Hadithi: Gamboshi

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,446
SEHEMU YA 01:

Baada ya kuwa ametumia miaka miwili nchini Irak akiripoti vita vya Ghuba kupitia televisheni ya SkyNews na kupokea Tuzo ya Kimataifa ya Boldness Award iliyoambatana na zawadi ya Dola za Kimarekani milioni moja, mwandishi mahiri wa Kimataifa Richard Massawe, anarejea nchini Tanzania kwa kazi moja tu; kumwoa mwanamitindo na mwanamuziki maarufu wa Kitanzania katika muziki wa Soul, Anitha Johnson.

Wakimaliza kufunga ndoa yao, lengo ni kurejea katika Jiji la Los Angeles, Carlifonia yaliko makazi ya Richard kwenye kitongoji cha Pasadena. Wazazi wake wanafurahi kupita kiasi, kitendo cha kuwaacha wanawake wa Kizungu kwenda kumuoa mwanamke wa Kitanzania kwao ni heshima kubwa, wamejisikia kuheshimiwa.

Je, kitatokea nini katika maisha ya watu hawa wawili? Anza hadithi hii ili upate kujifunza maajabu ya nguvu za giza katika kijiji maarufu cha kufikirika cha Gamboshi, kilichopo huko Shinyanga ambako indaiwa kuna watu wanaishi bila kuonekana baada ya kuondoka duniani wakidaiwa kufa.

Ukumbi wa Mwanza hoteli ulikuwa umefurika idadi kubwa ya watu, hapakuwahi kuwa na harusi hata moja iliyowahi kujaza ukumbi huo kama siku hiyo. Ulipambwa kwa maua mazuri ya kuvutia, wapambaji wakiwa ni Kampuni ya Dotnata Decoration ya Dar es Salaam, hakika ukumbi ulivutia, haikuwa rahisi kama mtu angechukuliwa kutoka Uingereza akiwa amefungwa na kitambaa machoni akaingizwa ndani ya ukumbi kisha kitambaa kuondolewa, kuelewa kwamba alikuwa Mwanza, Tanzania.

Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya ndani na nje ya Tanzania walikuwa wamefurika, kulikuwa na kamera kwenye kila kona, watu wakifuatilia harusi ya mtu maarufu katika tasnia ya habari duniani, aliyetokea Tanzania na kuiitingisha dunia kwa kuripoti mambo mazito yaliyowaogopesha watu wengine.

Baraza zima la Mawaziri lilikuwa limesafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kuhudhuria harusi hiyo, kwa harakaharaka mtu angeweza kufikiri kwa kuwepo hapo, labda alikuwa Bungeni Dodoma maana kila mtu alipogeuza shingo kuangalia kushoto na kulia, macho yake yalikutana ama na Waziri kamili au Naibu, hiyo ndiyo ilikuwa picha halisi ndani ya ukumbi wa Makutano.

Watu wote walikuwa wamependeza, wanaume wengi wakiwa ndani ya suti nyeusi na tai za rangi ya pinki, wanawake magauni ya rangi ya maruni yenye kumeremeta, kila kitu ndani ya ukumbi kilikuwa katika rangi zilizopangiliwa sawasawa.

Richard akiwa ameketi mbele pamoja na mke wake Anitha ndani ya shela ya kumeremeta iliyonunuliwa kutoka Marekani moja kwa moja tena si dukani bali kwa mbunifu maarufu wa mitindo raia wa Ufaransa aishie Marekani, Pierre Martin aliyeitengeneza maalum kwa ajili ya Anitha!

Macho ya akinamama wengi yalikuwa kwenye vazi hilo lenye kuvutia lililofanana kabisa na Tausi mweupe. Uso wa Anitha ulikuwa umejaa tabasamu, hata yeye hakuamini alichokuwa akikishuhudia mbele ya macho yake, ilikuwa ni sawa na kuota ndoto, maisha yaliyokuwa yakija mbele yake yaliashiria raha mustarehe, hakuwahi kukanyaga Marekani kabla, hivyo pamoja na kuwepo ukumbini akili yake ilikuwa ikifikiria maeneo kama Hollywood, Beverly Hills na kwingineko, alikuwa na uhakika kwa kuingia Marekani peke yake ungekuwa ufunguo wa yeye kufika kwenye umaarufu wa dunia badala ya Tanzania peke yake.

“Thanks God! My dreams are now going to be reality, I am going to be a megastar!” (Namshukuru Mungu! Ndoto zangu zitatimia, sasa nitakuwa nguli wa Kimataifa) aliwaza Anitha akimwangalia mume wake usoni, tabasamu zao zikagongana.
Hapakuwa na mtu asiyemfahamu Anitha nchini Tanzania, alikuwa miongoni mwa watu hamsini maarufu walioitwa The Tanzanian Top 50 Celebrities na kilichomfanya afike alipokuwa maishani mwake ni uanamitindo na kazi yake ya muziki.

Alizaliwa kutoka kwa mama Mtanzania na baba Muingereza, mchanganyiko wake huo wa rangi ulifanya uzuri wake uongezeke! Hakika alikuwa mwanamke mrembo si kwa sura tu bali pia umbile lake ambalo wengi waliliita namba sita, nyuma akiwa ameumbika kisawasawa.

“Hakika ameoa mwanamke mzuri, sikuwahi kufikiria hata siku moja kuna wanawake warembo kiasi hiki huku Afrika!” mmoja wa wageni kutoka Marekani alimwambia mwenzake.

“Sio utani, binti kaumbika, utafikiri namwangalia Alicia Keys au Beyonce? Siamini!”
“Ndio maana Richard alikimbilia huku kuoa, Marekani yote hakuona!”
“Kweli kabisa”

Maongezi ya watu hao yalikatishwa na sauti ya MC aliyekuwa akimkaribisha Anitha ukumbini, katika ratiba kulikuwa na sehemu ambayo alitakiwa kumwimbia mume wake wimbo maalum. Watu wote wakatulia kusubiri, Richard akamnyanyua mke wake taratibu kutoka kitini na kumuongoza hadi katikati ya ukumbi ambako alikabidhiwa kipaza sauti na kukohoa kidogo kisha kuendelea;

“This song is a dedication to my dear husband Richard, I love you so much and nothing gonna change my love for you!” (Wimbo huu ni maalum kwa mume wangu mpendwa Richard, nakupenda sana na penzi langu kwako halitabadilika!) akaongea na ukumbi ukafunikwa ka vifijo, nderemo na vigelegele, ilikuwa ni shangwe ya ajabu, midundo ya wimbo uitwao Nothings Gonna Change My Love For You wa George Benson ilianza kusikika na Anitha akaanza kuimba:
If I had to live my life without you near me
The days would all be empty
The nights would seem so long
With you I see forever oh, so clearly
I might have been in love before
But it never felt this strong
Our dreams are young and we both know
They’ll take us where we want to go
Hold me now, touch me now
I don’t want to live without you.
Chorus 1
Nothing's gonna change my love for you
You oughta know by now how much I love you
One thing you can be sure of
I’ll never ask for more than your love.
If the road ahead is not so easy
Our love will lead the way for us, like a guiding star
I’ll be there for you if you should need me
You don’t have to change a thing
I love you Richard just the way you are.
(Kama ningetakiwa kuishi maisha bila wewe karibu yangu,
Siku zote zisingekuwa na cha maana,
Usiku ungeonekana mrefu kuliko kawaida,
Nikiwa na wewe naona milele waziwazi,
Inawezakana nilishapenda kabla,
Lakini halikuwa penzi zito kiasi hiki
Ndoto zetu bado ni changa, sote tunafahamu,
Lakini zitatupeleka tunakotaka kwenda,
Nikumbatie, niguse sasa,
Sitaki kuishi bila wewe,
Kiitiko;

Hakuna kitakachoweza kubadilisha penzi langu kwako,
Unatakiwa kufahamu tangu sasa ni kiasi gani nakupenda,
Kitu kimoja lazima unaweza kuwa na uhakika nacho,
Sitakuomba kitu chochote zaidi ya penzi lako,
Kama njia mbele yetu itakuwa ngumu,
Penzi letu litatuonyesha njia kama nyota kiongozi,
Nitakuwepo kwa ajili yao, kama utanihitaji,
Hauhitaji kubadili kitu chochote,
Nakupenda Richard ulivyo, si kwa chochote bali jinsi ulivyo…)

Anitha aliimba kwa sauti ya kasuku, akionyesha hisia kali, ukumbi ulikuwa kimya, hakuna aliyeshangilia maneno aliyokuwa akiimba yaliwachoma watu mioyoni, alikuwa akiusema moyo wake!

Richard alishindwa kuvumilia akamnyanyua asiendelee kupiga magoti mbele yake, machozi yalikuwa yakimbubujika, hata yeye alimpenda Anitha kuliko kitu kingine chochote, wakakumbatiana! Hapohapo miale ya mwanga wa kamera za wapigapicha ilimulika, kwa muda wa karibu dakika kumi waliendelea kukumbatiana huku vigelegele vikisikika ukumbini, walipoachiana walitazamana na kutabasamu.

“I love you Anitha!” (nakupenda Anitha)
“Nakupenda pia Richard!”
Je, nini kitaendelea?

Fuatilia kesho. Usikose kusoma hadithi hii hadi mwisho ili uweze kujua ni kitu gani hufanyika kwenye kijiji cha Gamboshi, kinachodaiwa kuwa Makao makuu ya wachawi Tanzania nzima, huko ndiko Malkia wao anakoishi.

Itaendelea baadae nikitoka darasani.
 
SEHEMU YA 02:

ILIPOISHIA
“Nakupenda Anitha!”
“Nakupenda pia Richard, moyo wangu wote upo kwako, hakuna kitakachobalidi
sha pendo langu kwako, katika shida ama raha, daima nitakuwa wako!”
“Duh! Wewe kweli mwanamuziki, hapo pote umemwaga mashairi!” Richard akatania kwa sauti ya chini chini wote wakacheka.
Ukumbi ulikuwa umegubikwa na vifijo, nderemo na vigelegele, Wimbo wa Anitha ulikuwa umewasisimua watu wote, waliokuwa wakilia tayari walikuwa wakijifuta machozi ili kusubiri hatua iliyokuwa ikifuata, kila mtu alikiri kwamba kweli Anitha alikuwa na uwezo wa kuimba na alistahili tuzo zote alizowahi kupokea.
MC, Clay aliyekuwa akiendesha shughuli hiyo aliwarudisha maharusi moja kwa moja kwenye viti vyao ambako waliendelea kuketi wakinywa vinywaji taratibu na kuongea maneno machache, hakika ilikuwa ni siku ya furaha kwa wote wawili.
Saa sita kamili MC alitangazwa kuwa muda wa bwana na bibi harusi kuondoka ukumbini kwenda kupumzika kwenye Hoteli ya Tilapia ulikuwa umewadia, Anitha na Richard wakaongozwa moja kwa moja hadi nje ya ukumbi ambako waliingia kwenye gari na msafara ukaanza safari kwenda kwenye hoteli Tilapia iliyokuwa ufukweni mwa Ziwa Victoria, huko wote wawili walishuka na wapambe pamoja na wageni waalikwa wao na kusindikizwa hadi vyumbani kwao ambako walilala mpaka asubuhi ya siku iliyofuata.
Hoteli nzima ilikuwa imejaa wageni wa Richard toka sehemu mbalimbali za Tanzania na nje waliokuwa wamekuja kuhudhuria harusi, asubuhi hiyo wakati wa kustaftahi walianza kuongea juu ya mpango wa fungate lao, ambalo Richard alipanga kusafiri hadi kwenye hoteli ya Kitalii iitwayo Kijereshi ambayo iko mwanzo wa mbuga ya Serengeti upande wa Mkoa wa Mwanza baada tu ya kuondoka kwenye mji uitwao Lamadi, hakutaka kwenda nchi za nje, yeye na wageni wote aliongozana nao walipenda kutembelea mbuga hiyo kuona wanyama. Siku nne baadaye, msafara kuelekea kwenye fungate ulianza, wakawasili na kupokelewa kwenye hoteli hiyo iliyojificha katikati kabisa ya mbuga, wote iliwavutia.
Siku hiyo hawakutoka, lakini iliyofuata Richard akiwa amevaa fulana ndogo iliyoacha mabega wazi pamoja na bukta, Anitha akiwa ndani ya suruali nyepesi ya lineni na kiblauzi cha rangi ya pinki, wote wakiwa wamevaa miwani ya rangi nyeusi sababu ya jua walipanda ndani ya gari la kifahari aina ya Hummer nyeusi, Richard alinunua gari hiyo nchini Marekani mwaka mmoja kabla na kuituma nyumbani ili awe akiitumia anapokuja likizo, hakuwepo mtu mwingine mwenye gari ya aina hiyo katika nchi nzima ya Tanzania! Taratibu walikula kiyoyozi wakiendelea kusikiliza muziki na kuzama porini wakiangalia wanyama, Anitha alikuwa ametokeza kwa juu akipiga picha kila alipoona kitu kizuri.
Kwa masaa manne walitembea huku na kule bila kuchoka, kila kitu kiliwavutia hatimaye wakaamua kuegesha chini ya mti wenye kivuli na kuanza kupigana mabusu, katika hali ambayo hawakuitegemea ghafla walishtuka mvua kubwa ikianza kunyesha, iliambatana na radi na vimbunga! Wote walishindwa kuelewa ilitokea wapi kwani hapakuwa na dalili ya mawingu.
“Hii mvua sijui imetokea wapi?” Anitha aliuliza.
“Achana nayo sisi tuendelee kula raha zetu!”
“Lakini tunahitaji kurudi hotelini, giza litaanza kuingia!”
“Hakuna shida, hapa nilipo nina bastola iliyojaa risasi!”
Walibaki hapo kwa masaa matatu, ndipo Richard akaamua kugeuza gari ili waondoke, akashangaa tairi zilipozama udongoni kumbe sehemu waliyokuwa wameegesha palikuwa na udongo mbaya wa mfinyanzi, gari ikawa imekaa ardhini! Akijiamini, Richard alicheka na kuingiza gia nyingine fupi iliyoko mbele ya ndefu, hiyo iliitwa four wheel driver, kwa ajili ya kuzungusha tairi zote ili zing’oke kwenye tope, cha kushangaza zaidi haikusaidia, gari ikazidi kutitia! Moyo ukaanza kumdunda.
“Sijui tutafanya nini?”
“Wapigie simu waje watusaidie!”
“Sawa!” aliitikia Richard lakini alipotoa simu yake hapakuwa na mtandao eneo hilo.
“Vipi?”
“Hakuna network!”
“Sasa tutafanyaje?”
“Subiri!”
“Unataka kufanya nini?”
“Acha nikaangalie chini, inawezekana kuna tatizo!”
“Richard, tuko mbugani unaweza kuliwa na wanyama?”
“Sasa tufanyaje mke wangu?” aliuliza Richard huku miungurumo ya Simba ikisikika.
“Tusubiri mpaka asubuhi!”
“Hapana, acha nijaribu kufanya kitu!” aliongea Richard na kuchukua bastola yake ikiwa imewekwa tayari na kushuka hadi chini ambako alizama uvunguni mwa gari na kugundua kulikuwa na mzizi ulioshikilia tairi, kwa furaha akatoka uvunguni na kuzunguka hadi nyuma ambako alichukua shoka na kurudi kuukata, alipomaliza aliwasha gari na kuigiza gia fupi, mara moja gari ikang’oka na safari ikaanza.
“Hureeee!” Anitha alishangilia.
Usiku mzima walisafiri bila kufika hotelini, kulipokucha walishangaa kujikuta bado wako pale pale! Bila kusogea hata hatua moja, wakaangaliana kwa mshangao, walishindwa kuelewa ni jambo gani lilikuwa limetokea, walikuwa wameota ndoto? Walijiuliza swali hilo na kugundua haikuwa kweli, maana shimo walilokuwa wamezama lilikuwepo nyuma yao.
“Nini kimetokea?”
“hata mimi sielewi mke wangu, nimeendesha gari usiku mzima nashangaa kujikuta bado tuko hapa?”
“Mh! Hebu washa tena tujaribu” Anitha alishauri akiwa amejawa hofu, halikuwa jambo la kawaida hata kidogo, hakuna alichokifikiria akili mwake zaidi ya nguvu za giza.
Katika hali ya kushangaza kabisa, gari likaruka kama limeachiwa na watu, safari yao ikaanza na kusafiri kwa karibu masaa matatu bila kuongea chochote, mioyo yao ikiwa imejawa na hofu. Kwenye kona kali iliyokuwa mbele yao, Richard hakuwa mwangalifu, akashangaa kukutana uso kwa uso na lori kubwa aina ya Benzi ambalo liligonga gari lao na kupanda hadi juu, wakagandamizwa.
“Richard nisaidie nimebanwa!”
“Hata mimi nimebanwa!”
Je nini kitaendelea?
Je ni kitu gani kimetokea?

