Habari za jioni...

Habari za jioni...

mimi mgeni hapa.. utafiti nahisi wewe mwenyeji waweza. niambia kinachondelea hapa....
 
Last edited by a moderator:
Hapa naona kuna mambo ya chuma ulete kama sio kanyaboya au changa la macho...

Stori imeanzia hapa...

Naombeni mnisaidie kiasi cha pesa ili niweze kufanyia practical ktk masomo. Kwa atakayejaaliwa naombeni sana kwani itanisaidia kumaliza mapema na kujiandaa vizur ktk mitihan yangu ma pia itanirahisishia kufikia malengo.

Mdau mmoja akauliza hivi...
ulipata hela ya mtihani eeh?

Ghafla bin vuuu mhusika akajibu kwa ID yake nyingine...
Emmy lady said:
Mtihani nililipiwa na usajili umeshakamilika tayari. Kilichobaki ni juhudi zangu mimi mwenyewe ktk kujisomea.

Baada ya kujishtukia akaifuta fasta fasta kumbe kuna watu wapo fasta zaidi...

Teh teh teh.. Invisible au Moderator please hebu fanyeni mambo yenu yale hapa kabla watu hawajalizwa..
 
Last edited by a moderator:
Ahhah...m mwenyew sielew..kama alikua anasoma food science sua sasa mambo ya chemistry cjui yametoka wap....

kishanuka,ana ID mbili,emmy lady si ndo aliomba kukaribishwa huyu alievamia kama chopa za vita.
,haya kumbe ndo jac tenaaa...eh mods fanyeni yenu kina gilesi/bujibuji bado wapo wengi humu.
 
nimejiandikisha tirav, nitafanya masomo 10. Namaanisha saba ya kawaida na matatu ya science.

Hebu tukumbushe hayo masomo matatu ya science tena uliondoe somo la Biology ambalo lipo ktk masomo saba ya kawaida!
 
Hapa naona kuna mambo ya chuma ulete kama sio kanyaboya au changa la macho...

Stori imeanzia hapa...



Mdau mmoja akauliza hivi...


Ghafla bin vuuu mhusika akajibu kwa ID yake nyingine...


Baada ya kujishtukia akaifuta fasta fasta kumbe kuna watu wapo fasta zaidi...

Teh teh teh.. Invisible au Moderator please hebu fanyeni mambo yenu yale hapa kabla watu hawajalizwa..

Heee Emmy Lady ndo anaID mbili? jamani jamani mbona hatareeeeee
 
Kiukweli mmeshindwa kunielewa kwakweli. Mimi binafsi sina simu ila huwa natumia simu ya mtu ambaye ni jiran yetu. Kiukweli sikuwa nafahamu kama anatumia jamii forums au la. Nilichokifanya mimi ni baada ya kumuomba simu ni kuingia tu internet. Kiukweli sikuwa najuwa kabisa kama yeye amejiunga au la. Mimi sio kama msemavyo na wala sivyo mnifikiriavyo. Siwezi kudanganya kama mnavyodai na wala siwezi kujitangazia shida kama sina au nina raha.
 
Kamwe sijafunzwa kudanganya wala kutapeli. Namshukuru mungu kwa hali niliyokuwa nayo japo ina changamoto kadhaa. Kwa hakika siwezi kabisa kujisingizia shida! Mwenye hii simu sikuwa najua kama naye amejisajili na jamii forums. Tafadhali naombeni mniamini wakubwa zangu. Siwezi kuwa mhuni ikiwa kweli ni mhitaji. Ila kama hamtoamini sitakuwa tena na jinsi manake mtakuwa mmeshindwa kuniamini. Siwez jifanya ni mwanamke ikiwa mimi ni mwanaume. Ahsanteni.
 
Back
Top Bottom