Hadithi fupi: Jamani Aisha nisamehe

Hadithi fupi: Jamani Aisha nisamehe

MC Chere

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2015
Posts
586
Reaction score
400
PART 1

Toniiiiiiii,Toniiiii,Tonii twende,niliisikia sauti ya mpenzi wangu Aisha akiwa nje ikiniita usiku wa manane nami nikaitika najaaaa,nikavaa haraka kisha nikatoka nje na kumkuta na tayari tukaenda stendi ya bus ya Chinongwa kwa ajili ya kuanza safari ya kuelekea Chikukwe kwani aliniomba nimsindikize kwenye sherehe.

Lilikuwa ni busi la Najma ambalo lilikodiwa siku,abiria tulikuwa wengi,baada ya muda fulani wa safari nzuri,nikashuhudia gari likisimama mbele ya nyumba kubwa yenye umati wa watu wengi wanaosherekea,na hapo ndipo Chikukwe.

Shamra2 za kuwapokea wageni zilipamba moto,ila zilizidi tulipokuwa tukishuka sisi na nikaongozwa kwenye kiti maalumu mbele ya umati mithili ya mgeni mwalikwa.

Hakika watu walipendeza kwa mavazi na nyuso zao,ngoma ikapigwa huku nikipewa glasi ya juisi ya embe na wali kwa samaki.

Baada ya mimi kumaliza kula,ndipo mzee mmoja aliyesimama na kujitambulisha kwa jina na kuwa yeye ndiye hakimu wa eneo lile.

akatoa utambulisho wake
INAENDELEA......
 
story haina punch line..haimpi mtu hamasa ya kutaka kujua kinachoendelea..jitahidi uwe unamalizia vizuri ila mtu awe na shauku ya kusoma part inayofuata
 
PART 2

Akatoa utambulisho wake ulionifanya nibaki kinywa wazi hasa kwa hitimisho lake kuwa mimi ndiye mgeni rasmi na mtuhumiwa katika hafla hiyo na nitoe majibu kama nitamuoa/sitamuoa Aisha.

Nami nikajibu kuwa hata mnipe vitisho,sitamuoa Aisha hata kama ni mpenzi wangu.
Kwa kweli kilichofuata sikuamini macho yangu,kwani nianguka chini na kuzimia mara tu niliposikia mdundo wa nguvu wa ngoma,ile kufumbua macho,kila kitu mbele yangu kikawa ni cha ajabu,kwani macho yangu yalishugudua wato wote niliowaona ni wazuri na wamependeza kwa mavazi,sasa walikuwa uchi wa mnyama na maumbile yao si ya kawaida kwani,walikuw wana mguu mmoja na jicho moja linalotoa mwanga,na ndimi zao ndefu zitoazo moto.

Ninapoendelea kushangaa,nikakuta wananicheka huku wakirushiana kitu fulani ambacho sikuking'mua mapema,kumbe ilikuwa ni nyeti yangu,kujicheki nikakuta kupo flat,kwa kweli nikaanguka chini kwa kiwewe.
Lakini kumbe kama haitoshi,hata lile nililodhan ni bus,halikuwa bus bali ni chatu na tena maajabu zaid ni vile viti na vyakula
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom