HATA SIKULAZIMISHI USOME, IKIBIDI HATA USISOME BE.....
eti mmeachana unalalamika ohoo kanipotezea muda wangu, kupotezewa muda unalalamika? -------- kweli wewe, kuna watu wamepotezewa mpaka roho zao wako makaburini kimyaaa hawalalamiki, kwanza kwani huo muda aliUtumia peke yake? si mlikuwa wote nyie? sasa je? mmepotezeana muda au kakupotezea?
mwingine tena eti ohooo unajua nilimgharamia sana, unalalamika mwenyewe, ulimgaramia kwa lipi? kwani alikulazimisha? na we si ulikuwa unamgharamia ili upate unachokihitaji au? ulipata hukupata? kama ulikuwa unapata unalalamika nini, unataka kurudishiwa chenji? -------- wewe, tena ukute ulikuwa unampa vishikumikumi, hata hela ya vishete nayo ulimgharamia ha ha ha haa, umevurugwa siyo bure, kuna watu waliwanunulia nyumba mademu zao wameachana afu kimyaaa, we mweye hela za kuunga unga lo! kelele balaa, tutolee upumbavu wako hapa
eti unakonda, dume zIma huli kisa umeachwa! ebo! wendawazimu huu eti, we unajipa mateso kisa!, umeambiwa wanawake wameisha? ndo ujifunze, utamwaminije binadamu mwenzio mpaka unampa moyo wako wote, ndo mkome sasa, jifunzeni sio kulia lia hapa, au hamjui kama mapenzi ni ushenzi? mambwa nyie..
kama unataka mapenzi ya kweli jua hayapo, nakwambia tena mapenzi ya kweli yalizikwa miaka mingi, siku hizi mnapoteza muda tu,ni nadra kumpata mpenzi mwenye kupenda kweli kama WASTARA, siku hizi watu wanapenda pochi bwana, mengine wanatupia huko, NDO MTAFUTE HELA SASA MPENDWE NYIE SI MABWEGE BWANA, nakuambia tena wa kufa sijui na kuzikana kama COMPLEX NA VIVI hawapo. UKIWAPATA SHUKURU MUNGU.mjifunze kila siku si mnawasikia wanasema MKE MWEMA ANATOKA KWA MUNGU ILA MME BORA ANATOKA BANK, inamaana hamjawahi kusikia?, sasa mnajisumbua kuwapa mioyo yenu watu kama hawa ili?, MTENDWE TU MNAJITAKIA WENYEWE.
MWISHO nawaambia siku hizi hakuna ndoa, wadada wa mjini wanataka kuolewa siyo kwamba wanawapenda sana, KWA TAARIFA YENU WANATAKA KUOSHA NYOTA ZAO TU. ndo maana vindoa vyenu mlivyofunga kwa mbwembwe mkatupigia kelele mjini vinajivunjikia tu kama biscuti zilizolowana hivi.........NILIKUWA NA WASALIMIA TU JAMANI. MUWE NA SIKU NJEMA