Habari & Picha; Sugu na Elimu Mbeya Mjini - Part 1 & 2

Habari & Picha; Sugu na Elimu Mbeya Mjini - Part 1 & 2

Bukanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2010
Posts
2,857
Reaction score
1,938
IJUE PROGRAMU YA KOMPYUTA MASHULENI


Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph O. Mbilinyi anaendesha programu ya mafunzo ya kompyuta kwa wanafunzi wa sekondari za Kata zilizopo jijini Mbeya ambapo tayari ameanzisha madarasa ya kompyuta katika shule za sekondari tano (5)kati ya 10 ambazo zitafikiwa na mradi huu kwaawamu ya kwanza, shule hizo ni Shule ya Sekondari Mwakibete, Shule ya Sekondari Uyole, Shule ya Sekondari Forest, Shule ya Sekondari Iwambi na Shule ya Sekondari Iganzo.


Lengo la programu hii ni kuhakikisha wanafunzi wa shule za Mbeya wanapomaliza kidato cha nne (4) wawe na uwezo wa kutumia kompyuta hali iliyopelekea kuongeza hadhi za shule na elimu kwa ujumla katika shule za Kata jijini Mbeya




​

​
​

​

​

​
PART 2
MBUNGE JOSEPH O. MBILINYI ANASOMESHA KUPITIA MFUKO WA ELIMU


( muendelezo wa SUGU NA ELIMU - 2 ).....


Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph O. Mbilinyi "Sugu" anasomesha wanafunzi katika shule mbalimbali za sekondari, na hii ilitokana na baada ya kuanza kazi ya Ubunge moja ya changamoto aliyokumbana nayo ni wingi wa walezi na wanafunzi waliofika ofisini au waliomuona kwa ajili ya kuomba msaada wa kusaidiwa ada na gharama nyingine za shule, ndipo ikapelekea aanzishe Mbeya Education Trust Fund (METF) au Taasisi ya Mfuko wa Elimu Mbeya.


Ambapo taasisi hii METF katika moja ya jukumu lake imeweza kusaidia wanafunzi wa sekondari takribani 270 waliofaulu na hawakuwa na uwezo kutokana na kuwa wanatoka kwenye familia zenye uwezo mdogo kiuchumi kwa kuwalipia ada na sare za shule pamoja na mahitaji mengine ya elimu pale inapobidi, na ilipoanza mwaka 2013 ilianza na watoto wa kidato cha 1 mpaka 4 (o'level) lakini sasa imeweza kusaidia mpaka wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 (A level).



Imetolewa na
OFISI YA MBUNGE MBEYA MJINI


​
(Chini ni picha mbalimbali za baadhi ya watoto wanaosomeshwa na Mfuko huu wakiwa na Afisa wa METF)


​

​


​
 
Siasa za upinzani kichekesho sana baada ya miaka 5 ndiyo ameshtuka kama kuna kuomba kura tena.
 
Siasa za upinzani kichekesho sana baada ya miaka 5 ndiyo ameshtuka kama kuna kuomba kura tena.

Weweeeeee! Si bora huyo miaka 5!
Waliokaa miaka 30 wanarudi mda gani? Kwanza huyo dogo mdogo mwingi yuko jimbon kwake anaonekana hadi kwenye shughuli za kijamii!!
We naona unamvizia kwenye tv tu! !!!
 
Siasa za upinzani kichekesho sana baada ya miaka 5 ndiyo ameshtuka kama kuna kuomba kura tena.

Hizo picha zipo kwa Facebook tangu mwaka juzi! Wewe umeziona leo basi unadhani za leo, acha umbwisi! Haya tutajie program ya mbunge wako wa CCM!
 
Weweeeeee! Si bora huyo miaka 5!
Waliokaa miaka 30 wanarudi mda gani? Kwanza huyo dogo mdogo mwingi yuko jimbon kwake anaonekana hadi kwenye shughuli za kijamii!!
We naona unamvizia kwenye tv tu! !!!

Msanii mwingine amenunua hiace used old model 1995 carburetor engine ameipiga msitali mwekundu kama daladala za ubungu kariakoo na kuiandika Ambulance eti anawapa wana Arusha gari kama hiyo hata mimi siwezi kuitumia.
 
Kwa mtiti wa leo ulivyokuwa, Hakika hakuna wa kumng'oa Sugu Mbeya
 
Msanii mwingine amenunua hiace used old model 1995 carburetor engine ameipiga msitali mwekundu kama daladala za ubungu kariakoo na kuiandika Ambulance eti anawapa wana Arusha gari kama hiyo hata mimi siwezi kuitumia.
we kweli unaitaji elimu ya uraia,kwahyo we unadhani ambulance sio hiace.??
 
Msanii mwingine amenunua hiace used old model 1995 carburetor engine ameipiga msitali mwekundu kama daladala za ubungu kariakoo na kuiandika Ambulance eti anawapa wana Arusha gari kama hiyo hata mimi siwezi kuitumia.
we kweli unaitaji elimu ya uraia,kwahyo we unadhani ambulance haiwez kuwa hiace.??
 
Sugu hata asipige kampeni atashinda kwa kishindo awali aliishinda ccm kwa kula elfu 25 mwaka huu yaweza kuwa 70 . kila mtu aliye mbeya anajua jamaa anakubalika kafanya makubwa cheki mapokezi yake Jana jumapil mji ulizizima hiyo ni dalili njema kwake
 

Attachments

  • 1436736006462.jpg
    1436736006462.jpg
    69.2 KB · Views: 218
  • 1436736151582.jpg
    1436736151582.jpg
    80.6 KB · Views: 201
Back
Top Bottom