mFuKuZa nDoTo
JF-Expert Member
- Jan 17, 2021
- 492
- 635
Inaanza kupata moto..mwendelezo
Nimeitika wito mkuu,baada ya kusikia nimeitwa nilikuja spidi hatari,,,thanx
Nimefika bosiFATINAH
SEHEMU YA SANA
Inaendelea...
Saa 10 Alfajiri fahamu zilinirudia, nikafungua macho kwa kituo. Na kwa dakika kadhaa nikabaki nimetuamisha mwili wangu tu kuiruhusu akili yangu na mwili wangu vijipange katika utaratibu wake wa kawaida. Mwili ulijawa na uchovu tele. Mdomoni mwangu ilitawala harufu ya pombe za jana.
Kitambo kidogo kikapita nikitazama dari la chumba nilichokuwamo, haikuwa nyumba niliyoizoea, hapakuwa nyumbani kwangu, hakikuwa kitanda changu, halikuwa shuka langu na kila kilichokuwamo hakikuwa changu. Nikavuta kumbukumbu vizuri siku ya jana nilikuwa wapi na ikawaje. Matukio yakaanza kujipanga moja baada ya jingine. Nilipofikia moja ya tukio nikashtuka.
Nikatazama pembeni. Palikuwa na mtu mwingine. Mwanamke. Nikapigwa butwaa kama sio mshangao.
Nikajiinua kidogo sehemu ya kiwiliwili changu nimtambue huyo mwanamke.
"Fatinah...!!!" Nikajisemea kwa sauti ya chini. Tulikuwa ndani ya shuka moja!
"Khaa!" Kisha nikajikerehesha.
Yeye hakuwa na habari, alikuwa ametopea kwenye usingizi wa pono huku kageukia upande mwingine na kunipa mgongo. Nikafunua shuka kidogo kiasi cha kuruhusu sehemu ya miili yetu kuonekana kwa urahisi. Wote tulikuwa uchi wa mnyama.
"Tumefanya mapenzi!!" Yakanitoka tena kwa butwaa lililotukuka.
Nikamgusa bega kidogo ili kumuamsha, akashtuka toka usingizini akajinyoosha kidogo na kugeukia upande wangu. Kisha akafikicha kidogo macho yake kwa uchovu wa usingizi.
"Umemkaje kipenzi changu Almas..!" Akaongea kwa sauti ya chini bila kubabaika
"Kipenzi!!??" Mshangao ukaniponyoka kwa sauti ya chini vile vile huku nikiendelea kustaajabu, sikumjibu.
"Umeamka pensi la jeje?" Akasema, sikumuelewa.
"Pensi la jeje ndio nani?" Nikamuuliza nikiwa bado sielewi hali ya mambo ilivyo.
"Ulilewa Almas..." Akasema na kuinuka akaelekea maliwatoni. Hapo nikapata kulishuhudia lile umbo lake matata la kihaya lililositiriwa na ngozi nyeusi mororo kabisa, hakuwa japo na kipande cha khanga mwilini mwake na hakujali vile vile. Alijongea kuelekea maliwatoni kwa madaha yaliyotukuka. Kwa muda nikabaki nimesinyaa nikimtazama mpaka alipojongelea jumla. Kwisha kujisaidia akarudi na kujibwaga kitandani. Mimi bado nimeganda kama nyamafu tu, zumbukuku.
"Umesahau kuna jamaa alikuwa anaogelea amevaa bukta pana, ulicheka sana ukawa unamtania pensi la jeje?" Alisema huku anacheka sana.
"Pamoja na hayo Fatinah, Yaani kwako habari ya mimi kumtania mtu kuhusu bukta yake ndio habari kuliko hiki kilichotokea kati yangu na wewe hapa?" Nilizungumza kwa ukali karibia kumfokea.
"Kuna habari gani hapa Almas? Mimi na wewe? Kufanya mapenzi? Nilipanga, hainisumbui" akajibu akiwa mkavu kabisa, Niliingiwa na fadhaa kuu nisipate neno la kuzungumza.
"Kupanga au kutopanga sio habari sana, lakini hakuna mapenzi na kazi" Hatimaye nikabwata kwa hasira
"Tutaona" Fatinah hakuwa na mchecheto alinijibu kawaida kabisa.
"Almas mwanaume wangu kazi zilikuwepo kabla yako na utaziacha! Akaniongeza.
"Mwanaume wako? Tangu lini?" Hakujibu, akavuta shuka na kujifunika.
Mimi najijua, ghadhabu zinapopanda huziona tangu mbali na inapobidi kuzidhibiti huwa nafanya hivyo, labda niziruhusu tu. Kwa nafasi ya Fatinah kwangu sikutaka kuruhusu hasira, ilihitajika maamuzi ya busara, hivyo ilikuwa lazima nifanye jambo kisha nizungumze naye wakati mwingine nikiwa sina hasira tena. Halafu niliamini pia pengine anaendeshwa na kilevi, kikiisha tutazungumza lugha moja.
"Jully yuko wapi?" Nikamuuliza
"Chumba cha pili" akajibu akipiga miayo mfululizo kiasi kwamba nilitumia uzoefu tu kusikia alichosema. Nikamtazama kwa ghadhabu nikakosa maneno.
Baadae niligundua tulilala hapo hapo hotelini tuliposhinda siku nzima tukiburudika.
Nikatazama saa ya ukutani ilikuwa inakaribia saa 11 alfajiri. Nikazoa zoa mavazi yangu sakafuni nikavaa haraka bila kuzungumza jambo. Nikatoka na kuubamiza mlango, huko nyuma nikamsikia akiangua kicheko. Nikatamani nirudi ndani nimzabe japo kelbu mbili tatu, nikapiga moyo konde kuendelea na maamuzi yangu niliyoona ndio sahihi. Nikaondoka.
Itaendelea..
smart11 Panzi Mbishi moneytalk Duke Tachez Kelebe
Au nae ameipeleka telegramHatari sana... ngoja tuone...
Mkuu imekuwaje tena??? Naona mzigo umekata..... T11FATINAH