Habari njema kwa wanasimba: Kiemba asaini

Habari njema kwa wanasimba: Kiemba asaini

SERGIO

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2012
Posts
348
Reaction score
147

Hii nimekutana nayo kwenye blog ya Bin Zubeiry. Bila shaka ni taarifa njema kwa wapenzi wa Wekundu wa Msimbazi...

Na Mahmoud Zubeiry,
IMEWEKWA JUNI 11, 2013 SAA 9:30 ALASIRI
HATIMAYE kiungo Amri Ramadhani Kiemba amesaini Mkataba mpya na Simba SC mchana wa leo kuendelea kuichezea klabu hiyo kwa miaka miwili, hivyo kuzima tetesi kwamba alikuwa mbioni kurejea klabu yake ya zamani Yanga SC.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY mchana huu, Kiemba amesema amesaini mbele ya Kaimu Mwenyekiti wa Simba SC, Joseph Itang'are ‘Kinesi' mchana huu.
"Unajua mimi si muongeaji, wakati magazeti yanaandika mimi nimesaini Yanga nilikuwa nashangaa sana. Ila sikutaka kujibu, sasa ukweli ni huu nakupa Bin Zubeiry, nimesaini Simba kwa miaka miwili zaidi,"alisema.
Amesema kwa sasa anaelekeza nguvu zake katika kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars na anaamini mjadala wa Kiemba umekwisha salama, sasa ni zamu ya wengine.
Kiemba amesaini SImba SC leo ikiwa ni siku moja tu tangu arejee nchini kutoka Morocco alipokuwa na timu ya taifa, Taifa Stars.
Kiemba yuko juu kwa sasa kisoka na alikuwa lulu Morocco kutokana na kuifungia Tanzania, Taifa Stars bao la kufutia machozi ikilala 2-1 mbele ya wenyeji, Simba wa Atlasi Jumamosi Uwanja wa Marakech, Morocco.
Baada ya mchezo huo, mashabiki wa soka Morocco walianza kumfuatafuata Kiemba wakiomba kupiga naye picha na walimtambua rahisi kwa sababu ya rasta zake.
Kiemba aliendelea kusumbuliwa na Wamorocco hadi hotelini Pullman Stars ilipifikia na hadi wakati Stars inaondoka Marakech, madereva teksi wa hotelini hapo, walimuomba kupiga naye picha.
Hali hiyo iliendelea hadi Stars ilipotua Casablanca kwa ajili ya kupanda ndege kurejea Dar es Salaam na Kiemba hakuwafanyia hiana aliwapa ushirikiano na kwa ujumla Waarabu walimfuruhia mno kiungo huyo.
Kabla ya mchezo, mchezaji ambaye Waarabu walikuwa wanamtaja na kumuulizia sana alikuwa Mbwana Ally Samatta aliyewafunga mabao mawili katika ushindi wa Stars wa 3-1 Dar es Salaam.
Pamoja na Kiemba na Samatta, Waarabu wa Morocco wameiheshimu timu nzima ya Tanzania kwa mchezo uwezo wake kisoka na kusema ina vipaji vingi, Thomas Ulimwengu, Frank Domayo, Salum Abubakar na Shomary Kapombe wakiwa wachezaji wengine waliowachengua zaidi.
Stars ilifungwa 2-1 na wenyeji Jumamosi katika mchezo wa Kundi C kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia Brazil mwakani.
Hadi mapumziko, Morocco walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na Abderazak Hemed Allah dakika ya 37, baada ya yeye mwenyewe kujiangusha kwenye eneo la hatari baada ya kugongana na Aggrey Morris.
Morris alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya hapo na Stars wakabaki pungufu.
Dakika ya 25 Thomas Ulimwengu alifanya kazi nzuri ya kumtoka beki, lakini shuti lake likadakwa na kipa.
Kocha Kim Poulsen aliwapumzisha kwa mpigo washambuliaji Mrisho Ngassa na Ulimwengu dakika ya 44 na kuwaingiza beki Nadir Haroub ‘Cannavaro' na kiungo Khamis Mcha ‘Vialli'.
Kipindi cha pili Morocco walirejea na moto tena, wakiishambulia zaidi Stars iliyoonekana kudhoofika na katika dakika ya 50 Youssef El Arabi akafunga bao la pili kiulaini baada ya kuwatoka mabeki wa Tanzania na kubaki na kipa Juma Kaseja.
Hata hivyo, shambulizi la kushitukiza liliipatia Stars bao la kwanza dakika ya 61 lililofungwa na Amri Kiemba kwa shuti la mbali kutoka wingi ya kushoto.
Dakika ya 82 Kim alimpumzisha Vialli na kumuingiza John Bocco ‘Adebayor' ambaye aliongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji.
Kwa matokeo hayo, Stars inabaki na pointi zake sita baada ya kucheza mechi nne, kushinda mbili nyumbani na kufungwa mbili zote ugenini, nyingine ikiwa dhidi ya Ivory Coast.
Lakini Stars inabaki nafasi ya pili mbele ya Morocco yene pointi tano sasa, wakati Ivory Coast wanaongoza kwa pointi zao 10. Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook
 
.....kama amesaini ni jambo jema, ila ngoja tusubiri msemaji wa Club tuone anatueleza nini.
 
Kama amesaini kweli tunashukuru, ila viongozi wetu nao wamezidi ubabaishaji, wanatakiwa wamsajili na Kaseja bado tunamhitaji, hata kama atakuwa anakaa benchi lakini anatakiwa kuwepo kikosini.
 
Hivi wachezaji wa Taifa Stars na Tanzania kiujumla wana umri gani? Maana wapo ambao niko darasa la sita wanacheza Kagame Cup. Hadi leo niko chuo wanacheza tena wako first team je miaka yao haiongezeki?
 
hivi wachezaji wa taifa stars na tanzania kiujumla wana umri gani? Maana wapo ambao niko darasa la sita wanacheza kagame cup. Hadi leo niko chuo wanacheza tena wako first team je miaka yao haiongezeki?
tangu wamacheza kagame hadi leo uko chuo tu!? Anyway ni suala la kikatiba
 
Uhhhuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
.........SASA ZAMU YA WENGINE............Juma Kaseja?
 
Hivi wachezaji wa Taifa Stars na Tanzania kiujumla wana umri gani? Maana wapo ambao niko darasa la sita wanacheza Kagame Cup. Hadi leo niko chuo wanacheza tena wako first team je miaka yao haiongezeki?
Tuambie wakati uko darasa la sita ilikuwa ni mwaka gani? inawezekana uliruka madarasa ukaenda fasta fasta mwaka mmoja madarasa matatu.
 
hawa wanadanganya ama?
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1370965705630.jpg
    uploadfromtaptalk1370965705630.jpg
    146.8 KB · Views: 83
Na Khatimu Naheka
HATIMAYE aliyekuwa kiungo wa Simba, Amri Kiemba, amekubali rasmi kuachana na klabu hiyo na sasa atakuwa mchezaji wa Yanga msimu ujao.
Awali, Kiemba ambaye anatarajiwa kutua leo akitokea nchini Morocco alipokuwa na kikosi cha Taifa Stars, alikuwa na kigugumizi kizito juu ya kusaini mkataba mpya na Simba, kutokana na Wekundu hao kushindwa kukubali dau alilotaka la Sh milioni 30 na mshahara wa dola 1,500 (sawa na Sh milioni 2.4).
Ofa hiyo ilionekana ngumu kwa Wekundu hao ambao walitaka kumpa Sh milioni 20 pekee nyota huyo ambaye aliifungia timu hiyo mabao saba katika Ligi Kuu Bara msimu uliopita.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Jumatatu limezipata kutoka kwa kaka wa kiungo huyo, Ulimwengu Hamim, tayari Kiemba ameshakubaliana na Yanga juu ya uhamisho wake, ambapo mara baada ya kutua leo, atasaini mkataba na klabu hiyo wenye thamani ya Sh milioni 35.
Ulimwengu ambaye pia ndiye Meneja wa Kiemba, alisema mbali na dau hilo, kiungo huyo atakuwa akichukua mshahara mnono wa dola 2,000 (sawa na Sh milioni 3.2), ambapo makubaliano hayo ameyafanya akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Bin Kleb.
"Nilikwambia muda mrefu kwamba Yanga walikuwa wanamhitaji sana Kiemba, lakini mimi kama meneja wake niliwapa heshima sana Simba, niwe wazi, ofa ya Simba ilikuwa ndogo kulingana na mahitaji na thamani ya Kiemba na ndiyo maana tulishindwa kukubaliana," alisema Ulimwengu na kuongeza:
"Tumekubaliana kila kitu, namsubiri Kiemba arudi huko kesho (leo), nafikiri jioni yake tutakutana tayari kwa tendo la kusaini mkataba mpya na Yanga utakaomfanya kuwa Yanga kwa miaka miwili, nadhani hilo sasa limekwisha."
Kiemba ndiye mchezaji aliyekuwa akitumainiwa zaidi na Simba msimu uliopita. Kutua kwake Jangwani kunaifanya Simba iwe imepigwa bao mara mbili na Yanga. Awali Jangwani walimsajili beki Kelvin Yondani baada ya Wekundu kuonekana kuwa na kigugumizi juu ya kumsajili.

Source:Global publishers
 
........huyu mtu anayeitwa Khatimu Naheka alikosa habari za kuandika kwenye magazeti yake ya Udaku mpaka akaona habari ya kuandika ni hii inayomuhusu Kiemba!!!!, hawa waandishi wengine ni matatizo tupu.
 
Back
Top Bottom