Profesa
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 905
- 624
Wanasiasa na si chama, wakiwemo wa CCM, CHADEMA, CUF, TLP na vyama vingine vyovyote. Ni kauli iliyjaa hekima na inapaswa kutathminiwa kwa makini. Huyu katibu Mkuu ndie aliyeonya hivi majuzi kuwa swala la serikali mbili au tatu litategemea maamuzi ya wananchi na serikali ya CCM itafuata maamuzi ya wananchi na si matakwa ya watu wachache, ingawa kijana alivyoingia jukwaani povu lilimtoka akiongea kinyume kabisa na katibu wake kusisitiza hakuna hoja ya serikali tatu. Sasa hapa ni kujipanga au kuchanganyana?Na Said Mwishehe, Simiyu
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrhaman Kinana amesema wanasiasa ni watu hatari, kwani wengi wao wapo tayari kuona watu wanakufa kwa ajili ya wao kutaka madaraka.
Amesema zipo nchi nyingi ambazo zimeingia kwenye machafuko na mamia ya watu kupoteza maisha kwa sababu tu ya kusukumwa na baadhi ya wanasiasa ambao siku zote wanawaza mambo binafsi zaidi.
Akizungumza juzi katika ziara yake ya kwanza katika Mkoa wa Simiyu baada ya kumaliza ziara mkoani Shinyanga, Kinana alisema kuna wanasiasa wapo tayari kuona watu wanapoteza maisha ili tu wao waingie kwenye madaraka.
Wanasiasa ni watu hatari. Wapo tayari watu wafe wao wapate madaraka na kisha wakiwa kwenye nafasi wanachofanya ni kutoa pole kwa waliopoteza ndugu zao na jamaa zao.
Wanagawana vyeo wakati waliopoteza roho zao hawapo duniani. Hii si sawa lazima Watanzania muwe makini na wanasiasa wenye uchu wa madaraka na wapo tayari kuwatanguliza watu kufa ili wao wafikie malengo yao, alisema Kinana.
Alitoa mifano ya nchi jirani ya Kenya, ambapo watu zaidi ya 800 wa nchi hiyo walipoteza maisha baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo mwaka 2008, lakini waliosababisha wakaamua kugawana vyeo.
Kuna nchi nyingi ambazo zimeingia kwenye machafuko na watu kupoteza maisha kwa sababu tu kuna msukumo wa wanasiasa wenye malengo yao binafsi.
Wanahamasisha watu wanaingia mtaani kuandamana, lakini mwisho wake wanaokufa, kupoteza viungo vya mwili na kujeruhiwa ni wananchi ambao walikubali kushawishiwa.
Ikifika wakati wa kugawana vyeo wananchi walioingia kwenye maandamano hawapo tena na badala yake wanasiasa wanakaa na kuanza kugawana vyeo. Viongozi wanasema ni mipango ya Mungu. Waswahili wanasema akili za kuambiwa changanya na zako, alisema Kinana.
Akizungumzia zaidi katika hilo, alisema ni jambo jema kwa Watanzania kutambua kuna wanasiasa ambao hawana nia njema na nchi, hivyo wanakila sababu ya kuhakikisha amani na utulivu unapewa kipaumbele.
Kuhusu mchakato wa Katiba alisema ni vema ikapatikana, lakini haina maana kuwa ikipatikana basi kila Mtanzania atakuwa na maisha mazuri.
Wakati huo huo Kinana alisema CCM itahakikisha inaendelea kuwa karibu na mabalozi wa nyumba 10 kwani wanafanya kazi kubwa ya kujenga chama hicho.
Alisema CCM inao wajumbe milioni moja nchi nzima, na hao ndio msingi wa chama hicho kwani wanachama wapo kuanzia ngazi ya chini na si ngazi ya juu kwani huko hakuna wanachama.
Jambo Leo