ITAENDELEA BAADAE
 
SEHEMU YA 03:

ILIPOISHIA
“Ri..cha…rd!” Sauti ya Anitha akiomba msaada iliendelea kuita lakini Richard hakuitikia ulitokea ukimya wa ajabu tangu aongee mara ya mwisho na kudai hata yeye alikuwa amebanwa.
Dereva wa lori alishuka haraka akiwa na mikono yake yote miwili kichwani na kuangalia kilichotokea, machozi yalimtoka, hakuwa ametegemea kabisa kulikuwa na gari maeneo hayo, siku zote alipita hapo akiendesha gari lake kwa kasi ya ajabu bila kupata matatizo na ndicho alichokifanya siku hiyo akijua kusingekuwa na gari kwenye kona.
Aliendelea kusimama akiishangaa picha iliyokuwa mbele yake, gari la Richard na Anitha lilikuwa limeingia chini ya lori na kupondwapondwa kabisa, akajaribu kuchungulia ndani ili apate kujua hali za watu waliokuwemo ndani zilikuwaje, alichokiona kilimtisha, wote walikuwa wamebanwa kwenye vyuma, tairi za benzi zikiwa juu ya viti vya mbele. Akawa na uhakika kabisa alikuwa ameua.
Katika maisha yake yote udereva ilikuwa ni mara ya kwanza macho yake kukutana na gari aina ya Hummer zaidi ya kuiona kwenye video za wanamuziki wa nje, kitendo hicho tu peke yake kilimfanya aamini kabisa watu aliowaua kwa uzembe wake kwenye ajali hiyo hawakuwa wa kawaida, walikuwa matajiri mno, hivyo kuendelea kusubiri hapo kulimaanisha yeye kwenda jela jambo ambalo hakutaka litokee. Alijipa moyo na kusema ni heri wangekuwa hai angewabeba kuwapeleka hospitali lakini kwa sababu walikuwa wamekufa hakuwa na sababu ya kusubiri matatizo.
“Bukalindilagwa bugali,ete kesi!”(Huwa unasubiriwa ugali si kesi) aliongea kwa Kisukuma na kuanza kurudi kinyumenyume huku akiangalia huku na kule mpaka kwenye gari, akapanda na kuwasha kisha kuingiza gia iliyoandikwa R, gari likaanza kurudi nyuma likiliburuza gari la Richard mpaka akafanikiwa kuliondoa lori lake na kuingiza gia iliyondikwa D na kuondoka kwa kasi ya ajabu kwenda mbele akiliacha gari la akina Richard peke yake porini. Mwili wote ulikuwa ukimtetemeka kwa hofu, alikuwa ameua watu wawili asiowafahamu.
***
Hotelini Kijereshi hofu ilikuwa imemwingia kila mtu, jua lilikuwa limeanza kuzama na giza kuingia bila Richard na Anitha kurejea kutoka matembezini na mvua kubwa ilikuwa ikinyesha, hii iliwatia wasiwasi mkubwa wafanyakazi wa hoteli, ikabidi wapige simu kwa Meneja wa Mbuga aliyefika hotelini na kundi la maaskari la Wanyama pori wakiwa kwenye magari mawili na kukutana na uongozi wa hoteli pamoja na wageni waliomsindikiza Richard kwenye fungate lake.
“Waliondoka saa ngapi?” Meneja wa Mbuga aliuliza.
“Kwenye saa nne hivi”
“Saa nne ya asubuhi?”
“Ndio”
“Walikuwa na nani?”
“Peke yao!”
“Yaani mnawaaacha wageni wanaondoka kwenda Mbugani peke yao hakuna waongozaji?”
“Tulijua wanakwenda karibu na ndivyo walivyosema!”
“Siwezi kuwadanganya, nahisi hapa kuna tatizo! Mmejaribu kuwapigia simu?”
“Simu zao hazipatikani, tunahisi ni sababu ya mtandao kutopatikana huko waliko!”
“Basi watakuwa wamekwenda mbali sana, maana maeneo ya karibu yote mitandao yote ipo!”
“Kwa kweli hatujui, tunahitaji msaada wako!”
“Sasa sikilizeni, hapa hakuna kazi nyingine tunayoweza kufanya isipokuwa kuingia porini kwenda kuwatafuta, kama mko tayari twendeni!”
“Tuko tayari!”
“Basi ingieni kwenye magari tuondoke!”
Wote wakapanda, safari kwenda porini ikaanza, saa zao za mkononi zilionyesha tayari ilikuwa ni saa mbili na nusu usiku. Kazi hiyo ilifanyika mpaka asubuhi bila Richard na Anitha kupatikana, wasiwasi ukazidi kuongezeka, hofu ikawa pengine walikuwa wameliwa na wanyama wakali lakini Meneja wa Mbuga alipotajiwa aina ya gari waliyoondoka nayo, wasiwasi huo ukamwondoka .
“Rajabu!” Meneja wa Mbuga alisimamisha gari alilokuwa akiendesha kando ya la pili na kumwita dereva walipofika njia panda.
“Naam bosi”
“Pita Mashariki, mimi napita Magharibi tutakutana mbele, mawasiliano yetu yawe ni ya redio tu! Mkifanikiwa kuwaona huko tuwasiliane haraka iwezekanavyo”
“Sawa bosi!”
Msafara ukagawanyika mara mbili kama walivyokubaliana, kazi ikaendelea kwa masaa karibu matatu bila redio kuita wala kupokea taarifa kwamba upande wa pili walikuwa wamefanikiwa kuliona gari, wote walikuwa wamechoka na njaa iliwasumbua. Meneja akaanza kudai warudi hotelini kwanza kula ndipo waje waendelee na kazi hiyo. Gari nzima wakakubaliana lakini wakati akigeuza gari, redio ilisikika ikiita na sauti ya dereva Rajabu ikatambulika, alikuwa akiita huku akilia.
“Nini tena?”
“Bosi, wamekufa!”
“Mmewapata?”
“Ndio!”
“Wamekufaje?”
“Gari lao limegongana na gari jingine ambalo hatulijui na kubondwabondwa, wapo ndani ya gari wamebanwa, miili yao imesagwa vibaya, sijui hata kama tunaweza kuwatoa humu ndani, naomba uje tushauriane, ni ajali mbaya mno kuliko zote ambazo nimewahi kuziona katika miaka yote thelathini ambayo nimeendesha gari barabarani!” Rajabu aliongea akilia kwa uchungu na sauti za watu wengine wakilia pia zilisikika nyuma yake.
Meneja wa Mbuga hakuweza kuficha hisia zake, macho yalimtoka, jasho jembamba likamlowanisha, watu wote waliokuwemo ndani ya gari waliingiwa na wasiwasi na wengine kuanza kulia kwa uchungu kutoka na habari hizo. Haikuwa rahisi hata kidogo kuamini Richard na Anitha eti walikuwa wamekufa, baada ya harusi kubwa ya kifahari iliyofanyika mjini Mwanza, mtu yeyote mwenye akili zake timamu asingekubaliana na jambo hilo labda mpaka aone kwa macho yake.
Gari likageuzwa na kuendeshwa kwa kasi ya ajabu kuelekea mahali ambako dereva Rajabu alidai walikuwa, masaa mawili baadaye waliwasili na kukuta watu wakiendelea kulia, waandishi wa habari wakipiga picha za video na mnato kwa ajili ya vyombo vyao, mmoja alikuwa ameketi pembeni, kando yake kukiwa na kitu kama redio ambacho eria yake ilikuwa imechomolewa na kwenda urefu kama wa mita tatu hivi na alikuwa akiongea moja kwa moja na televisheni ya SkyNews kuelezea kifo cha Richard kilichoshtua dunia.
“Mungu wangu!” Meneja wa Mbuga alitamka maneno hayo baada ya kuiona gari akasogea mbele na kuchungulia ndani, Richard na Anitha walikuwa wamebanwa ndani ya gari lao, miili ikiwa imepondwapondwa kabisa, baadhi ya viungo vilikuwa vimekatika na kuanguka pembeni, yeye mwenyewe alikiri ilikuwa ni mara ya kwanza ya kuona ajali ya kutisha kiasi hicho.
“Tufanyeje?” dereva Rajabu alimuuliza bosi wake.
“Tuivute gari mpaka Kijereshi, huko tutafute gesi ili tukate gari na kutoa maiti, pia tutatoa taarifa polisi Lamadi ili wafike kutoa msaada!”
“Sawa”
“Sijui aliyewagonga ni nani masikini, wamekufa kifo kibaya tena siku mbili tu baada ya ndoa yao! Inasikitisha!”
Je, nini kitaendelea?
 
Mh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari mambo naitwa Mr Equator Nimeandika ujumbe huu kuku omba swala moja tu!
Mimi nimetengeza website ya ku share story ambayo ni http://www.equatorstory.com/
Je umekuwa ukipata tabu kupost story zako hapa?
Hili ndo suluhisho lako.
Mimi nataka nkupe nafasi ya kuwa mmoja wapo wa kwanza kutumia hii website
unda account yako na uweze kupost story yako mpya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom