiyo kaka? Sijakupata”
“Ni uganga flani hivi, unapewa hirizi, ukiwa nayo hiyo hakuna mwanamke anaweza kukukataa..!! Na sio tu kutongoza na kutokataliwa, bali unakua na mvuto kwa kila mwanamke unayepita mbele yake”. Maelezo haya ndiyo yaliyommaliza Zassor, akapata shauku ya kutaka kujua anaipataje Ndere.
“Sasa, mi naipataje kaka, daah maana wewe kwa uliyoyafanya jana usiku, tayari nshakuogopa”.
“Namna pekee ya kuipata ni mimi kukupeleka kwa mganga wangu.. Maana hata nikikuelekeza hatokufanyia hadi twende wote., na hii kesi ilivyo nzito unafikiri nitatoka leo kweli hapa?” Nilichomekea kwenye kesi yangu kuona Zassor atasemaje.
“Kaka, hapa hamna kesi wala nini, tena twende ukachukue mizigo yako uondoke mapema, mimi nitajua nasemaje..”. Sikuongeza neno, tukarudi ndani ya kituo, Afande Zassor akanikabidhi vitu vyangu na kunipa namba yake ya simu kisha akaniruhusu niondoke haraka pale kituoni.
Wakati haya yote yanafanyika sikufanikiwa kumuona Mwantumu tena. Nikahisi atakuwa amebaki kwenye kile kichumba tulipofanyia yetu.
Nikachomoka kwa kasi pale kituoni. Nikaona pikipiki ikitokea upande wangu wa kulia kunifuata. Nikaongeza spidi zaidi kuelekea njia ya nyumbani kwangu nilikopangisha. Nikasikia sauti ikiita “Mjomba unaenda?” Ndipo nikashusha pumzi za uoga na kujibu, “Naenda kaka”. Kisha nikapanda bodaboda ile huku nikimuelekeza wapi pa kumpeleka.
Nikiwa juu ya ile pikipiki ndipo nikakumbuka kumpigia Mjomba Mwinyi.
“Ndo najiandaa kuja huko kituoni mjomba” Alisema Mjomba Mwinyi mara baada ya kupokea simu yangu.
“Usije tena Mjomba, nimeshatoka pale kituoni”.
“Duuuh... Wamekuruhusuje hao jamaa?, kwahiyo unaelekea wapi saa hizi?” aliuliza kwa shauku mjomba.
“Naelekea kwangu, kupumzika” Nilijibu swali lake la pili nikijifanya kama sijasikia lile swali lake la kwanza.
“Ok, nitakuja huko basi kukusalimia nikishakunywa chai”. Aliongea mjomba baada ya kuona hakuna tena umuhimu wa kuwahi kutoka.
“Hapana mjomba, wala usije, pumzika tu.. Kama kutakua na tatizo nitakwambia”. Niliona hakukuwa na haja ya kumsumbua mjomba tena.
“Haya bwana, maisha yako unayajua mwenyewe wewe” aliongea mjomba na kukata simu.
Nilifika nyumbani na kujitupa kitandani nikitafakari mawili matatu. Hazikupita hata dakika tatu simu yangu ikaita. Nikaangalia mpigaji alikuwa Rahel, nikapokea.
“Baby mume wangu kasafiri alfajiri hii, niko njiani nakuja kwako”. Rahel hakutaka hata kunisalimia. Na kabla sijajibu chochote alishakata simu. Nikatoka na kwenda kuoga kisha nikakiweka sawa chumba changu. Nikatoa udi ambao alinipatia mganga wangu, nikachoma na kubadilisha harufu ya kile chumba. Nikakaa na kumsubiri Rahel.
Zilipita dakika chache nikasikia mlio wa sms katika simu yangu. Kabla sijafungua kuisoma mlango uligongwa. Nikainuka na kwenda kufungua mlango, naam alikuwa Rahel, nikamkaribisha na kuingia ndani huku ameshikilia kiuno changu. Tulitembea kama walevi wa gongo.
Baada ya kufika chumbani, Rahel hakuuliza chochote, wala kusema neno lolote, alitoa nguo zake zote na kubaki kama alivyozaliwa. Kisha akajitupa kitandani. Nikajikuta nasimamisha jogoo wangu ghafla sana. Nami nikaanza kuziporomosha pamba zangu kwa kasi.
Wakati naendelea na zoezi hili, mlio wa sms ulisikika katika simu yangu.. Hapa ndo nikakumbuka kuwa kuna sms ambayo sijaisoma. Nikaamua kuzisoma zote. Nikianzia na hii ya pili ambayo ilisomeka 'luv u xn' ilitoka kwa Jacq. Nikaipotezea, nikafungua ile nyingine ya kwanza ambayo ilisomeka *“Baby, pole sana kwa tukio la jana, ila yule askari wa kike uliyekutana nae hapo kituoni ni dadaangu, ameniambia umeshatoka kituoni, ila wazazi hawajui ndo wanajiandaa kuja huko.. Na mimi nasubiri watoke tu nije kwako my baby”*. Nikashusha pumzi ndefu na kuhisi kuishiwa na nguvu.
***********************************
*Usikose sehemu ya Saba*
 
*HIRIZI YA MAHABA*

Na:

Mdharuba, J.K & Saire, N.M.
0718274130
0653686008

*SEHEMU YA SABA*
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

Jumbe zile za Jacq zilinichanganya sana. Kwanza mara ya mwisho kuwasiliana na mimi alionesha kuua uhusiano wetu, sasa kwanini anarudi ghafla namna hii?.
Pia, itakuwaje kama Mwantumu ni dada yake? Na wameongea nini kuhusu mimi? Hili liliniumiza kichwa zaidi maana Mwantumu alikuwa ameingia moja kwa moja moyoni mwangu, nilianza kujihisi kumpenda kuliko wanawake wengine wote ambao nilikuwa nikitembea nao.
“Baby vipi kwani?” aliniuliza Rahel baada ya kuniona nikiwa nimezubaa baada ya kusoma ujumbe ule kwenye simu yangu.
“Aaaaah! Matatizo tu ya kidunia” nilimjibu kihuni huku nikijirudisha pale kitandani na kujaribu kujichangamsha ili kumfanya aachane na maswali ambayo alitaka kuyaanzisha. Lakini kiukweli nilikuwa nimetoka mchezoni tayari, hata sikuwa na mzuka wa kuendeleza ambacho Rahel alikuwa akikitaka, ila sikutaka kumuumiza, hivyo nikaendelea kuwepo pale nikishirikiana naye kibishi tu.
“Baby una matatizo gani kwani?” Rahel alisita kidogo na kurudia swali lake, nadhani hii ilitokana na kuniona nikicheza chini ya kiwango changu alichokizoea. Maana tayari alikwishanigusa maeneo yangu ambayo anapoyagusaga huwa ninasisimka vibaya. Ila leo hata jogoo wangu hakusimama.
Badala ya kujibu swali lake mimi nilimkamata na kumvutia kwangu kisha nikaanza kutembeza ulimi wangu mwilini mwake, mchezo ambao alikuwa akiupenda sana na mara zote ninapofanya hivyo Rahel hucheka kwa sauti ya juu sana akisisimka vibaya mno. Nilijua nikifanya hivyo hatokuwa na muda wa kuona kama sikuwa sawa na kweli nikafanikiwa.
Michezo ya hapa na pale ikaendelea na hatimaye nikaona kuwa Rahel alikuwa tayari kumalizia sehemu ya mchezo iliyobakia. Hivyo nikaamua kukamilisha. Niliendelea kuwepo juu ya kifua cha Rahel kwa kama dakika 45 bila kushusha wazungu hata mara moja wakati Rahel alikuwa ameshusha kama mara tatu hivi.
Hapa akapata tena nafasi ya kugundua kuwa sikuwa sawa, nikaona akinichomoa kutoka kifuani kwake...
“Hakuna maana ya jambo hili kuendelea kama hauenjoy, mimi sitaki kukutumia kama chombo cha ngono, nataka sote tufurahi” alisema Rahel huku akijifunika shuka kuonesha kuwa mchezo ule ulikuwa umesitishwa.
“Najua unajua kuwa ni wajibu wangu kukuridhisha na siku zote nafanya hivyo, naomba nivumilie kwa leo” niliamua kujisalimisha kwa kumwambia maneno ambayo nilijua lazima yamuingie, na kweli nikafanikiwa.
“Sawa nimekuelewa, lakini ningependa pia kuja tatizo ni nini” alisema Rahel.
“Nina matatizo kidogo ya kifamilia, ila nina uwezo wa kuyamudu, hata usijali”. Rahel akaamua kuwa mpole, tukabaki tukiongea hili na lile kama kwa nusu saa tu kisha akaniaga na kuniachia elfu hamsini kisha akaondoka akinitaka nimtafute nikiwa sawa.
“Hatujamalizana, ukiwa sawa utanitafuta” alisema Rahel akichukua mkoba wake na kutoka.

Mara tu baada ya Rahel kutoka, nikachukua simu yangu haraka na kupiga namba ya Jacq, simu haikuita sana ikawa imepokelewa..
“Hallo mpenzi” ndivyo alivyopokea simu Jacq, lengo la kumpigia nilitaka kujua kuhusu ukweli wa taarifa za Mwantumu kuwa dada yake na kutaka kufahamu kama ni kweli je wameongea nini juu yangu.
“Utanitia matatizoni wewe mtoto, angalau tutulie kidogo hii kesi ipite” nilimwambia Jacq ambae ilionekana kuona kuwa nilikuwa namwambia kitu kigumu mno.
“Mi siwezi bwana, kama vipi tutoroke tukaishi mbali ambapo hatutopata usumbufu wa familia yangu”. Alishauri Jacq bila kujua kuwa tayari nilikuwa nimetosheka naye na nilitaka penzi lile life muda wowote.
“Hapo ndipo ninapogombana na wewe, kila siku nakwambia ujifunze kuwa mwanamke wa kujitegemea, unadhani utawezaje kujitegemea ukiitupa elimu? Siku moja tutaishi kama tunavyotaka ila kwa sasa vumilia” nilijifanya kuleta busara huku nikitumia ile sauti yangu ya ukali kidogo ambayo huwa naitumia kwa mwanamke ambaye najiona kuwa nina uwezo wa kumtawala na sitaki abishane na kauli yangu.
“Sawa, mi nitavumilia ila kuonana na wewe ni lazima, sitoweza kusitisha” aliongea Jacq kwa sauti ya kudeka.
“Mwantumu ni dada yako kivipi? Mbona hukuwahi kuniambia habari zake kabla?” sasa nikauliza swali ambalo ndilo lilikuwa lengo langu hasa la kupiga simu. Nikiwa nimejua kuwa Jacq hakufahamu hata kidogo juu ya jambo nililofanya na Mwantumu kule kituoni maana kutokana na wivu alionao juu yangu tusingeongea vizuri kama angelijua jambo lile.
“Dada Mwantumu ni mtoto wa shangazi yangu yule wa Donge, amenigombeza sana mwenzio akanambia nataka kukusababishia ufungwe miaka 30” alielezea kwa kifupi Jacq.
“halafu?” nikauliza kutaka kujua zaidi.
“Akasema ataongea na mama ili hili jambo lisiende mahakamani ila akasema niachane kabisa na wewe na kama nikiendelea safari hii atanikamata yeye mwenyewe anipeleke kituoni” alielezea vizuri Jacq, nikaona hakuna ambacho kimeharibika.
“Usihofu, Mwantumu ni mtu mzuri tu naamini atanisaidia, hebu nitumie namba yake kwanza tupange mkakati wa kulimaiza hili jambo” nikaamua kumtumia Jacq kupata namba maana sikupata nafasi ya kuichukua wakati natoka kituoni, Jacq akakubali na kunitumia mara baada ya kukata simu.
“Haloo” iliita sauti ya Mwantumu baada kupokea simu.
“Haloo, nambie” nami nikitikia.
“poa, nani mwenzangu?” Mwantumu akajaribu kunifahamu nami nikajitambulisha..
“Jay anaongea”.
“Aisee, nilikuwa nawaza nitakupataje Jay, uko wapi?” aliuliza Mwantumu nikamwambia nilipoa akanitaka tuonane haraka.

Nilifika kwenye bar moja maarufu katikati ya mji ambapo Mwantumu alitaka tukutane hapo. Nikatoa simu na kumpigia kumwambia kuwa nilikuwa nimefika tayari, kumbe yeye alifika kabla yangu. Akanielekeza alipokaa nami nikaenda kujiunga naye, akaniagizia kinywaji na maongezi yakaanza.
“Aisee nimejaribu sana kumsihi mama yake Jacq kutopeleka kesi hii mahakamani ila imekuwa ngumu, sijui tufanyeje?” alinielezea Mwantumu habari ambazo zilinishtua.
“Mimi nategemea wewe unambie tunafanyaje maana mimi hata sijui nifanyeje” nilijibu.
“Cha kufanya itabidi ukimbie mji kwa muda mpaka hapo hali itakapokuwa shwari” alinipa maelezo ambayo sikuwa tayari kuyatekeleza, kabla sijajibu chochote simu yangu ikaita, nikaitoa na kukuta alikuwa ni afande Zassor.
“Haloo, mida ya saa 9 uje kituoni na mama yake Jacq atakuwepo tulizungumze hili jambo liishe” alinielekeza afande Zassor na kukata simu. Nikamjuza Mwantumu juu ya ujumbe ule....
“Hakuna ambacho kitaendelea, hawezi kuelewa kitu mama Jacq, mimi nimeongea nae sana” alisema Mwantumu nami nikamtaka asikate tamaa, tuitikie tu ule wito tuone nini kitatokea.
Saa yangu ilionesha kuwa ilikuwa saa saba na dakika kadhaa, nikaamua kurudi nyumbani kujiweka sawa kwa ajili ya kwenda kituoni saa 9. Nikaamua kumpigia mjomba Mwinyi na kumtaka ahudhurie pia pengine busara zake zingeweza kunitoa kwenye mkwamo ule. mjomba Mwinyi akakubali kuhudhuria.
Saa 9 na dakika 12 nilifika kituoni nikiambatana na mjomba, tukakuta tayari mama Jacq alikuwepo kituoni. Maongezi yakaanza, afande Zassor na Mwantumu wakiwa wasemaji wakuu wakimsihi mama Jacq kupunguza hasira na kunionea huruma kwani tayari nilikuwa nimelijua kosa langu na kuahidi kutorudia.
“Mna uhakika kuwa hatorudia?” aliuliza mama Jacq kwa ukali na wote wakajibu kuwa wana uhakika. Mara akachukua mkoba wake na kutoa simu ambayo niliitambua sana, ilikuwa simu ya Jacq. Akaonesha sms ambazo Jacq alinitumia kisha akaonesha historia ya simu ambayo nilimpigia Jacq tukaongea kwa dakika 8.
“Huyu hajakoma na hawezi kukoma mpaka nimkomeshe” alisema mama Jacq. Macho ya watu wote yakarudi kwangu, ilikuwa ni kama wananilaumu kwa kuyakoroga zaidi.
“Ni kweli nilimpigia Jacq ila ilikuwa ni kwa lengo la kumkanya kunitafuta” nilijitetea.
“Kumkanya kukutafuta sio jambo la kuchukua dakika 8, jamani naombeni huyu mtu afikishwe mahakamani kesho” alihitimisha mama Jacq na kuondoka bila kuaga.

Mara baada ya mama Jacq kuondoka, nikamuomba Mwantumu anipatie namba yake, wote wakataka kujua nikuwa na nia gani, nikawataka waniamini na Mwantumu akanipa namba.
“Haloo samahani mama tunaweza kuonana?” niliuliza baada ya mama Jacq kupokea.

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
*Usikose sehemu ya 8*
 
*HIRIZI YA MAHABA*

Na:

Mdharuba, J.K & Saire, N.M.
0718274130
0653686008

*SEHEMU YA NANE*
“Nani wewe?” Alijibu Mama Jacq na hapo ndio nikakumbuka kuwa sijajitambulisha wala kumsalimia.
“Mimi Jay” Nilijibu kwa ufupi.
“Unataka kuongea nini na mimi wewe mshenzi?” Ndilo swali lililofuata baada ya Mama Jacq kunitambua.
“Samahani mama, naomba tafaadhali tuonane”. Nilisisitiza, nikiwa najua nikionana nae na tukiangaliana machoni kwa dakika kadhaa, kesi itaisha tu.
“Tukutane hapo Kibarua Restaurant dakika kumi kutoka sasa”. Sikuwa na cha kuongeza, nikakata simu na kuagana na Mwantumu pamoja na Afande Zassor na safari ya kuelekea Stendi ya Zamani ambapo Kibarua Restaurant ilipatikana, ikaanza.
Nikafika ndani ya dakika chache tu kwani nilitumia usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda. Nilijijaza pale Kibarua Restaurant na kuangaza huku na huko. Nikafanikiwa kugundua kuwa Mama Jacq hakuwemo mle ndani. Nikatafuta kiti na kukaa. Mhudumu ambaye alivalia mavazi meupe kuanzia kichwani hadi miguuni, alifika pale nilipokaa haraka sana.
“Tukupe nini kaka?” Aliuliza muhudumu yule wa kiume kwa sauti nzito ya mkwaruzo. Nikanyanya uso kumtazama, kisha nikamjibu..
“Nipe supu kaka”.
“Supu gani? Ya kongoro, utumbo, mbuzi au ya maini?”
“Kaka, saa 10 yote hii masupu ya utumbo ya nini tena?! Namaanisha Pweza kaka, we mgeni nini hapa mjini?” Nilimjibu yule muhudumu kwa kumhisi kuwa hajielewi. Hakuongeza neno, akaondoka eneo lile haraka na kwenda kutekeleza 'oda' yangu.
Nilikua naambaza ambaza macho yangu kulia na kushoto, nikitegemea kumuona Mama Jacq muda wowote akiingia pale. Zikapita dakika kumi zaidi, si mama Jacq aliyeingia, wala muhudumu aliyeleta supu. Nikawa nipo tu pale nikishangaa.
Nikiwa katika mawazo mazito ya mambo mengi yanayonikabili, nikahisi kuguswa begani. Nikainua uso wangu na kukutana na sura ya mwanadada mweupe ambaye kimuonekano alikua ni shombeshombe, yaani mchanganyiko wa aidha muarabu au mhindi na mswahili wa sambaani. Mavazi yake yalitosha kumfahamu kuwa ni mmoja kati ya wahudumu wa hii Restaurant.
“Umeshahudumiwa?” Aliniuliza baada ya macho yetu kugongana.
“Hapana, naomba ukae hapa nikueleze kilichonitokea..” Nilimwambia huku nikimuelekeza kwa mkono akae katika kiti kilichokua mbele yangu. Akatii bila kuongeza neno lolote.
“Nimemwambia tangu mapema yule jamaa pale akuite nikuagize wewe, akakataa.. Matokeo yake nimemwambia alete supu ya pweza mpaka sasa kimya.., sasa hapa nimekaa kama mjinga yani”. Nililalama, lengo likiwa apate kunisikiliza kwa dakika kadhaa, anionee huruma, halafu nipate namba yake. Ndio, kwani hirizi ilikuwa na kazi gani nyingine zaidi ya hiyo?!.
“Ok, ngoja nikakuletee, usijali” Aliongea yule dada na kunyanyuka pale kwenye kiti. Nikamshika mkono na kumrudisha.
“Hapana, mwache tu ataleta, wewe hapa cha kunisaidia ni kitu kimoja muhimu sana..” Nilianza kuitafutia njia sahihi namba yake ya simu.
“Enhee kitu gani hicho?” Aliuliza yule dada..
“Jina lako tu..” Nilimjibu huku nikitabasamu. Nikamfanya na yeye acheke.
“Yaani wewe una vitukooo, mimi nilidhani kitu gaaniii.. Hahahaa... Ok, mi naitwa Ummul-kheir, kwa kifupi niite Ummy”.
“Jina zuri sana Ummy, asante sana kwa kukufahamu, mimi naitwa Jumanne, kwa kifupi Jay” Nikamjibu kama alivyojibu yeye, na kumfanya acheke tena.
“Hhahahah, yani wewe una vituko kweli, sawa basi karibu sana Kibarua Jay” Alionyesha uchangamfu wake.
“Nitakuwa mteja wa hapa wa kila siku endapo nitapata kitu kimoja tu” Nilifikia kuiomba sasa namba yake ya simu.
“Kitu gani tena hicho Jay, maana wewe, unaweza pia ukasema ni supu yako hahahha”.
“Hapana, namba yako ya simu Ummy, hiyo ndio muhimu kwa sasa..”
“Alaa hilo tu, nakuletea, ngoja nikahudumie mteja kwanza.” Aliongea Ummy na kunyanyuka pale alipokua na kwenda meza ya tatu. Nikamfuatilia kwa macho na kugundua kuwa mteja aliyeenda kumhudumia ni Mama Jacq, yawezekana hakuniona hapa nilipokaa. Au anahisi labda sijafika.
Nikaamua kunyanyuka pale nilipokuwa nimekaa na kwenda pale alipokaa yeye.
“Mama, mimi nilishafika muda mrefu sana” Nilimwambia Mama Jacq huku nikimtizama usoni.
“Ooh, pole sana, wakati natoka nikapigiwa simu kuwa jirani yangu mwanawe ni mgonjwa, kwahiyo nikabidi nianzie hospitali kwanza kwenda kumuangalia, kwahiyo umekaa sana hapa?”.
“Hapana, si sana mama”.
“Enhee nakusikiliza, ulikuwa unataka kunambia nini baada ya kuniharibia mwanangu?” Aliniuliza swali lile mama Jacq. Nikatia mfukoni mkono wangu na kuiminya ile Ndere yangu huku moyoni nikitaja Jina la “Mama Jacq” mara tatu.
Nilifanya hivi kwa sekunde tatu haraka haraka na kujifanya kama nimemeza mate.
“Bro, supu yako hii hapa” Ndiyo maneno niliyoyasikia kutoka kwa mhudumu baada ya zoezi langu lile la haraka haraka.
“Asante sana” Nilijibu. Na kabla sijaongea neno jingine lolote kuhusu swali la Mama Jacq, Ummy alikuja na gilasi mbili za Juisi ya parachichi, nadhani hiki ndicho alichoagiza Mama Jacq. Akaziweka pale mezani huku akiziwekea tishu chini yake. Wakati anaondoka alinifinya bega kijanja bila Mama Jacq kuona. Nikahisi katika hizi Juisi zilizoletwa kumeambatanishwa na namba ya simu, kwahiyo nikaongeza umakini.
“Mama, sio siri naomba unisamehe sana, maana sikuwa najua kuwa Jacq ana mama mrembo kama wewe, wala nisingehangaika nae yeye, ningekutafuta wewe mwenyewe” Niliongea wakati nimemaliza kupeleka kijiko kimoja cha supu kinywani kwangu, nikimpiga jicho la wizi Mama Jacq. Hakuongea neno lolote, aliendelea kunitazama tu. Nikaona niendelee.
“Taarifa za kuwa mumeo ni balozi wa nchi hii kule Sweden ninazo, na najua ni jinsi gani uko mpweke sana mwaka mzima. Na najua ni jinsi gani mumeo analazimisha uishi maisha ya kawaida licha ya nafasi uliyokuwa nayo, naomba niwe mfariji wako mama, nimetokea kukupenda sana”. Nikaweka nukta ndogo hapo nikijua sasa Mama Jacq atasema neno lolote.
“Unajua wewe Jay nashindwa kuelewa kwanini hizi dakika chache nilizokaa na wewe hapa nakuona tofauti sana sijui kwanini..?!! Yaani nakuona kama hujanifanyia chochote kibaya, maneno unayosema yanaingia moyoni mwangu kabisaa...” Alianza kuongea kwa hisia mama Jacq, nikajua kazi nimeshaimaliza. Kabla sijaongeza neno nikashtuka na kauli aliyoitoa Mama Jacq.. “Tuondoke hapa, sio sehemu sahihi kwetu kwa sasa”.
Japo nilishangaa sana, lakini sikuwa na cha kufanya zaidi ya kufuata amri yake. Wakati huu ile supu nilishaimaliza. Juisi nilikuwa nimeinywa nusu, nikaondoa ile glasi na kuchukua tishu iliyokuwa chini yake. Nikaikagua vizuri nikakuta imeandikwa namba ya simu, chini yake ikiwa na maneno *Lakini nimeolewa*. Nikatabasamu huku nikijisemea moyoni.. "cha mtu huliwa na mtu bana, chuma ndo huliwa na kutu".
Wakati huu Mama Jacq alishanyanyuka pale alipokuwa amekaa.
Tukatoka, Mama Jacq mbele mimi nyuma. Nikiwa sijui mama Jacq ananipeleka wapi. Tukaingia katika taxi moja pale nje ya Kibarua Restaurant, kisha nikamsikia mama Jacq akimwambia dereva “Regal Naivera”. Sikutia neno lolote, nilijikohoza kidogo tu. 'Jamaa' yangu huko ndani ya boxer nikamsikia akifurukuta kuashiria nafasi haimtoshi ndani ya boxer. Nikajua sasa supu ya pweza inaleta majibu.
“Vyumba vipo?” Aliuliza Mama Jacq pale mapokezi mwa Regal Naivera Hotel.
“Ndio” Alijibu mhudumu wa kike ambaye baada ya kumuangalia mara moja sikuvutiwa naye. Mama Jacq akafuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kujaza katika kitabu cha wageni. Tukazama chumba namba 103. Chumba kilichokuwa na kitanda kikubwa cha 5×6, sofa nzuri, meza ya kioo, kabati, choo safi na AC ilipuliza vizuri sana chumbani mle.
“Jay, nakupa penzi langu kwa lengo moja tu-usimsumbue mwanangu, muache asome” Alisema mama Jacq huku akigeuka na kumuomba nimsaidie kumfungua sidiria yake ya rangi ya bluu bahari. Sketi pamoja na blauzi alishavivua kitambo sana.

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
*Usikose sehemu ya 9*
 
Hii hadithi daah. Kubadilisha k tu. Kama mateso. Maana hutulii. Ila jamaa hirizi inafanya kazi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom