Habari za Kusikitisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Habari za Kusikitisha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Feb 3, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Feb 3, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Moshi wa jenereta wauwa wanne

  Na Salma Said,

  WATU wanne wa familia mmoja wamefariki dunia baada ya kuvuta hewa inayosadikiwa kuwa na sumu iliyotokana na moshi wa jenereta katika eneo la Kibweni Bububu Nje kidogo na mji wa Zanzibar.

  Ajali hiyo imetokea majira ya usiku mkubwa juzi huku madirisha ya vioo ya nyumba inayomilikiwa na Ali Shamsi Salum yalikuwa yamefungwa na kusababisha hewa inayotokana na genereta lenye ukubwa wa KVA 4.1. kuingia ndani na kushindwa kutoka nje ya nyumba hiyo.

  Naibu mkurugenzi wa makosa ya jinai Zanzibar, Mussa Ali Mussa alithibitisha kutokea ajali hiyo na kusema kwamba katika ndnai ya nyumba hiyo kulikuwa na watu sita lakini wanne alifariki na watu wanne ndio waliofariki watatu walifariki hapo hapo na mmoja wao alifariki baada ya kukimbizwa hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.

  Akiwataja walifariki dunia katika ajali hiyo Naibu Mkuruenzi huyo alisema ni pamoja na mama mwenye nyumba Safia Shaaban Shadadi (51) kaka wa mama huyo Ahmed Shaaban Shadadi (48), mgeni kutoka Canada Anwar Saleh (26) na mfanyakazi wa nyumba hiyo Sikuzani Nassor (18).

  Antar ambaye ni mgeni na alikuja visiwani Zanzibar kutoka nchini Canada alikuwa na mpango wa kusafiri na kurudi zake Canada siku ya Alhamisi (leo) huku mmiliki wa nyumba hiyo Ali Shamsi Salum alisalimika katika ajali hiyo kwa kuwa siku ya tukio alikuwa amelala katika nyumba yake ya pili kwa mke wake mwengine eneo la Michenzani Unguja.

  Wengine walionusurika katika nyumba hiyo ni Sharifa Ramadhan Mohammed (35) na mtoto wake Nahad Ali Said (12) ambao wamekimbizwa katika hospitali ya mnazi mmoja kupata matibabu zaidi baada ya kupata mshituko wa kumeza hewa chafu iliyotokana na moshi huo wa jenereta la KVA 4.1.

  Naibu mkurugenzi huyo amesema chanzo cha vifo hivyo kimetokana na kukosa hewa katika nyumba waliyokuwa wamelala wakati huo generetar likiwa likifanya kazi na kusababisha moshi wake kushindwa kutoka nje na watu hao kuvuta hewa ambayo ni mchanganyiko wa sumu ya carbon mono.

  Alisema kwa muhibu wa taarifa kutoka kwa majirani wakati wanataka kuingia ndani kuwaokoa watu waliomo ndani ya nyumba hiyo walikuwa wakikohoa kutokana na hewa nzito sana ndani humo jambo ambalo hadi asubuhi polisi walipoingia walishuhudia hali ya hewa hiyo.

  “Sisi tulipata taarifa kutoka kwa wananchi na baada ya kupata taarifa hizo tukafuatilia na ndipo tulipokwenda kufnaya ugaguzi na katika ukaguzi wetu wa awali tumeona sababu ya vifo vya watu hao ni moshi uliokuwa ndani uliosababishwa na jeneretor ambao haukuweza kutoka nje kwa kuwa madirisha yote ni ya vioo na yalikuwa yamefungwa kwa sababu sisi tulipoingia pia kulikuwa na hewa nzito sana” alisema naibu mkurugenzi huyo.

  Haji Ali Haji ni miongoni mwa mashuhuda katika ajali hiyo ambaye amesema walisikia mtu mmoja akipiga mayowe na ndipo walipokwenda lakini baada ya kuingia ndani walikumbana na moshi mzito sana na kusababisha kukohoa lakini waliweza kufungua milango na kujaribu kuwaoka watu waliomo ndani bila ya mafanikio.

  Alisema watu inaonesha moshi huo ulikuwa umeshaenea kwa kiwango kikubwa sana hivyo jambo la kwanza walijaribu kufungua madirisha na ili hewa hiyo itoke nje na kwenda nyumba kimoja kimoja ndipo walipowaona watu hao wamenyooka na wengine waliokuwa wamelala ukumbini wakiwa tayari wameshakufa.

  Naibu mkurugenzi wa makosa ya jinai zanizbar alitoa wito kwa wananchi kutoweka majenereta ndani ya nyumba na kushauri iwapo wanaogopa wizi basi wajenereta hayo wajajengee vibanda kando za nyumba zao ili kunusuru ajali kama hizo zisitokezee tena.
  Mussa aliwataka wananchi kuchukuwa hatua za tahadhari wakati wakiwa wamelala usiku na majenereta yanatakiwa kuwekwa sehemu mbali kwa ajili ya kuyapa nafasi ya kutoa moshi wake nje na usisambae ndani kwani huweza kusababisha ajali.

  Hili sio tukio la kwanza tokea kuzimika kwa umeme desemba 10 mwaka jana matukio kadhaa yameripotiwa kutokea ya kuripuka kwa majenereta na kusababisha ajali ikiwemo kuunguza nyumba na vitu kadhaa.
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ...duuh poleni sana.....wanatumia generator baada ya kukosa umeme wa Tanesco sio? so kungekuwa na umeme hii ajali haingetokea.....!

  Pole wote walifikwa na msiba huu!
   
 3. JS

  JS JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  RIP na pole sana kwa familia waliyopoteza ndugu. Tanesco you better do something quick sababu hizo ndo lawama zenyewe.
   
 4. m

  madule Senior Member

  #4
  Feb 3, 2010
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Poleni saana wafiwa, RIP
   
 5. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  that's CO2, Halogens and traces of VOC...
  so sad!

  R.I.P
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  RIP waungwana!
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,932
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Duh, Carbon Monoxide inauwa vibaya! kimyakimya!  Poleni wafiwa wote kwa msiba huu.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,731
  Trophy Points: 280
  Poleni sana wafiwa . Mwenyezi Mungu awalaze marehemu mahali pema peponi. Moshi wa jenereta za kuzalisha umeme ni sumu kali sana unaua mara moja.
   
 9. k_u_l_i

  k_u_l_i Senior Member

  #9
  Feb 3, 2010
  Joined: Jan 26, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni hatari sana kuwasha generator ndani ya nyumba au karibu na dirisha kwa sababu ya carbon monoxide. Viongozi inafaa kuwaelimisha wananchi utumiaji salama wa magenerator katika kipindi cha ukosefu wa umeme.
  Poleni sana kwa msiba - Mungu awalaze mahali pema Amen.
   
Loading...