Habari kuhusu KUTEKWA siku kama ya leo

Habari kuhusu KUTEKWA siku kama ya leo

Joined
Sep 17, 2018
Posts
25
Reaction score
23
Imeandikwa na Malisa GJ

Ilikua dakika, masaa, siku na hatimaye wiki imekatika. Habari ya kutekwa kwa MO ilipobreak kwa mara ya kwanza alhamisi kama leo wiki moja iliyopita ilileta taharuki nchi nzima. Kwenye mitandao na hata main streams ilikua ndio mjadala wa siku. Lakini kadri siku zinavyozidi kwenda uzito wa habari hiyo unazidi kupungua. Ni kama vile tunaanza kuzoea haya matukio ya utekaji. Hii si sawa. Hatupaswi kukaa kimya. Kukaa kimya ni kuwapa ahueni watekaji.

Kwa sasa dunia inapitia kipindi kigumu sana katika historia ya haki za binadamu. Giza hili la kutoheshimu utu wa binadamu mwenzio limetanda dunia nzima. Watu wanatekwa, wengine wanarudi wazima, wengine wanarudi vilema, wengine wanarudi maiti na wengine hawarudi kabisa.

Mwandishi wa habari na mkosoaji wa muda mrefu wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi alitoroka nchi hiyo mwaka jana na kwenda kuishi uhamishoni Uturuki baada ya kuhofia usalama wake. Tarehe 2 October mwaka huu aliitwa ubalozi wa Saudi Arabia mjini Instanbul kwenda kuchukua cheti chake cha ndoa kilichokua kinashikiliwa na serikali ya Saudia.

Alipoingia tu ubalozini hapo hakutoka tena. Lakini ubalozi ukakanusha vikali madai kwamba Khashoggi hakutoka. Taarifa ya ubalozi ikasema alitoka kupitia mlango wa nyuma. Lakini baada ya kelele nyingi za kimataifa serikali ya Uturuki ikaamua kuingilia kati hatimaye kulazimisha ukaguzi kwenye ofisi za Ubalozi huo.

October 15 wakapata ushahidi unaoonesha kuwa Khashoggi aliuawa ndani ya ubalozi huo kwa kucharangwa mapanga, na vipande vya mwili wake vilifichwa kwenye mifuko maalumu ndani ya ubalozi. Baada ya maafisa wa ubalozi huo kubanwa walieleza kwamba, walitekeleza ukatili huo kwa agizo la mwanamfalme wa Saudia Prince, Mohammad bin Salman.

Just imagine ukatili mkubwa hivi unafanywa na serikali, halafu serikali hiyohiyo awali ilikanusha hadi mataifa yalipoingilia kati. Maana yake ni kwamba kama kelele za kumdai Khashoggi zingepoa, basi dunia isingekaa ijue ukweli huu. Ingesemekana tu amepotea na story ingeishia hapi.

Mkuu wa Shirika la Polisi duniani (Interpol) Meng Hongwei aliingia China September 25, akitokea Ufaransa kupitia Stockholm. Alipotua tu akamtumia mke wake 'emoji' ya kisu kupitia whatsapp. Hiyo ilikua ni 'code language' kuonesha kuwa alikua kwenye hatari (niliwafundisha matumizi ya code language last week. Hakikisha una codes za kuwasiliana na watu wako).

Baada ya kutuma 'emoji' hiyo mkewe alielewa kwamba mumewe yupo kwenye hatari na hapohapo akaanza kumtafuta lakini simu zake hazikupatikana tena. Haraka akatoa taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa mumewe yupi hatarini. Akaripoti pia polisi.

Kelele za kumdai Meng zikaanzia hapo. Vyombo mbalimbali vya habari, taasisi za kiraia, mashirika ya haki za binadamu, balozi za nchi mbalimbali zote zikapiga kelele. Vyombo vya habari vikadai serikali ya China inamshikilia but as usual serikali ya China ikakanusha vikali.

Lakini pamoja na kukanusha kelele hazikukoma. Tarehe 04 Oktoba Interpol wenyewe wakaomba kuingia 'mzigoni' kumtafuta boss wao. Serikali ya China kwa vyovyote ilijua ingeumbuka kama Interpol wakituma makachero wao kuchunguza. Kwahiyo kabla hawajajibu ombi la Interpol, tarehe 06 Oktoba wakakiri kwamba ni kweli wanamshikilia Meng.

Serikali ya China kwa mara ya kwanza ikatoa official statement kwamba inamshikilia Meng na kwamba anahojiwa na National Supervisory Commission (NSC) kwa madai ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka alipokuwa Waziri nchini humo, kabla hajawa Rais wa Interpol.

Just imagine serikali ileile iliyokanusha kumshililia, ndio hiyohiyo iliyokubali baada ya kuona pressure imekuwa kubwa. Ina maana bila kelele za wanaharakati mbalimbali pengine wangeweza kumpoteza kabisa Meng na wakaendelea kukanusha kwamba hawamshikilii.

Alipoachia tu tarehe 8 Oktoba akatangaza kujiuzulu nafasi yake ya Urais Interpol. Hatujui alifanywa nini alipokuwa mateka hadi kuamua kujiuzulu lakini atleast yeye alirudi mzima.

Matukio haya mawili makubwa yaliyotikisa dunia (Khashoggi na Meng) yalifanywa na serikali za nchi zao. It was a state organised crime, yani uhalifu uliopangwa na kutekelezwa na dola. Ukiona dola imefikia hatua ya kupanga na kutekeleza uhalifu mkubwa kama huo ujue hakuna aliye salama. Jukumu la dola yoyote duniani ni kulinda watu wake kwa nguvu zote. Lakini ukianza kusikia zipo dola zinateka watu wake, kuwaua au kuwapoteza kabisa ujue dunia haipo salama.

Hata hivyo si kila utekaji unafanywa na dola. Asilimia kubwa ya utekaji duniani hufanywa na magenge ya wahalifu, na wengi wamekuwa wakiteka watu na kudai fidia (ransom). Huko nchi za Central na Latin America kama Mexico, Paraguay na Costa Rica matukio haya yameshamiri sana. Familia nyingi za matajiri zinatekwa then watekaji wanadai fidia wakilipwa wanamuachia mateka.

Watu mashuhuri wengi wamewahi kutekwa na watekaji kudai fidia. Mwaka 2011 Ivan Kaspersky mtoto wa 'sofware developer' mashuhuri duniani Eugene Kaspersky alitekwa na watekaji wakadai mamilioni ya dola.

Teddy Wang, mwenyekiti wa Chinachem na bilionea mmiliki wa majengo huko Hong Kong aliwahi kutekwa mara mbili, na watekaji wakadai dola milioni 60 sawa na Bilioni 130 za Kitanzania.

Bahati mbaya miongoni mwa watu waliowahi kutekwa au kupotea hapa Tanzania kama Ben Saanane, Azory Gwanda na hata MO hakuna aliyedaiwa fidia hadi sasa. Hatujui dhamira ya watekaji, maana ingekuwa ransom wangeshasema. Pengine malengo yao ni tofauti na ransom.

Tuwaombee watanzania wenzetu waliopotea, na tuziombee familia zao ili Mungu azitie nguvu katika kipindi kigumu wanachopitia. Waziri Kangi Lugola alisema kuna watanzania 75 waliotekwa na kupotezwa katika kipindi cha miaka mitatu ya utawala wa JPM. Hii ni habari ya kuogofya sana. Roho za watanzania wenzetu 75 si jambo dogo.

Tuiombee pia serikali yetu na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ili viweze kuchukua hatua stahiki juu ya matukio haya. Na pale vinapozidiwa visisite kuomba msaada nje ya nchi. Kama tunaweza kuomba msaada wa Condom Marekani, kwanini tuone aibu kuomba Scotland Yard kuja kutusaidia kuwatafuta akina Ben Saanane, Azory, MO na wengine?

Malisa GJ

Ingia hapa kwa mengine mengi www.facebook.com/criticalthinkerog/
FB_IMG_1539591849165.jpeg
FB_IMG_1539636846511.jpeg
 
Aisee nimesoma article moja huko Twitter kuhusu huyo Jamal Khashoggi dah kauwawa kinyama sana , jamaa aliyekuwa anamcharanga kwa kutumia msumeno akawa anawaambia wenzake "when am doing this job I normally listen to music , so do the same "akaweka head phones masikioni akaanza kumcharanga jamaa wakati akiwa hai, huku balozi huko ofisini kwake akisikia makelele..... Dah so barbaric.
 
Rais et anataka uchumi Wa kat, wa nini sasa Kama mtu Kama MO anapotea kifala namna hii
 
Back
Top Bottom