Hadithi hii inatufundisha nini?

Qunax

Senior Member
Oct 16, 2016
100
127
Familia yetu sasa ni miaka kadhaa imepita baba amefariki mama akaolewa tena, baba wa pili akamuacha mama akaolewa tena hivyo hivyo mpaka saizi tuko na baba yetu wa 5 huyu, baba zetu wote hakuna wa kufananishwa na baba etu mzazi ambae alionyesha upendo wa dhati na kujitoa kwa familia yake, mpaka aliamua kumuachia usia mama wa kufanya hata yale anayoyaona yanafaa ambayo yako nje yake yeye kama baba ili tu kuimudu familia. Alikuwa na hekima kama za nabii Suleiman, hawa baba zetu wengine wengi walimuoa mama kwa kuwa walijua familia yetu ina mali nyingi, kuna ambae alikuwa anamtesa mama lakini watoto anatupenda na kutujali, kuna ambae halikuwa hajali kabisa familia yetu tumekula hatujala ye hufanya tu mambo yake lakini familia haikuyumba,kuna ambae yeye pale nyumbani hata kaka etu mmoja aliekuwa anaiba vitu nyumban na kwenda kiviuza mtaani wala alikuwa hajali, baba yetu huyu wa sasa ni mzuri anaonyesha nia nzuri ya kuikuza familia yetu lakini tayari kaikuta familia ina watoto wengi, na wengi wana tabia chafu, kakuta maadili na maagizo mengi yalioachwa na baba zetu wa nyuma yamevurugika, alipokuja watoto tulikaa kimya kama ilivyo desturi ya watoto kuwa na nidhamu kwa wazazi, na alituahidi kusawazisha kila kitu kukiweka sawa,akatufuta machozi kwa ahadi zake,Lakini kuna Majukumu ambayo kawapatia kaka zetu na dada zetu wakubwa katika familia yanafanya watoto wadogo tukumbuke baba zetu wa nyuma, japo nao tuliwaona hawafai lakin tunasema afadhali lawama zile kuliko fedhea hizi, nakumbuka baba etu mzazi na baadhi ya baba zetu wengine tulikuwa tunakaa nao kuota moto jioni, na kila mtoto alikuwa anaeleza shida zake kwa uwazi na uhuru wa kutosha, lakin baba etu wa sasa ukimuongelesha anakuzaba kibao anakwambia huna heshima, baba yetu mzazi aliacha mali nyingi sana na kuacha usia vyote viwe kwa faida ya watoto wake lakin kaka zetu na dada zetu wanatumia mali hizo vibaya wametusahahu wadogo zao wao uchumi wao umepanda lakin sisi shuleni kwetu tunakosoma hakuna vyoo.kaka zetu walibebwa na mama mgongoni kwenda kliniki lakini leo hii kaka zetu na dada zetu hao hao wanamsema mama ni mvivu hafanyi kazi ndo maana masikini afanye kazi ili apate kipato, sisi watoto wanatwambia tujiajiri, baba yetu wa sasa licha ya kuwa na msimano na nia nzuri lakini nae hana sauti kwa wale ndugu zetu wakubwa kwa kuwa aliwakuta washaota mbawa.
R.I.P (Return if possible) baba wanao tunaumia na tumechoka.
 
Tatizo lipo kwenu watoto. Mnaacha watu wa ukoo mmoja hao hao ndo wanamuoa mama yenu. Ukoo wenyewe ushaonekana una matatizo na una wachawi kibao.. Acheni mama yenu aolewe koo zingine bhana
 
Tatizo lipo kwenu watoto. Mnaacha watu wa ukoo mmoja hao hao ndo wanamuoa mama yenu. Ukoo wenyewe ushaonekana una matatizo na una wachawi kibao.. Acheni mama yenu aolewe koo zingine bhana
Ameen nlikuwa na was was kama nitaeleweka na wasomaji naona CITY Owil umenielewa
 
Back
Top Bottom