CHAUSIKU (1)
SEHEMU YA KWANZA
Aya mdau ule wakati uliokuwa una usubiri kwa hamu ndio umewadia, katika utangulizi tumeweza mwona jinsi Chausiku
binti nguva alivyo hatari kwa vijana wadoezi wa kitumbua chake, ebu basi tuungane na mimi msimulizi wako katika
kisa hiki kingine tena cha kusisimua, mkasa unaazia siku moja jioni mida ya saa kumi na moja jioni, ni mwezi mmoja tu! toka
Chausiku alipomfanyia kitu mbaya Bwana Matata, huku kijijini kila mmoja akiongea la kwake, juu ya kupotea kwa Matata
ambae sifa yake ya ubakaji ilijulikana sana pale kijijini, wapo waliosema Matata amehamia kijiji cha pili yaani mandepwende,
wapo waliosema ameenda mjini kutafuta maisha, wengine walisema ameenda polini kupasua mbao, kiukweli kijijini pale hofu ya
ubakaji ilipungua maana wakina mama walishindwa atakuwaachia watoto wadogo wakike wacheze wenyewe, wakiofia Matata asije
akawapitia, mida hii ya jioni binti Chausiku alionekana akikatiza kwenye mitaa ya kijiji cha Matimila akilejea njia ambayo
siku zote utumia wakati wakuja, kwamaana hiyo ni kama alikuwa anarudi kwao, ambako vijana wengi walitamani kupajuwa ili
waweze kumpata kiulahisi kwa gia ya kuoa, Chausiku akiwa na ungo wake uliojaa ndizi kichwani na kisu chake kikali cha mkunjo
(chikwakwa) mkononi alitembea taratibu akikatiza eneo lililo changamka sana la kijiji hiki, ambalo lilitumika kama soko, kwa
walio muona walidhani kuwa binti huyu anatembea kwa madaha, akifanya makusudi kutikisa kamsambwanda kake ka wastani, maana
ukimwona anavyotenbea unge tamani asisogee, yani afanye kama wanavyo fanya askari wanapoambiwa chapa mguu, watu walimtazama
kwa macho ya husuda huku vijana wachache wakikosa uvumilivu na kumchokoza "dada umejaliwa" lakini yeye akuwajari zaidi
alitembea taratibu kuelekea nje ya mji, usawa wa mto matimila, Chausiku binti Nguva alitembea huku akiwaza jinsi alivyo
chelewa, maana uwa anapenda sana kurudi mapema kuogopa binadamu wasije kumdhuru, asa baada ya tukio la sikuile kuviziwa na
Matata, japo kwa wanao mfahamu binti huyu angeweza ata kukiangamiza kijiji kizima kwa mkono wake, lakini hakutaka
kuendelea kuwa umiza binadamu, nahii ni kutokana na kuanza kumpenda kijana mmoja ambae atajina lake bado alikuwa
ajalifahamu, licha yakuwa aliwai kumwona malambili mfurulizo, siku nyingi zilizo pita , lakini bado aliendelea kumkumbuka
kijana huyu, japo ajamwona mda mrefu sasa lakini sura yake ilimjia usoni, akakumbuka siku ya kwanza kumwona, yule kijana
alikuwa anakuja mbele yake akionekana mwenye mawazo mengi sana kichwani, yeye Chausiku alikuwa amebeba ndizi zake na mkononi
ame beba kisu chake kama kawaida, kiukweli alitokea kuvutiwa na kijana yule, ambae alionekana kuwa ni mtulivu sana, lakini
wakati wana pishana kwa bahati mbaya waka pigana kikumbo cha vibega, na kisu cha fadhira kikadondoka, "samahani sana dada
yangu, samahani sijuwi mawazo yangu yalikuwa wapi, yani sikukuona kabisa" alisema yule kijana huku akiinama na kuokota kile
kisu mkunjo, na kumkabidhi Chausiku mkononi, wakati anamkabidhi ndipo Chausiku aka mwona yule kijana akimtazama usoni, na
kumshangaa kwa uzuri wake alionao, haya mdau inaonyesha Binti Nguva amedata kwa kijana binadamu, itakuwaje? minaona nikupe offer mdau, chakufanya usizime data nakuletea sehemu ya pili baada ya kuona like na comment zakutosha, kwenye hii sehemu ya kwanza si
unajuwa vitu vya weekend, pia usikose sehemu ya pili