Hadithi: A Confession of a Madman

Chachasteven

JF-Expert Member
Jul 4, 2014
1,878
1,849
Tittle: A confession of a mad man

Author: DIZASTA VINA

Jina lake silikumbuki kwa sababu sikumuuliza anaitwa nani. Lakini kwa sasa hivi nikitafakari, ninaweza kumbatiza jina la Malaika. Ndiyo! Malaika kwa sababu ya mionekano yake. Lazima nikiri nimeona wanawake wengi warembo wa kila rangi na kabila, lakini huyu, ninayemuita Malaika alikuwa ni wa kipekee sana. Aliyemuumba alikuwa amempendelea kwa kiwango cha ajabu. Kuuelezea uzuri wake utanichukua muda mrefu sana na bado nisitoe taswira kamili. Labda nikuulize mpenzi msomaji, Umewahi kupigwa shoti ya umeme ghafla? Kama hapana, basi uzuri wa Malaika ulikuwa na uwezo wa kumpiga shoti yeyote atakayemtazama. Kuna muda ninahisi hata wanawake wenzake walimuonea wivu au na wao walitamani wawe wanaume ili wamtongoze yeye!

Huyo ndiye Malaika. Na sasa hadithi ndefu kwa ufupi ni kwamba nilikutana naye juzi. Nilikuwa nimekaa kiwanja f'lanif'lani hapa mjini mida ya usiku kupiga mbili tatu. Na kusema kweli, lengo langu ninapotembelea viwanja sio kunywa bia. Nilikuwa nipo mawindoni. Nikiwa natupa macho huku na kule, akaja huyu msichana mrembo hadi mahala nilipokaa. Kilichotokea nilihisi shoti mwilini mwangu! Labda ni kipindi hiki nilichokuwa nimezubaa ndiyo aliniambia jina lake, ila sikumsikia. Kusema kweli sijui. Nilikuwa nimeduwaa mpaka aliponistua.

"Dude, Upo mbali sana kimawazo? Umeachwa?"

"Hapana." Nilimjibu.

"Naomba nikujoin," Hakusubiri jibu langu akawa amekaa pembeni yangu. "Kaka, nimekuangalia toka umeingia hapa ndani na kusema kweli ilikuwa ni kama naona pepo. Kama naiona nchi ya ahadi. Nimevutiwa na wewe."

Sikusema kitu. Nilihisi pengine pombe zilikuwa zinamuendesha, lakini kila alivyoendelea kuongea niligundua ana hisia f'lani ambazo hawezi kuzizuia. Ni wazi alikuwa tayari hata kunipa mchezo kwa usiku uleule.

"Kwani hauamini kwenye 'love in a first sight?" Alinikurupua kutoka kwenye mawazo yangu.

"Mbona una kasi ya jini?" Nilimuuliza.

Kabla hajanijibu akacheka. Tabasamu lake likanipa mshangao mwingine.

Akaanza kuongea baada ya ukimya kidogo, "Brother, wasiwasi wa nini?" Sauti yake sasa hivi ilikuwa laini na ya kuvutia. Au zilikuwa ni pombe nilizokunywa?

"Wewe ni handsome, na pia ni mpole. Mchizi kama wewe unahitaji manzi kama mimi." Aliendelea kuongea.

Nilimtazama na kusema kweli nilimstahili. Alikuwa na Summer body. Kiufupi alikuwa ni pisi kali ya kwenda! Na machoni nilimtamani sana, ila nafsi ndiyo ikawa inagoma.

Nikayarudisha macho yangu kwenye pombe yangu. Ghafla akanishika sikio na kuninong'oneza kimahaba. "Dude, I love you."

Akaanza kuniita majina kama Babes mara Boo huku akijitomasatomasa kwenye chuchu. Waungwana f'lani waliokuwa meza ya pembeni yetu nikawasikia wanaambiana nina juju!

"Naomba unibusu!" Aliniambia.

