Hadithi hadithi

Verdy CB

Senior Member
Joined
Mar 19, 2013
Posts
149
Reaction score
67
.
SABABU YA NYANI KUKOSA NGOZI MAKALIONI
Hadithi hadithi...
Hapo zamani kidogo mbwa alikosea njia akaingia mbuga ya wanyama ya Serengeti, simba akamuona kwa mbali akajisemea,
"Haka tena kanyama gani? Ngoja nikaonje labda katamu....!!!!"
Akaanza kukasogelea kambwa, mbwa ghafla akamuona simba akahisi hatari, akataka kukimbia ghafla akaona mifupa mbele yake akainama akaanza kujifanya anatafuna, huku akijisemea....
"Dah nyama ya simba tamu sana.... Loh!!!"
Simba kusikia hayo akashtuka akajua hakakamnyama kashenzi. Akaanza kuondoka taratibu huku kafyata mkia....
Nyani alikuwa juu ya mti alikuwa kaona mchezo mzima, akaona hapa ndio mahala pakujipatia mihela toka kwa simba, akamuwahi simba na kumwambia...
"Bwana mkubwa ee unaogopa bure, nifwate mimi ukale kale kanyama, hakana lolote, mbwembwe tu zile...."
Wakati wanakuja mbwa si akawaona akajua mambo yameharibika, walipokaribia mbwa akajidai hajawaona ila amekasirika huku akinung'unika...
"Huyu nyani yuko wapi?!? Sinilimtuma aniletee simba mwingine?!?"
Duh!!!! Simba kusikia hivyo akamng'ata nyani nyuma kwenye makalio kwa hasira nakutokomea porini....
Na ndio maana mpaka leo nyani hana ngozi kwenye makalio aliipoteza siku hiyo....
Na hadithi yangu imeishia hapo!!!!

******
Nyongeza
MSICHANA: Namchukia mvulana wangu.
ZUZU: Kwa nini?
MSICHANA: Yaani ni mtu wa bei rahisi sana, hawezi hata kuninunulia dinner. Hivi wanaume wote mpo hivyo?
ZUZU: Hapana. huyo yeye tu, sisi hatupo namna hiyo. Hata mimi sipo namna hiyo.
MSICHANA: Nakwenda kuachana nae leo hii hii.
ZUZU: Sawa. Ila utakapoachana nae, unaweza kuja kwangu, sina msichana halafu nakuhitaji sana.
MSICHANA: (Akasimama na kutaka kuondoka, ZUZU akamshika mkono)
ZUZU: Ndio unataka kuondoka? Unakwendawapi sasa?
MSICHANA: Nakwenda kuvunja uhusiano na yeye ili niwe nawe kwa uhuru.
ZUZU: Hapana. Huwezi kuondoka.
MSICHANA: Kwa nini?
ZUZU: Sasa ukiondoka nani atakayelipia hiki chakula tulichokula?
Nmeziona CUA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…