Habari na Picha: Mwigulu Nchemba afungua kampeni jimbo la Kalenga kwa kishindo.

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264
1.jpg

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa, akizungumza na kuomba kura kwa wakazi wa mji Ifunda mapema leo jioni katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ifunda, Iringa Vijijini.
998154_673148509413890_866782362_n.jpg
Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Godfrey William Mgimwa akibebwa Juu na Wanachama/wapenzi wa CCM mara baada ya Kuwasili Viwanja Vya Stendi-kata ya Ifunda.
1920092_673149482747126_1709045094_n.jpg
1922456_673150029413738_1705757025_n.jpg
1902910_673150139413727_1773692866_n.jpg
1800203_673150216080386_1798829731_n.jpg
Mapokezi Mazito yakiendelea ya
Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara na Kijana Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey William Mgimwa kwenye uwanja wa Stedi-Kata ya Ifakara hii leo wakati wa Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo la Kalenga.

1921966_673148426080565_261341706_n.jpg
Mh:Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara akisaini Kitabu akiwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey William Mgimwa mara baada ya kuwasili Viwanja Vya Stendi Kata ya Ifunda.
1888549_673147896080618_348924720_n.jpg
1888549_673147976080610_661538409_n.jpg
1959988_673148062747268_1024847000_n.jpg
Chief Wa Wahehe,Chief Mkwawa ambaye pia ni Kada Mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi akishikana Mikono ya Baraka na Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga Godfrey William Mgimwa,Pia akisalimana na Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba hii leo kwenye Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni kata ya Ifunda-Kalenga.Kubwa zaidi CHIEF MKWAWA ambaye ni Mtoto wa Marehemu Mkwawa alikuwa anakanusha taarifa kuhusu Yeye Kuunga Mkono Chadema,Amesema hawezi kuunga Mkono chama ambacho hakieleweki kuanzia muundo wake na hata maamuzi yake ndani ya Chama.Yeye ni MwanaCCM damu damu,na ameapa atafia CCM.
1797426_673145792747495_18005571_n.jpg
Msanii Dokii ambaye ni kada wa Chama Cha Mapinduzi akitumbuiza kwenye ufunguzi wa kampeni wa Jimbo la Kalenga kwa Chama Cha Mapinduzi.Dokii ametunga wimbo rasmi kwaajili ya Kalenga na Umuhimu wa Kijana Godfrey William Mgimwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo,
1782048_673148132747261_723439966_n.jpg
1902727_673148216080586_1805694855_n.jpg
Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini Ndugu Mtatulu akionesha baadhi ya Mitego inayodaiwa kuwekwa na Vijana wa CHADEMA kwenye njia ili Magari ya CCM yanayozunguka kwenye Kampeni yapata matatizo.Pia Ndugu Mtatulu alitaja majina ya Wahusika na ameshayapeleka Polisi kwa hatua zaidi za kisheria.
1939913_673147369414004_1013933446_n.jpg
Naibu katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba akiteta Jambo na Kijana Godfrey William Mgimwa ambaye ni Mgombe Ubunge Jimbo la Kalenga.
1796508_673147039414037_1820245886_n.jpg
Wabunge wa Iringa(Wilaya+majimbo) wakitoa neno la kuomba Kura kwa Wananchi Wa Ifunda ili wamchague Mgombe wa CCM Kijana Godfrey William Mgimwa.
1604966_673147126080695_2047039991_n.jpg
1690017_673146509414090_417516203_n.jpg
1800268_673146769414064_902539448_n.jpg
1009973_673145979414143_612310108_n.jpg
1932458_673146076080800_1084116287_n.jpg
1798027_673146112747463_961830305_n.jpg
1966845_673146386080769_1801564682_n.jpg
Ni Naibu Katibu Mkuu CCM_Bara Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na mamia ya Wananchi waliofurika Viwanja Vya Stendi Kata ya Ifunda hii leo kuhudhuria Mkutano wa hadhara wa ufunguzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo la Kalenga(CCM).Mh:Mwigulu Nchemba amewaomba Wananchi wa Kalenga kumchagua Kijana Godfrey William Mgimwa kwa sababu anakila sifa za kuwatumikia Wananchi wa Kelenga,Lakini pia ni Kijana aliyependekezwa na Chama kuanzia ngazi ya Chini hadi Taifa kwa mtindo wa Kura za maoni na amewashinda wenzake 9.
Mh:Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa Kwa namna Marehemu Mgimwa alivyolitumikia Jimbo lake na kuiletea Heshima Nchi yetu na Jimbo la Kalenga,kuna kila sababu ya Kuipa nafasi CCM iendelee kutekeleza Ilani yake ndani ya Jimbo hilo.Mh:Mgimwa tangu kufariki kwake Vyama vya siasa vimekuwa mstari wa mbele kumsifia kutokana na Utendaji wake Kuanzia Wizara ya Fedha hadi Jimboni kwake hasa upande wa Miundombinu,Maendeleo yote yaliyofanyika ndani ya Jimbo la Kalenga ni Matunda ya sera nzuri za CCM na Ilani ya CCM ndani ya Jimbo hilo.
Pia Mwigulu amezungumzia kuhusu Amani na Mshikamano ulipo kwa Wananchi wa Kalenga ni lazima uendelee kudumishwa,Kitendo cha kukaribisha wapinzani kwenye jimbo hili ni sawa na kukaribisha Vurugu kwasababu Wapinzani hasa Chadema katika Taifa hili hawana rekodi nzuri ya kudumisha amani kwenye maneo wanayoongoza.
Kubwa zaidi Mh:Mwigulu Nchemba ameendelea kuwaomba Wanakalenga kufanya Kampeni za Ustaarabu,Kampeni za Amani na Utulivu.Kwa MwanaCCM kufanya Vurugu sio Jambo jema,bali tutumie Amani tuliyonayo kuwaelimisha hata wenzetu wa Upinzani kufanya siasa za kistaarabu,Waache michezo ya Kusababisha Vifo kwa Wananchi wasio na hatia yoyote ile.Siasa safi ni zile za Kupambanisha Sera na Uwezo wa Kujenga hoja majukwaani.
Hivyo tar.16/03/2014 Wanakalenga Wote wanajitokeze Kupiga Kura na Kumchagua Mgombea wa CCM Kijana Godfrey William Mgimwa kwa maendeleo ya Wote Wanakalenga.

1970810_673145652747509_662874180_n.jpg
Kijana huyu ameamua kurudisha Kadi ya Chadema baada ya Somo zuri Kutoka kwa Mh:Mwigulu Nchemba kwenye Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni Jimbo la Kalenga.
1975053_673145836080824_1402178756_n.jpg
1920468_673145896080818_1234731803_n.jpg
Naibu Katibu Mkuu CCM_Bara Mh:Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa Ubunge Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey Mgimwa hii leo kwenye Ufunguzi wa Kampeni Jimbo la kalenga.Uchaguzi unategemewa Kufanyika tar.16/03/2014.
 
CCM ni sera, CCM ni Ilani ya uchaguzi, CCM ni kimbilio la wapenda maendelea na CCM ni ushindi.

CCM ilithubutu, CCM iliweza na CCM inatenda.

Kidumu Chama cha Mapinduzi.
 
Enyi CCM mmemtuma Mwigulu kwa nini hamkuwatuma watu wenye busara kama mzee Mangula? Mwigulu ndio kaharibu njia maana itakuwa kama Arumeru na Igunda ambako walilazimisha ushindi.
 
Dah! kazi ipo! sasa mbona mchana kulikuwa na uzi hapa unaosema kwamba eti uzinduzi wenu huo ulitawaliwa na zomeazomea? sasa naanza kuelewa kwa nin Dr slaa jana katuambia kuwa amegundua kwamba siasa za keybord hazisaidii maana yeye yuko field anajionea!
 
...naona mmeamua kujiibia wenyewe,mnato kwenye mfuko wa shati na kuweka kwenye mfuko wa suruali...
 
Hivi siku hizi raia wa nje wanaruhusiwa kugombea?, huyu mgombea wa CCM hata Kalenga haifahamu vizuri, ni raia wa Uingereza,sasa wana kalenga atawasaidiaje?
 
CCM ni sera, CCM ni Ilani ya uchaguzi, CCM ni kimbilio la wapenda maendelea na CCM ni ushindi.

CCM ilithubutu, CCM iliweza na CCM inatenda.

Kidumu Chama cha Mapinduzi.

Vipi Mwingereza amaeshindwa kuongea kiswahili nini maana picha zote Mwigulu,

Yeye aliongea ila hakupigwa picha..,
 
CCM ni sera, CCM ni Ilani ya uchaguzi, CCM ni kimbilio la wapenda maendelea na CCM ni ushindi.

CCM ilithubutu, CCM iliweza na CCM inatenda.

Kidumu Chama cha Mapinduzi.

MwanawaDiwani umeona hayo mabasi ya Upendo hapo pembeni ya uwanja wa mkutano?? umeona na magari mengine madogo ya gharama pia??

Kiongozi yaani kumbe CCM haijaacha tabia za kuwabeba watu waende kuhudhuria mikutano yao?? Mmoja wa wamiliki wa mabasi ya Upendo Charles Nyagawa ni Diwani wa CCM kata ya Mlowa, unategemea nini?? na mwingine ni waziri wa serikali ya JK?? nimeona sura za watu wa Mlowa wengi sana hapo, nimeona sura za watu wa Iirnga mjini na Isman pia, hivi kubeba watu wahudhurie mikutano ndio kupendawa???

Mwigulu ana njia zake za kupata ushindi sio lazima ziwe kura, ndio mana kaleta watu toka sehemu zingine ionekane chama na mgombea wanapenda ili iwe rahisi kuhalalisha njia.

Tunataka uchaguzi ulio huru na haki sio kutumia polisi au kuiba kura.
Na hicho ndio kilio changu
 
Uzi mreeeeeeeefu picha za kudiarudia tu, pamoja na kutumia mabasi mengi kusomba watu toka vijijini lakini bado watu wamekuwa wachache.
1932458_673146076080800_1084116287_n.jpg


Mkuu kwa mara ya kwanza nampongeza Mwingereza kwa kusomba watu kwa mabasi, japokuwa watu ni wachache magari ni mengi...
 
Hivi siku hizi raia wa nje wanaruhusiwa kugombea?, huyu mgombea wa CCM hata Kalenga haifahamu vizuri, ni raia wa Uingereza,sasa wana kalenga atawasaidiaje?

Hizi Propaganda zimeshapitwa na muda, hebu CHADEMA wawaeleze wana Kalenga watawafanyia nini ili kukabiliana na changamoto mbalimbali!
 
"Harambee eeeeeh harambeeee jama harambeeee, Wapinzani tuwachape tuwashikeshike tuwatupe"

Misukule mtaweka wapi sura zenu mwaka huu
 
Hivi Mwigulu amwahi japo kupitia mafunzo ya mgambo? Manaake anapenda kujionyesha kama kiongozi wa majeshi vile....
 
Wizarani yupo nani sasa???!!!
Bungeni katiba inaendelea!!!!!

As if nchi haina watu!!!????
 
Back
Top Bottom