Mimi nikakataa. Angekuwa mtu mwingine hii bahati asingeiacha iteleze kwenye viganja vya mikono yake. Malaika akala mingo akanibusu kwenye shingo nikaguna tu. Hakuna mwitikio wowote! Ilimshangaza hata yeye! Nadhani hata shetani alishangaa pia.

"Umeoa?"

"No." Nilimjibu.

"Kwanini hunipendi?"

Nilimwangalia machoni halafu nikasema, "Dada, nakuonea huruma."

"Huruma ya nini? Au una vibinti bar?" Kabla sijajibu akaendelea, "Achana navyo ili niku-treat kama minister. Kwani hivi ninavyokupenda hadi nakufuata hauhisi raha. Nikubalie tuwe wote mbona hakuna ugumu. Au una UKIMWI unaogopa kuusambaza?"

Nikamwambia kwa sauti ya chini, "Sikia! Mimi nachinja watu nauza mioyo yao na figo."

Akacheka kwa mashauzi ya kinafki nafki. Ilikuwa wazi hakuamini kauli yangu. Na watu wengi ninapowaambia hivi huwa hawaamini. Sikushangaa!

Akatulia kidogo halafu akasema, "Au hauna kazi, huh! Hiyo mioyo na figo ukichinja unauza wapi?"

"Napigiwa simu za oda. Kuna watu wanahitaji hivi viuongo na huwa ninazisafirisha mpaka India."

Akacheka sana mpaka akaniegemea. Wakati kichwani ninajiambia '... Dada angejua kitachokwenda kumtokea, angebeba pochi yake angetembea.'

Nikamwambia, "Nenda nyumbani usigeuke nyuma. Kalale kesho uende ibadani ukatoe ushuhuda. Ninakupa nafasi ya kuishi uujuze umma ili ukaandike kumbukumbu umenusurika kufa."

"Sio mbaya nzi kufia kwenye kidonda. Nakupenda sana. Please niweke moyoni, na hata ukiwa muuaji n'tafurahi kufia mikononi mwako." Alinijibu.

Hakutaka kusikia mambo mengi. Kama ni bidhaa alikuwa amekwishalipia anasubiri huduma. Akanikaribia kisha akanibusu kimahaba tena shingoni.

"Do you have a car or some' brother?" Aliniuliza.

Alikuwa anataka kujua kama nina usafiri. Nikarudia kumwambia mimi muuaji akagoma. Akaniambia twende naye kwangu halafu akaniegemea kifuani ghafla. Ile nafsi ikanirudia tena. Nikajikuta najiambia kichwani '... Dada angejua kitachokwenda kumtokea, angebeba pochi yake angekwenda mbali.'

Baada ya ubishi nikajikokota naye tukazama kwenye Harrier yangu iliyokuwa maegeshoni. Safari kwenda nyumbani ikaanza. Tulitumia nusu saa barabarani na muda wote alikuwa anaongea kuhusu hisia zake kwangu.

Tulipofika nyumbani kwangu nikampa mvinyo wa baridi wa kiitalia. Kitu ambacho hakujua ni kwamba ndani ya glasi yake nilikuwa nimemuwekea Valium. Akapiga fundo kadhaa kisha akaweka glasi mezani. Muda wote nilikuwa namuangalia tu. Alitabasamu akasogea hadi jirani nilipokuwa nimekaa akaweka mkono wake begani kwangu.

"Honey, haujaniambia unafanya kazi gani?" Akaniuliza kiudadisi.

Nilinyanyuka nikamuonesha picha za mademu kama mia niliowachora. Zilimsisimua kwa kweli. Na nikuambie tu msomaji, Mimi ninajua kuchora sana.

"Baby, Wewe ni genius." Aliniambia.

"Niliowachora wote nishawachinja. Wewe ndiye unafuata!"

Akasema, "Baby, haupo serious. Anyways acha nikuoneshe kipaji changu pia"

Nilitulia kumtazama. Alianza kuniimbia wimbo. Mwanzo alikuwa anaimba vizuri, lakini maneno yakaanza kukata kama ishara ya kwamba dawa imeanza kumkolea. Alipozidiwa akaanguka nikampeleka mpaka chumbani.

Chumba chenyewe huwa sio cha kulala. Huwa hakuna kitanda ila meza tu. Nilimlaza mezani hapo kwa pozi f'lani la mvuto nikaanza kumchora. Kazi ya muda mrefu kidogo. Nilipomaliza nilimbusu kwenye paji la uso kisha nikatoa visu vitatu vikali na nyundo.

MWISHO.

As inspired by Dizasta Vina's song titled A confession of a mad man.
 
The verteller!
1638004344091.png
 
MKASA: USHUHUDA WA BWANA KICHAA II


ILIPOISHIA…

Chumba chenyewe huwa sio cha kulala. Huwa hakuna kitanda ila meza tu. Nilimlaza mezani hapo kwa pozi f'lani la mvuto nikaanza kumchora. Kazi ya muda mrefu kidogo. Nilipomaliza nilimbusu kwenye paji la uso kisha nikatoa visu vitatu vikali na nyundo.

SASA ENDELEA…

Kazi ukishakuwa mzoefu huwa ni nyepesi sana. Nilikuwa na uhakika wa kuimaliza kazi yangu ndani ya dakika arobaini tu. Nilimsogelea pale mezani akiwa amelala, kisha nikamuondoa nguo zake zote akabaki kama alivyozaliwa. Niliitawanya miguu yake huku na huko, huku nikiendelea kupiga mluzi ambao haukurandana na wimbo wowote ule–basi tu ilimradi nijifurahishe.

Niligeuka tena na kuchukua makasha yangu mawili, moja maalum kwa kutunzia moyo, na jingine lilikuwa na chemba mbili maalum kwa kutunzia figo mbili. Wakati huo wote ule mluzi kinywani mwangu haukutoka. Vitu hivyo vyote niliviweka karibu kabisa na ile meza ambayo nimemlaza yeye.

Nilijaribu kukumbuka kama kuna chochote nilichokisahau kabla sijaanza kazi. Ndiyo; nilikuwa nimesahau spirit. Nilirudi na kunyofoa pande la pamba, kisha nikamimina methylated spirit juu yakr, pande lile likalowa vyema.

Nilirudi mezani na kumpaka ile spirit tumboni, eneo ambalo figo hukaa (lower abdomen) kisha nikampaka na kifuani, juu kidogo ya titi lake la kushoto.

Sasa kazi ilikuwa imeiva. Nilichukua visu vyangu viwili nikamsogelea. Ghafla, bila mimi kutarajia, Malaika yule alifumbua macho, kisha akaidaka shingo yangu.

Ndugu msomaji, nilikuambia kuwa namwita malaika kwa sababu ya urembo wake? Basi hapa kuna sifa yake ya ziada. Wale malaika waliompiga na Lusifa kule mbinguni mpaka wakamshusha duniani, ndicho nilichokiona kwa malaika huyu mwenye mwili kama wa sisi binadamu. Alikuwa na nguvu mno, kiasi cha kunipiga kama mtoto mdogo pamoja na uzoefu wangu kwenye mapambano ya ana kwa ana.

Kwa kasi ya ajabu alinibamiza chini. Nilifyatuka ili nisimame haraka, lakini wapi. Alinitwanga ngumi kwenye paji la uso. Mwanzo, mokono yake niliiona laini sana, lakini aliponipiga ngumi nikahisi nimepigwa jiwe.

Niliinuka ili nijitetee, yeye akaniwahi. Mkononi tayari alikuwa na ile nyundo yangu, akanibonda kwenye bega langu la kushoto. Labda nikwambie kitu kingine ndugu msomaji; Mimi ni mtumiaji mzuri wa mkono wa kushoto (left-handed). Hata katika mapigano, huwa nautumia mkono huu kumaliza mchezo. Nitakupiga ngumi nyingi kwa mkono wa kulia lakini nitakuvizia ujae kwenye mkono wangu wa kushoto ili nikumalize. Malaika alikuwa ameniwahi, akaumaliza mkono wangu wa kushoto nguvu. Kwa maana hiyo alikuwa akinijua vyema. Mimi sikujua hilo.

Pamoja na uwezo alionionesha, sikukata tamaa, nikasimama ili kukabiliana naye. Bahati ilikuwa kwake! Alikuwa karibu na ile meza, hivyo akajiokotea kisu kimoja kati ya vile vilivyokuwepoezani. Mimi sikuwa na silaha yoyote. Tulishambuliana kwa muda mrefu kabla hajanipata tena. Kwa kutumia kile kisu akanigongomelea mkono wa kulia ukutani. Akachukua na kisu kingine, akaugongomelea mkono wa kushoto ukutani, nikaishia kutweta kwa maumivu, nikakosa la kufanya.

Haraka aliiendea blauzi wake akaivaa huku nikimwangalia. Sijui kwa nini sikuwa makini kiasi kile! Kifungo kimoja kilikuwa tofauti na vifungo vingine. Ilikuwa ni camera ndogo ya kijasusi iliyotengenezwa kwa mfano wa kishikizo cha blauzi. Ingawa mtengenezaji alijitahidi kuifanya ionekane sawa na vishikizo vingine, lakini kwa mtu makini angegundua kuwa kile hakikuwa kishikizo cha kawaida. Nilibaki nikijilaumu kwa nini sikuwa makini.

Bila hata kuvaa nguo yake ya chini, akaiendea pochi yake. Hakujihangaisha kuifungua, lakini aliikamata kisha akaongea maneno.
“I got him” (Nimempata!)” Maskini mimi! Kumbe hata ile pochi haikuwa pochi ya kawaida. Ilikuwa na kinasa sauti ambacho kilikuwa kikipeleka mawimbi ya sauti kwa washirika wake! Muda wote sikuyajua hayo.

Mara niliona hali ya yule malaika ikianza kubadilika. Akaanza kujipiga-piga kichwani, akijilazimisha hali ile isimpate, lakini haikuwa hivyo. Akajibwaga chini, ‘Pwaaaah!’ hapo ndipo nikapata majibu ya swali langu.

Bila shaka Malaika alitumia dawa iitwayo Amphetamine. Amphetamine ni dawa ya kuzuia usingizi ambayo hupingana na Valium (dawa ya usingizi). Mtu aliyetumia dawa ya Amphetamine hataweza kupata usingizi akipewa dawa ya Valium. Lakini kuna madhara makubwa kiafya kwa mtu kuchanganya dawa hizi mbili. Yaani ukimeza Amphetamine, halafu ukameza Valium baada ya muda mfupi unaweza kupata madhara kiafya kama vile kuathiri mapigo ya moyo na mzunguko wa damu ambao kama damu haitafika kwa wingi kwenye ubongo inaweza kukusababishia kizunguzungu na hata kuzimia.

Baada ya Malaika kuzimia, niliamua kutoroka upesi. Kwa bahati mbaya nilikuwa nimekwishachelewa, kwani muda huo huo waliingia wanaume watano waliovalia kiraia. Waliingia mapema kabla sijafanikiwa hata kujitoa pale ukutani.

Waliniondoa ukutani na kunivalisha pingu, kisha wakachukua kila kilichokuwepo pale chumbani kwa ajili ya ushahidi. Ushahidi mwingine yalikuwa ni maongezi ambayo Malaika alinirekodi tukiwa tunazungumza kuanzia kule bar mpaka nyumbani kwangu bila mimi kujua, pamoja na video iliyorekodiwa na camera ndogo iliyokuwa kwenye blauzi yake kwa mfano wa kishikizo.

Kama nilivyokuambia, hayo yote yalitokea siku ya juzi. Leo nikusimuliavyo mambo haya nipo mahakamani. Muda si mrefu nitapandishwa kizimbani kwa ajili ya kusomewa mashtaka yangu kwa mara ya kwanza. Namuona Malaika yupo salama salimini baada ya kutoka hospitali. Ananiangalia kwa makini huku akitabasamu; tabasamu lake la leo si la kuchombeza kama lile la juzi.

Ama kweli Malaika ameniweza!

MWISHO
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom